*Ni kutoka Karatu-Mbulu-Haydom-Sibiti-Lalago hadi Meatu
*Nyingine ni ya kutoka Haydom hadi Katesh
*Limo pia daraja la Magara linalounganisha Mbulu na
Babati
SERIKALI
imepanga kujenga barabara mbili kuu za lami ambazo zikikamilika zitasaidia
kuunganisha mikoa mitano ya Arusha, Singida, Simiyu, Shinyanga na Manyara.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo jana (Jumatatu, Februari 20, 2017) kwa
nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Haydom na Mbulu Mjini
kwenye mikutano wa hadhara iliyofanyika wilayani Mbulu, mkoani Manyara.
Waziri
Mkuu amezitaja barabara hizo kuwa ni ya
kutoka Karatu-Mbulu-Haydom-Sibiti-Lalago- Meatu hadi Maswa yenye urefu wa km.
389 (maarufu kama Serengeti Southern Bypass) na nyingine ni ya kutoka Haydom
hadi Katesh yenye urefu wa km. 74. Pia limo
daraja la Magara linalounganisha Mbulu na Babati.
Amesema
anatambua umuhimu wa barabara hizo na kwamba kukamilika kwake kutaharakisha kuufungua
mkoa huo na kuongeza fursa za kiuchumi kwa wakazi wake.
“Fedha
kwa ajili ya upembuzi wa awali imeshatolewa na kazi imeshaanza kwa ajili ya
barabara ya kutoka
Karatu-Mbulu-Haydom-Sibiti-Lalago hadi Meatu na Maswa lakini hii ya Katesh hadi
Haydom itaombewa fedha kwenye bajeti tunayoiandaa hivi sasa.”
“Lengo letu ni kuona
hospitali ya rufaa ya Haydom inafikiwa kwa urahisi zaidi.La sivyo wagonjwa
watakaoletwa hapa watafika wakiwa hoi zaidi,” ameongeza.
Akizungumzia kuhusu
hoja ya ujenzi wa daraja la Maraga ambayo iligusiwa na wabunge wote wa mkoa huo,
Waziri Mkuu alisema: “Waheshimiwa wabunge wasemea vikali kuhusu daraja la
Maraga. Napenda kuwathibitishia kwamba Serikali imeshatoa kiasi cha sh. milioni
950 kwa ajili ya ujezi wa daraja hili muhimu ambalo linaunganisha wilaya zetu
za Mbulu na Babati.”
Akizungumzia ahadi ya
Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa barabara ya lami wa
km. 5 Haydom, km. 6 Dongobesh na km. 5 mji wa Mbulu, Waziri Mkuu alisema
analibeba suala na kulipekea kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Prof. Makame Mbarawa ili alifuatilie.
Kuhusu tatizo la maji,
Waziri Mkuu alisema Serikali imeshatoa kiasi cha milioni 200 kwa ajili ya
Mamlaka ya Maji ya Mji wa Mbulu ili wafanye utafiti wa vyanzo vya maji vya
uhakika na pia imetoa sh. milioni 300 kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya
Mbulu ili watafute maeneo ya uhakika ya kuchimba visima.
“Huku
kwenye Halmashauri vijiji ni vingi. Kwa hiyo tumetoa sh.
Milioni 300 ili watafute ni wapi wanaweza kuchimba visima virefu na vya kati
ili kuondoa tatizo hili kwa wananchi wetu. Mkurugenzi wa Halmashauri sisitiza
wataalamu wako watafute vyanzo hivina watumie fedha hizi vizuri,” alisisitiza.
Waziri
Mkuu leo anaendelea na ziara yake ya kikazi ya siku sita mkoani Manyara kwa
kutembelea wilaya ya Hanang ambako atapokea taarifa ya wilaya hiyo atazungumza
na watumishi wa umma, na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.