Thursday, December 27, 2018

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA MJI WA SERIKALI


*Akuta baadhi ya wakandarasi wanasuasua, wengine wako vizuri
*Aitisha kikao cha Mawaziri, Makatibu Wakuu wote kesho saa 5 asubuhi
*Ataka leo jioni apewe taarifa ya kila taasisi inayohusika Ihumwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekagua ujenzi wa eneo la Mji wa Serikali lililoko Ihumwa na kubaini kuwa baadhi ya wakandarasi hawaendi na kasi inayotarajiwa na Serikali.

Waziri Mkuu ameamua kuitisha kikao cha Mawaziri wote na makatibu wakuu wote kesho (Ijumaa) saa 5 asubuhi ili waeleze kazi hiyo itakamilishwa lini.

Ametoa agizo kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Desemba 27, 2018) mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za wizara zote pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo la Mtumba lililoko km. 17 kutoka jijini Dodoma.

“Nimekagua maeneo yote na kukuta baadhi ya wakandarasi wanatakiwa kujenga majengo ya wizara nne hadi tano. Sijaridhika na baadhi ya kazi, nimeitisha kikao cha Mawaziri wote kesho ili tuangalie ni mkandarasi yupi anaweza kumudu hii kazi.”

“Nimebaini kuna tatizo kubwa la upatikanaji wa vifaa vya ujenzi kama kokoto, nondo, matofali na kikao cha kesho kitahusisha Mawaziri, Makatibu Wakuu, viongozi wa Mkoa na Jiji la Dodoma, wakandarasi wote ili tukubaliane kazi hii inaisha lini,” amesema.

Akitoa mfano, Waziri Mkuu amesema wajasiriamali wanaotengeza matofali Dodoma wako wengi lakini matofali tyao yako chini ya kiwango, kwa hiyo wanatakiwa watu wa kutengeneza matofali mengi yenye uimara. “Tuna ujenzi wa wizara 24, tunataka matofali imara siyo yale ambayo ukilishika tu, mchanga unamomonyoka,” amesisitiza.

Akisisitiza uharaka wa kazi hiyo, Waziri Mkuu amesema kazi hiyo ina malengo maalum na inatakiwa ikamilike haraka sana. “Tarehe ya mwisho ya kukamilisha ujenzi iliyotolewa na Mheshimiwa Rais ilikuwa Desemba 31, mwaka huu lakini kuna sababu zimetajwa kukwamisha ujenzi huo zikiwemo mvua na uhaba wa kokoto,” amesema.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesifia kazi nzuri iliyofanywa kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Utumishi, Ujenzi, Katiba na Sheria, Maji na Elimu. Kazi hizo zimefanywa na wakandarasi ambao ni Magereza, SUMA JKT, Wakala wa Majengo (TBA) na Vikosi vya Ujenzi vya Mwanza na Dar es Salaam vilivyoko chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Wakandarasi walioboronga ni JWTZ – Mzinga, National Housing na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Waziri Mkuu amemwagiza Katibu wa Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma, Bw. Meshack Bandawe ahakakishe anapokea taarifa kutoka kila taasisi inayohusika na ujenzi huko Ihumwa na akishaijumuisha, aiwasilishe kwake ifikapo leo jioni.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi ashirikiane na Mkurugenzi wenzake wa Chamwiono kuhakikisha vijana wengi wanapata fursa za ajira kwenye mradi huo.

“Mkurugenzi wa Jiji wasiliana na Mkurugenzi mwenzako wa Chamwino mhakikishe vijana na akina mama wanakuja kufanya kazi hapa. Pia itisha kikao cha waandishi wa habari uwaeleze wananchi wako fursa zilizopo, kuanzia ufyatuaji wa matofali, uuzaji wa nondo, kokoto na utengenezaji wa pavement blocks, hizi zote ni fursa, tuna wizara 24 na mahitaji ni makubwa,” alisisitiza.

Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Bw. Anthony Mavunde alisema zoezi la kusafisha eneo la ujenzi wa mji wa Serikali lilianza Novemba 28, mwaka huu.

Alisema wizara zote zimepata viwanja na zimeanza ujenzi isipokuwa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana) ambao bado wanasubiri kupatiwa fedha.

Alisema kazi ya ujenzi wa Mji wa Serikali inasimamiwa na Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma.
Read More

Thursday, December 20, 2018

MAJALIWA AKISALIMIANA NA KATIBU MKUU WA CCM BASHIRU NA SPIKA WA BUNGE NDUGAI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,  Dkt. Bashiru Ali na Spika wa Bunge, Job Ndugai  (kushoto)  wakati alipowasili kwenye eneo la Uwekaji Jiwe la Msingi la Mradi wa  Daraja na Barabara Unganishi toka Aga Khan hadi Coco Beach jiijni Dar es salaam, Desemba 20, 2018. Jiwe hilo la Msingi liliwekwa na Rais, Dkt, John Pombe Magufuli.

Read More

Tuesday, December 18, 2018

WAZIRI MHAGAMA; BILIONI 16 ZIMETUMIKA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KIGOMA NA DODOMA.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Biashara Manispaa ya Kigoma Ujiji, Festo Nashoni, juu ya Uboreshaji wa chanja za kuanika dagaa katika mwalo wa Soko la samaki la Kibirizi wakati akikagua shughuli za Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza mfanyabiashara, Justina Damas,  Soko la Jioni la Mwanga mkoani Kigoma, ambalo limeboreshwa na Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji,  tarehe 17 Desemba, 2018

Na. OWM, Kigoma.
Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Biashara, kupitia Mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji unaotekelezwa katika mkoa wa Kigoma na Dodoma, umefanikiwa kuboresha Mazingira ya Biashara na uwekezaji katika mikoa hiyo kwa kutumia  kiasi cha Shilingi bilioni 16 hadi kufikia Desemba 2018.

Mradi huo ambao utekelezaji wake unajikita katika Uwekezaji na Biashara katika Halmashauri kupitia mfuko wa (SIFF), Kuimarisha minyororo ya thamani pamoja na kuimarisha majadiliano kati ya Serikali na Sekta Binafsi, tayari umefanikiwa kuboresha Mazingira ya Biashara kwa Wakulima na wavuvi wa mkoani Kigoma. 

Akiongea katika ziara yake mkoani Kigoma wakati wa kukagua shughuli za utekelezaji za Baraza la Taifa la Biashara, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu), Jenista Mhagama amefafanua kuwa Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana na Mradi huo wameweza Kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia uwekezaji kwenye miradi midogo midogo inayochochea ongezeko la ajira na kipato.

“Nimetembelea Mwalo na Soko la Samaki la Kibirizi, hapa mkoani Kigoma nimeridhishwa jinsi Mradi huu ulivyoboresha miundo mbinu ya mwalo huu katika kuhakikisha wavuvi wanapunguza upotevu wa mazao ya samaki na dagaa. Niyaombe Mabaraza ya Biashara ya Mikoa na Wilaya yaendelee na mfumo wa majadiliano kati ya serikali na sekta binafsi ili kuhakikisha walengwa wa mradi huu wanaendelea kunufaika” Alisisitiza Mhagama.

Mhagama alifafanua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Biashara ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amekuwa akisisitiza kupunguza vikwazo na kero kwa wafanyabiashara lakini pia Kuimarishwa kwa mahusiano kati ya Serikalii na Sekta Binafsi na kuongezeka kwa  ushirikishwaji wa Sekta Binafsi katika Mipango ya Serikali.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo, Mratibu wa Mradi (Masuala ya Majadiliano ya Sekta ya Umma na Binafsi), Andrew Mhina alibainisha kuwa Mradi huo unalenga kuhakikisha kuwa unaboresha mazingira ya Biashara na  uwekezaji nchini tayari umeandaa mwongozo wa Majadiliano Kati ya Serikali na Sekta Binafsi ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kuyajengea uwezo Mabaraza ya Mikoa yaweze kuwa endelevu na yenye ufanisi ambapo Baraza la Taifa la Biashara kwa kushirikiana.

Katika ziara hiyo, Waziri Mhagama, pamoja na kutembelea mwalo wa soko la Samaki la Kibirizi waziri alitembelea Kituo cha Biashara (One Stop Business Centre – Kigoma), Soko la Jioni la Mwanga, na Mradi wa Kuwezesha Vijana Kushiriki katika Kilimo Biashara na Mnada wa Mifugo Buhigwe.

MWISHO.

Read More

Saturday, December 15, 2018

WAZIRI MKUU AZINDUA TANZANIA SAFARI CHANNEL


*Awataka waliopewa dhamana wazingatie viwango vya kimataifa

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amezinduaChaneli ya Taifa ya Utalii iitwayo Tanzania Safari Channel na amewataka watu wote waliopewa dhamana ya kuiendesha wahakikishe wanazingatia viwango vya kimataifa katika vipindi watakavyokuwa wanaviandaa. 

“Vipindi vyenu ni lazima vivutie kama vile tunavyoviangalia katika chaneli za wanyama za kimataifa kama vile National Geographic, Discovery, Travel na zingine ili lengo lililokusudiwa wakati wa kuanzishwa kwake litime.”

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Desemba 15) wakati akizindua chaneli hiyo kwenye Ofisi za TBC, Mikocheni, jijini Dar es Salaam, ambapo ametoa wito kwa Wizara zote zinazohusika na uanzishwaji wa Chaneli hiyo kuhakikisha zinailea wakati ikijijenga kujiendesha kibiashara.

Amesema Tanzania ni moja ya nchi duniani zilizotenga moja ya tatu ya eneo lote la nchi kwa ajili ya uhifadhi, ambapo kuna tamaduni za makabila mbalimbali, ngoma za kuvutia, vyakula vya asili, sinema za maisha yetu na lugha adhimu ya Kiswahili.

“Hivyo, kwa kuanzishwa kwa chaneli hii inayotengeneza vipindi na kuonesha vivutio hivi ndani na nje ya Tanzania itasaidia watalii huko waliko kujua huu utajiri wetu na kuchagua kuja kutalii nchini. Ni matumaini yangu kuwa hii Tanzania Safari Channel ninayoizindua leo itaongeza thamani katika kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea Tanzania.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametaja faidazinazotokana na utalii ambazo ni pamoja na kuliingizia Taifa fedha za kigeni, ambapo kiasi cha Dola za Kimarekani bilioni 2.3 zimeingia kwa mwaka 2017. Fedha hizo ni sawa na sh. trilioni 5.04.

Pia sekta hiyo ya utalii inatoa ajira kwa Watanzania zaidi ya milioni 1.5 wanaojihusisha katika shughuli mbalimbali zikiwemo usafiri wa ndani kwa watalii, uongozaji watalii kwenye maeneo yenye vivutio, kuuza bidhaa kwa watalii kama vyakula, vinywaji, vinyago, nguo, zawadi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema licha ya mafanikio hayo, lakini hatupaswi kuridhika nayo kwani Tanzania inapokea watalii milioni 1.3 kwa mwaka wakati nchi kama Misri na Afrika Kusini hupokea zaidi ya watalii milioni 10. 

“Lazima tujiulize, ni kwa nini sisi tulio na vivutio vingi kuanzia hifadhi maarufu ya Serengeti, Ngorongoro, Mlima Kilimanjaro, hifadhi ya Ruaha, Sadani (Hifadhi pekee iliyopakana na bahari), Zanzibar ambako  kuna fukwe maridadi, malikale, maporomoko ya maji na vingine vingi na baadhi ya hivi vivutio vimewekwa katika kundi la maajabu ya Dunia tunapata watalii wachache.”

Aidha, Waziri Mkuu amesisitiza kuhusu uboreshwaji wa bustani katika barabara inayotokea Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, ambapo amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isac Kamwelwe asimamie jambo hilo pamoja na matangazo yanayowekwa katika barabara hiyo yaoneshe vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Kadhalika uzinduzi huyo ni utekelezwaji wa maagizo ya Rais Dkt. John Magufuli aliyoyatoa Mei 16 mwaka jana alipotembea TBC kuwa, pamoja na mambo mengine aliwataka waangalie uwezekano wa kuanzisha chaneli itakayotangaza hifadhi na vivutio vya utalii nchini.

Pia Uzinduzi wa Chaneli hiyo ya utalii ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM Ibara ya 29 iliyoielekeza Serikali kuweka mkakati wa kimataifa wa utangazaji wa utalii ili kuwavutia watalii wengi zaidi na kufikia idadi ya 2,000,000 ifikapo mwaka 2020.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Khamis Kigwangala. Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isac Kamwelwe pamoja na maafisa wengine wa Serikali.
Read More

MAJALIWA AZINDUA CHANELI YA TANZANIA SAFARI YA TBC


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya kuzindua Chaneli ya Tanzania Safari Chanmnel Kwenye viwanja vya TBC,  Mikocheni jijini Dar es salam, Desemba 15, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel kwenye  Viwanja vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam Desemba 15, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, wapili kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel kwenye  Viwanja vya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jijini Dar es salaam Desemba 15, 2018.  Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Ryoba.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipozindua Chaneli ya  Tanzania Safari Channel kwenye viwanja vya Ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Mikocheni jijini Der es slaaam, Desemba 15, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Upendo Mbele wakati alipotembelea Studio mpya za TBC kabla ya kuzindua chaneli ya Tanzania Safari Channel, Desemba 15, 2018. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC,  Dkt. Ayoub Ryoba. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipoowasili kwenye Viwanja vya Ofisi za Shirika la Habari Tanzania (TBC), Mikocheni jijini Dar es salaam kuzindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel,  Desemba 15, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wakati alipowasili kwenye viwanja vya TBC, Mikocheni jijini Dar es salaam, kuzindua Chaneli ya Tanzania Safari Channel, Desemba 15, 2018.



Read More

Wednesday, December 12, 2018

MAJALIWA AMPOKEA WAZIRI MKUU WA MISRI, DKT. MOSTAFA MADBOULY

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkaribisha Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly ambaye aliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Desemba 11, 2018 kwa ziara ya siku mbili nchini.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na  Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly ambaye aliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Desemba 11, 2018 kwa ziara ya siku mbili nchini.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri Mkuu wa Misri, Dkt. Mostafa  Madbouly kwenye hoteli ya Hyyat Regency  jijini Dar es salaam, Desemba 12, 2018.

Read More

WAZIRI MKUU WA MISRI DKT. MOSTAFA MADBOULY AONDOKA NCHINI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Waziri Mkuu  wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly  kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaa wakati mgeni huyo  alipoondoka nchini kurejea nyumbani, Desemba 12, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Waziri Mkuu  wa Misri, Dkt. Mostafa Madbouly  kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaa wakati mgeni huyo  alipoondoka nchini kurejea nyumbani, Desemba 12, 2018

Read More

Friday, December 7, 2018

WAZIRI MKUU AWATOA HOFU WAKULIMA WA KOROSHO


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewatoa hofu wananchi hususan wakulima wa korosho nchini baada ya kuwahakikishia kuwa korosho zao zote zitanunuliwa.
Amesema Serikali kupitia Bodi ya Mazo Mchanganyiko itanunua korosho zote na hakuna korosho za wakulima nchini ambazo zitabaki bila ya kununuliwa.
Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha korosho cha Terra akiwa njiani kwenda Dodoma.
Waziri Mkuu amesema bodi hiyo inaendelea kufanya thamini na kujiridhisha kama kweli korosho hizo zimezalishwa nchini na kuangalia viwango vya ubora.
Amesema baada ya kujiridhisha kuhusu viwango vya ubora na mkulima aliyepeleka ndiye mwenyewe ndipo taratibu za malipo hufanyika.
Waziri Mkuu amesema Serikali iliamua kununua korosho baada ya wafanyabiashara kutaka kuzinunua kwa bei ya chini ambayo haikuwa na tija.
“Lengo la Serikali ni kuhakikisha mkulima ananufaika na ndipo Rais Dkt. John Magufuli alisitisha ununuzi baada ya kuona wakulima wanataka kudhulumiwa.”
Waziri Mkuu amesema kuwa hadi sasa tayari tani 181,000 zimeshakusanywa, hivyo amewataka wakulima wa zao hilo nchini waendelee kuiamini Serikali yao.
Kadhalika, Waziri Mkuu ameupongeza uongozi wa kiwanda hicho kwa kuunga mkono jitihada za Serikali kukuza uchumi kwa kupitia sekta viwanda.
Awali, Meneja Utawala wa kiwanda cha Terra, Peter Ngwale alisema uwezo wao ni kubangua tani 6,000 kwa mwaka, ambapo tayari wamebangua tano 3,000.
Pia aliiomba Serikali iwasaidie katika suala la ubora wa korosho kwa kuwa kiwango cha ubora kinachoandikwa kinakuwa tofauti na uhalisia wa korosho  yenyewe.

 (mwisho)
Read More

WAZIRI MKUU AMUAGIZA SIMBAKALIA AFUATILIE KIBALI WIZARA YA ARDHI


*Ni cha ujenzi wa kiwanda cha nyuzi Chalinze

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, George Simbakalia afuatilie Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu kibali cha ujenzi wa kiwanda cha nyuzi kinachotakiwa kujengwa Chalinze.
Ametoa agizo baada ya Mkuu wa mkoa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo kumuleza kuwa kuna muwekezaji wa kiwanda cha kutengeneza nyuzi cha H and J cha Chalinze ambacho ujenzi wake umekwama kutokana na mwekezaji kutopewa kibali cha ardhi.
Waziri Mkuu ametoa agzo hilo leo (Ijumaa, Desemba 7, 2018) alipozungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani akiwa njiani kwenda jijini Dodoma.
Waziri Mkuu amesema ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria kuwaunga mkono wawekezaji na kuwafanya wawekeze bila ya urasimu, hivyo amemuagiza kiongozi huyo wa EPZA kuhakikisha kibali kinapatikana.
“Nakuagiza Mkurugenzi ufuatilie kibali hicho na nikifika Dodoma nipate majibu. Hatuwezi kuchelewesha uwekezaji nchini kwa ajili ya urasimu, kila mtendaji ahakikishe anatekeleza majukumu yake ipasavyo.”
Akizungumzia kuhusu uwekezaji katika sekta ya viwanda kikiwemo na kiwanda cha Twyford, Waziri Mkuu amesema uwekezaji huo unafaida kubwa kwani licha ya mapato ya Taifa kuongezeka kupitia kodi pia wananchi wananufaika kwa kupata ajira
Kadhalika, Waziri Mkuu amesema faida nyingine itokanayo na ujenzi wa viwanda ni pamoja na kutatua changamoto ya masoko ya mazao iliyokuwa ikiwakabili wakulima kwa muda mrefu, hivyo Serikali itaendelea kuhamasisha wawekezaji wengi zaidi.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametembelea mradi wa kiwanda cha matunda cha Sayona kilichopo katika kijiji cha Mboga, Chalinze mkoani Pwani na kusema kuwa uwekezaji huo unatija kwa kuwa wakulima wamepata eneo la kuuzia matunda yao.
Waziri Mkuu amesema kwa muda mrefu wakulima wa matunda mbalimbali kama mananasi, maembe katika mkoa wa Pwani na maeneo ya jirani walikuwa hawana soko la uhakika kwa ajili ya kuuzia matunda yao na kusababisha mengi kuharibika.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amewataka wananchi waliopata kazi katika viwanda mbalimbali wawe mabalozi wazuri kwa Taifa na wafanye kazi kwa bidii na uadilifu ili kuviwezesha viwanda hivyo viendelee na uzalishaji na wengine wapate ajira.
Kwa upande wake,Msaidizi wa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Motisun Group, Aboubakary Mlawa amesema kiwanda cha matunda cha Sayona kimeajiri watumishi 470 kwa sasa huku matarajio ikiwa ni kuajiri watumishi 800.
Amesema licha ya ajira hizo pia mradi huo unawanufaisha wakulima zaidi ya 30,000 kutoka wilayani Bagamoyo kilipo kiwanda pamoja na maeneo mengine yanayolima matunda nchini kwani huuza matunda yao kiwandani hapo.
Akizungumzia kuhusu ujenzi wa mradi huo, Mlawa amesema umegharimu dola za Marekani milioni 55.5, pia kampuni ilitumia sh. milioni 500 kwa ajili ya uwekaji wa umeme mkubwa, uingizaji wa maji pamoja na ujenzi wa barabara kiwandani hapo.
Amesema kiwanda kina uwezo wa kusindika tani 18 za matunda kwa saa kwa line mbili ambazo tayari zimefungwa ila mpango wao ni kuongeza line zingine mbili ambazo zitakuwa na uwezo wa kusindika tani 48 kwa saa, hivyo kiwanda kuweza kusindika tani 66 kwa saa.


(mwisho)
Read More

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA MARUMARU CHA KEDA KILICHOPO CHALINZE


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani, Desemba 7, 2018.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zaynab Kawawa na wapili kukhoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho,Tony Zhifan.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama marumru aina ya  Twyford wakati alipotembelea kiwanda cha Keda kilichopo Chalinze mkoani Pwani Desemba 7, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kazi ya kutengeneza marumaru aina  ya Twyford wakati alipotembelea kiwanda cha Keda kiloichopo Chalinze Mkoani Pwani, Desemba 7, 2018.  Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi , Evarest Ndikilo na watatu kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda, Tonny Zhifan.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kiwanda cha Keda kinachotengeneza marumaru aina ya Twyford kilichopo Chalinze mkoani Pwani, Desemba 7, 2018.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Zaynab Kawawa na wapili kukhoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho,Tony Zhifan.

Read More

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUTENGEZA JUISI YA MATUNDA CHA SAYONA WILAYANI BAGAMOYO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama juisi aina ya Sayona Fruttis wakati alipotembelea kiwanda cha Sayona kilichopo eneo la Chalinze Mboga wilayani Bagamoyo, Desemba 7, 2018. Wapili kushoto ni  Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makapuni ya Motisun, Subash Patel na Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo,  Omari Mgumba.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha kutengeneza juisi ya matunda  cha Sayona kilichopo Chalinze Mboga wilayani Bagamoyo, Desemba 7, 2018,  Wapili kushoto ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Motisun, Subash Patel  na watatu kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo,  Omari Mgumba. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaitazama juisi aina ya Sayona Fruttis wakati alipotembelea kiwanda cha kutengeneza juisi ya matunda cha  Sayona kilichopo eneo la Chalinze Mboga wilayani Bagamoyo, Desemba 7, 2018.    Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi, Evarest Ndikilo na wapili kushoto ni  Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Makapuni ya Motisun, Subash Patel.
Read More

WAZIRI MHAGAMA AAGIZA HALMASHAURI KUSHIRIKISHA WATU WENYE ULEMAVU PROGRAMU YA MAFUNZO YA KILIMO CHA KITALU NYUMBA


Na; Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameagiza halmashauri zitakazojengwa vitalu nyumba kushirikisha vijana wenye ulemavu.
Waziri Mhagama ameyasema hayo alipofanya ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma na Iringa kukagua maeneo yatayojengwa na kutoa mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba (Green House).
Akizungumza wakati wa ziara hiyo alisema kuwa katika halmashari zote 83 ambapo teknolojia ya kilimo cha kitalu nyumba itaanzishwa, idadi ya vijana 100 watakaopata mafunzo hayo ijumuishe na wenye ulemavu.
“Halmashauri zitengeneze mfumo madhubuti wa kuwashirikisha vijana wenye ulemavu katika mradi huu, kwani wanaouwezo wa kufanya kazi kama ilivyo vijana wengine na wakiwezeshwa wanaweza”, alisema Mhagama.
Pamoja na hayo, Mhagama amehimiza halmashauri hizo zisimamie vyema mradi huo kwa kuufanya unakuwa endelevu na kuwaunganisha vijana kwenye vyama vya akiba na mikopo ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha kujiendeleza kiuchumi kupitia programu hiyo.
Aliongeza kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu imeshakamilisha maandalizi yote ikiwemo wataalamu watakao fundisha vijana kujenga kitalu nyumba, kutengeneza miundombinu ya umwagiliaji, upandaji wa miche na kuwaelimisha mifumo mizuri ya kutafuta masoko.
Naye, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bw. Lucas Kambelenjo amemuhakakikishia Mhe. Waziri kusimamia ipasavyo mradi huo na kuahidi kutekeleza maagizo aliyoyatoa pamoja na kuwahamasisha vijana zaidi kushiriki katika kujifunza teknolojia hiyo mpya ya kilimo cha Kitalu Nyumba.
Waziri Mhagama alifanya ziara hiyo Mbinga Mji eneo la Mji Mwema, Nyasa na Mkoga, Iringa. Mradi huo unategemea kuanza kwenye Mikoa 12 ikiwemo ya Dodoma, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Mwanza, Simiyu, Geita, Kagera, Manyara, Lindi, Shinyanga na Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Iringa Bw. Ahmed Njovu akimweleza jambo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara Mkoani humo.

Afisa Maendeleo ya Vijana Bw. Atilio Mgamwa akitoa taarifa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama juu ya hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa programu ya mafunzo kwa vijana kupitia teknolojia ya kitalu nyumba.

Mratibu wa Mradi wa Kitalu Nyumba Bi. Elizabeth Kalilowele akielezea utekelezaji wa mradi wa kitalu nyumba ulipofikia kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipofanya ziara ya kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba.

Baadhi ya Watendaji, vijana na wakazi wa Mkoga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo na ujenzi wa kitalu nyumba.

Baadhi ya Watendaji, vijana na wakazi wa Mkoga wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi kukagua maeneo yalitengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo na ujenzi wa kitalu nyumba.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Mkoga (kulia) akimuonesha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Kitalu Nyumba.

Muonekano wa eneo moja wapo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kitalu nyumba (Green House).

Read More

Thursday, December 6, 2018

KATIBU MKUU KIONGOZI ATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA MJI WA SERIKALI IHUMWA DODOMA.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akikagua michoro ya ramani ya Mji wa Serikali wa Ihumwa Jijini Dodoma alipotembelea kukagua hali ya ujenzi wa majengo ya Ofisi za Serikali, kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi na wa kwanza kushoto ni Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akimuonesha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi michoro ya ramani ya ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Serikali Ihumwa wakati wa ziara yake eneo la Ihumwa Desemba 6, 2018.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof.Kitila Mkumbo wakati alipotembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Wizara yake katika Mji wa Serikali Ihumwa Dodoma, Desemba6, 2018.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akiuliza jambo kuhusu ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mhandisi kutoka SUMAJKT, Zabron Mahenge wakati wa ziara yake eneo lililotengwa kwa ujenzi wa Ofisi za Serikali la Ihumwa Dodoma.

Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akimuongoza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi kuelekea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ihumwa Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akionesha jambo kwa Mhandisi kutoka TBA, Amon Nghamba wakati wa ziara yake katika eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Ihumwa Dodoma .

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akimsikiliza Msanifu Majengo Moses Wadelanga wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Serikali Ihumwa Dodoma.

Katibu wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw.Meshach Bandawe akizungumza jambo kwa baadhi ya wajumbe wa kikosi kazi cha Miundombinu wanaoratibu ujenzi wa miundombinu katika Mji wa Serikali wa Ihumwa.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akimsikiliza Msanifu Majengo Moses Wadelanga akifafanua jambo juu ya ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika eneo la Ihumwa Jijin I Dodoma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (mwenye kofia ya kijivu) akikagua ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora eneo la Ihumwa Jijini Dodoma wakati wa ziara yake eneo hilo.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi akifuatilia maelezo kuhusu michoro ya ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Serikali Ihumwa Kutoka kwa Mkurugenzi Wakala wa Serikali Mtandao Bw.Michael Moshiro wakati wa ziara yake eneo hilo.


Read More

MAJALIWA AFUNGUA KIWANJA KIPYA CHA TAIFA CHA BASEBALL JIJINI DAR

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball  kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018. Kulia kwake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto kwake ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto.  Kushoto ni Mkwe wa Jackie Robinson ambaye ni Muasisi wa mchezo wa Baseball Duniani, Rutti David Robinson na wapili kushoto ni Mjukuu wa Muasisi huyo, Busaro Robinson.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipowasili kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018 Kufungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano  ya Taifa ya Baseball.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Balozi wa Japan Nchini,    Shinichi Goto wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya  Taifa ya Baseball, kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza wakati alipofungua kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindu Mshindano ya Taifa ya Baseball   kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimtambulisha Mkwe wa Jackie Robinson, Muasisi wa Mchezo wa Baseball Duniani, Rutti David Robinson (katikati) na Mjukuu wa Muasisi huyo, Busaro David Robinson   (kulia) wakati alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya  Baseball   kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Kiwanja Kipya wa Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akirusha mpira huku Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto  (kushoto) akijiandaa kuuzuia wakati Waziri Mkuu alipofungua Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball na Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam, Desemba 6, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mmoja wa wadhamini wa Ujenzi wa Kiwanja Kipya cha Taifa cha Baseball, Dkt. Kazusue Konoike wakati alipofungua kiwanja hicho na  Kuzindua Mashindano ya Taifa ya Baseball kwenye Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es slaam, Desemba 6, 2018. Katikati ni Balozi wa Japan Nchini, Shinichi Goto. 

Read More