WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Bi. Theresia Mahongo
kuhakikisha kampuni zinazomilikiwa na madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo
hazipewi zabuni zinazotolewa katika maeneo yao kwa ajiliya kuepusha migongano ya kimaslahi.
Ametoa
agizo hilo leo (Jumatatu, Desemba 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa
halmashauri ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha katika ukumbi bwalo la
Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Karatu akiwa katika ziara yake ya kikazi
mkoani hapa.
"Hauzuiliwi
kufanya biashara ili mradi kampuni yako isifanye kazi katika halmashauri ambayo
wewe unaitumikia na una nguvu nayo ili kuepusha migongano ya kimaslahi kwani
miradi yote utajilundikia," amesema.
Pia
amewataka Wakuu wa Idara katika halmashauri hiyo walisaidie Baraza la Madiwani
katika kubaini vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la kuongeza mapato ya
halmashauri yao.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu
amewataka watumishi wa halmashauri wa umma kujitathmini na kujiridhisha kama wanafuata
misingi ya utumishi katika utendaji kazi wao wa kila siku. Amewasisitiza wawatumikie wananchi kwa uadilifu na uaminifu
mkubwa.
"Hatuhitaji kuwa na mtumishi
mvivu, asiyewajibika, mwizi, mla rushwa na asiyekuwa muadilifu mahali pa kazi.
Na atakayeona ameshindwa kutunza na kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi atoe taarifa hatutaki watu kufanya kazi kwa mazoea," amesema.
Na atakayeona ameshindwa kutunza na kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi atoe taarifa hatutaki watu kufanya kazi kwa mazoea," amesema.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa "
watumishi wa umma lazima mbadilike na muwe na nidhamu ya kazi. Muache
malalamiko fanyeni kazi na msitafute sympathy (huruma) kutoka kwa watu
kwani Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ," amesema.
Amesema
katika baadhi ya ofisi za Serikali kuna ugonjwa wa watumishi wanapoona wageni
wamelifika kwa ajili ya kupatiwa huduma wanawapita bila ya kuwasikiliza. "
sasa hatutaki watumishi wa namna hiyo, Jukumu lako ni kumtumikia Mtanzania na
tunataka kuona mabadiliko. Hatutaki kuona watu wakizubaa maofisini,".
Waziri
Mkuu amesema Serikali ikikuta wananchi wanalalamika kutokana na kutoridhishwa
na huduma zitolewazo na watumishi wa umma itahakikisha watumishi hao
wanachukuliwa hatua. Serikali ni ya Watanzania wote hivyo lazima wahudumiwe
vizuri bila ya kujali uwezo wao kifedha wala itikadi zao za kidini na kisiasa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.