Monday, January 7, 2019

TUCTA YAWATAKA WANASIASA KUTOWATUMIA KUJIPATIA UMAARUFU

*Waziri Mkuu apokea maandamano ya wafanyakazi wakimpongeza Rais 

SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) limeyataka makundi ya wanasiasa kutowatumia wao kama njia ya kujitafutia umaarufu kwa kuzungumzia masuala yao na badala yake wawaachie viongozi wa vyama hivyo kwa sababu wanajitosheleza.

Pia shirikisho hilo limesema litaendelea kuiunga mkono na kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano pamoja na rais wake Dkt. John Magufuli na kwamba watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia masharti ya ajira zao.

Hayo yamesemwa leo (Jumatatu, Januari 7, 2019) na Katibu Mkuu wa TUCTA, Yahya Msigwa katika hotuba yake aliyoitoa kwa wafanyakazi baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kupokea maandamano ya amani ya vyama vya wafanyakazi.

Watumishi wa taasisi mbalimbali leo wameandamana jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Squarekwa lengo la kumpongeza Rais Dkt. Magufuli kwa uamuzi wake kufuta kikotoo kipya cha mafao ya wafanyakazi kilichopendekezwa katika kanuni za sheria ya Mifuko ya jamii.

Katibu huyo wa TUCTA amesema mara nyingine makundi ya wanasiasa yamekuwa yakisema maneno ambayo wao hawajayasema jambo ambalo limekuwa likiwachonganisha na wadau wao wakiwemo wanachama pamoja na Serikali.

”Wafanyakazi wanaona fahari kwa sababu Rais Dkt. Magufuli anasikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuzitatua kwa wakati. Aliposema atafufua Shirika la Ndege Tanzanzia amelifufua na sasa tuna ndege saba pamoja na ujenzi wa miradi mkubwa ya umeme, barabara ambayo yote inaenda kutengeneza ajira.”

Hata hivyo, ameiomba Serikali ifanye uchunguzi kwenye miradi inayotekelezwa na mifuko ya hifadhi ya jamii kwa sababu hawana uhakika kama miradi hiyo imerejesha fedha. Pia ameiomba Serikali iongeze mishahara kwa watumishi wa umma.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu amesema Serikali ipo tayari wakati wote kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kuboresha mishahara na maslahi yao. “Wito wa Serikali ni kuwa wafanyakazi watekeleze majukumu yao kwa uadilifu,weledi na kujituma ikiwa ndio chachu ya kufikia malengo na ustawi wa nchi yetu.”

Kuhusu suala la kupandisha mishahara, madaraja  na maslahi ya wafanyakazi kwa ujumla, Waziri Mkuu amesema  Rais Dkt. Magufuli alishalitolea maelekezo na kwamba Serikali inayafanyia kazi maelekezo yake, hivyo amewaomba wafanyakazi waendelee kuwa wavumilivu.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kulipa stahili za watumishi wa umma kwa wakati  na kulipa madeni hatua kwa hatua, ambapo kati ya Julai 2018 hadi Septemba 2018, Serikali imelipa sh. bilioni 184.9 za madai mbalimbali ya watumishi.

“Kati ya kiasi hicho Serikali imelipa shilingi bilioni 49 kwa ajili ya malimbikizo ya mishahara kwa watumishi 28,214 ambayo yanajumuisha shilingi bilioni 19.2 walizolipwa walimu 16,214. Hata hivyo Serikali inaendelea na utafiti wa tathmini ya kazi katika wizara na taasisi mbalimbali ili kupanga vizuri mishahara na motisha kwa watumishi wa umma.”

Read More

Sunday, January 6, 2019

SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA


NA.MWANDISHI WETU

Serikali kupitia Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imezipa Kandarasi ya thamani ya shilingi 2.9 bilioni kampuni tatu za vijana wa Kitanzania ili kutekeleza mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House).

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akizindua mafunzo hayo  Januari 05, 2019 yanayoendelea katika Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro.

Programu hiyo ambayo itatumia jumla ya shilingi 2.9bilioni katika utekelezaji wake ambapo kampuni zilizoshinda kandarasi hiyo ni Kampuni za vijana wazalendo wa kitanzania ambao ni wabobezi katika masuala ya kilimo ikiwemo kampuni na Royal Agriculture Ltd, Holly Agriculture  Group Ltd, na SUGECO.

Mafunzo haya yatafanyika katika Mikoa yote Tanzania Bara na kuhakikisha Halmashauri 84 zinafikiwa kwa awamu hii ya kwanza lengo likiwa ni  kuwajengea vijana ujuzi kupitia kilimo cha kisasa ambapo tayari kwa mwaka huu wa fedha imeanza mafunzo hayo  kwa kutumia teknolojia ya Kitalu Nyumba (greenhouse).

“Kwa kuanzia tutahakikisha kila Halmashauri tunatoa mafunzo kwa vijana 100 na kati yao vijana 20 watapatiwa mafunzo ya kujenga Vitalu Nyumba ili kwa wale watakaopenda kuendelea na kilimo hiki wasikose wataalamu wa kuwajengea Vitalu hivyo ”Alisisitiza Mavunde.

Aidha, Amewataka vijana kutumia fursa ya kilimo katika kujikwamua na changamoto za ajira na kuelezea umuhimu wa kilimo katika kuongeza pato la Taifa na kuchangia katika uchumi wa viwanda nchini.

“Wote tunatambua kwamba kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa letu kwani kwasasa kimeajiri takribani asilimia 65.7 ya nguvu kazi nchini na kinachangia asilimia 29.1 ya pato la taifa, pia sekta ya kilimo ndiyo chanzo kikuu cha chakula, ajira, na malighafi ya viwanda”Alisisitiza Mavunde.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SUGECO Bw.Revocatus Kimario alieleza kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanafikia kundi kubwa la vijana nchini na kushukuru mchango wa serikali katika programu za ukujazi ujuzi kwa vijana.

“Kipekee naishukuru Wizara hii kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za kuhakikisha inatoa mchango mkubwa kwa vijana na kusaidia kuwakwamua kiuchumi.”Alisema Kimario

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Ally Msaki aliwataka vijana kutumia fursa hiyo kwa kujiimarisha kupitia mafunzo hayo watakayoyapata ili kujikwamua na tatizo la ajira nchini.

“Tunataka vijana wawe mstari wa mbele katika kilimo cha kisasa ili kuendana na mazingira ya sasa na kujikwamua katika kundi la wasio na ajira nchini”.Alisistiza Msaki.
Read More

SERIKALI YAZIPA KANDARASI YA THAMANI YA 2.9BN KAMPUNI ZA VIJANA KUTEKELEZA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na watendaji wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine pamoja na viongozi walioshiriki katika warsha ya uzinduzi wa Mafunzo kwa wakufunzi ya kilimo cha Kitalu Nyumba (Green House) yanayoendelea kwa siku tano katika Chuo hicho mkoani Morogoro.kushoto kwake ni Naibu waziri wa ofisi hiyo, anayeshughulikia wenye ulemavu Mhe.Stella Ikupa
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde pamoja na Mhe.Stella Ikupa (Wenye Ulemavu) wakiangalia karatasi inayotumika kama  kifungashio cha unga unaotengenezwa kwa viazi lishe.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Royal Agri.Co.ltd Bw. Jonathan Sangau akitoa maelezo kwa Manaibu Waziri kuhusiana na vifaa vinavyotumika katika  kufungia vitalu nyumba

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akimwaga zege kwa ajili ya kutengeneza vitalu nyumba kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akiangalia mapapai yaliyolimwa kwa njia ya kisasa katika mashamba ya SUGECO katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine Morogoro.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akipewa maelezo na Mtaalamu wa masuala ya lishe (SUGECO) Jolenta Joseph kuhusu ukaushwaji wa viazi lishe wakati akikagua kaushio la jua (solar dryer).
Mkurugenzi wa Ajira Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Bw. Ally Msaki  akizungumza wakati wa uzinduzi huo.


Manaibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu wakiangalia kiazilishe katika moja ya banda la maonesho la vijana walioshiriki mafunzo ya Kilimo cha kisasa cha kitalu nyumba. Katikati ni Mhe.Stella Ikupa anayeshughulikia Wenye Ulemavu na Kushoto ni Mhe.Anthony Mavunde

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na mtaalamu wa masuala ya kilimo cha kisasa kwa  kutumia mabwawa ya samaki (Acquculte) alipotembelea kukagua mradi huo, wa kwanza kulia ni Naibu Waziri Ofisi hiyo Mhe Stella Ikupa


Read More

MAJALIWA AMJULIA HALI DKT SALIMIN


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary   wakisindikizwa na Waziri Mkuu, Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakati alipomjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu huyo, jijini Dar es salaam Januari 6, 2018. Watatu kushoto ni Mama Amen Salim.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisindikizwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim wakati  alipomjulia hali  Waziri Mkuu Mstaafu huyo, jijini Dar es salaam, Januari 6, 2018. 

Read More

Saturday, January 5, 2019

WAZIRI MKUU ANUSA UFISADI UKARABATI WA JENGO SONGEA


*Ni la wajawazito wanaosubiri kujifungua, limegharimu sh. milioni 129 

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amenusa harufu ya ufisadi katika mradi wa ukarabati wa jengo la mama na mtoto  katika Hospitali ya Rufaa  ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO) na amesema kwamba hajaridhishwa na kiasi ya sh. milioni 129 zilizotumika.

Hivyo, amemuagiza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile afuatilie suala hilo ili kumbaini mtu ambaye amehusika katika kupitisha zabuni ya ukarabati wa jengo hilo na kisha kumpelekea taarifa.

Waziri Mkuu amenusa harufu ya ufisadi katika mradi huo leo (Jumamosi, Januari 5, 2019) wakati alipotembelea hospitali hiyo na kukagua ukarabati wa jengo la akinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua (mama ngojea) ambalo umegharimu sh. milioni 129.

“Sijaridhishwa na gharama za ukarabati wa jengo hilo kutokana na kiasi kikubwa cha fedha kilichotumika kwani Serikali inajenga vituo vya afya vyenye jengo la maabara, jengo la kujifungulia, wodi ya mama na mtoto, chumba cha upasuaji, nyumba ya watumishi kwa gharama za sh. milioni 400 hadi 500 sasa inawezekajane jengo moja linalokarabatiwa ligharimu kiasi hicho.”

Waziri Mkuu amesema kila mtumishi wa umma lazima azingatie maadili ya kiutumishi na kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa na Serikali. Amesema Serikali imeagiza miradi ijengwe kwa kutumia force accountna kuhakikisha miradi inalingana na thamani ya fedha.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia kikamilifu utoaji wa huduma ya watoto waliochini ya miaka mitano zinazotolewa katika hospitali kwani baadhi ya wahudumu wa afya wamekuwa wakiwatoza gharama za dawa wakati wanatakiwa watibiwe bure.

Waziri Mkuu amesema hayo baada ya Kanisia Fusi ambaye amelazwa na mtoto wake katika hospitali hiyo kumueleza kwamba ameandikiwa dawa na kuambia akanunue wakati mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu anatakiwa atibiwe bure.

Pia baada ya Dkt. Ndungulile kuangalia cheti cha mtoto huyo alisema dawa aliyoandikiwa ipo hospitalini hapo jambo ambalo lilithibitishwa na Mganga Mfawidhi wa hopitali hiyo Dkt. Majura Magafu, hivyo Waziri Mkuu amemuagiza mganga huyo amtafute mtendaji aliyemuambia mama huyo akanunue.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amezindua mpango wa usambazaji wa x-ray za kidigitali ambazo zitazambazwa kwenye hospitali mbalimbali za rufaa za mikoa ili kuboresha utoaji wa huduma zinazotolewa kwa njia ya mionzi.

Waziri Mkuu amesema kwa kuanzia x-ray hizo zitasambazwa kwenye hospitali za rufani katika mikoa 11 na kisha baadae zitasambazwa kwenye hospitali zingine 20, lengo ni kuhakikisha hospitali zote za rufaa za mikoa zinakuwa na x-ray hizo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dkt. Ndungulile amesema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeendelea kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za nchini.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma za afya zinawafikia Watanzania wote karibu na maeneo yao ya makazi tena kwa gharama nafuu. ”Katika kufikia azma hii moja wapo ya kipaumbele ni kununua vifaa vya kisasa vinavyoendana na teknolojia iliyopo.”

Amesema kwa sasa wizara hiyo imenunua mashine 11 za x-ray za kidigitali zenye thamani ya zaidi ya shilingi 2,027,029,794.60 ambazo zimekusudiwa kupelekwa kwenye hospitali 11 zenye x-ray za zamani. Hospitali hizo ni Amana, Bukoba, Katavi, Morogoro, Njombe, Ruvuma, Simiyu, Singida na zingine tatu zitafungwa katika hospitali za wilaya za Chato, Magu na Nzega.  
Read More

MAJALIWA AZINDUA X- RAY YA KIDIGITALI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA RUVUMA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza taarifa ya Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Majura Magafu kuhusu ukarabati wa Jengo la Wakinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2019. Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile,  wapili kulia ni Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga na kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiongozwa na  Kaimu Mganga Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma, Majura Magafu (kulia) kukagua  ukarabati wa jengo la wakinamama wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya Rufaa ya  mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2019.   Wapili kulia ni Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulie na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mtoto, Patric Chenya  wakati alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa  wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2019. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile. 

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa  akizungumza na Bibi Kanisia Fusi anayemuuguza mwanae, Mushidi Ngonyani wakati alipotembelea wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipozindua  X-Ray ya kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma, Januari 5, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt, Faustine Ndugulile na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu Mashine ya Kidigitali aliyoizindua katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kutoka Mtalaam wa tiba ya mionzi (Medical Technologist), Lincleth Gingo kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5,2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wtoto, Dkt. Faustine Ndugulile.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu Mashine ya Kidigitali aliyoizindua katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kutoka Mtalaam wa tiba ya mionzi (Medical Technologist), Lincleth Gingo kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5,2019. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Wtoto, Dkt. Faustine Ndugulile.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua mashine ya X- Ray ya Kidigitali kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma mjini Songea, Januari 5, 2018.

Read More

Friday, January 4, 2019

MAJALIWA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI WA LUHEYELA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua tangi la maji wakati alipoweka jiwe la msingi la  Mradi wa Maji wa Luyehe katika kijiji cha Muungano Zomba kwenye jimbo la Peramiho wilayani Songea, Januari 3, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda juu tangi la Maji ili kujiridhisha kuhusu  ubora  wake wakati alipoweka jiwe la msingi la  Mradi wa Maji wa Luyehela katika kijiji cha Muungano Zomba kwenye jimbo la Peramiho wilayani Songea, Januari 3, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipanda juu tangi la Maji ili kujiridhisha kuhusu  ubora  wake wakati alipoweka jiwe la msingi la  Mradi wa Maji wa Luyehela katika kijiji cha Muungano Zomba kwenye jimbo la Peramiho wilayani Songea, Januari 3, 2019.


Read More

MAJALIWA AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA MBINGA - MBAMBA BAY

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimina na Mbunge wa Nyasa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga- Mbamba bay kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 66, Januari 4, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya CHICCO kutoka China inayojenga barabara ya Mbinga – Mbamba bay  kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa Kilomita 66 wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, Januari  4, 2019. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,  Christina Mndeme.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Askofu wa Jimbo la Mbinga, John Ndimbo wakati alipowasili kwenye kijiji cha Nyoni wilayani Mbinga kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 4, 2019. Kulia ni Sheikh wa wilaya ya Mbinga, Said Majid.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Ruvuma na wafanyakazi wa Kampuni ya Ujenzi ya CHICCO kutoka China inayojenga barabara ya Mbinga – Mbamba bay yenye urefu wa Kilomita 66 wakati alipokagua ujenzi wa barabara hiyo, Januari 4, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi  wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga – Mbamba bay kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Kilomita 66 unaofanywa na Kampuni  kutoka China ya CHICCO, Januari 5, 2019.



Read More

BARABARA YA MBINGA-MBAMBA BAY KUKAMILIKA 2021



*Waziri Mkuu akagua ujenzi, aridhishwa na kasi ya mkandarasi


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekagua mradi wa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Mbinga kwenda Mbamba bey yenye urefu wa kilomita 69 itakayogharimu sh. bilioni 129.3.

Amekagua barabara hiyo leo (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akielekea wilayani Mbinga akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi ya siku nne mkoani Ruvuma.

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo wa barabara inayojengwa na kampuni ya Chico ya nchini China, ambapo ameuagiza uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kusimamia vizuri mradi huo.

“Kazi hii inafanywa kwa uhogari mkubwa, naipongeza kampuni ya Chico kwa hatua waliyoifikia na ninaamini kwamba barabara hii inayotarajiwa kukamilika Januari 2021 itakamilika mapema zaidi.”

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amesema kukamilika kwa barabara hiyo kutachochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi na mkoa kwa ujumla kwani itarahisisha usafiri kwa watu pamoja na usafirishaji wa mizigo.

Amesema pia barabara hiyo itakuza sekta ya utalii na uvuvi katika mkoa wa Ruvuma kwa sababu itawezesha watalii na wafanyabiashara kufika kwa urahisi katika wilaya ya Nyasa ambako ni kuingo cha biashara kati ya nchi jirani na mikoa inayopitiwa na ziwa Nyasa.

Mkuu huyo wa mkoa ametumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuwapelekea fedha za ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya hospitali, vituo vya afya, shule, nishati na maji.

Read More

RAIS AMEDHAMIRIA KUFUNGUA MILANGO LA MAENDELEO NCHINI

*Ni ile iliyokuwa imejifunga kwa muda mrefu kwenye mikoa mbalimbali

RAIS Dkt. John Magufuli amedhamiria kufungua milango na fursa za maendeleo iliyokuwa imejifunga kwa muda mrefu kwenye mikoa mbalimbali nchini ukiwemo mkoa wa Ruvuma.

Hayo yamesemwa leo (Ijumaa, Januari 4, 2019) na Waziri MKuuKassim Majaliwa apozungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji Nyoni, Mbinga.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Ruvuma kwa ziara ya kikazi ya siku nne amesema Serikali itahakikisha milango ya maendeleo katika maeneo yote nchini inafunguka.

Amesema miongoni mwa miradi inayotekelezwa na Serikali ambayo inalenga kufungua milango na fursa ya maendeleo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Waziri Mkuu ametolea mfano wa barabara inayojengwa kutoka Mbinga hadi Mbamba bey kwamba itafungua fursa za kiuchumi kwa wananchi pamoja na Taifa kwa ujumla.

Kadhalika, Waziri Mkuu amezungumzia suala ya utendaji kwa watumishi wa umma, ambapo amewataka watekeleze majukumu yao ipasavyo na hayo ndio matakwa ya Serikali.

“Lazima watumishi wa umma wawajibike kwa kuwatumikia wananchi ipasavyo na wazingatie wajibu wao. Serikali haitawavumilia watumishi wazembe, wala rushwa.” 

Pia Waziri Mkuu amewasisitiza watumishi wa umma kwenda kwa wananchi kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi.

Amesema kitendo cha wananchi kuwasilisha malalamiko yao kupitia mabango kwenye mikutano ya viongozi kinaonesha kwamba watumishi hawaendi kwa wananchi.

“Watumishi wa Mbinga acheni kukaa ofisini na badala yake tengeni siku tatu kwa wiki na kwenda vijijini kwa ajili ya kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zinazowakabili.”

Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga, Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

Wengine ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri OR-TAMISEMI Joseph KandegeMkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na maafisa wengine wa Serikali.
Read More

MARUFUKU KUSAFIRISHA KAHAWA YA MAGANDA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema hakuna kahawa itakayoruhusiwa kuuzwa nje ya nchi kabla ya kukobolewa, kwa lengo la kuiongezea thamani kabla ya  kuingizwa sokoni.

Pia, Waziri Mkuu ameziagiza halmashauri zinazolima kahawa nchini kuwa na kitalu chenye miche zaidi ya laki mbili ifikapo mwisho wa mwezi wa pili mwaka huu.“Wakati utakapofika uongozi wa Wizara ya Kilimo utakwenda kukagua iwapo agizo hili limetekelezwa’’.

Aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akizungumza na wadau wa kahawa wa mkoa wa Ruvuma kwenye ukumbi wa Jimboni wilayani Mbinga.

Waziri Mkuu alisema kuanzia sasa kahawa yote itakayozalishwa nchini ni lazima iongezewe thamani na hakuna kahawa yenye maganda itakayoruhusiwa kuuzwa nje ya nchi.

“Hairuhusiwi kutoa kahawa nchini na kuiuza nje ya nchi ikiwa bado na maganda, ni lazima iongezewe thamani ndipo ipelekwe katika masoko ya nje ya nchi ili iuzwe kwa bei nzuri. 
Hatua hii itasaidia kuongeza mnyororo wa thamani na kusaidia kulinda uwekezaji wa viwanda uliofanyika nchini’’

Akizungumzia kuhusu madeni ya wakulima, aliagiza watendaji wote wa AMCOS waliohusika watafutwe na walipe deni. “Kwa sasa Serikali haina taratibu za kununua madeni ya chama chochote cha ushirika. Kuendelea na utaratibu huo kunachochea viongozi wa ushirika kufuja mali za ushirika. Lazima watambue ukifuja fedha za wanaushirika , Serikali iko na wewe.”

Alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli haitorudi nyuma katika msimamo wake wa kuwasimamia wakulima nchini ili nao waweze kunufaika na kazi kubwa wanazofanya.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaagiza viongozi wa AMCOS wahakikishe wakulima wote wanasajiliwa na taarifa zao ikiwemo ukubwa wa mashamba,kiasi cha uzalishaji na mahali walipo zinatunzwa vizuri katika kompyuta.

Pia, Waziri Mkuu alimuagiza Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Ruvuma akague AMCOS zote na kujiridhisha kama ziko hai na kwenye tatizo la uongozi aitishe uchaguzi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu alisema minada yote ya kahawa itafanyika kwenye maeneo yanayolima ambayo yamegawanywa kwa kanda 1.Moshi (Kilimanjaro,Arusha,Tanga,Manyara) 2. Kagera ( Kigoma, Geita, Kagera, Mara) 3. Songwe ( Rukwa,Mbeya,Iringa,Katavi), na Mkoa wa Ruvuma utafanyika Mbinga 

Alisema lengo ya kufanya minada hiyo katika maeneo yanayolima kahawa ni kuongeza uwazi katika biashara hiyo na kuwawezesha wakulima kujua bei ya mnada na kulipwa kwa wakati. Mkulima anaruhusiwa  kupeleka kahawa katika mnada wowote nchini ilimradi azingatie sheria na taratibu husika 

“Kila kanda inayolima kahawa nchini itakuwa na maeneo yake ya kuuzia kahawa na kahawa ya Mbinga itauzwa katika minada itakayofanyika Mbinga na bei kila mtu ataijua siku hiyo.”

Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kuimarisha kilimo cha zao la kahawa ili kila mmoja anayehusika na zao hilo akiwemo mkulima aweze kunufaika na kuongeza tija.
Kwa upande wao, wadau walifurahishwa na uamuzi wa Serikali wa kulisimamia zao kwa ukaribu na hasa baada ya kutangaza minada yote ya kahawa kufanyika katika maeneo yao na kwa uwazi.
Read More

MAJALIWA AZUNGUMZA NA WADAU WA ZAO LA KAHAWA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wadau wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, Januari 4, 2019.   Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wadau wa zao la kahawa kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, Januari 4, 2019. 
Baadhi ya wadau wa zao la kahawa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mbinga, Janujari 4, 2019. 



Read More

WAZIRI MKUU ACHUKIZWA NA TAARIFA YA KUZUIWA KWA NGUZO ZA UMEME


*Aitisha kikao na viongozi wa maeneo hayo pamoja na Mawaziri husika

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amemuita Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Happi pamoja na Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zote zinazozalisha nguzo za umeme katika mkoa huo kufika ofisini kwake ili waeleze sababu za kuzuia nguzo za hizo zisitoke. 

“Wanieleze kwa nini wanazuia nguzo,Wakati wananchi wanasubiri kuunganishiwa huduma ya nishati ya umeme wao wanazuia nguzo wanasubiri posho,  Wanaidai Serikali wakati ni  wao ni sehemu ya Serikali  Tutakutana ofisini kwangu Januari 7, saa tano kamili asubuhi.”

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Ijumaa, Januari 4, 2019) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji Nyoni,  wilayani Mbinga akiwa katika siku ya tatu za ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma. Alisema jambo hilo linakwamisha zoezi la usambazaji umeme.

Aliyasema hayo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi ambao walilalamikia kitendo cha kutofikishiwa huduma ya umeme katika maeneo yao kutokana na kukosekana kwa nguzo ambazo zimezuiwa kwa sababu ya wahusika wanaidai Serikali posho.

Waziri Mkuu alisema viongozi wengine watakaokuwepo kwenye kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, Waziri wa nchi OR-TAMISEMI, Selemani Jafo, 
Wenyeviti wa halmashauri hizo zilizozuia nguzo ili wamueleze sababu za kuzuia nguzo hizo.

Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli iAlisema Serikali imedhamiria kusambaza huduma ya nishati ya umeme katika vijiji vyote nchini vikiwemo na wananchi hao wataunganishiwa umeme huo kwa gharama ya sh. 27,000 tu.

Pia Serikali imeondoa gharama za kulipia nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali na kwa vijiji ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo linalenga kufungua fursa za ajira na kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa.

Serikali imefanya maamuzi hayo kwa sababu huduma hiyo ya umeme ni muhimu kwani mbali ya kutumika katika matumizi ya majumbani, pia kwa kusogezwa karibu na maeneo ya pembezoni itawezesha zahanati, shule ,viwanda na vituo vya afya kuwa na umeme.
Read More

Thursday, January 3, 2019

MAJALIWA AZINDUA KITUO CHA KUCHOTEA MAJI KATIKA KIJIJI CHA LUGAGALA SONGEA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsaidia kubeba  ndoo ya maji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, ikiwa ni ishara ya kuzindua   kituo cha kuchotea maji  katika kijiji cha  Lugagala wilayani Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kumsaidia  kubeba ndoo ya maji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, ikiwa ni ishara ya kuzindua   kituo cha kuchotea maji  katika kijiji cha  Lugagala wilayani Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme. 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kumsaidia  kubeba ndoo ya maji, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, ikiwa ni ishara ya kuzindua   kituo cha kuchotea maji  katika kijiji cha  Lugagala wilayani Songea, Januari 3, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Maji, Juma Aweso na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.
Read More

WAKURUGENZI FUATILIENI UTENDAJI WA WATUMISHI-MAJALIWA


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wafuatilie utendaji kazi wa watumishi kwenye maeneo kubaini kama wanakwenda kwa wananchi na kuwahudumia ipasavyo.

‘Serikali inahitaji kuona watumishi wa umma wanakwenda kwa wananchi  kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kushirikiana nao katika kuzipatia ufumbuzi’’.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Alhamisi, Januari 3, 2019) wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Lugagala, wilayani Songea akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma.

“Rais wetu Dkt John Magufuli ni muumini wa maadili na mchapakazi ,ndio maana amesisitiza umuhimu wa watumishi wa umma kwenda kuwahudumia wananchi katika maeneo yao, kwani baadhi yao hawana uwezo wa kufikia maeneo ya kutolea huduma.”

Waziri Mkuu aliongeza kuwa ni vema kwa watumishi wa umma wahakikishe wanapanga muda wa siku tatu kwa wiki kutoka maofini kwenda kuwahudumia wananchi hususani waishio maeneo ya pembezoni.

Alitumia fursa ya mkutano huo kuwataka wananchi waendelee kuiamini Serikali yao pamoja na watendaji wake waliopo kwenye maeneo mbalimbali nchini kwani Serikali inatambua matatizo yao na kuahidi kuwa yatapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa Serikali haina msamaha na watumishi wazembe, hivyo wananchi waendelee kuwa watulivu na imani kwani watahudumiwa na ahadi zote zilizotolewa na Rais Dkt Magufuli katika maeneo yao zitatekelezwa.

Kadhalika, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Songea asimamie zoezi la kuwaondoa wananchi wote wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo katika maeneo ya vyanzo vya maji kwa sababu watasababisha vyanzo hivyo vikauke.

Awali, Waziri Mkuu aliweka jiwe la msingi katika mradi wa maji wa Luyehela kwenye kijiji cha Muungano Zomba, kuzindua kituo cha kuchotea maji cha kijiji cha Lugagala na kukagua mradi wa ujenzi ya zahanati wa kijiji hicho.

Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Peramiho na Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga.

Wengine ni Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, Naibu Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na maafisa wengine wa Serikali.

Read More