Thursday, May 14, 2020

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA RELI YA KISASA (SGR)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Yapi Markezi, Ardem Arioglu, akiwa ndani ya treni inayotumia umeme, wakati alipokagua mradi wa reli ya kisasa ya SGR, May 14, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Masanja Kadogosandani ya treni inayotumia umeme, wakati alipokagua mradi  wa reli ya kisasa ya SGR, May 14, 2020. 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na baadhi ya Mawaziri na Viongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL)ndani ya treni inayotumia umeme, wakati alipokagua mradi  wa reli ya kisasa ya SGR, May 14, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na baadhi ya Mawaziri na Viongozi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL)ndani ya treni inayotumia umeme, wakati alipokagua mradi  wa reli ya kisasa ya SGR, May 14, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mandhari ya nje, wakati akiwa ndani ya treni inayotumia umeme, alipokagua mradi  wa reli ya kisasa ya SGR, May 14, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mandhari ya nje, wakati akiwa ndani ya treni inayotumia umeme, alipokagua mradi  wa reli ya kisasa ya SGR, May 14, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akishukandani ya treni inayotumia umeme, wakati alipokagua mradi  wa reli ya kisasa ya SGR, May 14, 2020.


Read More

Wednesday, May 13, 2020

SERIKALI YAUNGWA MKONO MAPAMBANO JANGA LA CORONA NA KAMPUNI YA EVERWELL CABLE AND ENGINEERING CO. LTD


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye  Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Sh. 100,000,000/= kutoka kwa kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020. 

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza kwenye makabidhiano ya hundi ya Sh. 100,000,000/= , ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwawa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza baada ya kupokea hundi ya Sh. 100,000,000/=, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020. 



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (Kushoto)  pamoja na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge),  Tixon Nzunda  (Kulia), wakati wa  kupokea hundi ya Sh. 100,000,000/=, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 13, 2020.

Read More

KAMPUNI YA EVERWELL CABLE AND ENGINEERING CO. LTD YACHANGIA SH. MILIONI 100 KUKABILIANA NA CORONA

             
                                                                                         

KAMPUNI YA EVERWELL CABLE AND ENGINEERING CO. LTD YACHANGIA
 SH. MILIONI 100 KUKABILIANA NA CORONA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb), amepokea msaada wa hundi yenye thamani ya sh. milioni 100 iliyotolewa na kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, inayojishughulisha na uzalishaji wa nyaya za kusafirisha umeme kwenye miradi mbalimbali ya umeme hapa nchini, kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID- 19).

Waziri amepokea mchango huo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 13 Mei, 2020 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa, Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa kupokea mchango huo Waziri Mhagama ameipongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha inapambana na janga la ugonjwa wa COVID-19.

“Kwa niaba ya serikali nawashukuru sana kwa kuwa sehemu ya watanzania katika kipindi hiki cha mapambano ya janga la COVID-19. Tunawashukuru sana kwa kuendelea kuwa sehemu ya shida na raha za Taifa hili,” ameeleza Waziri Mhagama.

Aidha, Waziri Mhagama amewahakikishia watanzania kuwa michango hiyo inasimamiwa vyema na serikali kwa kuitumia michango hiyo katika kushughulikia majukumu yaliyopangwa ya kupambana na janga la ugonjwa wa COVID-19.

Awali, Waziri wa Nishati Dkt. Medadi Kalemani ameipongeza kampuni hiyo kwa mchango wao kwa Serikali  kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

“Kampuni hii ni moja ya wawekezaji waliojenga Kiwanda hapa nchini, lakini  pamoja na shughuli za uwekezaji wameguswa katika kipindi hiki wakati serikali inapambana na janga  hili la ugonjwa wa COVID-19, tunawashukuru sana kwa mchango wenu kwa watanzania ”amesema Dkt. Kalemani.  

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Everwell Cable and Engineering Co. Ltd, Bw. Jiaopeng Lu ameeleza kuwa Kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na watanzania katika uzalishaji wa bidhaa za kiwanda  kabla ya Janga hili la Ugonjwa wa COVID-19, hivyo hawana budi kuhakikisha  watanzania wanakuwa salama ili waendelee kushirikiana nao katika shughuli za uzalishaji
Read More

MAJALIWA: NIMERIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA OFISI YA NEC

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) linalojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya Suma JKT katika eneo la Njedengwa, jijini Dodoma.

Novemba 18, 2019, Waziri Mkuu alitembelea mradi huo na kuonesha kutoridhishwa na utendaji kazi wa mkandarasi aliyekuwa akijenga jengo hilo ambaye ni Wakala Majengo Tanzania (TBA) na kuagiza kuvunjwa kwa mkataba.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Mei 13, 2020) wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la NEC. Amesema amefurahishwa na hatua iliyofikiwa na anaamini litakamilika kwa wakati.

“…Ninahakika mkiongeza nguvu katika baadhi ya maeneo tutafika na haya ndio Serikali inataka kuona taasisi zake zikifanya. Kwenye jengo hili ndipo Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuchukua fomu.”

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuipongeza Kampuni ya Ujenzi ya Suma JKT kwa namna walivyoratibu vizuri ujenzi wa jengo hilo. “Miradi mingi waliyokabidhiwa Suma JKT imekuwa ikijengwa kwa weledi mkubwa.”

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Wenyeulemavu, Jenista Mhagama amesema Kampuni ya Ujenzi ya Suma JKT ilikabidhiwa mradi wa ukamilishaji wa jengo hilo Desemba 24, 2019 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, 2020.

Amesema mradi huo unaosimamiwa na Chuo Kikuu Ardhi (ARU) kama mshauri wa mradi hadi leo (Mei  13, 2020) ujenzi wa jengo kuu la ofisi umefikia asilimia 85, jengo la kutangazia matokeo ujenzi wake umefikia asilimia 68, kazi za nje zimefikia asilimia 85 huku jengo la ghala limefikia asilimia 92.

Naye, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera amesema mkataba wa mradi huo ulipaswa ukamilike Aprili 30, 2020 lakini baada ya kutembelea eneo la mradi wamekubaliana kuwa kazi hiyo iwe imekamilika ifikapo Mei 30, 2020 na Juni 1, 2020 watumishi wahamie na kuanza kazi.

Amesema mradi huo unagharimu zaidi ya sh. bilioni 12 na tayari zaidi ya sh bilioni sita zimeshatolewa na kwamba kazi zinazoendelea kwa upande wa jengo kuu la ofisi ni pamoja na kupachika milango na madirisha, kupaka rangi na kuweka vigae kwenye sakafu.

Read More

WAZIRI MKUU AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA TUME YA UCHAGUZI (NEC), LILILOPO NDEJENGWA, JIJINI DODOMA.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwasili kwenye Jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), Njedengwa, jijini Dodoma, wakati alipoenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo, linalojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT, May 13, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), Njedengwa, jijini Dodoma, May 13, 2020.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Msimamizi na Meneja Mradi, Godwin Maro, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), iliyopo Njedengwa, jijini Dodoma, May 13, 2020.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye  Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Tume ya Uchaguzi (NEC), lililopo Njedengwa, jijini Dodomalinalojengwa na Kampuni ya Ujenzi ya SUMA JKT, May 13, 2020.

Read More

Wednesday, May 6, 2020

SH. MILIONI 150 KUKABILIANA NA CORONA ZACHANGWA NA WADAU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye  Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Sh. 50,000,000/= kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya kuzalisha nguzo ya Qwihaya General Enterpises Co. Limited, Leonard Mahenda,  ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mai 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Sh. 50,000,000/= kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya kuzalisha nguzo ya POLES (T) Limited, Salim Bisher Huwel,  ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipokea hundi ya Sh. 50,000,000/= kutoka kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya kuzalisha nguzo ya Mufindi Woodpoles Plant and Timber Limited, Salim Ahmed Abeid, ikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza baada ya kupokea hundi tatu zenye thamani ya Sh. 150,000,000/=, zikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akizungumza baada ya kupokea hundi tatu zenye thamani ya Sh. 150,000,000/=, zikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza kwenye makabidhiano ya hundi tatu zenye thamani ya Sh. 150,000,000/= , zikiwa ni mchango kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za mapambano dhidi ya ugonjwawa homa kali ya mapafu- COVID - 19. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma, Mei 4, 2020. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).




Read More

WADAU WACHANGIA SH. MILIONI 150 KUKABILIANA NA CORONA



WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amepokea msaada wa hundi tatu zenye thamani ya sh. milioni 150 zilizotolewa na kampuni tatu zinazozalisha nguzo za umeme nchini kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID- 19).

Waziri amepokea michango hiyo kwa niaba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa leo tarehe 4 Mei, 2020 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Mlimwa, Jijini Dodoma. Michango hiyo imetolewa na kampuni Mufindi Woodpoles Plant and Timber Ltd, Qwihaya General Enterprises Co Ltd na Poles (T) Ltd ambapo kila kampuni imetoa sh. milioni 50.

Akizungumza wakati wa kupokea michango hiyo Waziri Mhagama aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha inapambana na janga la ugonjwa wa COVID-19.

“Nawashukuru sana kwa niaba ya Serikali na hii inaonesha uzalendo, utayari na kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa ni sehemu ya mapambano hayo kwa vitendo,”alieleza Waziri Mhagama.

Pia, Waziri Mhagama alitumia fursa hiyo kuwasihi wakandarasi wengine pamoja na Watanzania kuendelea kushirikiana na Serikali kwa kujitolea kwa hali na mali ili kuwezesha katika kukabiliana na janga hilo.

“Tunatoa wito kwa Watanzania wote kuona umuhimu na kuguswa na janga hili kwa kuchangia kwa kadiri inavyofaa ili kuendeleza uzalendo kwa hali ya kujali na kuonesha utayari ili kudumisha hali ya utamaduni uliopo tangu awali wa umoja na mshikamano ,”alisema Waziri Mhagama.

Aliwahakikishia wadau hao kuwa, michango hiyo itatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kuwaeleza kuwa imefika katika eneo salama.

Awali, Waziri wa Nishati Dkt. Medadi Kalemani aliwapongeza viongozi wa kampuni hizo kwa michanga waliyoitoa kwa Serikali ambayo inakwenda kuongeza nguvu katika kukabiliana na ugonjwa wa COVID-19.

“Niwapongeze wakandarasi hawa kwa kuonesha nia ya kushiriki katika mapambano haya na wito wangu kila anayeguswa na janga hili ni faraja kubwa mnayoitoa kwa Serikalini katika kuhudumia na kusaidia katika kipindi hiki. Pia nawaomba wakandarasi wengine waige, ”alisema Dkt. Kalemani.  


Read More

Wednesday, April 22, 2020

MAOMBI YA PAMOJA KUHUSU KUKABILIANA NA CORONA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Alex Malasusa wa KKKT Jimbo la Mashariki na Pwani (kushoto), Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi (wa pili kushoto), Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zubeir (wa tatu kushoto) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (wa nne kushoto) katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Alex Malasusa wa KKKT Jimbo la Mashariki na Pwani (kushoto), Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi (wa pili kushoto), Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakari Zubeir (wa tatu kushoto) na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (wa nne kushoto) katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. 

 Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020.  
 Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. 


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika  maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. Kushoto ni Askofu  Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi na kulia ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir.

Viongozi wa dini wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza katika maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika  maombi ya pamoja kuhusu kukabiliana na tishio la ugonjwa wa homa kali ya mapafu – COVID – 19 kwenye viwanja vya ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam, Aprili 22, 2020. Kushoto ni Askofu  Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu la Dar es salaam, Yuda Thaddeo Ruwaichi na kulia ni Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir. 

Read More

Tuesday, April 21, 2020

WAZIRI MKUU AONGOZA MAOMBI YA KITAIFA KUKABILIANA NA VIRUSI VYA CORONA

*Idadi ya wagonjwa yafikia 284, ataka tahadhari zaidi iongezwe
*Aomba viongozi wa dini wahakikishe mikusanyiko ibadani inapungua
*Akemea wanaopandisha bei za vyakula hasa sukari

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hadi kufikia jana (Aprili 21, 2020) jumla ya wagonjwa 284 wamethibitika kuwa na virusi vya ugonjwa wa corona (Covid-19) ambapo wagonjwa 256 wanaendelea vizuri, saba wako kwenye uangalizi maalum, 11 wamepona na 10 wamefariki.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Aprili 22, 2020) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa dini walioshiriki maombezi ya Kitaifa dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) yaliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Amesema jumla ya watu 2,815 waliokuwa karibu na wagonjwa wamefuatiliwa afya zao ambapo kati yao, watu 1,733 walikutwa hawana maambukizi na watu 12 walikutwa na virusi hivyo (wapo kwenye orodha ya watu 284).

“Shirika la Afya Duniani lilikadiria kuwa ifikapo mwishoni wa Aprili, 2020 nchi yetu ingekuwa na wagonjwa 524,716 lakini tunamshukuru Mungu kwa kuwa kadirio hilo hatujalifikia.”

Kuhusu hali ya maambukizi ilivyo nchini, Waziri Mkuu amesema Jiji la Dar es Saalam na kisiwa cha Zanzibar, yanaongoza kwa maambukizi na akataka tahadhari zaidi zichukuliwe. “Jiji la Dar es Salaam ndio lina maambukizi makubwa hivyo nawasihi wananchi kama huna jambo lolote la kufanya huna sababu ya kuzurura na kwa wafanyabiashara siyo lazima mje Kariakoo, unaweza kufanyia biashara katika eneo lako,” amesisitiza.

“Ni wakati kila mmoja kuendelea kuchukua tahadhari vya kutosha ili kuepuka maambukizi. Epuka misongamano isiyokuwa ya lazima, huna sababu ya kumuamini yeyote, ona kuwa kila mmoja ana ugonjwa.”

Kipekee, Waziri Mkuu amewaomba viongozi wa dini waendelee kuchukua hatua madhubuti za kujikinga na ugonjwa huo kwa kuwaelimisha waumini wachukue tahadhari zote muhimu. “Ninawaomba viongozi wa dini wachukue tahadhari zaidi kwa kuhakikisha mikusanyiko kwenye nyumba za ibada inapungua ikiwemo waumini kukakaa kwa nafasi, umbali wa angalau mita moja kutoka mtu mmoja hadi mwingine na kuweka maeneo ya kunawa kwa maji na sabuni pamoja na vitakasa mikono katika nyumba zote za ibada.

“Kupunguza idadi ya siku za kukutana kufanya ibada na masaa ya ibada au mahubiri kila inapobidi. Kwa mfano, mikutano au shughuli za mikusanyiko za vikundi vya uimbaji, vijana, akinamama au waumini kwa ujumla ni vema zikasitishwa katika kipindi hiki,” amesisitiza.

Kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali, Waziri Mkuu amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kudhibiti kuenea zaidi kwa ugonjwa huu zikiwemo za kutoa elimu ya namna ya kujikinga, kuunda Kamati za Kitaifa kwa ngazi za Mawaziri, Makatibu Wakuu, Timu ya Wataalam wa afya pamoja na kutoa maelekezo kwa Kamati za Ulinzi na Usalama.

“Tumetenga maeneo ya kutolea huduma kwa wagonjwa wanaohisiwa kuwa na ugonjwa huu, tumenunua vifaa vya kukabiliana na ugonjwa huu hususani kwa watoa huduma wa afya. Tumeimarisha maabara zetu kwa lengo la kupanua wigo wa kufanikisha upimaji wa sampuli, vituo zaidi ya saba nchini ambapo upimaji wa awali unaanzia huko na kwenda kuhakikishwa katika Maabara Kuu ya Taifa,” amesema.

Wakati huohuo, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetaja mikoa ambayo imepata wagonjwa wapya 30 kutoka idadi ya 254 iliyotangazwa mara ya mwisho.

Wagonjwa hao na idadi yao kwenye mabano wanatoka mikoa ya Dar es Salaam (10), Zanzibar (9), Mwanza (4), Pwani (2), Dodoma (2). Mingine ni Kagera, Manyara na Morogoro ambayo yote ina mgonjwa mmoja mmoja.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wanaopenda kupandisha bei za vyakula wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

“Wiki hii waumini wa Kiislamu wanaanza mfungo wa Ramadhan, hivyo natoa wito kwa wafanyabiashara kuhakikisha vyakula muhimu katika kipindi hiki vinauzwa kwa bei ya kawaida, Wakuu wa Mikoa na Wilaya wafanye ukaguzi wa mara kwa mara kwenye masoko ili kuhakikisha bei ni ile ile.”

Amesema kuwa hivi sasa kuna sukari ya kutosha nchini hivyo bei itaendelea kuwa ileile bila kujali msimu. “Ninaawagiza Wakuu wa Mikoa, yeyote atakayekutwa anauza sukari kwa bei ya sh.4,500, chukua hatua dhidi yake kwani hayo si malengo ya Serikali yetu,” amesisitiza.

Kwa upande wao, wakizungumza kwa nyakati tofauti, viongozi wa dini walioshiriki maombi hayo, wameipongeza Serikali kwa hatua ambazo imezichukua hadi sasa katika kukabiliana na ugonjwa huo.

(mwisho)
Read More

Monday, April 20, 2020

MAENDELEO YA UBUNIFU WA MJI WA SERIKALI YAJADILIWA



Na. OWM, Dodoma.

Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea na zoezi la kuratibu awamu ya pili ya uendelezaji wa mji wa serikali eneo la Mtumba, makao makuu ya nchi jijini Dodoma. Awamu hii ya pili inahusisha Ubunifu na ujenzi wa majengo makubwa ya Ofisi zitakazotumiwa na Wizara za serikali.

Akiongea, leo tarehe 20 Aprili, 2020,  katika kikao cha Kamati ya Makatibu wakuu na Wataalamu wa michoro ya Ubunifu na usanifu wa majengo, Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge),Tixon Nzunda, amefafanua kuwa awamu hii ya pili ya  inajikita katika kuboresha ubunifu na usanifu wa mji wa serikali, ulioko Mtumba, Jijini Dodoma.

Aidha, kufanikiwa kwa  mpango huo kutachangiza jiji la  Dodoma kuwa jiji bora na la kisasa linaloendana na mahitaji na mifumo ya majiji bora duniani. Ili kufikia azma hiyo, tayari Timu ya Wataalam  imepitia michoro ya ubunifu na usanifu. Pia Wakala wa majengo Tanzania (TBA), inaendelea kufanya kazi kwa karibu na  Taasisi nyingine zinazohusika na miundo mbinu katika mji wa Serikali kama vile TARURA, DOWASA, TANESCO,  TPDC, TTCL na eGA.

Hivi karibuni , Mwezi Februari mwaka huu, 2020, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alizindua Mpango Kabambe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, ambapo aliwataka wadau mbalimbali kutoa ushirikiano kwa kiwango cha juu katika utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa lengo la kulifanya kuwa jiji bora na la kisasa nchini.

Serikali, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kutekeleza zoezi la kuhamishia shughuli za Serikali Kuu Dodoma. Tangu utekelezaji wa zoezi hilo uanze mwezi Septemba 2016.
Uamuzi wa kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma ulifanyika mwaka 1973 ikiwa ni maelekezo ya Chama cha TANU kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Uongozi wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
MWISHO.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Bw. Tixon Nzunda akizungumza wakati wa kikao kazi cha makatibu Wakuu na Wataalam wa Ubunifu na Usanifu wa majengo leo Aprili, 20, 2020,  lengo ikiwa ni kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, Kikao kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi yake Dodoma,  kushoto kwake  ni Katibu wa kikosi kazi cha kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma, wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20, Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma, kulia ni, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Dkt. Jim Yonazi na (kushoto) ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael na  Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa  na Michezo ,Dkt. Hassan Abbas (katikati).
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma,  wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20, Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma. 


Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kujadili mpango kabambe wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma,  wakifuatilia kikao hicho leo tarehe 20, Aprili, 2020 katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma. 
 
 Prof. John Lupala akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Ubunifu wa mpango wa Ujenzi wa Ofisi za Wizara Awamu ya Pili katika eneo la Mji wa Serikali Mtumba Dodoma wakati wa kikao kazi cha makatibu Wakuu na Wataalam wa Ubunifu na Usanifu wa majengo leo Aprili, 20, 2020.
Read More