| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel wakati alipowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Chato kuanza ziara ya kazi mkoani Geita, Novemba 27, 2018. |
Home
All posts
Tuesday, November 27, 2018
MAJALIWA AWASILI CHATO KUANZA ZIARA YA MKOA WA GEITA
MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI WA GEITA.
| Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Geita wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Halmashauri hiyo, Novemba 27, 2018. |
WAKUU WA MIKOA, WILAYA NA WAKURUGENZI SIMAMIENI UWAJIBIKAJI-MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewaagiza Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wahakikishe wanasimamia vizuri uwajibikaji na utowaji wa huduma kwa wananchi katika maeneo yao bila ya woga.
Kadhalika, Waziri Mkuu amemtaka kila mtumishi wa umma nchini awajibike katika kufanya kazi kwa bidii na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano haitowavumilia watumishi ambao ni wezi, wabadhilifu, wavivu na haitosita kuwachukulia hatua.
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumanne, Novemba 27, 2018) alipozungumza na watumishi, viongozi wa mkoa, wilaya ya Geita na taasisi za umma katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mamlaka ya Mji Geita.
“Watumishi fanyeni kazi kwa bidii na msitarajie kuundiwa tume pale mnapofanya vibaya, ukiharibu kazi tunakushughulikia hapo hapo na huu ndio msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.”
Waziri Mkuu aliwaeleza watumishi hao kuwa wanatakiwa wafanye kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za kazi na pia watambue dhamana kubwa waliyonayo, ambayo ni kuwahudumia wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza watumishi wa umma hususani Wakuu wa Idara wahakikishe wanakuwa na kitabu cha Ilani ya Uchanguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili wapate muelekeo wa utekelezaji washughuli zao.
Waziri Mkuu amesema kitabu cha Ilani ya uchanguzi cha CCM 2015/2020 kina maelekezo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo kila idara inatakiwa kuangalia maelekezo yaliyotolewa kuhusu idara husika na kuyafanyia kazi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba yeye kwa kushirikiana na viongozi wenzake watayafanyia kazi maelekezo yote ambayo ameyatoa.
(mwisho)
SERIKALI IMEJIPANGA KUMALIZA TATIZO LA MAJI NCHINI-MAJALIWA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imepanga kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa kuchimba visima virefu na vifupi pamoja na kutumia maji ya maziwa na mito na kuyapeleka katika maeneo mbalimbali ya wananchi nchini.
Pia, Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa wilaya kusimamia uhifadhi wa maeneo ambayo yana vyanzo vya maji ili kuyafanya yaendelee kuwa chepechepe, hivyo kuhakikisha vijiji vyote vinapata maji ya uhakika. “Lazima maeneo hayo yatambuliwe na yahifadhiwe.”
Ameyasema hayo leo (Jumanne, Novemba 27, 2018) alipozungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa shule Sekondari Bugando kata ya Nzera wilayani Geita, wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi za siku nne mkoani Geita.
Waziri Mkuu amesemaSerikali kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani, itahakikisha wananchi katika maeneo yote nchini wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.
Amesema Serikali imejipanga vizuri kuhakikisha kila kijiji kinapata huduma ya maji safi na salama, hivyo amewaagizawatendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yote yenye misitu na vyanzo vya maji na kuhakikisha yanalindwa.
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema mbali na huduma ya maji, pia Serikali imedhamiria kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).
“Rais wetu Dkt. John Magufuli anataka kuona nyumba ya kila Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu na ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.
Naye, Mbunge wa jimbo la Geita Vijijini, Joseph Musukuma ameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi na ahadi zikiwemo na zile zilizotolewa za Rais Dkt. John Magufuli. “Nashukuru Serikali pia kwa kutuzindulia hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Geita.”
Kuhusu suala la umeme, Mbunge huyo ameishukuru Serikali kwa kuwa vijiji vyake vyote vimeshaunganishiwa umeme isipokuwa vitongoji vichache, ambapo ameomba navyo viunganishiwe nishati hiyo muhimu kwa maendeleo ya wananchi.
Awali,Waziri Mkuu alikagua na kuzindua hospitali ya wilaya ya Geita inayojengwa katika kata ya Nzera na aliupongeza uogozi wa halmashauri ya wilaya ya Geita kwa hatua waliyofikia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
(mwisho)
MAJALIWA AZINDUA MRADI WA MAJI WA IMALABUPINA - ICHWANKIMA
MAJALIWA AZINDUA KITUO CHA AFYA CHA BWANGA WILAYANI CHATO
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya kukagua na Kuzindua Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Bwanga wilayani Chato, Novemba 27, 2018. |
Monday, November 26, 2018
SERIKALI YAZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI
*Yawataka watakaopewa kufanya shughuli zilizoelekezwa kwenye vibali vyao
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezindua huduma za viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki na amewataka watu wote watakaopewa vibali hivyo kutii sheria kwa kufanya shughuli ambazo wameelekezwa kwa mujibu wa vibali vyao na si vinginevyo.
Amesema utoaji wa huduma hizo ni miongoni mwa jitihada za Serikali katika kuvutia uwekezaji, hususan katika sekta ya viwanda kwani hatua hiyo itarahisisha upatikanaji wa vibali hivyo kwa raia wa kigeni na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba 26, 2028) wakati akizindua huduma za viza na vibali vya ukaazi vya kielektroniki katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kwamba hatua hiyo itasaidia kuondoa urasimu na ucheleweshwaji wa huduma pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi.
Amesema Idara ya Uhamiaji inatarajia kuanza kutoa huduma tajwa kwa raia wa kigeni muda wowote kuanzia sasa na kwa kupitia huduma hiyo, raia wa kigeni wataweza kuomba vibali hivyo kwa njia ya kielektroniki wakati wowote na mahali popote walipo.
Waziri Mkuu amesema watakaopewa vibali wanatakiwa kufanya shughuli zao kwa mujibu wa vibali vyao kwa sababu kufanya shughuli tofauti na ilivyoainishwa kwenye kibali ni kosa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Uhamiaji.
Amesema matumizi ya mtandao katika utoaji wa huduma za viza na vibali vya ukaazi ni hatua ya mfano, kwani inakwenda sambamba na mabadiliko ya sayansi na teknolojia na sera ya Serikali ya matumizi ya TEHAMA katika shughuli za Serikali (e-government).
Amesema Serikali inatarajia kuwa, matumizi ya mifumo hiyo itaongeza ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali kwa kuwa mteja ataweza kulipia huduma hizo mwenyewe moja kwa moja pasipo kupitia kwa mawakala au mtu yeyote.
“Natoa wito kwa Maafisa, Askari pamoja na Watumishi wote wa Idara ya Uhamiaji kuhakikisha kuwa mifumo hiyo inatunzwa pamoja na kuendeleza miundombinu yote ya kiutendaji.”
Waziri Mkuu amesema kwa kuzingatia ahadi ya Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli ya kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na raia wa kigeni, Maafisa Uhamiaji wanatakiwa kutoa huduma hiyo kwa wakati, weledi na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Uhamiaji.
Amesema mfumo wa huduma hizo utaunganishwa na mifumo mingine ya Serikali, ambayo inatoa huduma kwa wananchi na wageni kama vile Mifumo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Idara ya Kazi – Ofisi ya Waziri Mkuu, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Mfumo wa Malipo ya Serikali Kimtandao (GePG).
(mwisho)
MAJALIWA AZINDUA VIZA NA VIBALI VYA UKAAZI VYA KIELEKTRONIKI
WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA KIWANDA CHA MATAIRI CHA GENERAL TYRE ARUSHA
![]() |
| Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo. |
Sunday, November 25, 2018
MAJALIWA AZINDUA KAMPENI YA SIKU 16 YA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA JIJINI DODOMA.
| Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozindua kampeni ya Siku 16 ya Kupinga Ukatili wa Kijinsia kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Novemba 25, 2018. |
MAJALIWA AKUTANA NA MWENYEKITI WA BARAZA LA TAIFA LA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI, DKT. FESTUS LIMBU
Friday, November 23, 2018
TUTAENDELEA KUSHIRIKIANA NA VYUO VIKUU VYOTE NCHINI-MAJALIWA
*Asisitiza lengo ni kuona vikitoa elimu yenye kukidhi ubora na viwango
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano na miongozo kwa vyuo vikuu vyote nchini, vya binafsi na vya umma ili viendelee kutoa elimu ya juu yenye ubora na viwango vinavyotakiwa kwa lengo la kukidhi matakwa na ushindani kwenye soko la kitaifa na kimataifa.
Amesema suala hilo ni muhimu likapewa uzito unaostahili kwani wahitimu hao wakitoka vyuoni wanakwenda kutoa huduma katika jamii ya Watanzania na pia ya kimataifa, hivyo ni muhimu elimu inayotolewa ikazingatia ubora na viwango vinavyostahiki.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Novemba 23,2018) kwenye mahafali ya tisa ya chuo kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania Kampasi ya Chifu Mazengo, Dodoma yaliyofanyika kwenye ukumbi wa CCM.
Amesema Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, inatambua na kuthamini mchango wa Sekta Binafsi hususan wa vyuo vikuu binafsi kama Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania, katika maendeleo ya elimu ya juu.
“Serikali inatambua mchango wa vyuo hivyo katika kupanua fursa kwa Watanzania wengi kupata elimu ya juu, ambapo hadi sasa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu kwenye vyuo vikuu binafsi nchini ni takriban asilimia 25 ya wanafunzi wote.”
Amesema Serikali inatambua mchango wa chuo kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania katika kutayarisha watalaamu wa fani mbalimbali. Aidha, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007, chuo hicho kimetoa wahitimu zaidi ya 10,000.
Amesema kati ya wahitimu hao wapo Wafamasia, Wauguzi, Walimu wa Sayansi, Walimu wa Sanaa, Wataalamu wa Maabara, na Wasimamizi na Waendeshaji wa fani mbalimbali kama Utawala, Masoko na Wahasibu, mchango ambao unahitajika kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa uchumi wa Taifa katika nyanja tajwa.
Waziri Mkuu amesema baadhi ya wahitimu watapata ajira lakini si kila mhitimu atapata fursa ya kuajiriwa, hivyo Serikali itaendelea kuunga mkono azma yao kama chuo kikuu ya kutoa wahitimu wenye tabia, utashi na uwezo wa kutengeneza kazi na siyo watafuta kazi tu.
Akizungumzia kuhusuchangamoto zinazokabili sekta ya elimu ya juu, amesema baadhi ya changamoto zinafanana katika vyuo vikuu vyote nchini na pia zipo changamoto zinazokabili vyuo vikuu binafsi na wakati mwingine zipo changamoto zinazohusu chuo kikuu kimoja kimoja.
Amesema moja ya changamoto kubwa katika elimu ya Juu ni uhaba wa Wahadhiri wenye sifa stahiki ili kuendana na ongezeko la wanafunzi wanaojiunga na vyuo vyao. “Nafahamu jitihada ambazo vyuo vikuu binafsi vinafanya katika kuendeleza Rasilimali Watu wao na hasa katika eneo la taaluma ili viwe na Wahadhiri na Maprofesa wa kutosha.”
Hivyo, Waziri Mkuu ametoa wito vyuo vingine binafsi nchini viwekeze katika eneo la kuendeleza Rasilimali Watu kwa bidii zaidi na kwa upande wa Serikali, ipo mikakati mbali mbali ya kuajiri lakini pia kusomesha wale waliopo kazini ili kufikia viwango vinavyokubalika Kitaifa na Kimataifa.
Waziri Mkuu amesema changamoto nyingine inayovikabili vyuo vikuu ni miundombinu ya kufundishia na kujifunzia kama vile mabweni na nyumba za watumishi, hivyo kusababisha baadhi ya vyuo kushindwa kukidhi matakwa ya ithibati zao na kuzuiwa kufanya udahili au kufungiwa kabisa.
“Ni kweli tunahitaji Watanzania wengi wapate elimu ya juu kwenye vyuo vyetu vikuu. Hata ninyi wanafunzi, mngependa kupata elimu iliyo bora itakayoweza kuwasaidia maishani na itakayowakomboa kifikra, itakayowapa ujuzi na maarifa ya kupambana na changamoto za maendeleo. Kila mmoja anataka elimu bora na si bora elimu.”
Waziri Mkuu amesema kuwa dhamira hiyo ndiyo inayoifanya Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu kuhakikisha kuwa vyuo vyote visivyokidhi matakwa ya ithibati yao haviendelei kutoa mafunzo ya aina yoyote. “Nitoe rai kwa vyuo vikuu vyote vizingatie matakwa ya ithibati zao ili viweze kutoa elimu iliyo bora itakayokidhi matamanio ya Watanzania na ushindani wa soko la ndani na nje.”
Kuhusu Chuo Kikuu cha Mtakatifu Yohana cha Tanzania ambacho kimeomba kuruhusiwa kufanya udahili baada ya kufungiwa, Waziri Mkuu amemuagiza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako kujiridhisha iwapo chuo hicho kimekidhi vigezo kabla ya kukipa kibali cha kudahili wanafunzi wapya.
(mwisho)
WAZIRI MKUU AHUDHURIA MAHAFALI YA SAINT JOHN
| Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasili kwenye Mahafali ya Tisa ya Chuo Kikuu cha Saint John (SJUT) yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Novemba 23, 2018. |
| Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wahitimu, kwenye Mahafali ya Tisa ya Chuo Kikuu cha Saint John (SJUT) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Novemba 23, 2018. |
| Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wahitimu, kwenye Mahafali ya Tisa ya Chuo Kikuu cha Saint John (SJUT) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Novemba 23, 2018. |
| Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wahitimu, kwenye Mahafali ya Tisa ya Chuo Kikuu cha Saint John (SJUT) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma Novemba 23, 2018. |
Subscribe to:
Posts (Atom)
MITANDAO YA KIJAMII
Popular Posts
-
Na. OWM, Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 y...
-
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama...
-
Na. OWM, ARUSHA Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri...
-
Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara w...
-
TAMOBA wafanya wasilisho la mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama wa Bodaboda na BajajiKampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa ...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ambaye ndiye anayesimamia Kamati ina...
-
*Aagiza fedha zilizotengwa zikatumike katika kujengea hospitali Dodoma Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya sik...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipokea maelezo ya namna mashine zinavyochakata mifuko chakavu na ...
-
Katika kuhakikisha malengo ya kutatua masuala ya ajira na kazi, yanafikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Mhe. Samia Suluhu H...
-
Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akiuliza jambo kwa Kaimu Meneja wa Uwa...
Formulir Kontak
Contributors
Powered by Blogger.







