| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama marumru aina ya Twyford wakati alipotembelea kiwanda cha Keda kilichopo Chalinze mkoani Pwani Desemba 7, 2018. |
Home
All posts
Friday, December 7, 2018
MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA MARUMARU CHA KEDA KILICHOPO CHALINZE
MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGEZA JUISI YA MATUNDA CHA SAYONA WILAYANI BAGAMOYO
WAZIRI MHAGAMA AAGIZA HALMASHAURI KUSHIRIKISHA WATU WENYE ULEMAVU PROGRAMU YA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA
Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameagiza halmashauri zitakazojengwa vitalu nyumba kushirikisha vijana wenye ulemavu.
Waziri Mhagama ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma na Iringa kukagua maeneo yatayojengwa na kutoa mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba (Green House).
Akizungumza wakati wa ziara hiyo alisema kuwa katika halmashari zote 83 ambapo teknolojia ya kilimo cha kitalu nyumba itaanzishwa, idadi ya vijana 100 watakaopata mafunzo hayo ijumuishe na wenye ulemavu.
“Halmashauri zitengeneze mfumo madhubuti wa kuwashirikisha vijana wenye ulemavu katika mradi huu, kwani wanaouwezo wa kufanya kazi kama ilivyo vijana wengine na wakiwezeshwa wanaweza”, alisema Mhagama.
Pamoja na hayo, Mhagama amehimiza halmashauri hizo zisimamie vyema mradi huo kwa kuufanya unakuwa endelevu na kuwaunganisha vijana kwenye vyama vya akiba na mikopo ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kujiendeleza kiuchumi kupitia programu hiyo.
Aliongeza kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu imeshakamilisha maandalizi yote ikiwemo wataalamu watakao fundisha vijana kujenga kitalu nyumba, kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji, upandaji wa miche na kuwaelimisha mifumo mizuri ya kutafuta masoko.
Naye, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bw. Lucas Kambelenjo amemuhakakikishia Mhe. Waziri kusimamia ipasavyo mradi huo na kuahidi kutekeleza maagizo aliyoyatoa pamoja na kuwahamasisha vijana zaidi kushiriki katika kujifunza teknolojia hiyo mpya ya kilimo cha Kitalu Nyumba.
Waziri Mhagama alifanya ziara hiyo Mbinga Mji eneo la Mji Mwema, Nyasa na Mkoga, Iringa. Mradi huo unategemea kuanza kwenye Mikoa 12 ikiwemo ya Dodoma, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera, Manyara, Lindi, Shinyanga na Kilimanjaro.
![]() |
| Muonekano wa eneo moja wapo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba (Green House). |
Thursday, December 6, 2018
KATIBU MKUU KIONGOZI ATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA MJI WA SERIKALI IHUMWA DODOMA.
![]() |
| Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akimsikiliza Msanifu Majengo Moses Wadelanga wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Serikali Ihumwa Dodoma. |
MAJALIWA AFUNGUA KIWANJA KIPYA CHA TAIFA CHA BASEBALL JIJINI DAR
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kiwanja Kipya wa Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. |
WAZIRI MKUU AFUNGUA KIWANJA CHA TAIFA CHA MCHEZO WA BASEBALL
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefungua kiwanja kipya cha Taifa cha mchezo wa Baseball na kuzindua mashindano ya Taifa ya Baseball nchini.
Amewaagiza viongozi wa Wizara ya Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni na Ofisi ya Rais-TAMISEMI waone umuhimu wa kuuendeleza mchezo huo.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Desemba 6, 2018) alipofungua kiwanja cha Baseball katika shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam.
Amesema iwapo mchezo huo utaratibiwa vizuri na kuingizwa katika michezo UMISETA na UMITASHUMTA utaleta tija kwa wanafunzi wanaoucheza nchini.
Waziri Mkuu amesema thamani ya uwanja huo ni takribani Dola za Kimarekani 80.234 ambazo zimetolewa kwa msaada kutoka Serikali ya Japani.
Amesema anaishukuru Serikali ya Japan na amefarijika kwa dhamira yao ya kuunga mkono utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi CCM 2015-2020 hususan ibara ya 161.
Waziri Mkuu amesema ilani inaielekeza Serikali kujenga na kuimarisha miundombinu ya michezo nchini na kuifanya sekta ya michezo kutoa ajira hususan kwa vijana.
“Pia naishukuru Osaka Rotary Club ya nchini Japan kwa msaada wao wa dola za Kimarekani 12,856 kwa kufadhili mashindano hayo ya sita ya mchezo wa Baseball.”
Amesema jitihada hizo zitaufanya mchezo wa baseball kuwa ni mmoja wa mchezo huo kukua kwa kasi na unachezwa kuanzia ngazi za shule ya msingi na sekondari.
“Nina hakika baada ya hapo Tanzania itaweza kushiriki kwenye mashindano ya kitaifa na kimaifaifa na hasa yale ya Olimpiki ya Tokyo Japan 2020.
Kadhalika, Waziri Mkuu ameagiza uwanja huo ulindwe na utunzwe ipasavyo ili utumike katika mashindano ya ndani na nje ili uwe sehemu ya kuitangaza nchi.
Awali, Balozi wa Japan nchini, Balozi Shinichi Goto alisema nchini Japan mchezo huo pia unasaidia katika kuwajenga vijana kukua kinidhamu na kujiamini.
Alisema anatarajia kwamba mashindano ya mchezo huo yatakuwa endelevu nchini na wachezaji watacheza vizuri kutokana na uwepo wa uwanja mzuri.
Balozi huyo alisema mchezo huo unafundishwa na walimu wa Kijapani katika mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Zanzibar.
(mwisho)
WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA WAPIGWA MSASA JUU YA SHERIA YA USIMAMIZI WA MAAFA
Na. OWM, DODOMA.
Timu ya wataalamu wa Ofisi ya waziri Mkuu wanaohusika na shughuli za kuratibu usimamizi wa maafa nchini, pamoja na timu ya wataalamu wa uokoaji ya Mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Profesa. Faustin Kamuzora wametoa elimu kwa wakuu wa mikoa na makatibu Tawala, juu ya menejimenti ya maafa nchini.
Akiongea wakati wa uwasilishaji mada za usimamizi wa maafa nchini kwenye mafunzo ya uongozi kwa viongozi hao yanayoendelea mjini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Faustin Kamuzora amewashauri viongozi hao kuizingatia sheria ya usimamizi wa maafa nchini ya mwaka 2015 inayozitaka kamati za maafa kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa kutafuta rasilimali za usimamizi wa maafa katika ngazi husika.
“Ningependa niwashauri tumieni kamati zenu katika mkoa na wilaya ambazo zitawasaidiia kujua rasilimali mlizo nazo na kujua utaalamu wa kutumia, hivyo mtaweza kujenga uwezo mkubwa wa kukabili maafa yanayowapata na hayatahitaji kufika ngazi ya kitaifa na kwa kuzingatia ngazi ya kitaifa tunategemea mfuko wa maafa ambao bajeti ni finyu hivyo jitahidini kutumia rasilimali zenu katika kujiandaa zaidi kuliko kusubiri kutumia rasilimali nyingi wakati wa kukabili“ Amesisitiza, Kamuzora.
Awali akiongea katika Mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Timu ya Wataalamu wa uokoaji ya Dar es Salaam, Dkt. Christopher Mzava, alifafanua kuwa timu hiyo imeundwa mahususi na mkoa huo ili kuwezesha kamati ya maafa ya mkoa huo kufanya shughuli za usimamizi wa maafa kwa weledi, tayari imefanikiwa kuzijumuisha asasi na taasisi zote za Serikali, zisizo za Kiserikali na za watu Binafsi zinazoshughulika na maafa katika Mkoa huo na kutengeneza Mpango mkakati wa kukabili maafa mkaoni humo.
Kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha majukumu ya kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika, pamoja na Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji wilaya au mkoa. Pia kutoa taarifa za tahadhari ndani ya eneo husika.
| Baadhi ya Makatibu tawala wakifuatilia uwasilishaji wa mada ya Usimamizi wa maafa nchini, kwa Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi yanayoendelea mjini Dodoma. |
| Mratibu maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka akiwasilisha mada juu ya Dhana ya Maafa, kwa Wakuu wa mikoa na makatibu Tawala wanaohudhuria mafunzo ya Uongozi yanayoendelea mjini Dodoma. |
MWISHO.
Wednesday, December 5, 2018
SERIKALI IMETOA KIPAUMBELE MATUMIZI YA TEHAMA NCHINI-MAJALIWA
*Atoa onyo kwa wanaotumia vibaya mitando ya kijamii, asisitiza sheria ipo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imetoa kipaumbele kwenye matumizi ya TEHAMA ili kuongeza uwazi, uwajibikaji na ufanisi katika utendaji kazi wa shughuli za Serikali za kila siku.
Hivyo, amewataka wananchi kutumia vizuri teknolojia hiyo ya habari na mawasiliano kwenye shughuli za uzalishaji mali na utoaji huduma katika sekta mbalimbali kwa lengo la kukuza uchumi na kuwapunguzia wananchi umaskini pamoja na kuongeza ajira.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Desemba 5, 2018) katika sherehe za utoaji tuzo za mashindano ya TEHAMA ya HUAWEI yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo ametumia fursa hiyo kuwaonya watu wote wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii nchini.
“Nawaonya watu wote wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii waache. Ni vema wakatumia mitandao hiyo kwa kuhamasishana mambo mema zikiwemo shughuli mbalimbali za maendeleo. Na kwa wataokiuka sheria ipo na inaendelea kufanya kazi.”
Amsema Serikali inaamini kuwa matumizi ya TEHAMA yataongeza ufanisi katika kuwahudumia ipasavyo wananchi, mfano katika sekta ya elimu mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi wengi kutoka katika shule tofauti kwa wakati mmoja.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa “Matumizi ya TEHAMA kwa kiasi kikubwa yatapunguza gharamaza za uendeshaji kwani yanaweza kufanikisha mawasiliano binafsi, warsha na maelekezo mbalimbali kuwafikia walengwa bila ya kusafiri nje ya vituo vyao vya kazi.”
Ametoa mfano Juni 2017 Rais Dkt. Magufuli alizindua mfumo wa ukusanyaji Mapato ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na Ushuru wa Bidhaa (Excise Duty) kwa njia ya kielektroniki na kudhihirisha kuwa, sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano ni muhimili muhimu wa maendeleo kwenye sekta zote, ikiwemo viwanda, utalii, ujenzi, elimu, afya, kilimo, uvuvi na ufugaji.
“Kwa kuzingatia hayo, mwezi Juni 2018 wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Serikali ilizindua mifumo tisa ya TEHAMA, ambayo inalenga kuimarisha utendaji wa Serikali hususan katika kuwahudumia wananchi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, ukusanyaji mapato na utoaji wa taarifa.”
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika kutengeneza mifumo ya TEHAMA ili kutekeleza kwa vitendo azmaya kuwapatia wananchi maendeleo hususani waishio maeneo ya vijijini huduma bora na kwa wakati.
Amesema kwa sasa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) inauwezo wa kuona na kubaini makusanyo yanayoendelea kukusanywa katika halmashauri mbalimbali nchini na kiasi kinachoingizwa benki kwa kupitia TEHAMA.
Pia, Waziri Mkuu amsema Serikali imeendelea kuunganisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye taasisi zake ili kufanikisha azma ya kutumia Serikali mtandao, zoezi ambalo linakwenda sambamba na kuunganisha baadhi ya shule za msingi, shule za Sekondari, Ofisi za Wakuu wa Wilaya, Polisi, Hospitali za Wilaya, Vyuo Vikuu na Vituo vya Posta.
Wakati huo huo,Waziri Mkuu ameipongeza kampuni ya HUAWEI kwa uzinduzi wa program yao ya Seed of the Futureambayo inalengo la kuwajengea uwezo wa TEHAMA wanafunzi mbalimbali nchini katika hatua za awali kabisa.
Amesema iwapo TEHAMA itatumika vizuri itatoa fursa kwa watu wote kupata elimu, kuleta usawa katika elimu, kujenga mazingira na mbinu bora za ufundishaji na kujifunza, kuongeza weledi wa walimu, kuimarisha usimamizi wa masuala ya elimu, uongozi na utawala.
Mashindano hayo ya TEHAMA ya HUAWEI yaliasisiwa mwaka 2015 na baadaye mwaka 2016 yakazinduliwa huko Afrika Kusini, ambapo hadi kufikia mwaka 2017 tayari wanafunzi wapatao 40,000 wameshiriki mashindano hayo.
Kwa upande wa Tanzania, yamezinduliwa mwaka huu, ambapo wanafunzi 500 walishiriki na baadaye kubaki 50, ambapo waliokabidhiwa tuzo ni saba na watatu kati yao na mkufunzi mmoja wamepata fursa ya kushiriki hatua inayofuata ya mashindano hayo nchini Afrika Kusini.
Sherehe hizo zimehudhuliwa na Balozi wa China nchini Tanzania, Balozi Wang Ke, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Wazri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye, Mkurugenzi Mtendaji wa HUAWEI Tanzania Frank Zhou na wawakilishi mbalimbali wa taasisi za Umoja wa Mataifa nchini.
(mwisho)
Tuesday, December 4, 2018
MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA UWEKEZAJI TANZANIA
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Wajumbe wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wakati alipotembelea Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Watendaji, kwenye Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Watendaji, kwenye Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es salaam, Desemba 4, 2018. |
WAZIRI MKUU ATEMBELEA TIC AITAKA IMALIZE URASIMU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekitaka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimalize urasimu ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.
Kadhalika, ameuagiza uongozi wa TIC uweke kipaumbele cha kwanza katika kulinda rasilimali za nchi na maliasili zake ikiwemo ardhi, mazao ya uvuvi, misitu, madini.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo jioni (Jumanne, Desemba 4, 2018) alipozungumza na Bodi ya Wakurugenzi wa TIC na Menejimenti, jijini Dar es Salaam.
“Katika kuvutia wawekezaji hasa wa nje ni lazima tuweke kipaumbe katika kulinda rasilimali zetu kama ardhi, madini fukwe ili zisiporwe kwa kisingizio cha uwekezaji.”
Amesema eneo hilo linahitaji umakini na uadilifu mkubwa, hivyo ni muhimu kwa kituo hicho kuhakikisha kinatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia maslahi ya Taifa.
Amesema ili kupata matokeo mazuri ni lazima waimarishe mawasiliano na uratibu miongoni mwa wadau wote sambamba na kutekeleza vipaumbele vilivyoainishwa.
“Serikali imedhamiria kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025, TIC inatakiwa iongoze kwa kuvutia wawekezaji wengi wa ndani na nje ya nchi.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa wawekezaji ambao TIC inatakiwa ivutie ni walio mahiri wenye nia thabiti ya kutufikisha huko na siyo wachuuzi au madalali.
Kadhalika,Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli inataka TIC iwe kioo cha nchi ambacho kitavutia wawekezaji.
Amesema Serikali inataka TIC mpya ambayo itakuwa kimbilio la wawekezaji wengi wa ndani na nje, badala ya kuwa kikwazo na kusababisha wawekezaji wakija kukimbilia.
Hivyo, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa kituo hicho ubadilishe muundo wa kuwapokea wawekezaji, wawapokee vizuri na wawaeleze fursa za uwekezaji zilizopo.
“ Pia, TIC iweke mazingira rafiki ya kuwawezesha Watanzania wengi kumiliki uchumi kwa kuanzisha miradi mipya wao wenyewe au miradi ya ubia kati ya wawekezaji.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kila mtumishi wa umma ni lazima afanye kazi kwa bidii, maarifa na ubunifu, uadilifu, weledi, uaminifu na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu.
Waziri Mkuu amesema ni lazima wahakikishe vitendo vya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma vinaepukwa na kila mtumishi.” Serikali haivumii watumishi wa aina hiyo.”
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa TIC, Geofrey Mwambe amemuomba Waziri Mkuu awasaidie kwa kuwapatia ofisi kwa kuwa eneo wanalofanyia kazi kwa sasa halitoshi.
Pia amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa rasilimali watu, sasa wanahitaji watumishi 31 wakiwemo mameneja 11.
Awali, Waziri Mkuu alitembelea eneo la kutolea huduma za pamoja zilizopo ndani ya Kituo hicho cha Uwekezaji Tanzania na kusema kwamba ameridhishwa na utendaji.
(mwisho)
Subscribe to:
Posts (Atom)
MITANDAO YA KIJAMII
Popular Posts
-
Na. OWM, Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 y...
-
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama...
-
Na. OWM, ARUSHA Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri...
-
Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara w...
-
TAMOBA wafanya wasilisho la mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama wa Bodaboda na BajajiKampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa ...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ambaye ndiye anayesimamia Kamati ina...
-
*Aagiza fedha zilizotengwa zikatumike katika kujengea hospitali Dodoma Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya sik...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipokea maelezo ya namna mashine zinavyochakata mifuko chakavu na ...
-
Katika kuhakikisha malengo ya kutatua masuala ya ajira na kazi, yanafikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Mhe. Samia Suluhu H...
-
Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akiuliza jambo kwa Kaimu Meneja wa Uwa...
Formulir Kontak
Contributors
Powered by Blogger.


















