Na.
Mwandishi Wetu
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama ameupongeza uongozi wa mkoa wa Kagera kwa hatua iliyofikiwa
katika kurejesha miundombinu mbalimbali iliyoathiriwa na tetemeko la
ardhi lililotokea Septemba10 mwaka 2016 katika Mkoa wa Kagera linalokadiriwa kuwa na ukubwa wa 5.9 katika vipimo vya
Richter.
Mhe.
Mhagama alionesha kuridhishwa kwake baada ya kufanya ziara Mkoani hapo mapema wiki hii kwa
lengo la kutathimini utekelezaji unaoendelea katika kurejesha miundombinu
ili wananchi waendelee kutumia huduma hizo kama kawaida.
Katika
ziara hiyo, Waziri Mhagama alitembelea Shule ya Sekondari Nyakato, Ihumo na
Omumwani, Kituo cha Afya cha Kabyaile-Ishozi na Kituo cha Kulelea Wazee cha
Kiilima na kubaini kuwa ujenzi wa Kituo kipya cha Afya cha Kabyaile-Ishozi
ambacho kimefikia asilimi 80 ambapo kimetumia kiasi cha shilingi 381, 506,
079.00.
“Nikiri
kwamba ukiacha baadhi ya mapungufu kwa watendaji wachache, wengi
mmetupa ushirikiano mzuri kwa kulinganisha hali ilivyokuwa kwa kuangalia tukio
lilivyotokea na hadi hatua za kukabili hatimaye kurejesha hali.”Alisema Waziri
Aliendelea kushukuru ushirikiano mzuri uliopo katika
kutekeleza majukumu hatimaye kufikia lengo “Kama sio ushirikiano wa pamoja kati
ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Ofisi ya Mkoa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania huwenda
tusingefika hapa hivyo tuna kila sababu ya kupongeza juhudi hizi kwa niaba ya
Serikali hususani Ofisi ya Waziri Mkuu tumefarijika kwa ushirikiano wenu”
Pamoja
na pongezi hizo, Waziri alimtaka Katibu Tawala wa Mkoa Kamishna Diwani
Athuman kuendelea kuzingatia taratibu za manunuzi na kila eneo linalofanyiwa
kazi kufuata taratibu, kanunuzi zilizopo kwani kwa atakaye kiuka sheria na
taratibu hakutakuwa na msamaha.”Hakutakuwa na msamaha kwa yeyote atakayefanya
uzembe lazima sheria zichukue mkondo wake hakuna kuoneana aibu” Alisisitiza
waziri.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mhe. Deogratius Kinawilo
alipongeza kwa kukiri kuwa kazi inayoendelea ya kurejesha hali imefanyika kwa
umakini mkubwa. “Tumefanya kazi kwa umakini mkubwa na kila mmoja alikaa kwenye
nafasi yake hivyo niendelee kuwaomba watendaji wote kufuata sheria na
kutekeleza yote yanayotupasa ili kuokoa mazingira ya wanakagera kwa ujumla”
Waziri mhagama alieleza pia pamoja na jitihada zote ifike
mahali kile kilichokusudiwa kitimie na miradi yote ifikapo mwezi Mei mwaka huu imekamilika”
Tuendelee kutekeleza majukumu yetu katika zoezi la kurejesha hali ili ifikapo
mwezi Mei angalau asilimia 80 iwe imekamiliza” Alisema waziri
Ziara
hiyo ilikuwa ni moja ya utekelezaji wa maagizo ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli
aliyoyatoa wakati wa ziara yake Januari mwaka huu na kuiagiza Ofisi ya
Waziri Mkuu kufanya tathimini za shughuli zote wakati wa kukabili na urejesha
hali baada ya kutokea kwa Tetemeko hilo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.