Home
Archives for April 2017
Thursday, April 27, 2017
WAZIRI MHAGAMA AKUTANA NA UONGOZI WA SHIVYAWATA
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/27/2017 08:33:00 PM
MATUKIO PICHA BUNGENI LEO APRIL 27,2017
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/27/2017 04:04:00 PM
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa
Kahama mjini , Jumanne Kishimba kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma
Aprili 27, 2017.
|
Monday, April 24, 2017
VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUHIMIZA NIDHAMU-MAJALIWA
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/24/2017 04:20:00 PM
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaomba viongozi wa dini nchini kutumia nafasi zao kuhimiza wazazi na walezi kuishi maisha yenye nidhamu, kuthamini kazi yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu na kusimamia malezi ya watoto na kuzingatia maadili ya Taifa kwa ujumla.
“Tabia na mwenendo mzuri ni lazima uanzie katika ngazi ya familia, mtaani na hatimaye katika jamii. Tukirudia utamaduni wetu wa zamani wa kusimamia maadili kwa pamoja, jamii yetu itanusurika kwa kiwango kikubwa,” amesema.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Aprili 24,2017) wakati akifungua kongamano kuhusu mmomonyoko wa maadili na athari za dawa za kulevya lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, lililofanyika mjini Dar es Salaam.
Amesema kila mzazi au mlezi aone aibu, uchungu na ajutie anapoona mtoto yoyote akienda kinyume na utaratibu wa kawaida wa maisha na ni vema wakatumia nafasi yao kwa kuwahimiza vijana hao waishi maisha ya nidhamu na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.
Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga jamii yenye kuzingatia maadili nchini na Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli amekuwa akiwasisitizia Watanzania wote kuzingatia maadili katika jamii kwa kufanya kazi kwa bidii na kujiepusha na vitendo vyote vya rushwa na ubadhirifu.
Amesema maadili katika Taifa ni moja ya tunu muhimu kwa kuwa ndicho kichocheo kikubwa cha maendeleo, ujenzi wa umoja, amani, upendo, uvumilivu na mshikamano kwa jamii.
Amesema maadili ni nyenzo muhimu sana katika ujenzi wa Taifa na huliepusha kuingia katika mifarakano na migogoro. “Hivyo hatuna budi nasi kuyalinda maadili hayo kwa uwezo wetu wote, ili tuyarithishe kwa vizazi vijavyo, kama vile sisi tulivyoyarithi kutoka kwa waasisi wa Taifa letu,”.
“Hata hivyo, ninyi ni mashahidi kuwa katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia vitendo vya mmomonyoko wa maadili na matokeo yake yanaonekana dhahiri kama kuongezeka kwa vitendo vya rushwa, kuiga tamaduni za nchi za kigeni ambazo sio njema na hazina tija kwa jamii, na Taifa kwa ujumla”.
“Ni ukweli usiopingika kuwa mmomonyoko wa maadili ni miongoni mwa vichocheo vinavyopelekea matumizi ya dawa haramu za kulevya. Hivyo ni matarajio yangu kuwa mtaliangalia kwa kina tatizo la mmomonyoko wa maadili ambalo kwa kiasi kikubwa linatuathiri kama Taifa katika mipango ya Serikali na maendeleo ya Taifa letu,” amesema.
Hivyo Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa BAKWATA kwa kuwa na wazo la kufanya kongamano hilo lenye kulenga kujadili namna ya kurejesha maadili katika jamii. Tukumbuke kuwa Watanzania tutaendelea kuishi kwa upendo, amani na utulivu iwapo tutazingatia maadili.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa mapambano na vita dhidi ya dawa za kulevya nchini inafanikiwa. Lengo ni kuhakikisha kuwa waathirika wote wa matumizi ya dawa hizo wakiwemo vijana, ambao ndio nguvu kazi ya Taifa wanakombolewa dhidi ya janga hilo.
Amesema Serikali itahakikisha inashughulikia mtandao wa wafanyabiashara wakubwa wanaojihusisha na dawa za kulevya bila ajizi, ambapo vyombo vyote vya kisheria vimeelekezwa kushirikiana katika mapambano dhidi ya matumizi ya dawa ya kulevya kwa kusimamia sheria ipasavyo.
Naye Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Bw. Rogers Siyanga amewaomba viongozi wa dini kuiunga mkono mamlaka hiyo kwa sababu inafanya kazi kubwa ambayo inahitaji msaada wa watu wote.
Kwa upande wake Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji Abubakary Zuberi amesema viongozi wa dini nchini wana jukumu la kukataza maovu na kuiamrisha jamii kufanya mambo mema badala ya kuiachia Serikali pekee kufanya kazi hiyo.
MAJALIWA ATEMBELEA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA KUKAGUA MAADALIZI YA SHEREHE ZA MUUNGANO
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/24/2017 03:21:00 PM
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Bw.Yusto Chuma (kulia) ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Muungano wakati alipotembelea uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2017 zitakapofanyika sherehe hizo. Kushoto kwake ni Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo. |
MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO KUHUSU MMONYOKO WA MAADILI
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/24/2017 02:50:00 PM
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Alhaji Abubakary
Zuberi akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili
lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na
kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24,
2017.
|
Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani
Jafo akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili
lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na
kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24,
2017.
|
Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya, Nchini, Rogers Siyanga akizungumza katika Kongamano kuhusu Mmonyoko wa Maadili lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kufunguliwa na Waziri Mkuu, kassim Majliwa kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius, kambarage Nyerere jijini Dar es salaam Aprili 24, 2017. |
MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO KUHUSU MMONYOKO WA MAADILI
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/24/2017 01:16:00 PM
Saturday, April 22, 2017
WAZIRI MHAGAMA: MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO YAKAMILIKA
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/22/2017 12:34:00 PM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameeleza kukamilika kwa maandalizi ya kuadhimisha sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika Viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma, siku ya jumatano Aprili 26, 2017.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Aprili 22, 2017 katika Ofisi yake Dodoma.
“Nipende kuwaeleza Watanzania wote kuwa hadi sasa maandalizi ya kuifikia siku ya Maadhimisho ya Sherehe za Muungano tayari yamekamilika kwa kuangalia mambo yote yaliyopangwa katika ratiba ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.”Alisema Waziri Mhagama.
Amesema sherehe hizo zitakuwa na upekee wa aina yake ukizingatia kuwa ni mara ya kwanza tangu Serikali ilipotimiza adhma yake ya kuhamia Dodoma.
Akitaja upekee huo, Waziri Mhagama amesema sherehe hizo zitapambwa na Gwaride la heshima lililoandaliwa na Vikosi vya Ulinzi na Usalama, Maonesho ya Kikosi cha Makomando, Onesho la Mbwa na Farasi waliofunzwa, onesho la Ukakamavu la Uzalendo la Wanafunzi kutoka shule za Sekondari za Dodoma, burudani za vikundi vya ngoma kutoka Kaskazini Pemba pamoja na Bendi ya mziki wa kizazi kipya kutoka Dodoma, Yamoto Bend na Mwenge Jazz.
“Ikumbukwe hii itakuwa mara ya kwanza kuiadhimisha sherehe hii ya Miaka 53 ya Muungano wetu kwa kuzingatia Serikali sasa imeshahamia Dodoma na tayari Watendaji wake wapo huku hivyo tuitumie fursa hii kuwaalika Wananchi wote kuudhuria kwa wingi ili kuifanikisha na kuonesha Umoja wetu.”Alisistiza Waziri.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) January Makamba ametoa wito kwa Watanzania wote wajitokeze kwa wingi kwenda kuangalia mafanikio yaliyotokana na uwepo wa Muungano huo.
“Muungano huu umetupa mafanikio mengi ikiwemo; kuijengea nchi heshima, kuwepo kwa Katiba, kuimarika kwa Taasisi za kimuungano, ongezeko la masuala ya kimuungano kutoka 11 hadi 22, ongezeko la usalama, Kuwepo Mfumo dhabiti wa kushughulikia changamoto za Muungano na ongezeko la ushirikiano kwa masuala yasiyo ya Kimuungano.”Alieleza waziri Makamba.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana alipongeza jitihada za Ofisi ya Waziri Mkuu hususan Kitengo cha Maadhimisho kwa kushirikiana na Ofisi yake kwa kuratibu na kuhakikisha maandalizi yote yamekalika kwa wakati uliopangwa.
“Niipongeze Ofisi ya Waziri Mkuu kwa jitihada zake kuiratibu siku hii muhimu kwa Taifa letu, na nitoe wito kwa Wakazi wa Dodoma na walioko nje ya Mji kuonesha mfano kuja kwa wingi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.”Alisisitiza Mhe.Rugimbana.
WAZIRI MHAGAMA: MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO YAKAMILIKA
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/22/2017 12:28:00 PM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akieleza mafanikio ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa maandalizi ya maadhimisho ya sherehe za Muungano Mjini Dodoma.
|
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho Bi. Flora Mazeleng’we wakifuatilia mkutano wa Waandishi wa habari ulioratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu katika maandalizi ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma. |
Friday, April 21, 2017
MAPOKEZI YA MWILI WA MAREHEMU DR ELLY MACHA BUNGENI LEO APRILI 21,2017
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/21/2017 06:16:00 PM
WAZIRI MKUU AUNGANA NA WABUNGE KUUAGA MWILI WA DKT. ELLY
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/21/2017 05:57:00 PM
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoa salamu za Serekali katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma 21/04/2017 wakati wa shughuli ya kuaga Mwili wa Maerehemu Mheshimiwa Dr Elly Marko Macha ambaye alifariki Nchini Uingereza alipokuwa katika matibabu. |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa mkono wa pole Glory Haika Peter (24) ambaye ni Mtoto wa Maerehemu Mheshimiwa Dr Ell Macha Mbunge viti Maalumu Chadema ,Wakati wakusindikiza Mwili wa marehemu katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma 21/04/2017
|
WAZIRI MKUU AUNGANA NA WABUNGE KUUAGA MWILI WA DKT. ELLY
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/21/2017 05:28:00 PM
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wabunge katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Dkt. Elly Macha aliyefariki Machi, 31, 2017 katika hospitali ya New Cross Wolverhampton nchini Uingereza.
Akizungumza katika tukio hilo Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia marehemu pamoja na wabunge wote.
Waziri Mkuu amesema enzi ya uhai wake marehemu Dkt. Elly alitoa mchango mkubwa na ushauri mzuri katika masuala ya elimu na uboreshaji wa maeneo ya watu wenye ulemavu.
Awali akisoma wasifu wa marehemu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa alisema Dkt. Elly alipata ulemavu wa macho akiwa na umri wa miezi mitano baada ya kuugua ugonjwa wa surua.
Mchungaji Msigwa alisema pamoja na kuwa na ulemavu huo wa macho lakini haukuwahi kuwa kikwazo kwake kwani aliweza kufanya jambo lolote lililokuwa ndani ya uwezo wake.
Mwili wa marehemu Dkt. Elly umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha na anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.
Dkt. Elly alizaliwa Juni 18, 1962 kwenye kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro, ambapo mbali na wadhifa wa ubunge pia aliwahi kuwa Mshauri Mwelekezi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu vya Afrika Mashariki.
MABALOZI WA TANZANIA KUTANGAZA FURUSA ZA UWEKEZAJI
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/21/2017 01:43:00 PM
MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO-DODOMA.
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/21/2017 12:12:00 PM
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana akizungumza wakati wa maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri Dodoma Aprili 21, 2017. |
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Muungano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani) wakati wa maandalizi ya sherehe hizo Aprili 21, 2017 Dodoma. |
WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA LOLIONDO
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/21/2017 10:11:00 AM
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea Taarifa ya Kamati Shirikishi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Mrisho Gambo ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo mkoani Arusha, ambapo atatoa maelekezo baada ya kuisoma.
Amepokea taarifa hiyo leo (Alhamisi, Aprili 20, 2017) katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa Spika, Bungeni mjini Dodoma. Aliiunda Kamati hiyo, Desemba mwaka jana, mara baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Arusha.
Kiini cha mgogoro huo ni eneo la pori tengefu la Loliondo ambalo linagombewa na wawekezaji, wakulima, wawindaji kwa sababu ni mapitio ya wanyama, chanzo cha maji, mazalia ya wanyama, malisho ya mifugo na makazi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Tate William Ole-Nasha, viongozi wa mkoa wa Arusha, wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
Wengine ni Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Bw. Rashid Taka, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa wa Arusha na wilaya ya Ngorongoro, wawakilishi wa wananchi, wawekezaji na asasi za kiraia ambao wote walishiriki katika uandaaji wa taarifa hiyo.
Waziri Mkuu amesema lengo la kamati hiyo ni kutaka kupata muafaka wa matumizi ya rasilimali zilizoko katika eneo hilo ili kila upande uweze kutekeleza majukumu yake bila ya kuathiri mwingine na kuwezesha wananchi wote kunufaika na rasilimali zilizoko katika eneo hilo.
“Serikali inataka watu wote tuwe kitu kimoja katika kutunza maeneo yetu, lakini pia shughuli za wananchi nazo ziweze kuendelea ili Watanzania wote tuweze kunufaika na rasilimali zilizoko kwenye maeneo yetu,” amesema.
Waziri Mkuu amesema Serikali inapenda kuona maeneo yote nchini yakiwa katika hali ya utulivu bila ya kuwepo kwa migogoro ya aina yoyote na ikitokea ni vema ikawa inapatiwa ufumbuzi kwa wakati ili shughuli za maendeleo ziweze kufanyika kwa ufasaha.
Thursday, April 20, 2017
MAJALIWA APOKEA TAARIFA YA KAMATI YA MGOGORO WA LOLIONDO
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/20/2017 05:01:00 PM
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuhusu ramani ya pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumishi ya ardhi kwenye pori hilo. Taarifa hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Spika mjini Dodoma Aprili 20, 2017. |
WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUIAMINI SERIKALI-MAJALIWA
✔
OFISI YA WAZIRI MKUU
4/20/2017 04:45:00 PM
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisikiliza swali wakati alipoulizwa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, bungeni mjini Dodoma, Aprili 20, 2017. |
* Asisitiza vyombo vya dola vipewe muda wa kufanya uchunguzi wa matukio ya kihalifu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuendelea kuiamini Serikali yao na kuvipa muda vyombo vya dola kuendelea kufanya uchunguzi dhidi ya matukio mbalimbali ya kihalifu yaliyotokea nchini ili kubaini chanzo cha matatizo na wahusika.
Aidha, Waziri Mkuu ametoa wito kwa Watanzania wote kuendelea na utamaduni wa kushirikiana na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa pindi vinapotokea vitendo vya kihalifu au viashiria vyake katika maeneo mbalimbali nchini.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Aprili 20, 2017) Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe aliyetaka kupata kauli ya Serikali juu ya hofu iliyotawala nchini kuhusu vitendo vya watu kuuliwa, kupotea na kutekwa.
Waziri mkuu amesema
“tukitoa taarifa mapema tunaweza kuharibu upelelezi, tuviachie vyombo vetu vya dola viendelee kufuatilia kuona nani anayesababisha vitendo hivyo na dosari iko wapi na nini chanzo chake alisisitiza,”.
Kadhalika Waziri Mkuu amewasii Watanzania kuendeleza utamaduni mzuri wa watu kuheshimiana, kufuata kanuni na kuviachia vyombo vya dola kutekeleza majukumu yake. “Moja ya majukumu ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wanaishi kwa amani kwa kuwa na ulinzi wa uhakika kwao wenyewe na mali zao wakati wote,”.
Hata hivyo, Mheshimiwa Mbowe aliishauri Serikali kushirikiana na vyombo vya kiuchunguzi vya kimataifa kuchunguza tukio la kupotea kwa msaidizi wake Ben Saanane lililotokea miezi sita iliyopita, ambapo Waziri Mkuu amesema kuwa Taifa lina mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali na inashirikiana nayo katika mambo mbalimbali likiwemo suala ya ulinzi ambapo si rahisi kuainisha namna wanavyoshirikiana.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa vyombo vyetu vina weledi,vifaa na uwezo wa kutosha kufanya uchunguzi juu mambo yanayotokea nchini hivyo amesisitiza wananchi kuendelea kuiamini kwani matukio haya ya kihalifu likiwemo la mtu kutoweka au kufariki na haina kikomo cha uchunguzi, mara zote uchunguzi unategemeana na aina ya tukio lenyewe au mazingira lilipo tokea
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali inafanya mapitio kwa vyama vyote vya Ushirika nchini kufuatia baadhi ya vyama hivyo kuwa na mwenendo mbaya hali inayochangia upotevu wa fedha nyingi na kukatisha tamaa wakulima.
Amesema hivi karibuni katika kikao cha wadau wa zao la korosho kilichofanyika wilayani Bagamoyo Bodi ya Korosho ilidaiwa kuhusika na ubadhilifu wa sh. bilioni 30 ambapo Serikali iliunda timu maalumu ya uchunguzi na kubaini upotevu wa sh. bilioni sita na siyo sh. bilioni 30.
Hata hivyo amesema kwamba hasara hiyo ya sh. bilioni sita haikusababishwa na bodi bali vyama vikuu na vya ushirikika vilivyopo kwenye ngazi ya Kata na wilaya, ambavyo vyote vilifanyiwa uchuguzi na hatua zimeanza kuchukuliwa.
Amesema matatizo hayo yako katika vyama vyote vya ushirika hususan vya mazao ya Tumbaku, Kahawa,Pamba, Chai na mazao mengine makuu, ambapo Serikali imeanza kupitia taarifa za ukaguzi kwa kina ili iweze kufanya ukaguzi na sasa wanaendelea na uchunguzi wa chama kikuu cha tumbaku.
Waziri Mkuu amesema wakimaliza kufanya uchunguzi katika chama kikuu cha tumbaku watachunguza vyama vingine vya pamba, kahawa na chai lengo likiwa ni kuwalinda wakulima na kuhakikisha wanapata tija.
“Naomba kusisitiza hatua zinaendelea kuchukuliwa na tutaendelea kuimarlisha na ushirika,”.
Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mheshimiwa Mama Salma Kikwete aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuhusu ubadhirifu wa sh. bilioni 30 uliofanywa na Bodi ya Korosho
Subscribe to:
Posts (Atom)
MITANDAO YA KIJAMII
Popular Posts
-
Na. OWM, Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 y...
-
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama...
-
Na. OWM, ARUSHA Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri...
-
Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara w...
-
TAMOBA wafanya wasilisho la mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama wa Bodaboda na BajajiKampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa ...
Formulir Kontak
Contributors
Powered by Blogger.