Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la barabara ya Tandahimba mjini, Mkoani Mtwara, yenye urefu wa kilomita tatu, ilityojengwa kwa fedha za halmashauri, Februari 28, 2018. |
Wednesday, February 28, 2018
UZINDUZI WA BARABARA TANDAIMBA
WAZIRI MKUU AKIWA ZIARANI TANDAHIMBA
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa mzee Ally Hassan Mauji, katika Kata ya Nanyamba, Wilayani Tandahimba baada ya mkutano wa hadhara. Februari 28, 2018. |
Wananchi wa Kata ya Nanyamba, Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara, wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika mkutano wa hadhara, aliofanyika jana, Februari 28, 2018. |
Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, akipokea zawadi kutoka kwa mzee Ally Hassan Mauji, katika Kata ya Nanyamba, Wilayani Tandahimbabaada ya mkutano wa hadhara, kushoto ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa mzee Ally Hassan Mauji, katika Kata ya Nanyamba, Wilayani Tandahimba baada ya mkutano wa hadhara. Februari 28, 2018. |
Monday, February 26, 2018
WATAALAM WA AFYA MOJA WAJIPANGA KUDHIBITI VIMELEA HATARISHI
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi, mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018. |
Baadhi ya Wataalamu wa Afya moja wakifuatilia mkutano wa wataalamu wa
Afya moja uliojikita katika ulinzi
na usalama wa vimelea hatarishi, mjini Morogoro, tarehe 26 Februari, 2018.
|
Na. Mwandishi Maalum
Wataalam wa Afya moja nchini ambao ni wataalam wa
sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira
wamejipanga kudhibiti vimelea hatarishi kwa kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli
za vimelea hivyo .
Vimelea hatarishi vinaweza sambaza magonjwa kwa
wanyama na binadamu iwapo ulinzi na usalama wake hautaimarishwa wakati wa
kuvichukua kwa wanyama, binadamu na
mimea au
wakati wa kusafirisha vimelea hivyo na
kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi pia wakati wa kuviharibu mara baada ya
kuvifanyia uchunguzi.
Akiongea wakati
wa mkutano huo Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri
Mkuu, Bashiri Taratibu alibainisha kuwa serikali kupitia Dawati la uraribu wa Afya moja lilipo chini ya Ofisi
ya Waziri Mkuu imeamua kuandaa mpango wa kudhibiti vimelea hivyo ambavyo
husababisha magonjwa ya mlipuko na hatimaye kuleta majanga kwa jamii na
pia kamati maalum ya wataalam hao
imeundwa ili kuufatilia na kusimamia mpango huo.
“Ofisi ya Waziri Mkuu idara ya Maafa ndiyo yenye
dhamana ya kuratibu maafa kama ya
magonjwa ya mlipuko kama kimeta, Hivyo jitihada za serikali za kuwakutanisha wataalam hawa ili kuweza kuijenga jamii salama ambayo haiathiriki na magonjwa yanayotoka kwa
wanyama kwenda kwa binadamu
kupitia mpango huu.” Alisema Taratibu.
Nao waratibu wa masuala ya Ulinzi na Usalama wa
vimelea hatarishi katika wizara ya Afya na Mifugo Bw. Jacob Lusekelo na Joseph
Masambu walibainisha kuwa kuandaliwa kwa mpango wa kuzishirikisha sekta zote za
afya kutaimarisha afya za binadamu kwakuzingatia kuwa upo mwingiliano mkubwa
kati ya binadam na. wanyama.
Afya Moja ni dhana ni dhana inayojumuisha
sekta ya afya ya binadamu , wanyamapori, mifugo na mazingira katika kujiandaa , kufuatilia na kukabili magonjwa yanayoathiri binadamu
,wanyamapori na mifugo. Kwa kutambua umuhimu huo Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu
kwa kushirikiana na Shirika la DTRA wameandaa mkutano wawadau hao.