Monday, February 13, 2017

MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA ZIARANI SINGIDA

MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa rai kwa Wanzania kujenga tabia ya kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji maalumu.

Wake hao wa viongozi pia wamewatahadharisha watumishi wanaofanya kazi katika vituo vya kulelea wazee wasiojiweza wahakikishe misaada inayotolewa na wadau mbalimbali inawafikia walengwa bila ya kuchakachuliwa.

Wameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 13, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Sukamahela wilayani Manyoni Mkoani Singida.

Katika kituo hicho wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage, ambapo Mama Janeth amewataka viongozi wa kituo kuhakikisha chakula hicho hakichakachuliwi.

Akizungumza na wazee wa makaazi hayo, viongozi mbalimbali na wananchi wanaozunguka eneo hilo Mama Janeth amesema “Naomba chakula hiki kitunzwe vizuri na hakikisheni kinawafikia walengwa na kisichakachuliwe hii ni sadaka,”.

Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza na kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulelea walemavu na wasiojiweza nchini kwa sababu wanakabiliwa na changamoto nyingi.

“Watanzania wote popote mlipo tukumbuke kutembelea vituo vya kulelea wazee kikiwepo na hiki tulichokitembelea leo cha Sukamahela na kutoa misaada mbalimbali kkwa kadri tutakavyojaaliwa,” amesema.

Awali Mkuu wa Makazi hayo Bw. Yeremia Ngoo alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1974 chini ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa lengo la kuwasaidia watu wenye ukoma na wazee wasiojiweza mkoani Singida.

Bw. Ngoo alisema kituo hicho chenye wakazi 62 kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa wapishi ambapo kwa sasa yupo mmoja huku mahitaji yakiwa ni wapishi wanne. Pia nyumba nyingi ni chakavu na zina nyufa.

Naye Mwenyekiti wa Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee Andrea Yohana aliwashikuru wake hao wa viongozi na kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza.
Read More

Saturday, February 11, 2017

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AONGOZA MAZOEZI YA VIUNGO YA KITAIFA MKOANI DODOMA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza mazoezi ya viungo kwa Mawaziri Wabunge pamoja nawananchi waliuhudhiria katika kushiriki mazoezi hayo ambayo yamefanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma yakiwa nalengo la kupambana na maradhi yasiyo ambukizika Mazoezi hayo yamefanyika kitaifa Mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongoza mazoezi ya viungo kwa Mawaziri Wabunge pamoja nawananchi waliuhudhiria katika kushiriki mazoezi hayo ambayo yamefanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma yakiwa nalengo la kupambana na maradhi yasiyo ambukizika Mazoezi hayo yamefanyika kitaifa Mkoani Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia Mawaziri Wabunge Watumishi na Wananchi wa Mkoa wa Dodoma ambao wajitokeza katika kushiriki Mazoezi ya Viungo yenyelengo la Kupambana na Magonjwa yasiyo ambukizika Mazoezi hayo Kitaifa yamefanyika katika Uwanja wa Jamuhuri Mkoani Dodoma.

Read More

Thursday, February 9, 2017

MAJALIWA ATEMBELEA OFISI KUU YA ATCL NA KUZUNGUMZA NA VIONGOZI

Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati alipokwenda kwenye Ofisi kuu ya ATCL kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato , Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi .
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Regini Masoud (kulia) kuhusu mfumo mpya wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki wakati alipotembelea ofisi kuu ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL)  jijini Dar es salaam kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato, Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakati alipokwenda kwenye Ofisi kuu ya ATCL kufuatilia mwenendo wa uendeshaji wa Shirika na usimamizi wa mapato , Februari 9, 2017. Kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano, Profesa Makame Mbarawa na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa ATCL.  Mhandisi Ladislaus Matindi.

Read More

CAG KUCHUNGUZA MAPATO YA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuchunguza ukusanyaji wa mapato ya Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL).

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamis, Februari 9, 2017) alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.

“Nitamuagiza CAG  aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili kuanzia mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa manufaa ya Taifa.

Pia amewataka waache kukusanya mapato kwa kutumia  risiti za kuandika kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.

“Vitu vingi vinavyoenda manual ni rahisi kufa. Serikali tumeagiza malipo yote yafanyike kielektroniki na kote tunakotumia mfumo huu tumepata mafanikio,”amesema.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa mapato.

Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingaria ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.
Read More

Wednesday, February 8, 2017

VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA NI YETU SOTE

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa mapambano ya kukabiliana na tatizo la Dawa za Kulevya ni jukumu la kila mwananchi na wala sio suala la kuiachia Serikali peke yake.

Ameyasema hayo bungeni jana wakati akijibu hoja za wabunge waliochangia juu ya Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya UKIMWI na Dawa za Kulevya iliyoibua maswali kwa Serikali kuendelea kupambana na wanaoshiriki katika biashara haramu ya dawa za kulevya nchini.

Waziri Mhagama alieleza kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha jamii yote kwa ujumla inakuwa mstari wa mbele katika kutokomeza tatizo hili linalowaathiri vijana kwa kiasi kikubwa.
“Mapambano haya ni yetu sote, yasichague mtu na iwe agenda ya Kitaifa inayowahusu Watanzania wote na ikumbukwe kuwa tatizo la dawa za kulevya lina historia tangu mwaka 1990 na Serikali imekuwa ikipambana kwa jitihada nyingi hivyo niombe watanzania wote tuunge mkono vita hii ili kumaliza kabisa tatizo hili”. Alisema Waziri

Aliongezea kuwa, dhamira hii ya Serikali ilianza kuonekana tangu kuwepo kwa sheria namba 9 ya mwaka 1995 hadi ilipofanyiwa marekebisho mwaka 2014 na kubaini kuwa asilimia 56 ya nguvu kazi ya vijana ndiyo imeathiriwa na tatizo la dawa za kulevya.

Aidha pamoja na mapambano hayo, tayari sheria namba 5 ya mwaka 2015 na miundo ya mapambano inaelekeza namna ya kupambana na vita dhidi ya dawa za kulevya.
Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe alieleza Bunge kuwa ziwepo jitihada za makusudi za kuunga mkono mapambano haya yawe ya Watanzania wote kwa kutoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano na kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda kwa namna alivyojidhatiti kupambana na wote wanaoshiriki katika biashara hizi za dawa ya kulevya.

“Nieleza wazi kuwa jitihada za Serikali pekee hazitoshi ni lazima jamii iunge mkono kwa kuwafichua wanaojihusisha na mtandao huu wa Dawa za Kulevya na Mhe.Paul Makonda nampongeza kwa kuthubutu kuingia kikamilifu katika vita hii”.Alisema Mwakyembe

Alimalizia kwa kueleza kuwa, kinachohitajika ni dhamira ya dhati na si fedha, hivyo Serikali imedhamiria kukomesha kabisa tatizo hili nchini.

Read More

Tuesday, February 7, 2017

MAJALIWA AKUTANA NA ASKOFU GAMANYWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO MISSION INTERNATIONAL kabal ya mazungumzo yao,Ofisini kwa Waziri Mkuu, Jijini Dar es salaam Februari 6, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO MISSION INTERNATIONAL, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 6, 2017.

Read More

DAWA YA MSONGAMANO WA MBAGALA YAPATIKANA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Wilaya za Temeke na Mkuranga kuangalia namna ya kupunguza msongamano uliopo katika eneo la Mbagala.
               
Moja ya hatua alizowashauri kuchukua ni pamoja na kuhamisha kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kutoka Temeke hadi Mkuranga.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na viongozi wa wilaya hizo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafua njia za kuondoa msongamano huo.

Amesema kwa sasa hakuna namna ambayo wataweza kuondoa msongamano huo zaidi ya kuhamishia kituo cha mabasi ya mikoa ya kusini wilayani Mkuranga.

Waziri Mkuu amesema eneo la Mbagala kwa sasa lina msongamano mkubwa ambao ni lazima Serikali ichukue hatua za haraka za kuuondoa.

“Ikiwezekana mabasi ya mikoa ya kusini yaishie Mkuranga, hivyo kirikianeni kutafuta  eneo la kujenga kituo kikubwa cha kisasa cha mabasi,” amesema.

Amesema kituo hicho watakachokijenga kiwe na uwezo wa kuhudumia mabasi yote yatokayo mikoa ya kusini na kituo cha Mbagala kiwe cha daladala za kawaida.

Pia Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa kituo hicho kutawezesha kuongeza mapato ya Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga.

Aidha Waziri Mkuu amewataka viongozi hao kwenda kujadiliana katika vikao vya mabaraza ya Madiwani juu ya mkakati huo na kisha kumpelekea taarifa ifikapo Februari 15 mwaka huu.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Bw. Filberto Sanga amesema wazo hilo ni zuri na wilaya yake ina maeneo ya kutosha kujenga miundombinu hiyo.

“Ni kweli wilaya ya Temeke imeelemewa kwa maana ya maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maendeleo na haina pa kupumulia zaidi ya Mkuranga , hivyo tupo tayari kushirikiana nao,” amesema.

Wakati huo huo, Bw. Sanga ameiomba Serikali itakapoanza awamu ya tatu ya ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendo kasi ufike hadi Mkuranga mjini badala ya kuishia Vikindu.

Amesema kwa sasa wilaya yake ina viwanda 67 ambavyo kati yake vipo vinavyofanya kazi na vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za ujenzi, hivyo mabasi hayo yatarahisisha usafiri kwa wafanyakazi.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bw. Felix Lyaniva amesema amefurahishwa sana na mawazo hayo ya kuhamisha kituo cha mabasi cha Mbagala kwani katika vitu vilivyokuwa vinamnyima usingizi ni pamoja na msoingamano wa mabasi na wafanyabiashara wadogo wadogo katika eneo hilo.


Read More

MAJALIWA AKUTANA NA VIONGOZI WA WILAYA ZA MKURANGA NA TEMEKE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa wilaya za Mkuranga na Temeke, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 7, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa wilaya za Mkuranga na Temeke, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Februari 7, 2017.


Read More

WAZIRI MKUU AWATAKA MABALOZI KUTAFUTA WAWEKEZAJI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanatumia uwakilishi wao kutafuta wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta ya viwanda nchini.

Amesema  mkakati wa Serikali ni kuimarisha uchumi  hadi wa kati kupitia sekta ya viwanda, hivyo jukumu la mabalozi hao ni kuhakikisha jambo hilo linafanikiwa.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 7, 2017) alipokutana na mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Brazil, China, Italy, Ufaransa, Jamuhuri ya Kidemkrasi ya Congo (DRC) na Uswisi.

Mabalozi hao ni Balozi Dk. Emmanuel Nchini (Brazil), Balozi Elizabeth Kiondo (Uturuki), Balozi George Madafa (Italy), Balozi James Msekela (Uswisi),Balozi Samuel Shelukindo (Ufaransa), Balozi Paul Mella (DRC), Balozi Mbelwa Kairuki (China).

“Serikali inahitaji watu wa kuja kuwekeza katika viwanda ili kuongeza thamani ya mazao kabla ya kuyauza nje ya nchi, hivyo jukumu lenu ni kuhakikisha tunapata wawekezaji wenye sifa,” amesema.

Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kutumia uwakilishi wao katika nchi hizo kwa kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania.

“Tulinde bidhaa za ndani ya nchi yetu mfano madini ya tanzanite ambayo yanazalishwa Tanzania pekee lakini leo zinazalisifiwa nchi nyingine kwa uzalishaji huo zikiwemo India na China, hivyo jukumu lenu ni kuhakikisha mnatangaza madini yetu ipasavyo,” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kulinda maslahi ya Taifa katika nchi hizo ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na mataifa hayo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao kuhakikisha wanawatambua Watanzania wanaoishi katika mataifa hayo na kushirikiana nao katika kutafuta wawekezaji wa kuja kuwekeza nchini.


Kwa upande wake Balozi Mella ambaye alizungumza kwa niaba ya mabozi wenzake alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba watakwenda kutekeleza wajibu wao ipasavyo.
Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA NA MABALOZI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akizungumza na mabalozi ambao wanaiwakilisha Tanzania nje ya nchi na wanatarajiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi hivi karibuni, Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017. Kutoka kushoto ni Samwel Shelukindo (Ufaransa), Dkt. James Msekela (Uswisi), Mbelwa Kairuki (China), Paul Mella (DRC), Dkt. Emmanuel Nchimbi (Brazil) George Madafa (Italy) na Elizabeth Kiondo (Uturuki).
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akisalimiana na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa akisalimiana na mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam, Februari 7, 2017.

Read More

Monday, February 6, 2017

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA AJIRA KWA VIJANA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa Serikali imejipanga kusaidia vijana kutambua na kuchangamkia fursa mbalimbali za ajira zilizopo nchini ili kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira na  kutimiza adhma ya kuleta maendeleo hususani kwa vijana.

Mhe. Mhagama ameyasema hayo jana wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Kinondoni Mhe. Maulid Mtulia iliyohoji juu ya jitihada za Serikali katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana wakati wa Mkutano wa Tano wa Bunge unaoendelea Mkoani Dodoma.

Katika Mkutano huo Mhe. Waziri alisisitiza kuwa Serikali ina mipango na mikakati madhubuti inayokusudiwa yakusaidia vijana wa Kitanzania ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na kuondokana na umasikini.

Serikali ya Awamu ya Tano imeendelea kuweka mikakati ikiwemo uwanzishwaji wa programu mbalimbali zitakazo saidia kutatua changamoto ya ajira kwa vijana kwa kuangalia matokeo ya tafiti mbalimbali ambazo zimepelekea kuwa na programu zinazolenga kukabili tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana” Alisema Waziri

Alisisitiza kuwa programu hizo ni pamoja na; kurasmisha ujuzi usio rasmi kuwa rasmi, mfumo wa mafunzo kwa vitendo, mfumo wa uanangezi pamoja na kukuza mafunzo kwa watanzania kulingana na soko lililopo kwa sasa.

Pamoja na juhudi hizo zinazotarajiwa kuzaa matunda bado Waziri aliwatoa hofu wananchi wote kwa kuwepo kwa fursa hizo za ajira zitakazo jali hali za watu pasipo kuangalia makabila yao, rangi wala dini.

“Katika kutatua changamoto ya ajira kwa vijana hatuta angalia kabila, rangi wala dini ya mtu bali kutakuwa na haki na usawa”.Alisisitiza Waziri

Aliongezea kuwa, Serikali pia inajitihada za kuvutia uwekezaji kwenye sekta mbalimbali na urasimishaji wa sekta isiyo rasmi ili kupunguza kiwango cha ukosefu wa ajira.

“Serikali itatumia sekta zenye uwezo wa kutoa ajira kwa wingi ikiwemo zile za Kilimo, majenzi, Mawasiliano na Utalii ili kuzitumia kuweka mazingira mazuri kwa vijana kupata fursa za ajira”.

Mhe. Mhagama alisisitizia bungeni kuwa kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika zitatumika kama chachu ya kuangalia maeneo yanayohitaji kusaidia kwa haraka na kupunguza changamoto hiyo kwa vijana.

“Kwa kuangalia tafiti ya Hali ya Ajira Nchini ya mwaka 2014 imeonesha kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kimepungua kutoka asilimia 11.7 mwaka 2006 hadi asilimia 10.3 mwaka 2014 na ukosefu wa ajira kwa vijana umepungua kutoka asilimia 14.2 mwaka 2006 hadi asilimia 11.7 mwaka 2014”,alisema.

Hata hivyo, Waziri Mhagama alieleza kuwa pamoja na jitihada hizo Serikali bado ina wajibu wa kuongeza jitihada zaidi ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa ajira na kuboresha maisha ya vijana.

==Mwisho==
Read More

CDF MABEYO AAPISHWA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,  Paul Makonda na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Siro (kulia) katika hafla ya kumwapisha Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, Ikulu jijini Dar es salaam Februari 6, 2017.
 Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein  akiteta na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  katika hafla ya kumwapisha Jenerali,  Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania, Ikulu jijini Dar es salaam Februari 6, 2017.
 Rais  John Pombe Magufuli akifurahia katika mazungumzo kati yake na  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania(CDF), Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) na Mkuu wa Majeshi ya  Ulinzi ya Tanzania Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange baada ya kumwapisha  CDF Mabeyo, Ikulu jijini Dar es salaam Februari 6, 2017.
Rais John Pombe Magufuli akiteta na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  baada ya Rais kumwapisha Mkuu wa majeshi ya Ulinzi, Jenerali  Venance Mabeyo, Ikulu jijini Dar es salaam  Februari 6, 2017.

Read More

BUNGENI DODOMA LEO 2017

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja za wabunge mbalimbali waliochangia wakati wa kujadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Ukimwi Bungeni Dodoma Februari 6, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (kulia) akizungumza na baadhi ya wabunge mara baada ya kuhairishwa kwa Mkutano wa Bunge Mjini Dodoma Februari 6, 2017 katikati ni Mbunge wa Singida Mhe. Ashyrose Matembe.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mhe.Hawa Ghasia nje ya viwanja vya bunge Dodoma Februari 6, 2017.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde (kulia) akizungumza na Mhe. Machano Othman nje ya ukumbi wa Bunge Dodoma mara baada ya kupitishwa kwa Taarifa ya Kamati ya Ukimwi na Dawa za Kulevya Februari 6, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba baada ya kupitishwa kwa Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI kuwa makadirio ya Bunge wakati wa Mkutano wa Sita wa Bunge linaloendelea Mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akibadilishana mawazo na baadhi ya wabunge nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuhairishwa kwa Mkutano wa Sita wa Bunge Februari 6, 2017 Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira na Muungano Mhe.January Makamba wakipongezana mara baada ya kupitishwa kwa Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Ukimwi na Dawa za Kulevya Februari 6, 2017.

Read More

Sunday, February 5, 2017

MAJALIWA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 40 YA CCM YALIYOANDALIWA NA CCM MKOA WA DODOMA

 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wana CCM walioshiriki katika Maadhimisho ya Ndani ya Miaka 40 ya CCM  yaliyoandaliwa na Mkoa wa Dodoma kwenye Kituo  cha Mikutano cha Dodoma  (Dodoma Convention Center) Februari 5, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Anne Kilango, Mbunge wa Kuteuliwa na Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela (katikati)  katika Maadhimisho ya Miaka 40 ya CCM yaliyofanyika  kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma (DODOMA CONVETION CENTER) Februari 5, 2017.
  Mjumbe  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kwenye Kituo cha Mikutano cha Dodoma  Dodoma convetion Center) , Februari 5, 2017.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasalimia wana CCM walioshiriki katika Maadhimisho ya Ndani ya Miaka 40 ya CCM  yaliyoandaliwa na Mkoa wa Dodoma kwenye Kituo  cha Mikutano cha Dodoma  (Dodoma Convention Center) Februari 5, 2017.

Read More