Home
All posts
Tuesday, March 20, 2018
WAZIRI MKUU AMKABIDHI MSAADA BIBI TACLA HAMIDU (MLEMAVU)
| Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemkabidhi Bibi Tecla Hamidu ambaye ni mlemavu wa miguu sh. milioni tano ili aweze kuongezea katika mtaji wake.Ametoa fedha hizo leo (Jumanne, Machi 20, 2018) ikiwa ni katika kutimiza ahadi yake aliyoitoa Februari 22, 2018 kwenye Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes). |
Monday, March 19, 2018
WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA 65 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA AFYA AFRIKA (ESCA )
Sunday, March 18, 2018
WAZIRI MKUU ASHUHUDIA MCHEZO WA KIRAFIKI VIJANA WA NGORONGORO HEROES NA MOROCCO KATIKA UWANJA WA UHURU
Saturday, March 17, 2018
WIZARA SABA KUKUTANA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI MPAKANI MWA TANZANIA NA ZAMBIA
Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini, imeamua kuzikutanisha wizara saba zinazohusika moja kwa moja na changamoto zinazopunguza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na Wawekezaji mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Akiongea wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji katika mkoa wa Songwe na maeneo yaliyopo mpakani mwa Tanzania na Zambia, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora amesema mara baada ya kuhitimisha ziara yake tarehe 17 Machi, 2018, atakutana na makatibu wakuu wa wizara zinazopaswa kutoa suluhisho la changamoto hizo.
“Nitakutana na makatibu wakuu wenzangu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Ofisi ya Rais-Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) na naamini maazimio tutakayotoa katika kikao hicho yatakuwa suluhisho la kuondoa changamoto zinazojitokeza hapa mpakani mwa Tanzania na Zambia” , amesema Kamuzora.
Akibainisha changamoto za mazingira ya Biashara na uwekezaji mpakani mwa Tanzania na Zambia, Mkuu wa mkoa wa Songwe, Luteni Mstaafu, Chiku Galawa amesema, changamoto kubwa mpakani hapo ni usalama kwa wafanyabiashara na biashara zao, ambapo kwa mazingira ya mpaka huo imekuwa vigumu kuuimarisha.
“Mpaka wetu umejengwa kila mahali , hivyo uhalifu unakuwa mgumu kuuzuia Kuna watu wanakunywa pombe Zambia ambazo tumezizuia hapa nchini kuuzwa, na kurudi wamelewa Tunduma, suala la biashara haramu ya ubadilishaji wa fedha inayofanywa mtaani kinyume na sheria na taratibu za nchi ni changamoto , lakini wafanyabiashara wanakwepa kodi kutokana na kuwa kunabaadhi ya watanzania sehemu ya nyumba zao zipo Zambia nyingine ipo Tanzania hivyo ushuru wa forodha haukusanywi kwa madai wanapeleka bidhaa hizo kwa watanzania kwani hawapitishi bidhaa hizokwenye lango husika” alisema Galawa
Galawa amebainisha mipango ambayo Mkoa umejipanga katika kuhakikisha wanakabili changamoto hizo, kuwa ni kuliweka Daftari la wakaazi katika mfumo wa kielektroniki ambalo litajumuisha wakaazi wote wa Tunduma kuanzia umri wa mwezi mmoja na litakuwa linahuishwa kila wakati, Upimaji wa mji waTunduma nao unaendelea na kila mmiliki wa ardhi atapewa hati, pia litajengwa soko kubwa mpakani hapo ili kufanya menejimenti ya biashara mpakani.
Aidha, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu alikutana na wadau wa sekta binafsi, pamoja na wateja katika Kituo cha Forodha cha Pamoja Tunduma, ambao walishauri sekta zinazohusika na Mazingira ya Biashara na Uwekezaji mpakani hapo kwa upande wa Tanzania na Zambia zikutane ili kuharakisha kutatua changamoto zinazopunguza ufanisi wa biashara mpakani hapo.
Lengo la Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji Nchini ni Kupunguza gharama za Kufanya biashara nchini kwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara na Wawekezaji, mpango huo unaotekelezwa na Idara, Wizara na Wakala wa Serikali kwa uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu.
WIZARA SABA KUKUTANA KUTATUA CHANGAMOTO ZA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI MPAKANI MWA TANZANIA NA ZAMBIA
| Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa, Faustin Kamuzora akiendesha kikao kilicho jumuisha watendaji wa serikali na sekta binafsi wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya utekelezaji wa Mpango wa maboresho ya Mazingira ya biashara na uwekezaji mkoani Songwe, tarehe 17 Machi, 2018. |
Friday, March 16, 2018
MAJALIWA AKUTANA NA MAKAMU MKUU WA UDSM
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa William Anangisye, ofisini kwa Waziri Mkuu mini Dodoma, Machi 16, 2018. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa William Anangisye ofisini kwa Waziri Mkuu mini Dodoma, Machi 16, 2018. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Profesa William Anangisye ofisini kwa Waziri Mkuu mini Dodoma, Machi 16, 2018. |
Sunday, March 11, 2018
WAKULIMA 2000 WAONGEZA KIPATO KWA UJENZI WA DARAJA LA MIVARF
Monday, March 5, 2018
WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA UFARANSA NCHINI
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Machi 5, 2018. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frederic Clavier, kwenye makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Machi 5, 2018 |
Sunday, March 4, 2018
WAZIRI MKUU ASHIRIKI UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI MATAMBALALE
| Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akichanganya udongo wa tofali, wakati akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale,Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018, |
| Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akiweka udongo wakati akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale,Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018, |
| Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akiweka udongo wakati akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale,Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018, |
| Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akiweka udongo wakati akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari Matambalale, katika kata ya Matambalale,Wilayani Ruangwa. Machi 4, 2018, |
WAZIRI MKUU AKIWA SIZARANI JIMBONI RUANGWA
| Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chikwale kata ya Mbwemkulu, Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo Wilayani ruangwa kwenye Ziara yake ya kikazi jimboni. Machi,3 2018. |
WAZIRI MKUU AKABIDHI PIKIPIKI MBILI KWA JESHI LA POLISI
| Waziri Mkuu, Kassim.Majaliwa akikabidhi pikipiki mbili kwa Kamanda Mkoa wa Lindi, ACP. Pudensiana Protas, zilizotolewa na kampuni ya WU ZHOU Investment Company kwa Jeshi la Polisi, wakati alipo tembelea kituo hicho jana, Machi 4, 2018 , Wilayani Ruangwa. |
Thursday, March 1, 2018
WAZIRI MKUU AWEKA JIWE LA MSINGI ZAHANATI MBECHA
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsalimia mtoto Shafii Khamis, katika kijiji cha Mtakuja, Kata ya Nanganga Wilayani Ruangwa, Machi 1, 2018. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akuzungumza na wananchi wa kijiji cha Mtakuja, Kata ya Nanganga Wilayani Ruangwa, Waziri Mkuu yupo Wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi jimboni, Machi 1, 2018. |
Subscribe to:
Posts (Atom)
MITANDAO YA KIJAMII
Popular Posts
-
Na. OWM, Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 y...
-
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama...
-
Na. OWM, ARUSHA Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri...
-
Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara w...
-
TAMOBA wafanya wasilisho la mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama wa Bodaboda na BajajiKampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa ...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ambaye ndiye anayesimamia Kamati ina...
-
*Aagiza fedha zilizotengwa zikatumike katika kujengea hospitali Dodoma Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya sik...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipokea maelezo ya namna mashine zinavyochakata mifuko chakavu na ...
-
Katika kuhakikisha malengo ya kutatua masuala ya ajira na kazi, yanafikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Mhe. Samia Suluhu H...
-
Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akiuliza jambo kwa Kaimu Meneja wa Uwa...
Formulir Kontak
Contributors
Powered by Blogger.