Friday, February 12, 2021

Mpango wa kukabiliana na Vitendo vya kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini wazinduliwa

 

Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya waziri Mkuu kwa kushirikiana serikali ya Japan na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), wamezindua mpango wa Kukabiliana na Vitendo vya Kiuhalifu katika Maziwa na Bahari nchini. Mradi huo utaimarisha juhudi za kupambana na vitendo vya kihalifu hususani; uvuvi haramu, uhamiaji haramu, usafirishwaji wa nyara za serikali pamoja na upitishwaji wa madawa ya Kulevya.

Akiongea wakati wa kuuzindua Mradi huo Jijini Dodoma, leo tarehe 12 Februari 2021, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko, amefafanua kuwa mpangoi huo utatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, lengo lake ni kuimarisha usalama katika maziwa na bahari na utanufaisha wavuvi kwa kuwapa elimu ya njia bora za uvuvi na kujenga miundombinu ya kisasa ya kukausha samaki.

 

“Serikali inakusudia kutekeleza mpango huu kwa ufanisi kwa kuhakikisha wadau wa mradi huu wananufaika na utekelezaji wake. Kupitia mradi huu serikali itaweza kununua boti ili kuimarisha doria katika bahari na hivyo kuweza kupunguza vitendo vya kihalifu. Ni matarajio yangu mpango kazi huu  utakidhi mahitaji tulionayo ya kuainisha mfumo wa kitaasisi, makundi ya wadau na wajibu wao katika kupambana na uhalifu katika maziwa na bahari.” Amesisitiza Mwaluko

 

Awali akiongea katika uzinduzi huo; Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Christine Musisi,  ameeleza kuwa wanaamini Maendeleo ya Uchumi na ustawi wa watu hauwezi kupatikana bila kuwa na ulinzi imara katika maziwa na bahari pamoja na uboreshwaji wa  maisha ya watu wanaoishi katika maeneo ya maziwa na bahari. Ameongeza kuwa Kupitia mpango huo wataiwezesha serikali ya Tanzania kufanikisha malengo yake ya kuimarisha uchumi wa bluu.

 

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah ameeleza kuwa mpango  huo ni muhimu kwa nchi kwa kuwa utajikita katika kupambana na uvuvi haramu ambao umekuwa ukisabbisha uharibifu wa rasilimali katika Bahari. Ameongeza kuwa kwa sasa nchini asilimia 30 hadi 40 ya samaki wanaovuliwa na wavuvu wadogo wadogo wanaharibika, hivyo ujio wa mpango huo utakuwa ni mkombozi kwa wavuvi kwa kuboresha miundo mbinu ya kukausha samaki ambayo itawezesha kuongeza thamani samaki na kupata soko la kikanda.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio, ameongeza kuwa mpango huo utaisiadia wizara hiyo katika uwezo wa kudhibiti vitendo vya kiuhalifu hususan kwenye meneo ya ufukwe wa bahari na maziwa. Amesisitiza kuwa utekelezaji wa mpango huo utawezesha katika kuimarisha uchumi  wa nchi na ustawi wa jamii.

Utekelezaji wa mpango huo utasimamiwa na Kamati ya Usimamizi ambayo pamoja na kusimamia jukumu la utekelzaji wa Mradi huo, kamati itakuwa na jukumu la kuidhinisha mpango kazi  na taarifa ya utekelezaji. Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu). Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Makatibu wakuu wa Wizara ya TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais, Feddha na Mipango; Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Mambo ya ndani, Maliasili na Utaliina Ujenzi na Uchukuzi.

Ends-

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto) akikata utepe kwenye vitabu vya Mpango wa Utekelezaji wa  kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine ni kutoka kulia; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto) akionesha  Kitabu cha  Mpango wa Utekelezaji  wa Mradi wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine ni kutoka kulia; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto) akikabidhi   Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah na  Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio anayeshuhudia ni Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi,  Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto)  akionesha Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine ni kutoka kulia; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Paul Sangawe,  akifafanua jambo juu ya Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wakati wa uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Japan na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),  Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Baadhi ya wadau  Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini wakifuatilia uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Japan na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,  Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) akileleza umuhimu Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, utakavyoboresha miundombinu ya kisasa ya kukausha samaki,  wakati wa uzinduzi wa mradi huo, kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Baadhi ya wadau  wa Utekelezaji Mpango wa  kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini wakifuatilia uzinduzi wa mpango huo, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021. Mradi utaimarisha juhudi za kupambana na vitendo vya kihalifu hususani; uvuvi haramu, uhamiaji haramu, usafirishwaji wa nyara za serikali pamoja na upitishwaji wa madawa ya Kulevya.

Baadhi ya wajumbe wa sekretarieti walioshiriki katika shughuli ya uzinduzi wa Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021, mradi huo unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (wa pili kushoto walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mpango wa  kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine; kulia kwake ni ; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP,Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio (wa kwanza kulia walio kaa) na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah(wa kwanza kushoto walio kaa), Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.


Read More

Saturday, January 9, 2021

SERIKALI KUTUMIA MBINU YA MAKAMBI KWA WANAFUNZI WASICHANA KUWAWEZESHA KUFIKIA MALENGO

Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania imepanga kutumia Mbinu ya kuwaweka kwenye Kambi wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini,  kwa kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga na VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati, ili waweze kufanya vizuri kwenye masomo, kujitambua, kujiamini na kuweza kutimiza malengo yao.

Kwa mara ya Kwanza Ofisi ya Waziri Mkuu, kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania imeratibu kambi ya majaribio ya siku tano, kuanzia tarehe 4-8 Januari, 2021, Jijini Dodoma, kwa  wanafunzi wasichana 105 wa shule 18 kutoka kaya masikini zilizo chini ya mpango wa TASAF za Halmashauri ya wilaya ya Bahi, jijini Dodoma.

Akiongea wakati wa kufunga kambi hiyo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko amebainisha kuwa kufanikiwa kwa majaribio ya kambi hiyo kutawezesha serikali kupitia ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, kuendesha kambi za namna hiyo kwenye Halmashauri nyingine hapa nchini ili kuweza kuwasaidia wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kaya masikini kuweza kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda, amefafanua kuwa wilaya hiyo wamepanga kuwa na utaratibu wa kuwa na kambi za wanafunzi wasichana balehe kila baada ya miezi sita kwa wanafunzi 1,324 walioko ndani ya shule. Aidha, ameeleza kuwa wilaya hiyo tayari inao mfuko wa elimu wa Halmashauri ambao utawaendeleza kieleimu wanafunzi hao hadi elimu ya chuo kikuu.

Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mwitikio wa Taifa, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Audrey Njelekela, amefafanua kuwa Kambi hiyo ni sehemu ya Utekelezaji wa mradi wa TIMIZA MALENGO unaowalenga Wasichana Balehe na Wanawake Vijana walioko ndani na nje ya shule kutimiza malengo yao. Kwa sasa mradi huo unatekelezwa katika Halmashauri 10 nchini za mikoa ya Dodoma, Singida na Morogoro ambapo mikoa ya Tanga na Geita imeongezwa kwenye mradi huo. Amesisitiza  kuwa Mradi wa kambi utatekelezwa pia katika Halmashauri za mikoa hiyo.

Wakiongea kwa nyakati tofauti baada ya kufunga Kambi hiyo Mratibu wa Mradi huo  wa Kambi Salum Kilipamwambu ambainisha kuwa Tafiti za elimu ya sekondari zinaonesha wanafunzi wasichana wa sekondari wamekuwa wakishindwa kuhitimu masomo yao kwa kukosa uelewa na kutojitambua na kujiamini, naye, Mwajuma Hamisi kutoka shule ya sekondari Kigwe, Bahi jijini Dodoma, ameeleza kuwa mafunzo hayo yamewawezesha kujitambua, kujiamini na wameongeza weledi kwenye masomo ya sayansi na Hisabati hivyo wataweza kufanya vizuri kwenye masomo na hatimaye kuweza kutimiza elimu.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka shule 18 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, wakati wa kufunga kambi ya siku tano katika shule ya Sekondari ya Dodoma iliyolengo kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati.
Baadhi ya wanafunzi wa kike kutoka shule 18 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, wakifuatilia shughuli za kufunga kambi ya siku tano katika shule ya Sekondari ya Dodoma waliyoshiriki kwa lengo la kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga na VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati
Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda, akizungumza na wanafunzi wa kike kutoka shule 18 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, wakati wa kufunga kambi ya siku tano katika shule ya Sekondari ya Dodoma iliyolengo kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati.
Baadhi ya wanafunzi wa kike kutoka shule 18 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, wakionesha vipaji vyao wakati wa kufunga kambi ya siku tano katika shule ya Sekondari ya Dodoma, lengo ni kuwapa Mafunzo ya namna ya Kujikinga na VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati\
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mwitikio wa Taifa, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, Audrey Njelekela akieleza umuhimu wa kambi kwa wanafunzi wa kike kutoka shule 18 za Wilaya ya Bahi walio katika mpango wa kuhudumia kaya masikini, kambi hiyo imefanyika jijini, Dodoma ikihusisha wasichana 105, kutoka Halmashauri ya Bahi.
Baadhi ya wawezeshaji wa Kambi wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakifuatilia shughuliza kufunga kambi hiyo, Jijini Dodoma, Mafunzo ya namna ya Kujikinga na VVU na UKIMWI, Stadi za Maisha na Mafunzo ya masomo ya Sayansi na Hisabati, yalifundshwa.
Mwakilishi wa shirika la Peae corps, Tanzania Bw. Allanse Mbilu akieleza kuwa shirika hilo lipo tyari kushirikiana na Serikali kupitia TACAIDS katika utekelezaji wa Mradi wa kuwaweka kwenye Kambi wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tano jijini Dodoma
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akimkabidhi, Irine Emmanuel Mallya kutoka shule ya sekondari Kigwe, Bahi jijini Dodoma, kwa ushiriki hodari kwenye kambi ya wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tano jijini Dodoma.
Wanafunzi walioshiriki kwenye kambi ya wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakisoma risala yao wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tano jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walioshiriki kambi ya wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tano jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Bi. Dorothy Mwaluko akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawezeshaji walioshiriki kufundisha wanafunzi wakati wa kambi ya wanafunzi wasichana balehe wanaotoka kwenye kaya masikini, wakati wa kufunga kambi hiyo ya siku tano jijini Dodoma.
Read More

Friday, December 4, 2020

FAO yaanza na halmashauri 3 kujenga uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa

Mratibu Taifa Dawati la Afya Moja, Ofisi ya Waziri Mkuu, Harrison Chinyuka akifafanua umuhimu wa kutumia Dhana ya Afya moja wakati wa mafunzo wa Kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana ya Afya moja, Mafunzo yameratibiwa na Ofisi hiyo pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), mjini Morogoro, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Baadhi ya Washiriki kutoka Halmashauri za mikoa ya Arusha, Dar es salaam na Mwanza wakifuatilia mafunzo ya Kuwajengea Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana ya Afya moja, Mafunzo yameratibiwa na Ofisi hiyo pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), mjini Morogoro, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Mratibu wa Mafunzo kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Tanzania, Elibariki Mwakapeje, akieleza dhamira ya Shirika hilo katika Kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana ya Afya moja, Mafunzo yameratibiwa na Shirika hilo pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, mjini Morogoro, kuanziatarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Baadhi ya Washiriki kutoka Halmashauri za mikoaya Arusha, Dar es salaam na Mwanza wakifuatilia mafunzo ya Kuwajengea Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana ya Afya moja, Mafunzo yameratibiwa na Ofisi hiyo pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), mjini Morogoro, kuanziatarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Mtaalumu wa masuala ya Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Gibonce Kayuni akifundisha namna ya kupambana na usugu huo kwenye sekta ya mifugo wakati wa mafunzo ya kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana ya Afya moja, Mafunzo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), mjini Morogoro, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Mtaalumu wa masuala ya Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kutoka Chuo kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi- Muhimbili, Hussein Mohamed akifundisha namna ya kupambana na usugu huo kenye Nyanja ya afya ya binadamu,wakati wa mafunzo ya kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana yaAfya moja, Mafunzo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), mjini Morogoro, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali RBA linalojihusisha na kuelimisha jamii kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa, Erick Venant, akifundisha namna kuishirikisha jamii wakati wa mafunzo ya kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana ya Afya moja, Mafunzo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), mjini Morogoro, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa wa kijadili mbinu za kupambana na usugu huo wa wakati wa mafunzo yaliyoratibiwa na Ofisiya Waziri Mkuu pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO),mjini Morogoro, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Mtaalumu wa masuala ya Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kutoka Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine, Abubakar Hoza akifundisha namna ya kupambana na usugu huo kwa kwenye nyaja ya mifugo wakati wa mafunzo ya kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana ya Afya moja, Mafunzo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO),mjini Morogoro, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa wa kijadili mbinu za kupambana na usugu huo wa wakati wa mafunzo yaliyoratibiwa na Ofisiya Waziri Mkuu pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO),mjini Morogoro, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi), Mkoa wa Dar es salaam, Elizabert Mshote akitoa uzoefu wa shughuli za uratibu kama mshiriki wa mafunzo ya kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana ya Afya moja, Mafunzo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), mjini Morogoro, kuanziatarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Katibu Tawala Msaidizi (Uchumi), Mkoa wa Arusha, Hargeney Chitukuro akitoa uzoefu wa shughuli za uratibu kama mshiriki wa mafunzo ya kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana ya Afya moja, Mafunzo yameratibiwa na Ofisi ya Wazir Mkuu pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), mjini Morogoro, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020.
Washiriki na wawezeshaji wa mafunzo ya kuzijengea Halmashauri Uwezo wa kupambana na Usugu wa vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa kwa kutumia Dhana ya Afya moja wakiwa katika picha ya pamoja, Mafunzo yameratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), mjini Morogoro, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Desemba, 2020. F
Read More

Friday, November 27, 2020

TAARIFA KWA UMMA

Read More

Monday, November 16, 2020

JE UNAWAFAHAMU MAWAZIRI WAKUU WOTE KUANZIA MWAKA 1961 HADI SASA?

Read More

Thursday, November 12, 2020

RAIS MAGUFULI AMPENDEKEZA KASSIM MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU

Mpambe wa Rais Kanali Benard Paulo Masala Mulunga akimkabidhi spika wa Bunge Job Ndugai barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli yenye pendekezo la la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyemteua, Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 12, 2020.

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akionesha kwa wabunge barua kutoka kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli yenye pendekezo la la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyemteua, Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 12, 2020.

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisoma kwa wabunge barua kutoka kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli yenye pendekezo la la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyemteua, Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 12, 2020.

Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimpongeza Waziri Mkuu Mteule na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kusoma jina lake baada ya kupendekezwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 12, 2020.

Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimpongeza Waziri Mkuu Mteule na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kusoma jina lake baada ya kupendekezwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 12, 2020.

Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakimpongeza Waziri Mkuu Mteule na Mbunge wa Ruangwa Kassim Majaliwa baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kusoma jina lake baada ya kupendekezwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 12, 2020.

 Mpambe wa Rais Kanali Benard Paulo Masala Mulunga (katikati) akisindikizwa na wapambe wasaidizi wa Bunge kukabidhi barua kwa spika wa Bunge kutoka Rais, Dkt. John Pombe Magufuli,  yenye pendekezo la jina la Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 12, 2020.


Read More

WABUNGE WAMTHIBITISHA MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU

 


*Apata asilimia 100 ya kura zote 350 zilizopigwa

*Amshukuru Rais na aahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii

 

 

SPIKA wa Bunge la 12 Job Ndugai amesema wabunge wamemthibitisha mbunge wa jimbo la Ruangwa mkoani Lindi, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kuwa Waziri Mkuu kwa miaka mitano mingine (2020-2025) kwa kupata kura zote 350 zilizopigwa na wabunge sawa na asilimia 100.

 

“Kura zote zilizopigwa ni 350 hakuna iliyoharibika, hakuna kura ya hapana. Kura zote 350 zimemthibitisha Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, kwa hiyo ndugu wabunge Mheshimiwa Majaliwa amethibitishwa na Bunge hili kuwa Waziri Mkuu kwa kura 350 sawa na asilimia 100.”

 

Spika Ndugai ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 12, 2020) Bungeni jijini Dodoma baada ya kupokea jina la Waziri Mkuu lililowasilishwa bungeni na Mpambe wa Rais na kisha wabunge kupiga kura kwa ajili ya kulithibitisha jina hilo.

 

Akizungumza baada ya kuthibitishwa Mheshimiwa Majaliwa amesema amepokea uteuzi huo kwa mikono miwili na anamshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ameendelea kuwapa uhai wote na kushuhudia hayo, Pia ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa imani kubwa aliyoionesha juu yake.

 

“Mheshimiwa spika naomba nitumie nafasi hii kwa dhati yangu ya moyo kumshukuru sana Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi mkubwa alioupata kutoka kwa Watanzania kupitia uchaguzi ambao ulifanyika hivi karibuni kwa kushinda kwa kishindo. Uchaguzi uliofanyika kwa uhuru na haki.”

 

 “Jambo hili si dogo, Mwenyezi Mungu ameliongoza, namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa imani kubwa aliyonayo juu yangu na kuendelea kuniamini. Namshukuru sana na Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ushiriki wake katika kuridhia jina langu.”

 

“Pia, nampongeza Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ushindi mkubwa alioupata katika uchaguzi huo na namna ambavyo Watanzania wameridhishwa na kazi aliyoifanya na imani waliyonayo kwamba viongozi hao wataendelea kuwatumikia vizuri zaidi.”

 

Ametumia fursa hiyo kumpongeza Spika wa Bunge Job Ndugai kwa kuchaguliwa bila kupingwa kuwa mbunge wa Kongwa pamoja na kurudi katika nafasi yake ya uspika baada ya kupigiwa kura nyingi na waheshimiwa wabunge, hakuna siri kwamba umefanya kazi nzuri miaka mitano iliyopita umeisaidia sana serikali na kuiwezesha kufanya mambo makubwa.

 

“Kazi uliyoifanya miaka mitano iliyopita tunaifahamu vizuri zaidi na Serikali itaendelea kukupa ushirikiano wa dhati. “Mheshimiwa spika niendelee kushukuru kwa kuwashukuru wabunge wenzangu, waheshimiwa wabunge wenzangu mmenifanyia jambo kubwa kwangu na familia yangu.”

 

“…idadi ya kura zenu mlizonipigia mmenipa changamoto sana. Haijawahi kutokea mmepiga kura kwa asilimia 100, haijawahi kutokea nawashukuru sana. Nitaendelea kushirikiana na wabunge wenzangu wote nikijua nyie ni wawakilishi wa Watanzania wanaotamani kupata maendeleo kupitia uwakilishi wenu. ”

 

Pia, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa jimbo la Ruangwa na mkoa wa Lindi, familia na CCM kwa ushirikiano alioupata katika kutekeleza majukumu yake katika kipindi cha miaka mitano na anaimani wataendelea kumpa ushirikiano katika kipindi cha miaka mitano mingine.

 

Awali, kabla ya kuthibitisha jina la Waziri Mkuu wabunge mbalimbali walizungumzia utendaji kazi wa Mheshimwa Majaliwa ambapo Mbunge wa Tunduma David Silinde alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumrudisha tena Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika nafasi hiyo.

 

Amesema kuwa Waziri Mkuu Majaliwa ni kiongozi mwenye uwezo wa kusimamia maono ya Rais Dkt. Magufuli katika kuibadilisha nchi na pia anauwezo wa kuunganisha nchi yote kupitia Bunge na hivyo kufanya kazi ya rais kuwa nyepesi.

 

“Sifa kuu ya kiongozi ni unyenyekevu, kujishusha na kusikiliza na sifa hizo Mheshimiwa Majaliwa anazo, ninaamini wote tutampitisha kwa asilimia 100 ili kuliambia Taifa nini tunakwenda kukifanya kwa miaka mitano baada ya miaka mitano ya mafanikio ambayo imeleta ushindi wa kimbunga.”

 

Amesema anaamini kwamba katika kipindi cha miaka mitano Serikali inakwenda kufanya mabadiliko makubwa katika Taifa na dunia inajua kuwa viongozi wao ni mahiri na kila mahali wanatetemeka kusikia kazi inayofanywa na viongozi hao.

“Naomba wote tumpitishe ili aweze kuongoza tena.”

 

Naye, Mbunge wa Ismani, William Lukuvi amesema Mheshimiwa Majaliwa ni binadamu mwenye upendo, mchapakazi asiyekuwa na majivuno na kwa mara ya kwanza ameshuhudia Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM akizunguka kwenda kuwatetea wabunge nchi nzima. “Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli ametutendea haki Watanzania Mheshimiwa Majaliwa anatosha sana kuwa Waziri Mkuu.”

 

Kwa upande wake, Kapten Mstaafu George Mkuchika amesema Mheshimiwa Majaliwa anamfahamu vizuri na amewahi kufanya kazi wakiwa Ofisi ya Rais –TAMISEMI kwamba ni mtu mstarabu kama Mheshimiwa Majaliwa ni mtu msikivu, asiyejikweza na hajipendekezi anatenda haki kwa kila mtu.

 

“Katika kipindi cha miaka mitano hakubagua wabunge katika uetekelezaji wa shughuli za bunge na ni mtu msikivu sana. Amesimamia sana katika kufufua uchumi hasa mazao ya biashara, amerejesha mamlaka ya mkonge mikononi mwa Serikali. Ameratibu vizuri shughuli za wizara zote.”

 

Naye, Mama Salma Kikwete Alisema Mheshimiwa Majaliwa hakuwa mbaguzi katika kipindi cha miaka mitano iliyopita na amefanya mambo makubwa, hivyo anampongeza Rais Dkt. Magufuli  kwa kuwarejeshea kwani anastahiki kuwa Waziri Mkuu na hakuna anayeweza kupinga jambo hilo.

 

Mbunge mwingine, Fakharia Shomari alisema anamshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa uteuzi alioufanya katika nafasi ya Waziri Mkuu kwa sababu ni uteuzi ambao walikuwa wanaufikiria ila hawakuweza kuamua kabla ya yeye kutamka. “Mheshimiwa Majaliwa amefanya ziara nchi nzima na alikuwa anafanya kazi na kila rika na jamii. “Nawaomba wabunge wenzangu tuibariki hoja ya mheshimiwa Rais.”

 

Kwa upande wake, Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba alisema Mheshimiwa Majaliwa ni kiongozi msikivu, muadilifu, mnyenyekevu, hodari, mchapakazi na ni kiongozi shupavu ambaye nafasi hiyo anaimudu na anaiweza na hakuna shaka yoyote kwamba nafasi hiyo kwamba ataitendea haki. “Kumpigia kura nyingi tunaonesha imani kwa ndugu yetu na imani na busara kwa rais.”

 

 

 (mwisho)

Read More

RAIS MAGUFULI AMPENDEKEZA KASSIM MAJALIWA KUWA WAZIRI MKUU

 

Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini, Kepteni Mstaafu George Mkuchika  akitoa pongezi kwa Waziri Mkuu Mteule Kassim Majaliwa baada ya jina lake kupendekezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 12, 2020

Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Lukuvi  akitoa pongezi kwa Waziri Mkuu Mteule Kassim Majaliwa baada ya jina lake kupendekezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 12, 2020

Waziri Mkuu Mteule na mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa akitoa shukrani kwa Rais Dkt. Magufuli kwa kumpendekeza kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupitishwa na wabunge kwa asilimia mia moja, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 12, 2020.

Waziri Mkuu Mteule na mbunge wa jimbo la Ruangwa, Kassim Majaliwa akitoa shukrani kwa Rais Dkt. Magufuli kwa kumpendekeza kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kupitishwa na wabunge kwa asilimia mia moja, Bungeni jijini Dodoma, Novemba 12, 2020.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Prof. Adelardus Kilangi akisoma wasifu wa Waziri Mkuu Mteule Kassim Majaliwa baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kumpendekeza kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 12, 2020.

Read More

Tuesday, November 10, 2020

WAZIRI MKUU MSTAAFU, KASSIM MAJALIWA AAPA KUWA MBUNGE WA RUANGWA

  Waziri Mkuu Mstaafu, na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Iramba Magharibi Dkt. Mwigulu Nchemba, Bungeni Jijini Dodoma Novemba 10, 2020.

Waziri Mkuu Mstaafu, na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa akiapa kuwa mbunge wa Ruangwa, Bungeni Jijini Dodoma Novemba 10, 2020.

Waziri Mkuu Mstaafu, na Mbunge wa Jimbo la Ruangwa Kassim Majaliwa akipokea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanuni za Kudumu za Bunge kutoka kwa Katibu wa Bunge Stephen Kagaigai wakati alipoapa Bungeni Jijini Dodoma, Novemba 10, 2020.

 

Read More

Sunday, November 8, 2020

WAZIRI MKUU MSTAAFU, KASSIM MAJALIWA AWAJULIA HALI MZEE KING KIKI NA MKUU WA WILAYA YA MLELE.

Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Msanii mkongwe wa muziki wa dansi  Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama (King Kiki) , wakati alipomjulia hali msanii huyo anayesumbuliwa na matatizo ya pingiri za mgongo, nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ali, Novemba 8, 2020.

Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa akimjulia hali Msanii mkongwe wa muziki wa dansi  Kikumbi Mwanza Mpango, maarufu kama (King Kiki) , anayesumbuliwa na matatizo ya pingiri za mgongo, nyumbani kwake Temeke kwa Azizi Ali, Novemba 8, 2020. 

Waziri Mkuu Mstaafu, Kassim Majaliwa, akimpa pole Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Rechal Kasanda ambaye amelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu baada ya kupata ajali ya gari Wilayani Mlele, Mkoani Katavi alipokuwa kwenye ziara ya kikazi, Novemba 8, 2020. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera. 

 

Read More