Saturday, March 13, 2021

Waziri Mhagama: Mashine za kuongeza virutubishi kwenye unga kutengenezwa nchini

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amesema serikali ya wamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na lishe bora,  inakamilisha taratibu kwenye wizara za kisekta kupitia taasisi za serikali za SIDO, VETA, COSTECH pamoja na wadau wengine,   ili kutengeneza mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga hapa nchini na  zitakazotumiwa  na wasindikaji  wadogo na wakati


Mhagama ameeleza hayo leo tarehe 13 Machi, 2021 wakati akigawa na kuzindua utumiaji wa   ya  kuongeza virutubishi kwa wasindikaji wadogo na wakati jijini Tanga. Mashine hizo  5 zenye thamani ya takribani shilingi milioni  tano kwa kila moja,  zimetolewa na Mradi wa Utoaji wa vyakula  vilivyorutubishwa shuleni unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya ufadhili wa shirika lisilo la kiserikali la GAIN Tanzania.


Amefafanua kuwa serikali imelenga kutengeneza mashine hizo hapa nchini, kwa kuwa mashine hizo ambazo huagizwa nje ya nchi, gharama yake ni kubwa kwa wasindikaji wadogo, hali inayosababisha  urutubishaji wa unga wa mahindi kwa viwanda vingi kutofanya vizuri kwani ni asilimia saba (7%) pekee ya unga unaozalishwa nchini ndiyo unaongezewa virutubishi,  hivyo watumiaji wengi wa unga  wanakosa Vitamini na Madini muhimu mwilini.


 “Mashine hizi zikitengenezwa, hapa nchini zitaweza kuwafikia wasindikaji wadogo wengi. Wasindikaji wengi wakitumia mashine hizi tutakuwa na jamii yenye afya bora  na  uwezo wa kupambana na maradhi. Wastani wa msindikaji mdogo kwa siku anaweza kusindika unga  kati ya tani 5 hadi 10 za unga  kwa siku.  Hivyo mashine hizi  5 kwa hapa Tanga zitasaidia kusindika unga uliyorutubishwa wa tani 50  kwa siku” Amesisitiza Mhagama


Aidha, ameeleza kuwa serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu, inaendelea na jitihada za kusimamia masuala ya lishe kwa ngazi ya Taifa kwa kuwa tayari sera na sheria zimesha tungwa. Pia, ameeleza kuwa tayari maagizo yametolewa kwa zabuni zote za usambazaji wa chakula katika shule lazima chakula kiwe na virutubishi. Vilevile, TBS wanaedelea kukagua ubora wa chakula nchini hususani kwa wazalishaj wakubwa.


“Tunawahamasisha wasindikaji wadogo wa unga na mahindi waungane na kutengeneza ushirika ili  waweze  kupata unafuu wa kuagiza mashine za kuongeza virutubishi. Lakini pia tunaedelea kuzisisitiza Halmashauri kuangalia namna ya upatikanaji wa mashine hizi, hata kwa njia ya kuwakopesha,  lakini pia tumezitaka Halmashauri kutengeneza sheria ndogo ndogo  zitakazo wataka wazalishaji wadogo na wa kati wa mahindi kuongeza virutubishi. Naomba pia mkoa  huu uibebe hii agenda ya lishe ” Amesisitiza Mhagama.


Awali,  Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye pia ni mbunge wa  jimbo la Tanga mjini, Ummy Mwalimu,  ameeleza kuwa Ofisi hiyo wameamua kuibeba agenda ya kuhakikisha wananchi wanakuwa na  lishe bora. Amebainisha  kuwa watakuwa na mpango wa kupanda miti ya matunda hususan; maembe, mapera, maparachichi na malimau, kwa shule zote nchini ikiwa ni  shule za msingi na shule za sekondari. Pia amesisitiza  kuwa mpango huo utaanzia jimbo la Tanga mjini.


Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela amelishukuru shirika lisilo la kiserikali la GAIN Tanzania kwa kushirikiana na serikali katika kuhakikisha masuala ya lishe mkoani  humo yanakuwa bora kwa kutoa  bure mashine za kuongeza virutubishi kwenye unga kwa wasindikai wadogo pamoja na virutubishi. Aidha, amefafanua kuwa  Tanga haitakuwa nyuma tena kwenye masuala ya lishe kwa kuwa wamejaliwa kulima mboga mboga, maharage,  Maziwa yapo pamoja na samaki na mazao yake.


Naye Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, ameeleza kuwa shirika hilo limetoa mashine 10 za kuongeza virutubishi kwenye unga ikiwa mashine 5 kwa mkoa wa Kagera na mashine 5 kwa mkoa wa Tanga. Pia amefafanua kuwa wametoa virutubishi kilo 700 kwa mkoa wa Kagera na Tanga kilo 700.


Akiendelea kutaja mafanikio ya mradi huo, ameeleza kuwa katika kujenga usimamizi bora wa masuala ya lishe kwenye mikoa hiyo, wamewanunulia maafisa lishe mashine za kupima madini ya chuma ili waweze kuhakiisha yameongezwa kwenye chakula kwa mujibu wa sheria. Aidha, amesema kuwa wamewajengea uwezo zaidi ya wazalishaji 40 wa mikoa hiyo pamoja na zaidi ya shule 30 kwa kila mkoa  zimepata mafunzo juu ya masuala   ya lishe. Pia kamati za mikoa hiyo za usimsmizi masuala ya lishe nazo zimejengewa uwezo .


Shirika lisilo la kiserikali la GAIN Tanzania limetekeleza agizo la serikali la upatikanaji wa chakula  chenye virutubishi shuleni, kwa kuanza na mkoa wa Kagera na Tanga. Lengo la mradi huo ni kuwapatia chakula kilichorutubishwa  wanafunzi elf 12 kwenye  shule 30 za mkoa wa Kagera na Tanga. Mradi huo umetekelezwa kuanzia Desemba 2019 na Machi 2021 utekelezaji wa awamu ya kwanza unakamilika. Wadau wanaoutekeleza mradi huo chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu ni; TAMISEMI, TFNC, TBS pamoja na RITA.

ENDS.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa  Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, namna  ya mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga inavyoweza kumsaidia msindikaji mdogo wa unga mara  bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashune hiyo jijini Tanga.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu,  Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela Wakipata maelezo kutoka kwa  Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, namna  ya mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga inavyoweza kumsaidia msindikaji mdogo wa unga mara  bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashune hiyo jijini Tanga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela, Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, wakizindua mashine ya kuongeza virutubishi kwenye unga kwa msindikaji mdogo wa unga mara  jijini Tanga.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akifurahia mara baada ya kuzindua utumiaji wa  mashine  ya kuongeza virutubishi kwenye unga hapa nchini ninayotumiwa na wasindikaji  wadogo mara baada ya kuizindua utumiaji wa  mashine hiyo jijini Tanga kwenye kiwanda cha Shenkonde.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu,  Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela wakiangalia unga uliongezwa virutubishi na  mashine  maalum ya  kuongeza virutubishi kwenye unga inayotumiwa na  msindikaji mdogo wa unga mara  bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashine hiyo jijini Tanga.

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela akiwaeleza wananchi wa mkoa huo umuhimu wa kutumia unga uliongezwa virutubishi na  mashine  maalum ya  kuongeza virutubishi kwenye unga inayotumiwa na  msindikaji mdogo wa unga mara  bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashine hiyo jijini Tanga

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini, akiwaeleza wananchi wa jimbo hilo umuhimu wa kutumia unga uliongezwa virutubishi na  mashine  maalum ya  kuongeza virutubishi kwenye unga inayotumiwa na  msindikaji mdogo wa unga mara  bada ya kuzinduliwa utumiaji wa mashine hiyo jijini Tanga.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza umuhimu wa kutengeneza mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga hapa nchini na  kutumiwa   na wasindikaji  wadogo kwa wadau wa lishe na Kamati ya Usimamizi wa Lishe jijini Tanga.

Baadhi ya Wadau wa lishe na Kamati ya Usimamizi wa Lishe jijini Tanga wakifuatilia shughuli ya  uzinduzi wa  mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga hapa nchini na  kutumiwa   na wasindikaji  wadogo kwa Lishe jijini Tanga.

]Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika pucha ya pamoja na kikundi cha Tanzania Girls Guide cha mkoani Tanga amabcho kinajihusisha na masuala ya kuhamasisha masuala ya lishe  mara baada ya kuzindua utumiaji wa mashine  za kuongeza virutubishi kwenye unga na  kutumiwa   na wasindikaji  jijini Tanga

Read More

Friday, March 5, 2021

Waziri Mhagama: Wasindikaji wa Vyakula zingatieni sheria ya Chakula.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amewataka wamiliki wa viwanda vikubwa vya usindikaji wa chakula nchini (Unga wa ngano,Unga wa Mahindi na Mafuta ya kula) kuhakikisha wanaweka virutubishi katika bidhaa hizo kama inavyowataka Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2010.


Sheria hiyo chini ya kanuni zake inawataka wamiliki wa viwanda vikubwa vya usindikaji wa chakula nchini kuongeza  virutubishi vya madini joto kwenye chumvi na  kuongeza virutubishi vya madini ya chuma, zinki, Asidi ya foliki na Vitamini B 12 kwenye unga wa ngano na mahindi pamoja na  virutubishi vya vitamin A kwenye mafuta ya kula.


Waziri Mhagama ametoa agizo hilo jijini Dar es salaam wakati wa ziara ya kujionea hali ya urutubishaji wa vyakula hivyo, katika viwanda vya 21st Century Food and Packaging, Lina Millers Ltd na Neelkanth Salt Ltd pamoja na kuangalia wigo wa urutubishaji wa vyakula katika kuwafikia walengwa.


Waziri Mhagama amesema kwenye urutubishaji wa unga wa mahindi bado viwanda vingi havifanyi vizuri kwani ni asilimia saba (7%) pekee ya unga unaozalishwa nchini ndiyo unaongezewa virutubishi hivyo hali inayosababisha watumiaji wengi wa unga kukosa Vitamini na Madini muhimu Mwilini.


“Tumeweka sheria na tayari tumeanza kuitumia toka mwaka 2013 kuhakikisha vyakula vinavyozalishwa nchini vinaongezwa virutubishi,  hivyo ni jukumu la kila mwenye kiwanda kuzinzingatia sheria hii kwani vyakula hivi vitasaidia kupunguza tatizo la udumavu nchini, ambalo kwa kiasi kikubwa tumeweza kukabiliana nalo,” Amesema Waziri Mhagama


Amefafanua kuwa Katika kukabiliana na tatizo hilo, Serikali imefanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuandaa Sheria ya Chumvi ya Mwaka 1994. Sheria hiyo imefanyiwa mapitio na kuwa kanuni chini ya Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2010 ili kuhakikisha kuwa chumvi yote inayotumika nchini kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama inaongezewa madini joto.


Akizungumzia kiwango cha uongezaji virutubishi kwenye mafuta ya kula yanayozalishwa nchini,   Waziri Mhagama amesema kwa upande wa mafuta wamiliki wengi wa Viwanda hivyo wameonekana kuweka jitihada kwani mpaka sasa mafuta yanayozalishwa na viwanda vya ndani asilimia 73 yanaongezewa virutubishi.


“kuna faida nyingi sana katika urutubishaji wa unga na mafuta, bila shaka kila mmoja wetu anafahamu, vyakula hivi vitasaidia kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano, pamoja na vifo vya wanawake wajawazito.” Amesema Waziri Mhagama


Katika Hatua nyingine Waziri Mhagama pia aliutaka uongozi wa Kiwanda cha kuzalisha Chumvi cha Neelkhanth Salt kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani ambapo  nao amewataka kuzingatia sheria ya Chumvi ya Mwaka 1994 kama ilivyofanyiwa mapitio na kuwa kanuni chini ya sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi  ya mwaka 201 inavyowataka wazalishaji wa chumvi kuhakikisha chumvi yote inavyozalishwa nchini inawekewa madini joto.


Aidha, Waziri Mhagama amezipongeza Taasisi zisizo za kiserikali,  kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa Wamiliki wa viwanda vya usindikaji wa chakula (Unga wa ngano, unga mahindi na mafuta ya kula) wanakuwa mstari wa mbele katika zoezi la urutubishaji linafanyika ipasavyo kwa mujibu wa kanuni na taratibu.


Nae Mkurugenzi wa kiwanda cha kuzalisha unga cha Lina Millers Ltd Lina Kimaro alisema bado jamii inahitaji elimu zaidi kuhusu vyakula vinavyoongezwa virutubishi, kwani changamoto ambayo wamekutana nayo kwa baadhi ya wateja wao ni kushindwa kukubali vyakula vilivyo ongezwa virutubishi.


Wakiongea kwa nyakati tofauti katika ziara hiyo, Meneja Mrad kutoka Technoserve Tanzania George Kaishozi pamoja na Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, wamebainisha kuwa watendelea kuunga mkono jitihada za serikali  juu ya urutubishaji na uzalishaji bora wa chakula nchini.


Mwaka 2011 Viwango na kanuni za uongezaji virutubishi kwenye vyakula viliandaliwa, ambapo Mwaka 2013, Uongezaji virutubishi ulizinduliwa rasmi hapa nchini. Hadi sasa jumla ya viwanda vikubwa na vya kati 35 vya ngano, mahindi na mafuta ya kula vinaongeza virutubishi kwenye vyakula. Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 88 ya ngano na asilimia 68 ya mafuta yanayozalishwa na viwanda vikubwa  vinaongezwa virutubiishi ipasavyo.

ENDS.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama maelezo kwenye kifungashio cha virutubishi vinavyotumiwa na kiwanda cha 21st Century Food and Packaging, jijini Dar es salaam,  lengo likiwa ni kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha cha 21st Century Food and Packaging namna wanavyohakiki urutubishaji wa mikate kwenye maabara yao, wakati wa ziara ya kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini, jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza umuhimu wa kuzingatia Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2010, kwa Mtaalamu wa maabara kiwanda cha 21st Century Food and Packaging, Norbeth Mwingira wakati wa ziara ya  kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini, jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha cha 21st Century Food and Packaging, Govind Rathod,  namna wanavyohakiki urutubishaji wa vyakula  kwenye maabara yao, wakati wa ziara ya  kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini, jijini Dar es salaam.

Sehemu ya Virutubiushi vinavyotumika kwenye vyakula vinavyozalishwa  na Kiwanda cha cha 21st Century Food and Packaging, jiini Dar es salaam. Hadi sasa jumla ya viwanda vikubwa na vya kati 35 vya ngano, mahindi na mafuta ya kula vinaongeza virutubishi kwenye vyakula.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiangalia mashine inayotumika katika usindikaji wa vyakula kwenye kiwanda cha Lina Millers Ltd, jijini Dar es salaam,  lengo likiwa ni kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisistiza umuhimu wa urubishaji vyakula kwa Kiwanda cha Lina Millers Ltd, jijini Dar es salaam,  wakati wa ziara ya kujionea hali ya urutubishaji vyakula.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akielezwa namna chumvi inavyopimwa madinijoto na  Mtaalamu wa maabara kiwanda cha Neelkanth Salt Ltd mkoani Pwani, wakati wa ziara ya  kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza umuhimu wa kuzingatia Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2010, kwa kiwanda cha Neelkanth Salt Ltd mkoani Pwani, wakati wa ziara ya  kujionea hali ya urutubishaji vyakula nchini.


Read More

Thursday, March 4, 2021

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amekerwa na waajiri nchini wasiotekeleza Sheria na.6 ya mwaka 2014 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2019, sheria hiyo inamtaka mwaajiri kumpa mkataba wa ajira mfanyakazi pamoja na kutoa haki ya kuwa na vyama vya wafanyakazi.

Waziri Mhagama akiwa katika ziara ya kujionea hali ya urutubishaji vyakula kwenye viwanda vikubwa vya usindikaji wa chakula (Unga wa ngano, unga wa mahindi na mafuta ya kula) jijini Dar es salaam, wafanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkanth Salt Limited pamoja na Kampuni ya Unique Consultants Services, wamejitokeza kueleza kero zao zilizojikita kwenye mikataba ya ajira, kutokuwepo na haki ya vyama vya wafanyakazi, kima cha mshahara pamoja na michango yao kutopelekwa NSSF.

“Afisa kazi mkoa wa Pwani  nakupigia hii simu nikiwa hapa kwenye kiwanda cha Neelkanth Salt Ltd nataka kesho uje hapa na timu yako nataka mkague mikataba, hakikisheni kinaundwa chama cha wafanyakazi, angalia mishahara  na posho zinazingatia kazi wanazofanya, angalieni vitendea kazi. Huyu mwekezaji anafanya kazi nzuri hapa nchini na amewekeza hadi Tanga, lakini tunataka uwekezaji wenye tija uendane na kazi zenye staha kwa watanzania” Amesisitiza Mhe. Mhagama.

Baada ya kuongea na wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants Services, Waziri Mhagama alipiga simu hapo hapo na kumwelekeza Afisa kazi wa mkoa wa Dar es salaam ndani ya saa moja kuhakikisha anafanya ukaguzi wa ghafla kuwasikilza wafanyakazi hao kero zao.

“Watanzania wanao wajibu wa kutafuta haki zao mahala pa kazi, nataka Afisa kazi Dar e salaam uje hapa na meneja wa Tawi wa NSSF, kwani nimeelezwa wafanyakazi hawa kwa miaka miwili michango yao ya mishahara haipelekwi NSSF.Pia nipewe taarifa ya utekelzaji wa suala hili mara moja likikamilika. Niwatake wafanyakazi mtulie serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ipo tayari kushughulikia kero za wananchi kwa wakati” Amesema Mhagama.

Katika hatua nyingine, Waziri Mhagama amewataka waajiri kuhakikisha michango ya mishaha ra ya wafanyakazi inapelekwa kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa mujibu wa sheria. Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii sura na. 50 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2018, inakata mwajiri awasilishe michango ya wafanyakazi kwenye mfuko huo kila mwenzi ambapo mwajiri  na mwajiriwa kila mmoja huchangia 10% ya mshahara.

ENDS.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisoma malalamiko ya wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants Services walipo usimamisha msafara wake ili kueleza changamoto zao mahaha la pa kazi, jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akimueleza Afisa Rasilimali watu wa Kampuni ya Unique Consultants Services, Isaya Vangisheria, umuhimu wa kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii, jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akimpigia simu Afisa Kazi na Meneja wa NSSF mkoa wa Dar es salaam na amewapa maelekezo ya kutatua kutatua changamoto za  wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants Services wakati walipomsimamisha kueleza changamoto zao za ajira, jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwa anaongea na  Afisa Kazi  na Meneja wa NSSF mkoa wa Dar es salaam huku akiwapa maelekezo pamoja na Afisa Rasilimali watu wa Kampuni ya Unique Consultants Services, Isaya Vangisheria kutatua kutatua changamoto za  wafanyakazi wa Kampuni ya Unique Consultants Services wakati walipomsimamisha kueleza changamoto zao za ajira, jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiongea na wafanyakazi wa wa kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkanth Salt Limited, mkoani Pwani, wakati walipotembelea kiwanda hicho kujionea hali ya urutubishaji wa chumvi na kuwataka wamueleze changamoto zinazowakabili kwenye ajira yao..

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwasikiliza  wafanyakazi wa wa kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Neelkanth Salt Limited, mkoani Pwani, wakati walipotembelea kiwanda hicho kujionea hali ya urutubishaji wa chumvi na amemwagiza Afisa kazi na timu yake kufika kiwandani hapo kutatua changamoto za kutokuwa na vyama vya wafanyakazi, vitendea kazi na mikataba ya ajira pamoja na michango kutopelekwa NSSF.


Read More

Monday, March 1, 2021

Waziri Mhagama: Jengeni Viwanda vya kutengeneza Virutubishi vyakula nchini.

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama ameushauri ushirika wa wazalishaji wakubwa wa vyakula nchini kujenga viwanda vya kutengeneza Virutubishi vinavyoongezwa kwenye vyakula badala ya kuviagiza virutubishi hivyo nje ya nchi. Virutubishi hivyo ni madini ya chuma, Zinki, Asidi ya foliki na Vitamini B 12.

Waziri Mhagama ametoa ushauri huo baada ya kutembelea viwanda vya S.S Bakhresa Plant na Murzah Wilmar complex, jijini Dar es salaam, tarehe 1 Machi 2021,  lengo likiwa ni kujionea hali ya urutubishaji, ambapo wamiliki hao wa viwanda vya usindikaji wa chakula (Unga wa ngano, unga wa mahindi na mafuta ya kula) wamebainisha kuwa wamekuwa na changamoto ya kupata virutubishi hivyo kwa wakati kutoka nje ya nchi.

“Sisi kama serikali tupo tayari kushirikiana na nyie na tutatengeneza mazingira mazuri ya kuwawezesha kufanya uwekezaji wa viwanda hivyo. Tunaamini virutubishi hivi vikizalishwa hapa nchini gharama mnayotumia kununua virutubishi hivyo itapungua, lakini pia tutakuwa na uhakika zaidi wa aina ya virutubishi tunavyotumia kwenye vyakula vyetu” Amesisitiza Mhagama.

Ameongeza kuwa uanzishwaji wa viwanda hivyo utaongeza ajira kwa watanzania ambao bado wapo kwenye soko la ajira, pia amebainisha kuwa viwanda hivyo vitapunguza matumizi makubwa ya fedha za kigeni kwa kufanya manunuzi nje na fedha za kigeni zitaongezeka nchini kwa kuwa kuna nchi jirani ambazo wameamza kutekeleza sheria na Programu za kuongeza virutubishi hivyo zitakuja kununua virutubishi hivyo hapa nchini.

“Eneo jingine ambalo tungependa mfikirie ni kutengeneza vifaa vya kurutubisha chakula (dosifier). Mkiweza kuvitengeneza hivi vifaa hapa nchini na mkatumia nyie wenyewe lakini vikatumiwa na wasindikaji wa Kati na wadogo tutakuwa tumetengeneza vizuri mnyororo wa kuongeza virutubishi kwenye vyakula” Amesisitiza Mhagama.

Kwa upande wake mwakilishi wa Viwanda vya S.S Bakhresa, Husein Sufian amefafanua kuwa ujenzi wa viwanda hivyo ni muhimu kwa kuwa kiwanda hicho hutumia gharama kubwa ikiwa ni takribani shilingi bilioni 1.4/=, kwa kila mwaka hutumika kununua virutubishi vya kuongeza kwenye vyakula vinavyozalishwa na kiwanda hicho.

Awali, wakiongea kwa nyakati tofauti  wakati Waziri Mhagama alipokutana na wadau na Taasisi zisizo za serikali zinazojishughulisha na  masuala ya urutubishaji,  kutoka Technoserve Tanzania Meneja Mradi, George Kaishozi pamoja na Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, wamebainisha kuwa wanaendelea kushirikiana na serikali katika ufuatiliaji wa uhakiki wa udhibiti wa ubora wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi nchini.

Aidha; wamesisitiza kuwa wanaendelea kuwasaidia wasindikaji wadogo kupata   virutubishi na vifaa vya kufanyia urutubishaji pamoja na kuhamasisha wasindikaji hao kuzalisha, kusindika na kuyafikisha kwa walaji mazao yaliyorutubishwa kibaiolijia. 

Mwaka 2011 Viwango na kanuni za uongezaji virutubishi kwenye vyakula viliandaliwa, ambapo Mwaka 2013, Uongezaji virutubishi ulizinduliwa rasmi hapa nchini. Hadi sasa jumla ya viwanda vikubwa na vya kati 35 vya ngano, mahindi na mafuta ya kula vinaongeza virutubishi kwenye vyakula. Tafiti zinaonyesha kwamba asilimia 88 ya ngano na asilimia 68 ya mafuta yanayozalishwa na viwanda vikubwa  vinaongezwa virutubiishi ipasavyo.

ENDS.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo ya namna ya Kifaa maalumu cha kuongeza virutubishi kwenye vyakula (dosifier) kinavyofanya kazi wakati alipo tembelea kiwanda cha S.S Bakhresa Plant, tarehe 1 Machi, 2021 jijini Dar es salaam,  lengo likiwa ni kujionea hali ya urutubishaji.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akipata maelezo ya namna kiwanda cha S.S Bakhresa Plant kinavyo hakiki ubora wa virutubishi  kwenye vyakula vinavyozalishwa na kiwanda hicho,  jijini Dar es salaam, wakati alipofanya ziara ya kubaini fursa na changamoto zilizopo kwa wasindikaji wakubwa ili kuimarisha  urutubishaji wa vyakula nchini, tarehe 1 Machi 2021.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiangalia sehemu ya mitambo ya kiwanda cha S.S Bakhresa Plant jijini Dar es salaam tarehe 1 Machi, 2021,  wakati alipofanya ziara,  lengo likiwa ni kujionea hali ya urutubishaji wa vyakula.

Sehemu ya mitambo ya kiwanda cha S.S Bakhresa inayotumika katika usindikaji wa chakula (Unga wa ngano na unga wa mahindi). Kiwanda hicho ni miongoni mwa  viwanda vikubwa na vya kati 35 vya ngano, mahindi na mafuta ya kula kwa sasa vinavyoongeza virutubishi kwenye vyakula.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Murzah Wilmar complex, jijini Dar es salaam, wakati alipotembelea kiwanda hicho lengo likiwa ni kujionea hali ya urutubishaji wa vyakula , tarehe 1 Machi 2021.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akimsikiliza Meneja Mradi, Technoserve Tanzania, George Kaishozi akimueleza namna viwanda vikubwa vinavyoweza kuimarisha urutubishaji wa vyakula wakati walipotembelea  Kiwanda cha Murzah Wilmar complex, jijini Dar es salaam, tarehe 1 Machi, 2021.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kiwanda cha Murzah Wilmar complex, jijini Dar es salaam wakiendelea na shughuli za kuzalisha  mafuta ya kula. Kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda vikubwa vinavyongeza virutubishi kwenye mafuta hayo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa  Kiwanda cha Murzah Wilmar complex, jijini Dar es salaam. Lengo la ziara hiyo ni kujionea hali ya urutubishaji katika kiwanda hicho, tarehe 1 Machi 2021.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akisisitiza umuhimu wa kuwa na viwanda vya ndani vya kutengeneza virutubishi vya vyakula wakati alipokutana na wadau na Taasisi zisizo za serikali zinazojishughulisha na  masuala ya urutubishaji,  Jijini Dar es salaam, tarehe 1 Machi 2021.

Meneja Mradi wa urutubishaji vyakula, Gain Tanzania, Archad Ngemela, akieleza namna ya Taasisi hiyo inavyendelea  kushirikiana na serikali katika ufuatiliaji wa uhakiki wa udhibiti wa ubora wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi nchini, wakati wa mkutano wa Mhe. Waziri Mhagama na wadau na Taasisi zisizo za serikali zinazojishughulisha na  masuala ya urutubishaji,  jijini Dar es Salaam, tarehe 1 Machi2021.

Baadhi ya wadau wa masuala ya lishe wakifuatailia mkutano wa Mhe. Waziri Mhagama na wadau na Taasisi zisizo za serikali zinazojishughulisha na masuala ya urutubishaji, wakati alipokutana nao  jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kubaini fursa na changamoto zilizopo kwa wasindikaji wakubwa ili kuimarisha  urutubishaji wa vyakula nchini, tarehe 1 Machi 2021.

Meneja Mradi Technoserve Tanzania , George Kaishozi , akieleza namna ya Taasisi hiyo inavyendelea  kushirikiana na serikali katika ufuatiliaji wa uhakiki wa udhibiti wa ubora wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi nchini, wakati wa mkutano wa Mhe. Waziri Mhagama na wadau na Taasisi zisizo za serikali zinazojishughulisha na  masuala ya urutubishaji,  jijini Dar es Salaam, tarehe 1 Machi 2021.






 



Read More

Friday, February 12, 2021

Mpango wa kukabiliana na Vitendo vya kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini wazinduliwa

 

Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya waziri Mkuu kwa kushirikiana serikali ya Japan na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), wamezindua mpango wa Kukabiliana na Vitendo vya Kiuhalifu katika Maziwa na Bahari nchini. Mradi huo utaimarisha juhudi za kupambana na vitendo vya kihalifu hususani; uvuvi haramu, uhamiaji haramu, usafirishwaji wa nyara za serikali pamoja na upitishwaji wa madawa ya Kulevya.

Akiongea wakati wa kuuzindua Mradi huo Jijini Dodoma, leo tarehe 12 Februari 2021, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko, amefafanua kuwa mpangoi huo utatekelezwa kwa kipindi cha mwaka mmoja, lengo lake ni kuimarisha usalama katika maziwa na bahari na utanufaisha wavuvi kwa kuwapa elimu ya njia bora za uvuvi na kujenga miundombinu ya kisasa ya kukausha samaki.

 

“Serikali inakusudia kutekeleza mpango huu kwa ufanisi kwa kuhakikisha wadau wa mradi huu wananufaika na utekelezaji wake. Kupitia mradi huu serikali itaweza kununua boti ili kuimarisha doria katika bahari na hivyo kuweza kupunguza vitendo vya kihalifu. Ni matarajio yangu mpango kazi huu  utakidhi mahitaji tulionayo ya kuainisha mfumo wa kitaasisi, makundi ya wadau na wajibu wao katika kupambana na uhalifu katika maziwa na bahari.” Amesisitiza Mwaluko

 

Awali akiongea katika uzinduzi huo; Mwakilishi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Christine Musisi,  ameeleza kuwa wanaamini Maendeleo ya Uchumi na ustawi wa watu hauwezi kupatikana bila kuwa na ulinzi imara katika maziwa na bahari pamoja na uboreshwaji wa  maisha ya watu wanaoishi katika maeneo ya maziwa na bahari. Ameongeza kuwa Kupitia mpango huo wataiwezesha serikali ya Tanzania kufanikisha malengo yake ya kuimarisha uchumi wa bluu.

 

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah ameeleza kuwa mpango  huo ni muhimu kwa nchi kwa kuwa utajikita katika kupambana na uvuvi haramu ambao umekuwa ukisabbisha uharibifu wa rasilimali katika Bahari. Ameongeza kuwa kwa sasa nchini asilimia 30 hadi 40 ya samaki wanaovuliwa na wavuvu wadogo wadogo wanaharibika, hivyo ujio wa mpango huo utakuwa ni mkombozi kwa wavuvi kwa kuboresha miundo mbinu ya kukausha samaki ambayo itawezesha kuongeza thamani samaki na kupata soko la kikanda.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio, ameongeza kuwa mpango huo utaisiadia wizara hiyo katika uwezo wa kudhibiti vitendo vya kiuhalifu hususan kwenye meneo ya ufukwe wa bahari na maziwa. Amesisitiza kuwa utekelezaji wa mpango huo utawezesha katika kuimarisha uchumi  wa nchi na ustawi wa jamii.

Utekelezaji wa mpango huo utasimamiwa na Kamati ya Usimamizi ambayo pamoja na kusimamia jukumu la utekelzaji wa Mradi huo, kamati itakuwa na jukumu la kuidhinisha mpango kazi  na taarifa ya utekelezaji. Mwenyekiti wa Kamati hiyo ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu). Wajumbe wengine wa Kamati hiyo ni Makatibu wakuu wa Wizara ya TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais, Feddha na Mipango; Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Mambo ya ndani, Maliasili na Utaliina Ujenzi na Uchukuzi.

Ends-

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto) akikata utepe kwenye vitabu vya Mpango wa Utekelezaji wa  kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine ni kutoka kulia; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto) akionesha  Kitabu cha  Mpango wa Utekelezaji  wa Mradi wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine ni kutoka kulia; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto) akikabidhi   Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah na  Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio anayeshuhudia ni Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi,  Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (kushoto)  akionesha Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine ni kutoka kulia; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP, Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Paul Sangawe,  akifafanua jambo juu ya Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wakati wa uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Japan na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP),  Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Baadhi ya wadau  Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini wakifuatilia uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Serikali ya Japan na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kuratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,  Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (katikati) akileleza umuhimu Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, utakavyoboresha miundombinu ya kisasa ya kukausha samaki,  wakati wa uzinduzi wa mradi huo, kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio na, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.

Baadhi ya wadau  wa Utekelezaji Mpango wa  kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini wakifuatilia uzinduzi wa mpango huo, Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021. Mradi utaimarisha juhudi za kupambana na vitendo vya kihalifu hususani; uvuvi haramu, uhamiaji haramu, usafirishwaji wa nyara za serikali pamoja na upitishwaji wa madawa ya Kulevya.

Baadhi ya wajumbe wa sekretarieti walioshiriki katika shughuli ya uzinduzi wa Mpango wa Utekelezaji wa kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021, mradi huo unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu), Bi. Dorothy Mwaluko (wa pili kushoto walio kaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Mpango wa  kukabiliana na Vitendo vya Kihalifu katika Maziwa na Bahari kuu nchini, wengine; kulia kwake ni ; Mwakilishi kutoka Shirika la UNDP,Bi. Christine Musisi, Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya ndani, Christopher Kadio (wa kwanza kulia walio kaa) na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah(wa kwanza kushoto walio kaa), Jijini Dodoma, tarehe 12 Februari 2021.


Read More