Na. OWM, Dodoma.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 ya Mwaka 2003, ya Usalama na Afya mahali pa kazi, ambapo maeneo 1,187 yalikaguliwa na kusajiliwa na Idara na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo , Idara ya kazi, OSHA, NSSF, PSSSFna WCF, ili kuhakikisha wafanyakazi nchini wanakuwa ni wenye afya na wanakuwa na mahali pa kazi salama.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 ya Mwaka 2003, ya Usalama na Afya mahali pa kazi, ambapo maeneo 1,187 yalikaguliwa na kusajiliwa na Idara na Taasisi za Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwemo , Idara ya kazi, OSHA, NSSF, PSSSFna WCF, ili kuhakikisha wafanyakazi nchini wanakuwa ni wenye afya na wanakuwa na mahali pa kazi salama.
Akiongea, Jijini Dodoma, wakati wa
kupokea ripoti ya ukaguzi huo kwenye Kikao na Wakuu wa Idara na Taasisi za Ofisi hiyo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye
Ulemavu), Andrew Massawe amefafanua kuwa ukaguzi huo ni muhimu kwa kuwa kuwekeza kwenye Afya na Usalama kazini
kunasaidia kuzuia madhara kwa
wafanyakazi na kuilinda nguvu kazi muhimu kwa Taifa letu.
Aidha, Katibu Mkuu, Massawe
amefafanua kuwa iwapo sheria Na.5 ya Mwaka 2003, ya Usalama na
Afya mahali pa kazi itatekelezwa ipasavyo itasaidia kuleta hamasa na ari ya
kufanya kazi kwa bidii miongoni mwa wafanyakazi, kuimarisha mahusiano mazuri na
jamii, kuongeza ubora wa bidhaa au huduma inayotolewa na wizara, Idara za serikali , kampuni au taasisi husika.
Ameongeza kuwa
ameipokea ripoti hiyo ambayo itamsaidia kuweka mikakati ya kuzuia vihatarishi
vinavyoweza kujitokeza ili kuweza kuzuia wafanyakazi wasiweze kupata ajali na magonjwa
yatokanayo na kazi.
“Ni vyema waajiri na
wafanyakazi na umma kwa ujumla kushirikiana na serikali katika ukaguzi wa utekelezaji
wa sheria hii ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi, ili tuweze kuimarisha afya na usalama kazini
na mstakabali wa kazi, kwa kuwa tayari serikali tumefanya juhudi katika kuboresha mazingira ya kazi na
kuweka mifumo ya afya na usalama kazini iliyo imara na inayoleta tija katika
sehemu za kazi” amesisitiza Massawe.
Katika kuhakikisha
kuwa nchi inapunguza au kuondoa vifo, ajali, magonjwa na madhara
yatokanayo na kazi, mnamo mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu ulifanyika ukaguzi
wa utekelezaji wa sheria Na.5 ya Mwaka 2003,
ya Usalama na Afya mahali pa kazi nchini kwa kuhusisha Idara na
taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo.
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana,
Ajira na Watu wenye Ulemavu ndio yenye jukumu la kuboresha na kusimamia Usalama
na Afya mahali pa Kazi kupitia Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA).
Wakala huo ulianzishwa mnamo tarehe 31 Agosti, 2001 chini ya Sheria ya Wakala
za Serikali Na. 30 ya mwaka 1997, ambapo miongoni mwa majukumu yake ni Kusimamia
Utekelezaji wa Sheria hiyo ili kuweza kuongeza tija na uzalishaji mali hivyo kukuza pato la
taifa
MWISHO.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.