| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, leo Januari 14, 2020 ameondoka nchini kwenda Msumbiji, ambako atamwakilisha Rais John Pombe Magufuli, kwenye uapisho wa Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi. Kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Benjamin Mkapa, ambaye pia yupo katika msafara huo. |
Home
All posts
Tuesday, January 14, 2020
WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI, KWENYE UAPISHO WA RAIS WA MSUMBIJI, FILIPE NYUSI.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA YA WILAYA YA RUANGWA, MKOANI LINDI.
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiweka jiwe la msingi la Mahakama ya Wilaya Ruangwa, mkoani Lindi, kushoto Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa, Ibrahim Juma. Januari 13, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipeana mkono na Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa, Ibrahim Juma, baada ya kuweka jiwe la msingi la Mahakama ya Wilaya Ruangwa, iliyopo mkoani Lindi, Januari 13, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikata utepe, wakati alipozindua jengo la Mahakama ya Wilaya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua Jengo la Mahakama ya Wilaya Ruangwa, baada ya kuzindua rasmi jengo hilo, Januari 13, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua Jengo la Mahakama ya Wilaya Ruangwa, baada ya kuzindua rasmi jengo hilo, Januari 13, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya ruangwa, baada ya kuzindua Jengo la Mahakama ya Wilaya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwahutubia wananchi wa Wilaya ya ruangwa, baada ya kuzindua Jengo la Mahakama ya Wilaya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimwagilia mti, mara baada ya kuupanda, kwenye uzinduzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. |
MAHAKAMA KAMILISHENI UJENZI WA MIUNDOMBINU-MAJALIWA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa uongozi wa Mahakama nchini
uhakikishe unakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Mahakama ili
kuwapunguzia wananchi adha ya kutembea umbali mrefu na kutumia gharama
kubwa katika kutafuta haki zao.
Amesema
kuna wilaya 139 Tanzania Bara, kati ya wilaya hizo wilaya 111 zilizo na
huduma ya Mahakama za Wilaya na wilaya nyingine 28 bado zinahudumiwa na
Mahakama za Wilaya za jirani ambazo zimepewa mamlaka ya kisheria
kuhudumia Mahakama zisizo na majengo ya Wilaya.
Ametoa wito huo leo (Jumatatu, Januari 13, 2020) wakati akizindua jengo la Mahakama
ya wilaya ya Ruangwa. Amesema ni vema uongozi wa Mahakama uhakikishe
kuwa yale yote waliyojipangia kwenye mpango wao wa Miaka Mitano wa
Maendeleo ya Miundombinu ya Mahakama 2016/17 – 2020/21 unatekelezwa kwa
wakati.
Waziri
Mkuu amesema kabla ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Wilaya Ruangwa mwaka
2009, wananchi wa wilaya hiyo walilazimika kusafiri umbali wa kilomita
180 kufuata huduma za mahakama wilayani Lindi. Mahakama hiyo
itarahisisha upatikanaji wa haki wilayani Ruangwa.
“Umbali
huo mrefu ulisababisha wananchi wengi kupoteza muda mwingi ambao
wangeutumia kwa shughuli za uzalishaji mali. Wakati mwingine wananchi
hao walikosa haki zao kwa kushindwa kumudu gharama za usafiri kuhudhuria
mashauri yao wilayani Lindi.”
Waziri
Mkuu amesema Mahakama ni muhimu katika kudumisha amani na kuleta
maelewano ndani ya nchi au jamii ambayo huwa ni kichocheo cha shughuli
za kiuchumi, hivyo ameipongeza Mahakama ya Tanzania kwa kuamua kujenga
Mahakama hiyo Wilayani Ruangwa pamoja na sehemu nyingine nchini.
Amesema kupitia Mahakama, migogoro mingi hupata usuluhishi na hivyo kuimarisha hali ya amani na utulivu. “Kwa lugha nyingine,Mahakama
inapokuwa imara Taifa letu huvutia uwekezaji kwa kuwa wawekezaji
wanakuwa na uhakika na usalama wao pamoja na mali zao.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema Serikali kwa upande wake itaendelea kushirikiana na
Mahakama kuhakikisha kuwa mipango yake iliyojiwekea inatekelezwa kama
ilivyokusudiwa, kwani bado kuna kazi kubwa mbele yao.
Wakati hu huo, Waziri Mkuu ameipongeza Mahakama
ya Tanzania kwa kukusanya mapato kupitia mfumo wa Kielekitroniki wa
Ukusanyaji wa Maduhuli ya Serikali (Government electronic Payment
Gateway, GePG) kwani Serikali ilielekeza kila taasisi itumie mfumo huo
ili kupunguza mianya ya rushwa na upotevu wa fedha.
Amesema
amefurahi kusikia kuwa kwa kutumia mfumo wa GePG, Mahakama iliweza
kuongeza kiwango cha makusanyo kutoka sh. bilioni 1.6 mwaka 2017 hadi
sh. bilioni 2.5 mwezi Desemba 2019 baada ya kuanza kutumia GePG. “Fedha
hizi zitatumika kuchangia ujenzi wa mahakama na miundombinu mingine ya
kiuchumi unaoendelea katika kila kona nchini.”
“Ni
ukweli usiofichika kwamba hata wananchi nao wanafarijika kuona kuwa
kile mnachowatoza kinaenda moja kwa moja kwenye mfuko mkuu wa Serikali,
na baadaye kiasi fulani kinarudi kwenu kujenga miundombinu ya kisasa kwa
ajili ya kuwahudumia wananchi.”
Waziri
Mkuu amesema kuwa hayo ndiyo malengo na dhamira ya Serikali ya Awamu ya
Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli. “Aidha, kwa kufanya
hivyo, mnachangia utekelezaji wa malengo yaliyoainishwa vema kwenye
Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.”
Kwa upande wake,
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma amesema kwa muda mrefu,
Mahakama ya Tanzania imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba,
na uchakavu wa majengo katika ngazi zote za Mahakama, yaani Mahakama za
Mwanzo, Mahakama za Wilaya, Mahakama za Hakimu Mkazi (Mahakamaza Mikoa),
Mahakama Kuu na hata Mahakama ya Rufani.
Amesema
ili kukabiliana na ukubwa wa changamoto ya upungufu na uchakavu wa
majengo yake, Mahakama ya Tanzania ilitayarisha Mpango wa Miaka Mitano
wa Maendeleo ya Miundombinu (2016-2021). “Mpango huu umetathmini hali ya
majengo ya Mahakama katika Mikoa na Wilaya zote za Tanzania Bara.”
Jaji
Mku amesema mpango huo umelenga kupunguza au kuondoa kabisa uhaba na
uchakavu. Jengo jipya la Mahakama ya Wilaya ya Ruangwa ni kielelezo cha
utekelezaji wa Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Miundombinu ya
Mahakama ya Tanzania.
Pia,
Jaji Mkuu ametumia ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa watumishi wa
Mahakama, majengo kwamba hayo ya kisasa na miundombinu bora, iambatane
na upatikanaji wa huduma bora kwa mwananchi.
“Kila
mtumishi wa Mahakama (kama walivyo watumishi wote wa umma) anao Mkataba
na watumiaji wa huduma za Mahakama. Kipimo chetu cha kutimiza masharti
ya Mkataba huu, ni nguzo ya pili ya Mpango Mkakati wa Mahakama ambayo ni
‘Upatikanaji na Utoaji wa Haki kwa Wakati’, hivyo siku zote watumishi
wa Mahakama tukumbuke kuwa Mahakama hii ni mali ya wananchi na wananchi
wana haki ya msingi ya kupata huduma iliyo bora kwa wakati.”
Monday, January 13, 2020
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, AZINDUA JENGO LA TAASISI YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA RUSHWA (TAKUKURU) WILAYANI RUANGWA.
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikata utepe, wakati alipozindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipanda mti, baada ya kuzindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 13, 2020. |
TAKUKURU KAMILISHENI UCHUNGUZI MAPEMA-MAJALIWA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Taasisi ya Kuzua na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) ukamilishe mapema uchunguzi dhidi ya madudu
yaliyoibuliwa katika mbio za Mwenge wa Uhuru 2019 na wizi uliofanywa na
viongozi wa AMCOS kwa wakulima wa ufuta na korosho ikiwemo wilaya ya
Ruangwa.
Ameyasema
hayo leo wakati akizindua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) wilaya ya Ruangwa lililogharimu zaidi ya sh. milioni
142. Ametoa wito kwa TAKUKURU kuwa imara na kuweza kutembea kifua mbele
katika mapambano hayo.
Waziri
Mkuu amesema pamoja na TAKUKURU kuendelea na utekelezaji wa majukumu
yao ya kila siku pia ameuagiza uongozi wa taasisi hiyo ukamilishe mapema
utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli
aliyoyatoa kwao kwa nyakati tofauti.
Amesema
ameshuhudia kazi nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kuifanya kupitia
uchunguzi na ufuatiliaji wa madai ya malipo ya wakulima wa zao la ufuta
na korosho.“Kamilisheni chunguzi hizi zote kwa wakati ili hatua stahiki
za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya wale wote waliopatikana na
hatia.”
Amesema
rushwa huathiri utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Kutokana na ukweli huo, Serikali imetoa msukumo wa pekee katika
kushughulikia vitendo vya rushwa na ufisadi. Msukumo huo, umechangia kwa
kiasi kikubwa hususan katika kipindi hiki, utekelezaji wa miradi
mikubwa na ya kimkakati kwa ufanisi na kwa wakati.”
Amesema
wananchi wanatakiwa wafahamu kwamba kwamba nchi yoyote ambayo rushwa
imetamalaki siyo rahisi kuwa na uwezo wa kiuchumi utakaoiwezesha nchi
hiyo kumudu kulipa madeni ya ndani na ya nje. “Hata hivyo, kwa upande wa
Tanzania tunashuhudia jinsi Serikali ya awamu ya tano inavyolipa
madeni.”
Kwa
mfano, kati ya Julai na Septemba, 2019, sh. bilioni 85.72 zimetolewa
ikiwemo bilioni 50 za madai ya pensheni; bilioni 22 za madai ya
watumishi wa umma ikiwemo kiinua mgongo kwa wastaafu 3,019 na
malimbikizo ya mishahara kwa watumishi 1,435; bilioni 10.24 zimelipa
watoa huduma na zaidi ya bilioni 2 kwa ajili ya wakandarasi na wahandisi
washauri. Hayo ni matokeo ya jitihada za kupambana na rushwa
zinazofanywa na Serikali.
Amesema
tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imekuwa
ikijipambanua na vita dhidi ya rushwa na ufisadi. Hivyo, kitendo hicho
cha kuendelea kulipa madeni ni ishara ya mafanikio ya Serikali katika
jitihada zake za kuzuia na kupambana na rushwa nchini. Serikali
itaendelea kudhibiti mianya yote ya rushwa katika utendaji mzima wa
Serikali.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amesema tafiti za hivi karibuni zilizofanywa na
wadau wa mapambano dhidi ya rushwa na Utawala Bora kama vile
Transparency International (TI), MO Ibrahim na Afrobarometer zinaonesha
kuwa kwa miaka mitatu mfululizo, yaani 2016 hadi 2018 Tanzania
imeendelea kufanya vyema katika mapambano dhidi ya rushwa na utawala
bora.
Amesema
mafanikio hayo ya kujivunia ni jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano
inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kusimamia kwa dhati
mapambano dhidi ya rushwa kwa usimamizi wa Taasisi ya Kuzua na Kupambana
na Rushwa (TAKUKURU) ambayo ndicho chombo kilichopewa dhamana
kisheria.
“Tambueni
kwamba uongozi mzima wa juu kabisa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania (Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Makamu wa Rais na Mheshimiwa
Waziri Mkuu) uko pamoja nanyi katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi.
Pia
ameagiza kuanzishwa kwa vilabu vya kupambana na rushwa katika shule ili
wanafunzi waweze kuwa na uelewa na kuweza kutoa taarifa za rushwa.
Akizungumzia
kuhusu jengo alilolizindia amesema muhimu sana kwa taasisi nyeti kama
ya TAKUKURU kumiliki majengo yake yenyewe. Kuhusu hali ya majengo ya
ofisi za TAKUKURU katika ngazi ya mikoa na hata wilaya, amemwagiza Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Dkt Mary Mwanjelwa alishughulikie suala hilo.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Mbungo amesema jengo hilolimejengwa kwa muda wa miezi saba kuanzia tarehe 11/06/2018 na kukamilika tarehe 25/01/2019.“Hadi kufikia hatua hii ya uzinduzi, jengo hili limegharimu jumla ya Sh. 142,857,142.86.”
Akizungumzia kuhusu uchunguzi kiongozi huyo amesema kwa
kipindi cha mwaka 2019 TAKUKURU imefanya uchunguzi kwenye tuhuma kubwa
ikiwemo ya utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. Magufuli aliyoyatoa
Jumanne Oktoba 15, 2019 kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani
Ruangwa.
“Kupitia uchunguzi ule, tumebaini kwamba zaidi ya vyama 30 vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) vya Mkoani Lindiviliwadhulumu wakulima wa zao la ufuta kiasi cha zaidi ya sh.Bilioni sh. 1.23. Kupit ia uchunguzi huo tuliwakamata na kuwahoji zaidi ya viongozi 300 wa AMCOS zilizokuwa zinahusika katika dhuluma hii. Tulifanikiwa kuokoa zaidi ya sh.
bilioni 1.042. Fedha hizi zilikuwa ni mali ya wakulima wa ufuta ambao
walidhulumiwa fedha hiyo na Viongozi wa Vyama vya AMCOS.”
Kadhalika Brigedia Jenerali Mbungoamesema
pamoja na kufanikiwa kujenga majengo ya ofisi za TAKUKURU katika wilaya
saba bado inakabiliwa na uhaba wa majengo ya kudumu ya ofisi. Amesema
TAKUKURU ina jumla ya ofisi 28 za mikoa na ofisi 117 za wilaya huku
mahitaji halisi ni majengo 28 kwa ofisi za Mikoa na majengo 117 kwa
ofisi za wilaya.
Naye, Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Dkt Mary Mwanjelwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria
kuendeleza mapambazo dhidi ya rushwa, hivyo uzinduzi wa jengo hilo ni
miongozi mwa harakati hizo.
Thursday, January 9, 2020
WAZIRI MKUU AFUTA MNADA WA NAFAKA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefuta mnada wa nafaka ulioendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Januari 7, 2020 na kuuagiza uongozi wa mamlaka hiyo kutangaza upya zabuni baada ya kutoridhishwa na taratibu zilifanyika awali.
Mnada huo ambao unahusisha mahindi tani 5,000 na ngano tani 460.12 unafanyika baada ya wahusika kushindwa kutimiza masharti ya kiforodha, hivyo Serikali imeamua kuuza ili kufidia gharama zake. Nafaka hizo ziliingia nchini Machi 2017.
Waziri Mkuu amesitisha mnada huo leo (Alhamisi, Januari 9, 2020) wakati akizungumza na Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA, Bw. Ben Asubisye, ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu ameagiza kutangazwa upya kwa mnada mwingine wa kuuza mahindi hayo sambamba na ngano na wahakikishe masuala yote kuhusu mnada huo yanakamilika ndani ya siku tatu kuanzia leo tarehe 09 Januari 2020.
“Mahindi yameuzwa kwa bei ya sh. 340 kwa kilo moja ambayo ni chini na bei ya soko kwa sababu bei ya mahindi sokoni kwa sasa ni sh. 800. Zabuni imetangazwa kwa muda mfupi watu wameshindwa kushiriki. Ilifunguliwa saa 8 mchana na imefungwa saa 5 usiku.”
Kadhalika, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa TRA uhakikishe mnada unaofuata unakuwa wa wazi, huru pamoja na kutoa muda wa kutosha kwa wananchi wote kushiriki ili kuondoa malalamiko.
“Kwa kuwa mnada unafanyika kwa njia ya mtandao, hakikisheni matumizi ya mtandao yanakuwa rafiki kwa wananchi wote watakaovutiwa kuwasilisha zabuni zao.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesisitiza kuwa TRA ishirikiane na mamlaka nyingine za Serikali kuhakikisha wanunuzi wa nafaka hizo hawaziingizi sokoni kwa ajili ya matumizi ya binadamu. Nafaka hizo zimepimwa na kuthibitika kuwa zinafaa kwa matumizi ya wanyama.
Wednesday, January 8, 2020
WAZIRI MHAGAMA ARIDHISHWA NA HATUA ZA UJENZI WA JENGO LA NEC DODOMA
NA.MWANDISHI WETU
Read More
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametembelea na kukagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedenwa Jijini Dodoma na kusema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa.
Alikagua mradi huo, Januari 07, 2020 ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoyatoa Novemba 18, 2019 alipotembelea na kukagua mradi huo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na kutoa maagizo hayo baada ya TBA kusimamisha zoezi la ujenzi kwa ongezeko la gharama za kutoka bilioni 13 hadi bilioni 32 na hivyo kumtaka Waziri Mhagama kufuatilia.
Ziara ya Waziri Mhagama imebaini maendeleo mazuri ya ujenzi na kufikia hatua ya asilimia 75 baada ya Tume hiyo kuingia mkataba SUMA JKT kuwapongeza wakandarasi kwa hatua hiyo wanayoendelea nayo.
“Kwa kipindi chote ambacho SUMA JKT imeendeela na kazi ya ujenzi wa jengo hili hali inaridhisha na ni vyema kuhakikisha mnaendana na kasi inayotakiwa kwa kuzingatia gharama zilizokubalika za bilioni 16,”Alisistiza Waziri Mhagama
Alieleza kuwa ujenzi wa majengo ya Serikali ni moja ya hatua za kuhakikisha zoezi la kuhamisha watumishi Dodoma linafanikiwa kwa kuendelea kuweka miundombinu rafiki ya ofisi zao.
“Mpaka sasa tayari watumishi wapatao 14868 wameshahamia hapa Dodoma hivyo tutaendelea kuandaa mazingira ikiwemo ujenzi wa ofisi hizo kwa kuzingatia kazi ya Uratibu huo ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu,”alisema Mhagama
Alifafanua kuwa, kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kuhakikisha watumishi wa ofisi hiyo wanatoa huduma vizuri kwa kuzingatia mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi mkuu ambapo itasadia utendaji wa kazi.
Waziri Mhagama ameendelea kueleza kuwa , miongoni mwa majukumu ya Ofisi yake ni kuhakikisha inaratibu shughuli zote za kuhamisha watumishi wa Serikali na kuweka mazingira mazuri ya ofisi zao ili kuendelea kuitumikia nchi kwa weledi na kujiletea maendeleo yao kwa kutoa wa huduma bora zinazostahili.
Kwa upande wake mmoja wa wasimamizi wa ujenzi wa majengo hayo Mhandisi Michael Mussa alieleza kuwa, wataendelea kufanya kazi kwa viwango vinavyotakiwa ili kuwa na majengo yenye ubora kwa kuzingatia gharama zilizofikiwa kwenye mkataba wa ujenzi huo.
“Tumefarijika kwa ujio wa Mhe. Waziri na tunaahidi tutajenga kwa kipindi kilichopangwa kwa kuzingatia gharama zilizopo kwenye mkataba wa ujenzi huu,”alieleza Mhandisi Michael.
Muonekano wa sehemu ya jengo la Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.
|
Saturday, January 4, 2020
MRADI WA HOTELI NI MUHIMU KWA UTALII-MAJALIWA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema mradi wa ujenzi wa hoteli ya Golden Tulip
Airport Zanzibar ni muhimu katika kuimarisha sekta ya utalii na
huduma za malazi kwa wageni wanaotumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume.
Amesema
mradi huo unakwenda sambamba na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar za kuimarisha uwanja wake wa ndege ili kuongeza uwezo wake
katika kutoa huduma bora kwa abiria na wafanyakazi wa mashirika ya ndege
ya ndani na nje ya nchi.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumamosi, Januari 4, 2020), wakati akiweka
jiwe la msingi la ujenzi wa hoteli hiyo. Miongoni mwa watakaonufaika na
mradi huo ni pamoja na wasafiri wanaopita Zanzibar kwa ajili ya
kuunganisha ndege na baadaye kuendelea na safari.
Waziri
Mkuu ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport
Zanzibar inayojengwa katika eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Abeid Amani Karume ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 56 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yam waka 1964.
Ujenzi
wa hoteli hiyo unatarajiwa kugharimu Dola za Marekani milioni 8.5. sawa
na sh. bilioni 19.55. “Ama kwa hakika uwekezaji huu ni mkubwa na
naamini wawekezaji hawa wengeliamua kuwekeza katika nchi nyingine
yoyote, nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wangelipokelewa kwa
mikono miwili.”
“Hata
hivyo, mazingira mazuri ya uwekezaji hapa Zanzibar na uzalendo alionao
Mhe. Mohamed Raza, Mwenyekiti wa ‘Royal suites group of companies’
vilipelekea ushawishi mkubwa wa hoteli ya aina hii kujengwa hapa
Zanzibar.”
Waziri
Mkuu amesema kuwa “Nyote mtakubaliana nami kuwa viwanja vingi vya ndege
vilivyopo kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki, havina hoteli kubwa na
za kisasa zilizopo karibu na viwanja hivyo. Uamuzi wa kujenga mradi huu
ni sahihi, kwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla ni mahali salama na
wezeshi kwa biashara na uwekezaji.”
Amesema
kwa upande mwingine, Serikali zinaendelea kuimarisha amani na utulivu,
miundombinu wezeshi ya kiuchumi, huduma za fedha na mifumo ya kodi ili
kuvutia uwekezaji. “Mambo haya ni muhimu sana katika kuvutia wawekezaji
katika sekta mbalimbali kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.”
Hivyo,
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kutoa pongezi za dhati kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein
kwa juhudi wanazoendelea kuzifanya za kushajiisha uwekezaji.
“Tunawashukuru sana.”
Amesema
kwa upande wa Zanzibar, katika kipindi hiki cha miaka tisa ya Awamu ya
Saba, ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, jumla ya miradi ya uwekezaji
304 yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.74 imeidhinishwa na
mingine iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Utekelezwaji
wa miradi hiyo, umetoa mchango mkubwa katika kukuza ajira, teknolojia,
kuongeza mapato ya Serikali na kuimarisha ustawi wa Wananchi wetu.
“Hivyo, nawapongeza wawekezaji wetu wote waliowekeza na wanaoendelea
kuwekeza hapa nchini. Wawekezaji hawa wameonesha imani na upendo mkubwa
kwetu, nasi tunaahidi kufanya nao kazi kwa ushirikiano makubwa.”
Kwa upande wake,
Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi
Mohammed Ramia amesema mradi huo ni muhimu kwa kuwa utakapokamilika
utaenda kuongeza mapato ya Serikali.
Amesema
hoteli hiyo ni ya kwanza kwa Zanzibar kwa sababu mbali ya kuwa na
ukumbi wa watu mashuhuri (VIP Business Lounge) ambao wageni wake
watakuwa na uwezo wa kukamilisha taratibu za abiria wa ndege (check in)
na taratibu za uhamiaji moja kwa moja kutoka katika ukumbi huo.
Awali, Afisa Mtendaji Mkuu wa Royal
Group of Companies, Bw. Hassan Mohammed Raza alisema ujenzi wa hoteli
hiyo yenye vyumba 61, kumbi tatu za mikutano zenye uwezo uwezo wa
kuchukua watu 600 ina hadhi ya nyota nne, ulianza februari 2019 na
unatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu.
Alisema
nembo ya Golden Tulip ni sehemu moja ya kampuni ya pili kwa ukubwa
duniani kwa upande wa hoteli ukiwa chini ya mwavuli wa Louvre Hoteli
ambayo inamilikiwa na Shanghai Municipal Council. Mtandao huo una hoteli
zaidi ya 8,000 duniani, hivyo hoteli yao italazimika kufuata na
kutimiza vigezo bora vya hoteli katika sekta ya hoteli duniani.
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua Jengo la Hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar, baada ya kuweka jiwe la msingi la hoteli hiyo, Januari 4, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua Jengo la Hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar, baada ya kuweka jiwe la msingi la hoteli hiyo, Januari 4, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi wa Jengo la Hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar, Januari 4, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi mara baada ya kuweka jiwe la msingi wa Jengo la Hoteli ya Golden Tulip Airport Zanzibar, Januari 4, 2020. |
Thursday, January 2, 2020
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, AWAJULIA HALI WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA RUANGWA, MKOANI LINDI.
| Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, akimjulia hali Mzazi, Zena Issa, wakati altpotembelea Wodi ya Wazazi, katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 2, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya wakiwajulia hali wagonjwa, katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 2, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwa na Mkewe Mary, wakimsalimia Mzazi, Zulfa Juma, wakati wakiwajulia hali wagonjwa, katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 2, 2020. |
| Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwa na Mkewe Mary, wakimsalimia Mzazi, Zulfa Juma, wakati wakiwajulia hali wagonjwa, katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi, Januari 2, 2020. |
Subscribe to:
Posts (Atom)
MITANDAO YA KIJAMII
Popular Posts
-
Na. OWM, Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 y...
-
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama...
-
Na. OWM, ARUSHA Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri...
-
Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara w...
-
TAMOBA wafanya wasilisho la mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama wa Bodaboda na BajajiKampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa ...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, ambaye ndiye anayesimamia Kamati ina...
-
*Aagiza fedha zilizotengwa zikatumike katika kujengea hospitali Dodoma Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha maadhimisho ya sik...
-
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipokea maelezo ya namna mashine zinavyochakata mifuko chakavu na ...
-
Katika kuhakikisha malengo ya kutatua masuala ya ajira na kazi, yanafikiwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Mhe. Samia Suluhu H...
-
Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akiuliza jambo kwa Kaimu Meneja wa Uwa...
Formulir Kontak
Contributors
Powered by Blogger.
