Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mbunge wa Korogwe Vijijini,
Steven Ngonyani ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki, Mikocheni
jijini Dar es salaam akitibiwa Januari 2, 2017.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na
kumpa pole Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Steven Ngonyani (Profesa
Majimarefu) aliyelazwa katika Hospitali ya Kairuki akipatiwa matibabu.
Akiwa hospitalini hapo leo (Jumatatu, Januari
2, 2017), Waziri Mkuu amesema amefurahi baada ya kumkuta Mbunge huyo anaendelea
vizuri na kwamba afya yake inaridhisha.
Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumtakia afya
njema Mhe. Ngonyani. Amesema anaamini hivi karibuni atapona na kuruhusiwa kutoka
hospitali.
Kwa upande wake Mbunge huyo ambaye amelazwa katika hospitali ya
Kairuki iliyoko Mikocheni jijini Dar es
Salaam, amemshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kumjulia hali.
Pia amesema anaendelea vizuri na anatarajia
kwenda nchini India kwa matibabu zaidi mara taratibu zitakapokamilika.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.