Thursday, December 6, 2018

WAZIRI MKUU AFUNGUA KIWANJA CHA TAIFA CHA MCHEZO WA BASEBALL


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua kiwanja kipya cha Taifa cha mchezo wa Baseball na kuzindua mashindano ya Taifa ya Baseball nchini.
Amewaagiza viongozi wa Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni na Ofisi ya Rais-TAMISEMI waone umuhimu wa kuuendeleza mchezo huo.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Desemba 6, 2018) alipofungua kiwanja cha Baseball katika shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam.
Amesema iwapo mchezo huo utaratibiwa vizuri na kuingizwa katika michezo  UMISETA na UMITASHUMTA utaleta tija kwa wanafunzi wanaoucheza nchini.
Waziri Mkuu amesema thamani ya uwanja huo ni takribani Dola za Kimarekani 80.234 ambazo zimetolewa kwa msaada kutoka Serikali ya Japani.
Amesema anaishukuru Serikali ya Japan na amefarijika kwa dhamira yao ya kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi CCM 2015-2020 hususan ibara ya 161.
Waziri Mkuu amesema ilani inaielekeza Serikali kujenga na kuimarisha miundombinu ya michezo nchini na kuifanya sekta ya michezo kutoa ajira hususan kwa vijana.
“Pia naishukuru Osaka Rotary Club ya nchini Japan kwa msaada wao wa dola za Kimarekani 12,856 kwa kufadhili mashindano hayo ya sita ya mchezo wa Baseball.”
Amesema jitihada hizo zitaufanya mchezo wa baseball kuwa ni mmoja wa mchezo huo kukua kwa kasi na unachezwa kuanzia ngazi za shule ya msingi na sekondari.
“Nina hakika baada ya hapo Tanzania itaweza kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa na kimaifaifa na hasa yale ya Olimpiki ya Tokyo Japan 2020.
Kadhalika, Waziri Mkuu ameagiza uwanja huo ulindwe na utunzwe ipasavyo ili utumike katika mashindano ya ndani na nje ili uwe sehemu ya kuitangaza nchi.
Awali, Balozi wa Japan nchini, Balozi Shinichi Goto alisema nchini Japan mchezo huo pia unasaidia katika kuwajenga vijana kukua kinidhamu na kujiamini.
Alisema anatarajia kwamba mashindano ya mchezo huo yatakuwa endelevu nchini na wachezaji watacheza vizuri kutokana na uwepo wa uwanja mzuri.
Balozi huyo alisema mchezo huo unafundishwa na walimu wa Kijapani katika mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar.


 (mwisho)
Read More

WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WAPIGWA MSASA JUU YA SHERIA YA USIMAMIZI WA MAAFA


Na. OWM, DODOMA.
Timu ya wataalamu wa Ofisi ya waziri Mkuu wanaohusika na shughuli za kuratibu usimamizi wa maafa nchini, pamoja na timu ya wataalamu wa uokoaji ya Mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa. Faustin Kamuzora wametoa elimu kwa wakuu wa mikoa na makatibu Tawala, juu ya menejimenti ya maafa nchini.
Akiongea wakati wa uwasilishaji mada za usimamizi wa maafa nchini kwenye mafunzo ya uongozi kwa viongozi hao yanayoendelea mjini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustin Kamuzora amewashauri viongozi hao kuizingatia sheria ya usimamizi wa maafa nchini ya mwaka 2015 inayozitaka kamati za maafa kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa kutafuta rasilimali za usimamizi wa maafa katika ngazi husika.
“Ningependa niwashauri tumieni kamati zenu katika mkoa na wilaya ambazo zitawasaidiia kujua rasilimali mlizo nazo na kujua utaalamu wa kutumia, hivyo mtaweza kujenga uwezo mkubwa wa kukabili maafa yanayowapata na hayatahitaji kufika ngazi ya kitaifa na kwa kuzingatia ngazi ya kitaifa tunategemea mfuko wa maafa ambao bajeti ni finyu hivyo jitahidini kutumia rasilimali zenu katika kujiandaa zaidi kuliko kusubiri kutumia rasilimali nyingi wakati wa kukabili“ Amesisitiza,  Kamuzora.
Awali akiongea katika Mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Timu ya Wataalamu wa uokoaji ya Dar es Salaam, Dkt. Christopher Mzava, alifafanua kuwa timu hiyo imeundwa mahususi na mkoa huo ili kuwezesha kamati ya maafa ya mkoa huo kufanya shughuli za usimamizi wa maafa  kwa weledi, tayari imefanikiwa kuzijumuisha asasi na taasisi zote za Serikali, zisizo za Kiserikali na za watu Binafsi zinazoshughulika na maafa katika Mkoa huo na kutengeneza Mpango mkakati wa kukabili maafa mkaoni humo.
Kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha  majukumu ya  kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika, pamoja na  Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji  wilaya au mkoa. Pia kutoa taarifa za tahadhari ndani ya eneo husika.
 
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akifafanua juu ya masuala ya menejimenti ya maafa wakati wa  majadiliano  ya mada ya Usimamizi wa maafa nchini kwa Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi  yanayoendelea mjini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akifuatilia majadiliano wakati wa  majadiliano  ya mada ya Usimamizi wa maafa nchini kwa Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi  yanayoendelea mjini Dodoma.

Baadhi ya Makatibu tawala wakifuatilia uwasilishaji wa mada ya Usimamizi wa maafa nchini, kwa Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi  yanayoendelea mjini Dodoma.

Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka akiwasilisha mada juu ya Dhana ya Maafa,  kwa Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi  yanayoendelea mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa Timu ya Uokoaji mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Christopher Mzava akiwasilisha jinsi Mkoa wa Dar es salaam ulivyoweza kutekeleza Sera ya maafa,  kwa Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wanaohudhuria mafunzo hayo  yanayoendelea mjini Dodoma.

 MWISHO.
Read More

Wednesday, December 5, 2018

SERIKALI IMETOA KIPAUMBELE MATUMIZI YA TEHAMA NCHINI-MAJALIWA



*Atoa onyo kwa wanaotumia vibaya mitando ya kijamii, asisitiza sheria ipo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imetoa kipaumbele kwenye matumizi ya TEHAMA ili kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa shughuli za Serikali za kila siku. 

Hivyo, amewataka wananchi kutumia vizuri teknolojia hiyo ya habari na mawasiliano kwenye shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma katika sekta mbalimbali kwa lengo la  kukuza uchumi na kuwapunguzia wananchi umaskini pamoja na kuongeza ajira.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Desemba 5, 2018) katika sherehe za utoaji tuzo za mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo ametumia fursa hiyo kuwaonya watu wote wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii nchini.

“Nawaonya watu wote wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii waache. Ni vema wakatumia mitandao hiyo kwa kuhamasishana mambo mema zikiwemo shughuli mbalimbali za maendeleo. Na kwa wataokiuka sheria ipo na inaendelea kufanya kazi.”

Amsema Serikali inaamini kuwa matumizi ya TEHAMA yataongeza ufanisi katika kuwahudumia ipasavyo wananchi, mfano katika sekta ya elimu mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi wengi kutoka katika shule tofauti kwa wakati mmoja. 

Waziri Mkuu ameongeza kuwa “Matumizi ya TEHAMA kwa kiasi kikubwa yatapunguza gharamaza za uendeshaji kwani yanaweza kufanikisha mawasiliano binafsi, warsha na maelekezo mbalimbali kuwafikia walengwa bila ya kusafiri nje ya vituo vyao vya kazi.”

Ametoa mfano Juni 2017 Rais Dkt. Magufuli alizindua mfumo wa ukusanyaji Mapato ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty) kwa njia ya kielektroniki na kudhihirisha kuwa, sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano ni muhimili muhimu wa maendeleo kwenye sekta zote, ikiwemo viwanda, utalii, ujenzi, elimu, afya, kilimo, uvuvi na ufugaji.

“Kwa kuzingatia hayo, mwezi Juni 2018 wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Serikali ilizindua mifumo tisa ya TEHAMA, ambayo inalenga kuimarisha utendaji wa Serikali hususan katika kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, ukusanyaji mapato na utoaji wa taarifa.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza mifumo ya TEHAMA ili kutekeleza kwa vitendo azmaya kuwapatia wananchi maendeleo hususani waishio maeneo ya vijijini huduma bora na kwa wakati.

Amesema kwa sasa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inauwezo wa kuona na kubaini makusanyo yanayoendelea kukusanywa katika halmashauri mbalimbali nchini na kiasi kinachoingizwa benki kwa kupitia TEHAMA.

Pia, Waziri Mkuu amsema Serikali imeendelea kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye taasisi zake ili kufanikisha azma ya kutumia Serikali mtandao, zoezi ambalo linakwenda sambamba na kuunganisha baadhi ya shule za msingi, shule za Sekondari, Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Polisi, Hospitali za Wilaya, Vyuo Vikuu na Vituo vya Posta.

Wakati huo huo,Waziri Mkuu ameipongeza kampuni ya HUAWEI kwa uzinduzi wa program yao ya Seed of the Futureambayo inalengo la kuwajengea uwezo wa TEHAMA wanafunzi mbalimbali nchini katika hatua za awali kabisa. 

Amesema iwapo TEHAMA itatumika vizuri itatoa fursa kwa watu wote kupata elimu, kuleta usawa katika elimu, kujenga mazingira na mbinu bora za ufundishaji na kujifunza, kuongeza weledi wa walimu, kuimarisha usimamizi wa masuala ya elimu, uongozi na utawala.  

Mashindano hayo ya TEHAMA ya HUAWEI yaliasisiwa mwaka 2015 na baadaye mwaka 2016 yakazinduliwa huko Afrika Kusini, ambapo hadi kufikia mwaka 2017 tayari wanafunzi wapatao 40,000 wameshiriki mashindano hayo. 

Kwa upande wa Tanzania, yamezinduliwa mwaka huu, ambapo wanafunzi 500 walishiriki na baadaye kubaki 50, ambapo  waliokabidhiwa tuzo ni saba na watatu kati yao na mkufunzi mmoja wamepata fursa ya kushiriki hatua inayofuata ya mashindano hayo nchini Afrika Kusini. 

Sherehe hizo zimehudhuliwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Balozi Wang Ke, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Wazri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Tanzania Frank Zhou na wawakilishi mbalimbali wa taasisi za Umoja wa Mataifa nchini.


(mwisho)
Read More

Tuesday, December 4, 2018

MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa wa Kodi na Forodha wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Leonard Mapunda   (kulia) na Helen Haule  ( wapili kulia) wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi  wa TIC, Geofrey Mwambe.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakati alipotembelea Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwenye viwanja vya  Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. Kushoto kwake ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa, Faustine Kamuzora na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa wa Kodi na Forodha wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Leonard Mapunda  (wapili kulia) na Helen Haule  (kulia) wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi  wa TIC, Geofrey Mwambe.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza, Afisa wa NEMC  katika Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Linda Mutafungwa wakati alipotembelea Kituo hicho, Desemba 4, 2018. Wapili kulia ni Mkurugenzi  wa TIC, Geofrey Mwambe.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Watendaji, kwenye Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na  Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Watendaji, kwenye Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018.

Read More

WAZIRI MKUU ATEMBELEA TIC AITAKA IMALIZE URASIMU


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekitaka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimalize urasimu ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Kadhalika, ameuagiza uongozi wa TIC uweke kipaumbele cha kwanza katika kulinda rasilimali za nchi na maliasili zake ikiwemo ardhi, mazao ya uvuvi, misitu, madini.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jioni (Jumanne, Desemba 4, 2018) alipozungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa TIC na Menejimenti, jijini Dar es Salaam.
“Katika kuvutia wawekezaji hasa wa nje ni lazima tuweke kipaumbe katika kulinda rasilimali zetu kama ardhi, madini fukwe ili zisiporwe kwa kisingizio cha uwekezaji.”
Amesema eneo hilo linahitaji umakini na uadilifu mkubwa, hivyo ni muhimu kwa kituo hicho kuhakikisha kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.
Amesema ili kupata matokeo mazuri ni lazima waimarishe mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote sambamba na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.
“Serikali imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025, TIC inatakiwa iongoze kwa kuvutia wawekezaji wengi wa ndani na nje ya nchi.” 
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa wawekezaji ambao TIC inatakiwa ivutie ni walio mahiri wenye nia thabiti ya kutufikisha huko na siyo wachuuzi au madalali.
Kadhalika,Waziri Mkuu amesema Serikali  ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inataka TIC iwe kioo cha nchi ambacho kitavutia wawekezaji. 
Amesema Serikali inataka TIC mpya ambayo itakuwa kimbilio la wawekezaji wengi wa ndani na nje, badala ya kuwa kikwazo na kusababisha wawekezaji wakija kukimbilia.
Hivyo, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa kituo hicho ubadilishe muundo wa kuwapokea wawekezaji, wawapokee vizuri na wawaeleze fursa za uwekezaji zilizopo.
“ Pia, TIC iweke mazingira rafiki ya kuwawezesha Watanzania wengi kumiliki uchumi kwa kuanzisha miradi mipya wao wenyewe au miradi ya ubia kati ya wawekezaji.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kila mtumishi wa umma ni lazima afanye kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu, uadilifu, weledi, uaminifu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
Waziri Mkuu amesema ni lazima wahakikishe vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma vinaepukwa na kila mtumishi.” Serikali haivumii watumishi wa aina hiyo.”
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe amemuomba Waziri Mkuu awasaidie kwa kuwapatia ofisi kwa kuwa eneo wanalofanyia kazi kwa sasa halitoshi.
Pia amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa rasilimali watu, sasa wanahitaji watumishi 31 wakiwemo mameneja 11.
Awali, Waziri Mkuu alitembelea eneo la kutolea huduma za pamoja zilizopo ndani ya Kituo hicho cha Uwekezaji Tanzania na kusema kwamba ameridhishwa na utendaji.


 (mwisho)
Read More

Friday, November 30, 2018

WAZIRI MKUU: TUTABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WOTE WA UMMA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha maslahi ya watumishi wote wa umma wakiwemo wa kada ya afya kupitia Bodi ya Mishahara na Motisha baada ya kukamilisha uhakiki wa taarifa za kiutumishi.

Amesema kukamilika kwa uhakiki huo wa taarifa za kiutumishi kwa watumishi wa umma kutaiwezesha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kupanga upya mishahara na motisha kwa watumishi.

Waziri Mkuu alitoa taarifa hiyo jana jioni (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na watumishi wa Kituo cha Afya cha Ushirombo wilayani Bukombe baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi mradi wa uboreshaji miundombinu wa kituo hicho uliogharimu sh. milioni 500.

Alisema Serikali inaendelea kushughulikia maslahi ya watumishi, hivyo aliwataka waendelee kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote. “Tunataka mwananchi akifika kwenye maeneo ya kutolea huduma apokelewe, asikilizwe na ahudumiwe.”

Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kujenga Zahanati katika kila kijiji kwa kuwa wilaya hiyo imebakisha vijiji 2 kati ya 52 kumalizia ujenzi huo.

Waziri Mkuu alisema kwa sasa wananchi wa Ushirombo hawana sababu ya kusafiri umbali mrefu hadi Geita mjini au wilayani Kahama kwa ajili ya kufuata huduma za afya kwa kuwa huduma zote zitakuwa zikipatikana kituoni hapo.

Alizitaja huduma ambazo zitakuwa zikipatikana kwenye Kituo cha Afya cha Ushirombo kuwa ni pamoja na za mama na mtoto, huduma za upasuaji wa aina zote mdogo na mkubwa, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Dionis Myinga alisema ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ushirombo ulianza Juni 22, mwaka huu na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.

Alisema lengo la mradi huo ni kukiwezesha Kituo cha Afya cha Ushirombo kutoa huduma bora za upasuaji wa dharura kwa akinamama wajawazito pindi wapatapo matatizo yatokanayo na uzazi. Majengo yote ya kipaumbele yamekamilika kwa asilimia 99.

“Mradi huu ambao tunaujenga kwa kutumia force account, pamoja na lengo la kutatua matatizo yatokanayo na uzazi kwa akinamama mradi huu utakapokamilika, Kituo cha Afya cha Ushirombo kitaweza kuhudumia watu wapatao 54,271.”

Mkurugenzi huyo alisema mradi wa ukarabati wa kituo hicho cha afya unakadiriwa kutumia sh. milioni 436.933 hadi utakapokamilika na sh. milioni 63.066 zilizosalia kwenye ukarabati huo zitatumika kujenga njia za kuunganisha wodi na kukarabati majengo ya zamani.

 (mwisho)
Read More

Thursday, November 29, 2018

WAZIRI MKUU ACHUKIZWA NA WANAFUNZI KUKATISHWA MASOMO


*Ni baada ya wanafunzi 72 wa kike kupewa ujauzito wilayani Nyang’hwale

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amechukizwa na vitendo vya watoto wa kike kukatisha masomo yao kwa kupata ujauzito wilayani Nyang’hwale ambapo jumla ya wanafunzi 72 wamepata ujauzo katika kipindi cha miaka mitatu cha kuanzia mwaka 2016 hadi 2018.

Kutokana na wilaya hiyo kuwa na idadi kubwa ya watoto wa kike wanaokatisha masomo kutokana na ujauzito, Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gwiyama kufanya operesheni katika kila kijiji na kubaini waliowapa wanafunzi ujauzito na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni (Jumatano, Novemba 28, 2018) alipozungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba,kijiji cha Kalumwa wilaya ya Nyang’hwale, akiwa katika ziara yake mkoani Geita.

“Jambo lingine litakalowawezesha kukabiliana na tatizo la ujauzito kwa wanafunzi wa kike ni kuanzisha miradi ya ujenzi wa mabweni ili watoto wa kike waweze kusoma bila ya kupata vishawishi vinavyosababisha wao kupata ujauzito.” 

Waziri Mkuu alisema Serikali haiwezi kuacha jambo hilo likiendelea, hivyo aliwataka wananchi washirikiane katika kuwalinda watoto wa kike na Serikali itawachukulia hatua watendaji wote ambao katika maeneo yao watoto wa kike watabainika kuwa na ujauzito.

 “Watoto wa kike lazima waheshimiwe waachwe wasome bila ya usumbufu na atakayekatisha masomo adhabu yake ni kali. Tukikukuta umesimama na binti katika kona isiyoeleweka tutakukamata. Ole wenumtakaobainika kuwapa ujauzito wanafunzi, adhabu yake ni miaka 30 jela.”

Waziri Mkuu pia, alitoa onyo kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto kike ambao bado ni wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto wao wa kiume kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.

Katika kuoneshwa kuchukizwa na jambo hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mwita Waitara ambaye anashughulikia elimu, amemueleza Waziri Mkuu kwamba Novemba 30, 2018 yeye arudi wilayani hapo kwa  ajili ya kuwashughulia wote wanaokatisha masomo wanafunzi kike. Ametoa namba ya simu ili wananchi waanze kumpa taarifa za wahusika.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu alisemaSerikali imedhamiria kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nishati hiyo nchini vitaunganishiwa katika awamu ya tatu ya Mradi wa Nishati Vijijini (REA).

“Rais wetu Dkt. John Magufuli anataka kuona nyumba ya kila Mtanzania inapata umeme tena kwa gharama nafuu na ametenga fedha nyingi zitakazotosheleza kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini. Gharama za kuunganishiwa umeme huo ni sh. 27,000 tu.”

Kuhusu suala la gharama za kulipia nguzo, Waziri Mkuu alisema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo pamoja na zile za fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

Awali, Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Nyamigogo ambapo alikagua miundombinu ya kiwanda hicho na kisha aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa kiwanda hicho, ambacho muwekezaji wake ni mzawa.
(mwisho)
Read More

MAAGIZO 5 YA WAZIRI MHAGAMA KWA KAMATI YA USIMAMIZI WA MENEJIMENTI YA MAAFA YA MKOA WA DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliye kuwa akimueleza juu ya ujenzi wa mfereji wa mto Ngo’mbe, wakati wa ziara yake  ya kukagua miundo mbinu ya kukabili maafa ya mafuriko mkoani Dar es Salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza, Bibi, Nuru Damson, mkazi wa Dar es Salaam, aliye kuwa akimueleza  jinsi ujenzi wa mfereji wa mto Ngo’mbe, ulivyowasaidia kutopata athari za maafa ya mafuriko wakati wa ziara yake  ya kukagua miundo mbinu ya kukabili maafa ya mafuriko mkoani Dar es Salaam. 
 NA MWANDISHI WETU:
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amefanya ziara ya siku moja mkoani Dar es salaam, lengo la ziara hiyo ni kukagua miundo mbinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko pamoja na kutaka kujua mikakati ya kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa mkoani humo ya kukabiliana na maafa hayo.

Katika ziara hiyo Waziri Mhagama emetembelea wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam hususan katika maeneo ambayo mkoa huo umeboresha miundo mbinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko. Maeneo hayo ni Jangwani, Mto Mbezi, Mto Ng’ombe, Mto Bungoni na mfereji wa Mtoni kwa Azizi Ally.

Pamoja na kuridhishwa na jitihada zilizofanywa na mkoa wa Dar es salaam za kuboresha miundombinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko, pia na mikakati ya kukabiliana na maafa hayo waliyomueleza, Waziri Mhagama ametoa maagizo 5 kwa kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa ya mkoa huo kuyatekeleza  ili menejimenti ya maafa ya mafuriko mkaoni Dares salaam iwe endelevu.

“Nimeridhishwa na juhudi zilizofanywa na serikali kuu chini ya uongozi wa Dkt.Joh Pombe Magufuli za kuboresha miundo mbinu ya kakabiliana na maafa ya mafuriko, na nimeona jinsi serikali ya ngazi ya mkoa na wilaya zote zinavyo jitahidi kujenga uwezo   wa kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa. Pamoja na jitihada hizo ninge penda kuishauri  na kuielekeza kamati na Mkuu wa mkoa ayasimamie maelekezo yangu.” Amesisitiza  Mhagama

Mhagama ameiagiza Kamati ya Usimamizi wa menejimenti ya maafa kusimamia suala la uharibifu wa mazingira hususani maeneo ya mito na mabondeni kwa mujibu wa sheria ya menejimenti ya maafa ya mwaka 2015. Aidha alifafanua kuwa Maafa mengi ya mafuriko mkoani humo yanatokana na uharibifu wa mazingira unaochangiwa na  ujenzi  katika maeneno yasiyo stahili kama kingo za mito na mabondeni hali ambayo huzuia maji kutiririka na kusababisha mafuriko.

Aidha Mhagama ameitaka kamati hiyo  kusimamia suala la usafi wa mitaro, mifereji na mito iliyopo  jijini  Dares salaam, ambayo hujaa maji wakati wa msimu wa mvua kutokana  na uchafu na takataka zilizotupwa katika mifereji na mitaro hiyo hali ambayo husababisha maji kushindwa kutirirka kuelekea baharini na hatimaye mitaro hiyo hujaa na kusababisha mafuriko.

Ameitaka kamati hiyo kuwasiliana na sekta nyingine zenye miundmbinu katika mitaro na mifereji inayojengwa na kuondoa miundo mbinu hiyo ili uboreshaji wa miundo mbinu hiyo kuwa wa ufanisi. Mhagama alibainisha kuwa Mkoa umefanya  juhudi nzuri za kujenga mitaro na mifereji lakini ndani ya  miundo mbinu hiyo  kuna miundombinu mingine kama vile mabomba ya  maji safi,  hivyo,  sekta nyingine husika hazina budi kushrikishwa na kuhakikisha miundo mbinu hiyo inatolewa ili kulifanya zoezi la kuboresha miundombinu ya maafa ya mafuriko linakuwa bora na ufanisi.

Kamati imetakiwa kuhakikisha miradi yote inayolenga kuboresha miundombinu ya kukabiliana na maafa ya mafuriko ndani ya mkoa wa Dar es salaam inashirikiana katika hatua ya kupanga utekelezaji wake. Mhagama amefafanua kuwa Mkoa una miradi mingi ya kuboresha miundo mbinu ya kukabiliana na maafa hivyo ni vyema miradi hiyo ikae pamoja ili kujua ni namna gani ya kutekeleza malengo yake hususani kujua miundo mbinu husika inawekwa wapi bila kuathiri utekelezaji wa mradi mwingine.

Mhe.Mhagama ameitaka kamati kuendelea kutoa elimu kwa umma juu ya sheria ya menejimenti ya maafa ya mwaka 2015. Amebainisha kuwa kila mmoja katika jamii analojukumu la kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na maafa, hivyo jamii ikiwa na elimu ya kutosha juu ya menejimenti ya maafa hususani ya mafuriko jamii haitapata athari kubwa za uharibifu wa mali na vifo vitokanavyo  na maafa ya mafuriko.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akioneshwa ujenzi wa miundombinu ya kukabili maafa ya mafuriko mkoani Dar es saaam na  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati wa ziara yake  ya kukagua miundo mbinu hiyo mkoani humo.

Read More

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA, MASUMBWE WILAYANI MBOGWE.

 Wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018.

Wananchi wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipoingia kwenye Kiwanja cha Shule ya Misngi ya Masumbwe wilayani Mbogwe kuhutubia Mkutano wa Hadhara, Novemba 29, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia Mkutano wa Hadhara kwenye Kiwanja cha Shule ya Msingi ya Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018. 

Read More

SERIKALI KUWANUFAISHA WACHIMBAJI WADOGO-MAJALIWA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imeweka mikakati mizuri kuhakikisha wananchi hususani wachimbaji wadogo wadogo wananufaika na uwepo wa rasilimali hiyo.

Hivyo, Waziri Mkuu amewashauri wachimbaji wadogo wadogo wajiunge katika vikundi ili Serikali iweze kuwapatia misaada mbalimbali ikiwemo mkopo ili waongeze mitaji.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi jengo la halmashauri ya Mbogwe.

Amewahamasisha wachimbaji hao watumie taasisi mbalimbali za kifedha na kukopa fedha na kununua mitambo ya uchimbaji na uchenjuaji kwa lengo la kujiongozea tija.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Geita kwa ziara ya kikazi, amesema wachimbaji wadogo wadogo waendelee kuwa na imani na Serikali yao, kwa kuwa imewapangia mambo mazuri.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kwamba Serikali imedhamilia kumaliza tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama.

Amesema katika kumaliza tatizo la maji Serikali imetoa zaidi ya sh. bilioni moja kwa ajili ya  uchimbaji visima virefu 11 na visima vifupi 43 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina mikakati ya kumaliza tatizo la maji nchini kupitia Kampeni ya Rais Dkt. John Magufuli ya kumtua mama ndoo kichwani.

Waziri Mkuu amesema kampeni hiyo inalenga kuhakikisha wananchi katika maeneo yote wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao ya makazi.

“Serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wote nchini wakiwemo na wa wilaya ya Mbogwe wanapata huduma ya maji safi na salama karibu na makazi yao.”

Kuhusua suala la wanafunzi kukatishwa masomo kwa kupata ujauzito wilayani Mbogwe, Waziri Mkuu ameitaka jamii kukemea vitendo hivyo. Wanafunzi 54 wamepata ujauzito.

Amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu wanafunzi 20 wa shule za msingi na 34 wa sekondari wameacha shule baada ya kupata ujauzito.

“Hali ni mbaya, Mbogwe inatia aibu kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto waliopewa ujauzito. Naagiza msiwaguse wanafunzi wa kike ni moto utawaunguza. Tukikukamata jela miaka 30.”

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Madini, Dotto Biteko amesema wilaya ya Mbogwe inafanya vizuri katika sekta ya madini, ambapo ina viwanda 27 vya kuchenjulia dhahabu.

Amesema katika kuhakikisha wachimbaji wadogo wadogo wanawezeshwa kufanya shughuli zao vizuri, Serikali imetenga eneo la hekta 547.64 kwa ajili ya kuwagawia wachimbaji hao.

Akizungumzia kuhusu leseni za uchimbaji mkoani Geita amesema kuna jumla ya leseni 971 za uchimbaji mdogo wa madini na kati yake zinazofanyakazi ni leseni 184 tu.

Waziri huyo amewataka wachimbaji wadogo wadogo waendelee na shughuli zao za uchimbaji kwenye maeneo yao waliyopangiwa na kwamba hakuna atakayewaondoa.

Awali, Waziri Mkuu alikagua na kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mbogwe katika kijiji cha Kasosobe. Ujenzi huo utagharimu sh. bilioni 4.3. Pia alikagua mradi wa uboreshaji miundombinu na kuzindua maabara ya Kituo cha Afya Masumbwe.
 (mwisho)
Read More

MAJALIWA AFUNGUA JENGO LA MAABARA LA KITUO CHA AFYA CHA MASUMBWE WILAYANI MBOGWE.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Ilembela wilayani Mbogwe akiwa katika ziara ya mkoa wa Geita, Novemba 29, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua jengo la Maabara ya Kituo cha Afya cha Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazazi waliolazwa kwenye Kituo cha Afya cha Masumbwe wilayani Mbogwe, Novemba 29, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Frola Samwel aliyelazwa katika Kituo cha Afya  cha Masumbwe wilayani Mbogwe akimuuguza mwanae  Mathias Paschal wakati alipofungua jengo la Maabara ya Kituo hicho, Novemba 19, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bibi Frola Samwel aliyelazwa katika Kituo cha Afya  cha Masumbwe wilayani Mbogwe akimuuguza mwanae  Mathias Paschal wakati alipofungua jengo la Maabara ya Kituo hicho, Novemba 19, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi, Robert Gabriel. 

Read More

WAZIRI MKUU: TUTABORESHA MASLAHI YA WATUMISHI WOTE WA UMMA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuboresha maslahi ya watumishi wote wa umma wakiwemo wa kada ya afya kupitia Bodi ya Mishahara na Motisha baada ya kukamilisha uhakiki wa taarifa za kiutumishi.

Amesema kukamilika kwa uhakiki huo wa taarifa za kiutumishi kwa watumishi wa umma kutaiwezesha Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kupanga upya mishahara na motisha kwa watumishi.

Waziri Mkuu alitoa taarifa hiyo jana jioni (Alhamisi, Novemba 29, 2018) alipozungumza na watumishi wa Kituo cha Afya cha Ushirombo wilayani Bukombe baada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi mradi wa uboreshaji miundombinu wa kituo hicho uliogharimu sh. milioni 500.

Alisema Serikali inaendelea kushughulikia maslahi ya watumishi, hivyo aliwataka waendelee kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi bila ya ubaguzi wa aina yoyote. “Tunataka mwananchi akifika kwenye maeneo ya kutolea huduma apokelewe, asikilizwe na ahudumiwe.”

Kadhalika, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Serikali la kujenga Zahanati katika kila kijiji kwa kuwa wilaya hiyo imebakisha vijiji 2 kati ya 52 kumalizia ujenzi huo.

Waziri Mkuu alisema kwa sasa wananchi wa Ushirombo hawana sababu ya kusafiri umbali mrefu hadi Geita mjini au wilayani Kahama kwa ajili ya kufuata huduma za afya kwa kuwa huduma zote zitakuwa zikipatikana kituoni hapo.

Alizitaja huduma ambazo zitakuwa zikipatikana kwenye Kituo cha Afya cha Ushirombo kuwa ni pamoja na za mama na mtoto, huduma za upasuaji wa aina zote mdogo na mkubwa, maabara, chumba cha kuhifadhia maiti.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Bukombe, Dionis Myinga alisema ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ushirombo ulianza Juni 22, mwaka huu na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.

Alisema lengo la mradi huo ni kukiwezesha Kituo cha Afya cha Ushirombo kutoa huduma bora za upasuaji wa dharura kwa akinamama wajawazito pindi wapatapo matatizo yatokanayo na uzazi. Majengo yote ya kipaumbele yamekamilika kwa asilimia 99.

“Mradi huu ambao tunaujenga kwa kutumia force account, pamoja na lengo la kutatua matatizo yatokanayo na uzazi kwa akinamama mradi huu utakapokamilika, Kituo cha Afya cha Ushirombo kitaweza kuhudumia watu wapatao 54,271.”

Mkurugenzi huyo alisema mradi wa ukarabati wa kituo hicho cha afya unakadiriwa kutumia sh. milioni 436.933 hadi utakapokamilika na sh. milioni 63.066 zilizosalia kwenye ukarabati huo zitatumika kujenga njia za kuunganisha wodi na kukarabati majengo ya zamani.

 (mwisho)
Read More

ZIARA YA MAJALIWA MKOANI GEITA


Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akikagua ukarabati wa Kituo cha Afya cha ushirombo wilayani Bukombe, Novemba 29, 2018. 
 Wanakwaya wa Ushirombo wakiimba wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia Mkutano wa hadhara kwenye Stendi ya Ushirombo, Novemba 29, 2018.


Bibi Mageni Simon akiwa mwenye furaha baada  ya kujifungua katika mazigira safi na salama ya  hospitali ya wilaya ya Geita ya Nzera iliyokaguliwa na kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Novemba 28, 2018.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   akiweka Jiwe la Msingi la Ukarabati wa Kituo cha Afya cha Ushirombo wilayani Bukombe, Novemba 29, 2018. Kulia ni Mbunge wa Bukombe na Naibu waziri wa Madini, Doto Biteko na wapili kushoto ni  Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel.

Read More