Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu), Mhe. Jenista
Mhagama, amewataka wananchi wote kushirikiana na
kusherehekea uhuru wa Tanzania bara kwa kuunga juhudi za serikali ya awamu ya
Tano ya kupinga ufisadi na rushwa nchini.
“Kwa niaba ya serikali natoa wito kwa wananchi wote nchini kusherehekea
siku hii kwa kuwakumbuka waasisi wetu waliotetea na kutuletea Uhuru wa nchi
yetu. Aidha niwaombe wananchi wote kuunga mkono juhudi za Rais wetu Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika kuimarisha uchumi wa viwanda kwa
maendeleo ya nchi yetu” amesema Mhagama.
Kauli mbiu ya sherehe
za kutimiza Miaka 55 ya uhuru ni “Tuunge
Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa
maendeleo yetu”
Mgeni Rasmi katika
Maadhimisho hayo atakuwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na,
Kitengo cha
Mawasiliano serikalini
Ofisi ya Waziri Mkuu
TAREHE
08, DESEMBA, 2016.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.