Tuesday, November 26, 2019

WAZIRI MHAGAMA KUTANGAZA UTARATIBU MPYA WA KUNUNUA NYUMBA ZA MRADI BUYUNI



Na. OWM, DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama leo  tarehe 26 Novemba, 2019 anatarajia kutangaza utaratibu mpya wa kununua Nyumba  za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni,  Jijijni Dar es Salaam.

 Akiongea mara baada ya kumaliza kukagua  mradi huo wa nyumba  zinazomilikiwa na  Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), tarehe 25 Novemba 2019, Mhe. Mhagama amebainisha kuwa atatoa utaratibu huo mpya wa namna ya kununua nyumba hizo zilizo wazi ili wananchi waweze kunufaika kwa kupata makazi bora na salama.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), unaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, na umeanzishwa na Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2018, Jukumu kuu la mfuko huo ni kukusanya michango na kulipa mafao ya kustaafu kwa watumishi wa umma.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi , Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Andrew Massawe (Kulia) na kushoto kwake Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba, kukagua Nyumba  za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni,  Jijijni Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi , Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Andrew Massawe wakati alipokagua Nyumba  za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni,  Jijijni Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mkazi wa Buyuni, Benjamini Mvungi wakati alipokagua Nyumba  za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni,  Jijijni Dar es Salaam.

Muonekanao wa mojawapo ya nyumba Nyumba  za gharama nafuu 480 za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni,  Jijijni Dar es Salaam zinazonilikiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa wananchi waliofanikiwa kununua Nyumba  za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni,  Jijijni Dar es Salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa wananchi waliofanikiwa kununua Nyumba  za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni,  Jijijni Dar es Salaam wengine ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana ,Ajira na Watu wenye Ulemavu) Andrew Massawe na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Hosea Kashimba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na mmoja wa wananchi  waliofanikiwa kununua Nyumba  za gharama nafuu za Mradi wa Buyuni zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya Ilala, Chanika -Buyuni,  Jijijni Dar es Salaam.

Read More

Monday, November 25, 2019

WAZIRI MHAGAMA AKAGUA VITEGA UCHUMI VYA PSSSF JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba akifafaua jambo wakati wa ziara ya kukagua vitega uchumi vya Mfuko huo iliyofanya na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama  hayupo pichani, Novemba 25, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama(watatu kulia), akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana ,Ajira na watu wenye Ulemavu) Bw. Andrew Massawe (Wanne kulia), Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba (Wapili kulia) na maafisa wengine wa juu wa PSSSF, mwanzoni mwa ziara ya Waziri kutembelea vitegauchumi vya Mfuko huo jijini Dar es Salaam Novemba 25, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Andrew Massawe (Kazi, Vijana ,Ajira na watu wenye Ulemavu )  kulia, Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), wakati akikagua jengo la PSSSF Twin Towers lililopo katikati ya jiji la Dar es Salaam Novemba 25, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  (Kazi, Vijana ,Ajira na watu wenye Ulemavu )Bw. Andrew Massawe wakati alipofanya ziara ya kukagua jengo la PSSSF Twin Towers Novemba 25, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama(katikati), akiongozana na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Andrew Massawe (Kazi, Vijana ,Ajira na watu wenye Ulemavu ) kushoto, Mkurugenzi Mkuu, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hosea Kashimba, (kulia), wakitoka kwenye moja ya majengo ya vitegauchumi vya Mfujo huo jijini Dar es Salaam Novemba 25, 2019. Mhe. Jenista ameanza ziara ya siku mbili kukagua vitegauchumi vya Mfukjo huo hususan majengo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu  (Kazi, Vijana ,Ajira na watu wenye Ulemavu ) Bw. Andrew Massawe akifafaua jambo wakati wa ziara ya kukagua vitega uchumi vya Mfuko huo iliyofanywa na Waziri huyo  Novemba 25, 2019.

Read More

Sunday, November 24, 2019

KIJIJI KUHAMISHWA KUPISHA ATHARI ZA MAAFA YA MAFURIKO





Kamati ya menejimenti ya Maafa wilayani Korogwe imeelekezwa kutekeleza maazimio ya Mkutano Mkuu wa Kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge Wananchi wa kijiji hicho chenye kaya zaidi ya 250 ambazo ziliridhia kuhama kijiji hicho baada ya baadhi ya nyumba zao kuvunjwa na mawe makubwa yanayoporomoka na maji kutoka milimani  na mmomonyoko wa ardhi uliozingirwa na mifereji ya maji,  kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kwa takriban siku 40 mfululizo kijijini hapo.

Akiongea  mara baada ya kukagua shughuli za urejeshaji wa hali na kabla ya  kukabidhi misaada kutoka Mfuko wa Maafa unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shuhghuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe amesema katika menejimenti ya maafa  hatua za urejeshaji hali baada ya maafa  zinazingatia urejeshaji ulio bora zaidi kuliko wa awali hivyo  kwa kuwa kijiji hicho kipo eneo hatarishi wananchi hawanabudi kuishi eneo salama kwa afya zao na mali zao.


Kanali Matamwe ameeleza kuwa kwakuwa serikali imeamua kukihamisha kijiji hicho ili wananchi hao waweze kuishi maeneo salama na wameanza kuwasaidia wananchi hao kupitia Mfuko wa maafa unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu, amewataka wadau wengine kuendelea kuwasaidia wananchi hao ili waweze kukamilisha ujenzi wa nyumba bora na salama katika eneo litakalo ainishwa na serikali.

Ofisi ya Waziri Mkuu , Kupitia Mfuko wa Maafa  imeikabidhi  Kamati ya Menejienti ya Maafa  ya Wilaya hiyo misaada  kwa kaya zilizoathirika  na maafa ya  wa mafuriko Wilayani humo ikiwa ni pamoja na magodoro100, bati 200,mikeka 200,blangeti 200,ndoo 200, sleeping bag 100 vikiwa na thamani ya shilingi milioni kumi.

 Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe,Kissa Kasongwa aliishukuru ofisi ya Waziri Mkuu , Idara ya Uratibu wa maafa kwakuona umuhimu wa kuwasaidia waathirika wa mafuriko hayo Wilayani humo na kwamba mahitaji hayo yemewafikia walengwa kwa wakati muafaka.

 “Tumekuwa tukifanya jitihada mbalimbali za kurejesha hali na sasa tayari Kamati ya maafa ya wilaya tumeshaainisha eneo lenye ukubwa wa ekari 150 kwa ajili ya kuanzisha kijiji kipya, lakini nimefuatilia nimeona bado Halmashauri haijaenda kupima eneo hilo, nimemuelekeza mkurugenzi  jumatatu hii aende kwenye wnwo hilo nw upimaji uanze mara moja na zoezi hili likamilike ” alisistiza Kasongwa

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Timotheo Mzava alimshukuru Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, kazi, ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama ambaye ana dhamana ya kuratibu maafa nchini kwa kumsikiliza baada ya kuwasilisha matatizo ya wananchi wake na hatimaye kuwatuma wasaisdizi wake kwa ajili ya kushughulikia matatizo hayo ambapo maombi ya wananchi hao yametekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa.

Kwa nyakati tofauti wakazi wa kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge, Aliamini Mrutu na Asha Hizza wameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa misaada waliyowapatia na kubainisha kuwa wako tayari kuhamia katika kijiji kipya kitakacho anzishwa na serikali kwa kuwa wanapoishi sasa maisha yao yako hatarini kw akuwa tayari kaya 63 nyumba zao zimeathirika huku kaya 38 hazina mahala pa kuishi.

Kwa mujibu wa sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha  majukumu ya  kamati za usimamizi wa Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, jukumu la msingi ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika ngazi husika, pamoja na  Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji  wilaya au mkoa. Pia kutoa taarifa za tahadhari ndani ya eneo husika.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, akisisitiza umuhimu wa kijiji hicho kuhama katika eneo salama lilioainishwa na wilaya hiyo mara baada ya kupokea msaada vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Mfuko wa Maafa  kwa ajili ya  waathirika wa mafuriko kijijini hapo
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge Wilayani Korogwe wakifuatilia mkutano wa Mkuu wa wilaya hiyo Kissa Kasongwa  na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe hawapo pichani wakati walipopeleka misaada kwa waathirika wa maafa ya mafuriko kutoka  Ofisi ya waziri Mkuu, Mfuko wa maafa

Diwani wa Kata ya Kerenge, Shebila Idd akimuonesha  Mkuu wa wilaya  ya Korogwe  Kissa Kasongwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, maeneo yaliyoathirika  mafuriko katika kijiji cha Mapangoni kata ya Kerege.

Baadhi ya nyumba zilioathirika na mafuriko katika kijiji cha Mapangoni kata ya Kerenge wilayani Korogwe
Mkuu wa wilaya  ya Korogwe  Kissa Kasongwa akisisitiza umuhimu wa kijiji hicho kuhama katika eneo salama lilioainishwa na wilaya hiyo mara baada ya kupokea msaada vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Mfuko wa Maafa  kwa ajili ya  waathirika wa mafuriko kijijini hapo.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Mapangoni Kata ya Kerenge Wilayani Korogwe wakifuatilia mkutano wa Mkuu wa wilaya hiyo Kissa Kasongwa  na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe hawapo pichani wakati walipopeleka misaada kwa waathirika wa maafa ya mafuriko kutoka  Ofisi ya waziri Mkuu, Mfuko wa maafa

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akipokea  msaada kwa ajili ya waathirika wa maafa  mkoani humo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe,  msaada huo umetolewa na ofisi hiyo kupitia Mfuko wa maafa.
Gari la Jeshi la Wananchi likiwa limebeba misaada kwa ajili ya waathirika wa mafuriko wa kijiji ch aMapangoni kata ya Kerenge, misaada hiyo imetolewa na Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Mfuko wa Maafa  kwa ajili ya  waathirika wa mafuriko kijijini hapo
Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kisa Kasongwa akipokea  msaada kwa ajili ya waathirika wa maafa  wilayani humo kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe,  msaada huo umetolewa na ofisi hiyo kupitia Mfuko wa maafa
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Mapangoni kilichopo Kata ya Kerenge wakishirikiana na wanajeshi kushusha baadhi ya vitu vya msaada vilivyotolewa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Kupitia Mfuko wa Maafa  kwa ajili ya  waathirika wa mafuriko kijijini hapo.

Diwani wa Kata ya Kerenge, Shebila Idd akimuonesha  Mkuu wa wilaya  ya Korogwe  Kissa Kasongwa na Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, maeneo yaliyoathirika  mafuriko katika kijiji cha Mapangoni kata ya Kerege.
Mkuu wa wilaya  ya Korogwe  Kissa Kasongwa akimueleza Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe hatua walizochukua katika kurejesha hali ya daraja la Mandera lililokuwa limeathirika na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo,


Read More

SEKTA ISIYO RASMI KUONGEZEWA TIJA-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali zote mbili (Jamhuri ya Muugano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar) zinatambua mchango wa sekta isiyo rasmi, hivyo zimekuwa zikifanya juhudi mbalimbali kuendeleza na kuongeza tija katika sekta hiyo. 

Amesema katika kuhakikisha sekta hiyo inaendelea, Serikali imeendelea kuweka mazingira rafiki ya ufanyaji biashara kwa wajasiriamali wa Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuendelea kuwapatia vyeti vya uasili ambavyo vimetoa unafuu mkubwa wa kodi na tozo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Novemba 24, 2019)wakati akifunga Maonesho ya Wajasiriamali wa Tanzania kusherehekea miaka 20 ya uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyofanyika Fumba, Zanzibar.

Amesema wanapohitimisha maonesho hayo sambamba na kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanatakiwa wajitathmini kuona kama wametimiza malengo ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo. 

“Vilevile, tuendeleze ujirani mwema, kupanua na kuimarisha ushirikiano wa watu wa Afrika Mashariki ili kuharakisha ukuaji wa kiuchumi sanjari na kuboresha maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki kiuchumi, kisiasa na kijamii.”

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuzungumzia kuhusu vikwazo visivyo vya kiforodha vinavyozorotesha wajasiriamali kufanya biashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambapo amesema vimeendelea kutatuliwa kupitia majadiliano baina ya Tanzania na nyingine ndani ya Jumuiya hiyo kwa lengo la kuvipunguza na kuviondoa kabisa.

Waziri Mkuu amesema  kupitia majadiliano hayo, Serikali imefanikiwa kuratibu zoezi la uondoaji wa vikwazo vya biashara visivyo vya kiforodha 15kati ya 24vilivyoripotiwamwaka 2019 navikwazo tisa vilivyobakiahatua ya kuvipatia ufumbuzi inaendelea.

Hata hivyo,Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kutekeleza mkakati wa kutoa elimu kwa umma ili kuhakikisha wajasiriamali wanachangamkia fursa za kibiashara zitokanazo na Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Waziri Mkuu amesema mkakati huo unahusisha zoezi la kufanya utafiti wa uelewa wa Watanzania kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki na matokeo ya utafiti huo yatatumika katika kutoa elimu kwa umma kulingana na mahitaji.

Katika kutatua changamoto ya mitaji kwa wajasiriamali, Waziri Mkuu amesema Serikali inatekeleza maelekezo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/2020 ya kuweka mfumo wa kuvitambua, kuvisajili na kuviwezesha vikundi vyenye mwelekeo wa ushirika na ujasiriamali. 

Amesema miongoni mwa hatua zinazochukuliwa ni kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kwa taasisi za fedha na mifuko mbalimbali ya umma na binafsi kutoa mikopo kwa wajasiliamali kwa riba nafuu na ikiwezekana isiyo na riba.

“Katika kipindi cha Julai, 2018 hadi Juni, 2019 mikopo yenye thamani ya sh.   bilioni 42.06 kwa vikundi11,487 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ilitolewa. Vilevile, mikopo hiyo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri imeendelea kuzingatia uwiano wa asilimia nne kwa vikundi vya wanawake, asilimia nne kwa vijana na asilimia mbili kwa watu wenye ulemavu.” 

Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali inahamasisha uundwaji wa vikundi vya wajasiriamali, kusimamia utoaji wa elimu ya ujasiriamali kwa vikundi hivyo sambamba na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kuwezesha wajasiriamali na wawekezaji wengine kufanya shughuli zao bila bughudha.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeanzisha mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa lengo la kutoa mitaji na huduma nyingine za kifedha zenye masharti nafuu kwa wananchi wa Unguja na Pemba. Mfuko huu umelenga wananchi wenye kipato kidogo ili waweze kuzalisha mali kwa kujiajiri na kupunguza umaskini.
Amesema hadi kufikia Juni 2019 kupitia mfuko huo mikopo yenye thamani ya sh. bilioni 3.5 ilikuwa imetolewa na kuzifikia jumla ya Shehia 346. “Mfuko huu kupitia mradi wa mbogamboga na matunda umetoa mikopo 263 kwa wakulima wa mbogamboga na matunda 384 wa Pemba yenye thamani ya sh. milioni 60.6 na wakulima 384 wa Unguja yenye thamani ya sh. milioni 151.3.
Amesema Serikali imeendelea kufanya maonesho mbalimbali ya Wajasiriamali wa Sekta isiyo rasmi ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Maonesho hayo yametoa fursa kwa wajasiriamali kupata ujuzi, taarifa za masoko, teknolojia, mbinu na taratibu mbalimbali za kufanya biashara ili kukuza shughuli zao. 
Maonesho hayo yamewapatia wajasiriamali uthubutu wa kushiriki wao binafsi katika maonesho mengine kwenye nchi za Afrika Kusini, Malawi, Zambia, Sudan Kusini, Msumbiji na Marekani. Pia wameweza kufanya ziara katika nchi ya China ambako walijifunza na kununua mashine za kisasa kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa bidhaa zao ili ziweze kushindana katika soko la ndani na nje.


Read More

Friday, November 22, 2019

TANZANIA YA KWANZA KUTOA MAFUNZO YA KUTUMIA AFYA MOJA KUTATHIMINI HATARI YA VIMELEA HATARISHI VYA MAGONJWA



Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe akifafanua umuhimu wa Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja  kutoka ngazi za Halmashauri mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba , 2019.

Na. OWM, Arusha.

KWA mara ya kwanza Barani Afrika, Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kufanya mafunzo katika ngazi ya mkoa na Halmashauri kwa kutumia dhana ya Afya moja  kuwajengea uwezo wadau wa Afya moja juu ya namna ya  kufanya tathmini ya vimelea hatarishi vya magonjwa. Mafunzo hayo yamewakutanisha wadau wa Afya moja na wataalam kutoka sekta za afya ya binadamu, wanyama pori, mifugo, kilimo na mazingira. Wadau hao na wataalam kutoka sekta hizo za afya wamepata mafunzo ya namna ya kufanya tathmini hiyo kwa magonjwa ya Kichaa cha mbwa, Kimeta na Ugonjwa wa Brusela (Ugonjwa wa Kutupa mimba kwa wanyama).

Kufuatia nchi ya Tanzania kuwa imepiga hatua katika uratibu wa  masuala  ya Afya moja, ambayo ni dhana inayojumuisha sekta ya afya ya binadamu, wanyamapori, mifugo, kilimo na  mazingira katika kujiandaa, kufuatilia  na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu. Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO) imeratibu mafunzo hayo  yaliyotolewa na wakufunzi wa hapa nchini waliojengewa uwezo  na wataalamu kutoka Makao makuu ya  Shirika la Afya Duniani (WHO), Makao makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO), pamoja na Shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (OIE).

Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo tarehe 22 Novemba 2019,Jijini Arusha, Mkurugenzi wa Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, amebainisha kuwa ushirikiano wa wadau wa Afya moja na wataalam na sekta za Afya  kwa kutumia dhana ya Afya Moja hivi sasa ni agenda ya dunia nzima. Aidha amefafanua kuwa  dhana hiyo inapunguza gharama katika kushughulikia tishio la magonjwa  yanayotokana na vimelea vyenye uwezo wa kutoka kwa wanyama na kwenda kwa binadamu na hata mimea (mazingira) na kusababisha magonjwa na hata usugu wa vimelea vya magonjwa.

“Wadau wa afya moja wanawajibika kupanga mikakati mbalimbali ya udhibiti, ulinzi na usalama katika kuzuia, kujiandaa na kukabali magonjwa ambukizi. Moja ya mkakati ulioibuliwa Kitaifa na kimataifa ni kujiandaa kwa kuwafundisha  wataalam wa sekta mbalimbali za  afya jinsi ya kufanya tathmini ya  hatari ya vimelea vya magonjwa ambukizi kwa ushirikiano.” Amesema . Kanali Matamwe.

Kwa upande wake, Mwezeshaji wa Mafunzo hayo kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO), Tanzania, Bi. Niwael Mtui amefafanua kuwa Shirika hilo moja ya kipaumbele chake ni kupunguza umasikini na kuongeza kipato cha wananchi, hivyo Shirika hilo linashirikiana na serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, katika kujenga uwezo wa  ndani ya nchi kwa kuwafundisha wataalam wa sekta za Afya katika kudhibiti magonjwa ambapo uwezo huo utasaidia kuimarisha afya ya binadamu na mifugo na hatimaye kipato kitaongezeka na umasikini utapungua 

Wakiongea kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo  hayo wamebainisha kuwa  wamekuwa wakifanya tathmini za vimelela hatarishi vya magonjwa hapa nchini lakini tathmini hizo zimekuwa ni za kisekta kwani hazikuwa zinazingatia ushirikiano kwa maana ya dhana ya Afya moja. Aidha walifafanua kuwa mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kutumia Dhana ya Afya moja kwa kuwa inapunguza gharama katika kushughulikia tishio la magonjwa  yanayotokana na vimelea vyenye uwezo wa kutoka kwa wanyama na kwenda kwa binadamu na hata mimea (mazingira) na kusababisha magonjwa na hata usugu wa vimelea vya magonjwa. 


Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughuli za Afya moja nchini. Kwa kutambua umuhimu huo  Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Dawati la Uratibu wa Afya moja  kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO) na wadau waliandaa na kuratibu mafuzo hayo, ambapo wataalamu wa sekta za Afya na Wadau wa Afya moja kutoka Halmashauri nne za mkoa wa Arusha (Halmasahauri ya Arusha, Monduli, Ngorongoro na Karatu) walishirki mafunzo hayo.

MWISHO
Mwezeshaji wa   Kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Benezeth Lutege akifafanua namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja kutoka  ngazi za Halmashauri mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba , 2019.
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu na Mifugo pamoja na wadau wa Afya moja wakijadiliana namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja kutoka  ngazi za Halmashauri mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba , 2019.
Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO), Tanzania, Bi. Niwael Mtui akifafanua namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja kutoka  ngazi za Halmashauri mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba , 2019.
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu na Mifugo pamoja na wadau wa Afya moja wakijadiliana namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja kutoka  ngazi za Halmashauri mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba , 2019
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu na Mifugo pamoja na wadau wa Afya moja wakijadiliana namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja kutoka  ngazi za Halmashauri mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba , 2019
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu na Mifugo pamoja na wadau wa Afya moja wakijadiliana namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja kutoka  ngazi za Halmashauri mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba , 2019
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu na Mifugo pamoja na wadau wa Afya moja wakijadiliana namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja kutoka  ngazi za Halmashauri mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba , 2019.
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu na Mifugo pamoja na wadau wa Afya moja wakijadiliana namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakati  wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja kutoka  ngazi za Halmashauri mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba , 2019
Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya  kuwajengea uwezo  wa namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja  kwa wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja kutoka  ngazi za Halmashauri mkoani Arusha akiendelea na mafunzo hayo tarehe 22 Novemba , 2019.
Waratibu na Wawezeshaji wa mafunzo kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa  (FAO) wakijadiliana jambo wakati wa mafunzo ya  namna ya kufanya Tathmini  ya vimelea hatarishi vya magonjwa kwa kutumia Dhana ya Afya moja kwa  wataalamu wa sekta za afya na wadau wa Afya moja kutoka  ngazi za Halmashauri mkoani Arusha, tarehe 22 Novemba , 2019.


Read More