Friday, May 31, 2019

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KUAPISHWA KWA RAIS WA MALAWI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehudhuria sherehe za kumwapishwa Rais wa Malawi, Profesa, Arthur Peter Mutharika zilizofanyika jijini Blantyre.

Amehudhuria sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzi, Blantyre. leo (Ijumaa, Mei 31, 2019) kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Akizungumza baada kuapishwa, Rais Mutharika aliwaahidi wananchi wa Malawi kuwa atawatumikia bila ubaguzi wa itikadi za kisiasa, kidini au ukabila.

Pia alisisitiza kuwa hatavumilia kuona vyama vya siasa, madhehebu ya dini au mtu yeyoye anaanzisha vurugu kwa nia ya kuikwamisha Serikali.

Rais Mutharika alisema kuwa waliomchagua na wasiomchagua wote ni rafiki zake na amedhamiria kuwatumikia kwa moyo wa upendo na haki.

“Uchaguzi umekwisha mshindi amepatikana, hivyo mnapaswa kuiunga mkoano serikali iliyodhamiria kuwaletea maendeleo wananchi wa Malawi.”

Alisema wananchi wa Malawi wameamua kumchagua Profesa Mutharika na Chama cha Democratic Progressive Party (DPP) hivyo lazima waheshimiwe.

Awali, Waziri Mkuu alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Chileka alipokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben Botolo.

Viongozi wengine waliokuwepo uwanjani hapo ni pamoja na Balozi wa Tanzani nchini Malawi, Ben Mashiba na Balozi wa Malawi nchini Tanzania, Chembe Muntali.

Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais Mstaafu wa Malawi, Bakili Muluzi. Mheshimiwa Majaliwa amerejea nchini leo jioni.

 (mwisho)
Read More

MAJALIWA AMWAKILISHA JPM KATIKA SHEREHE ZA KUMWAPISHA RAIS WA MALAWI PROFESA ARTHUR MUTHARIKA

Waziri Mkuu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben Botolo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Chileka uliopo Blantyre Malawi kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi, Profesa  Arthur Peter Mutharika, Mei 31, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi,  Bw. Ben Botolo wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Chileka uliopo Blantyre nchini Malawi kuwakilisha, Rais Dkt John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi, Profesa, Arthur Peter Mutharika, Mei 31, 2019.
Waziri Mkuu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akizungumza na , Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Malawi, Ben Botolo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Chileka uliopo Blantyre Malawi kumwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi, Profesa  Arthur Peter Mutharika, Mei 31, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika wakati Rais huyo alipohutubia baada ya  alipoapishwa kwenye Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Mei 31, 2019. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais huyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika wakati Rais huyo alipohutubia baada ya  alipoapishwa kwenye Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Mei 31, 2019. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais huyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika wakati Rais huyo alipohutubia baada ya  alipoapishwa kwenye Uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Mei 31, 2019. Mheshimiwa Majaliwa alimwakilisha Rais Dkt John Pombe Magufuli katika sherehe za kumwapisha Rais huyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa zamani wa Malawi, Bakili Muluzi katika sherehe za kumwapisha Rais wa Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika zilizofanyika kwenye uwanja wa Kamuzu mjini Blantyre, Mei 31, 2019.

Read More

WATAALAM WA SHERIA WAITAKA SHERIA MPYA YA KUDHIBITI VIMELEA HATARISHI NCHINI

Na. OWM, ARUSHA

Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri kutungwa kwa sheria mpya itakayohusika na ulinzi na usalama wa vimelea hatarishi ili kusaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa sampuli za vimelea hivyo kutoweza kueeneza magonjwa kwa binadamu.

Sheria hiyo imeshauriwa kuzingatia dhana ya Afya moja ambayo hujikita katika kujumuisha sekta zote za Afya katika kujiandaa, kufuatilia na kukabili magonjwa yanayomuathiri binadamu, lengo nikusaidia katika kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa kuvichukua vimelea kwa wanyama, binadamu na mimea au wakati wa kuvisafirisha na kuvipeleka maabara kwa ajili ya Uchunguzi na wakati wa kuviharibu mara baada ya kuvifanyia uchunguzi.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, uliofanyika kwa siku tatu na kufungwa leo tarehe 31 Mei , 2019, Jijini Arusha, kwa pamoja, wataalam wa sekta za Afya na wanasheria wa sekta hizo wamebainisha kuwa uwepo wa sheria hiyo utasaidia kuimarisha usalama na ulinzi kwa wanaohusika na shughuli za vimelea hivyo, mafunzo kwa wataalamu hao, miundo mbinu ya maabara, pamoja na kuainisha orodha ya vimelea hivyo.

Wataalamu wa sekta za Afya walioshiriki mkutano huo, wamebainisha kuwa, sheria hiyo ni ya muhimu kwa kuzingatia kuwa, Dunia imekuwa na tishio kubwa la magonjwa ya kuambukiza yanayoweza kusambaa kwa muda mfupi na kusababisha madhara makubwa kwa binadamu, mifugo, wanyama pori na kuleta uharibifu wa mazingira. Wamefafanua kuwa, Tafiti zinabainisha kuwa kila mwaka huibuka magonjwa ambukizi mapya kati ya matano hadi Nane duniani. Hivyo inakadiriwa ifikapo mwaka 2030, dunia itakuwa na magonjwa ambukizi mapya 30.


Akiongea wakati wa akifunga mkutano huo, Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe amebainisha kuwa serikali imedhamiria kuijenga jamii ya watanzania yenye Afya bora kwa kuikinga na majanga yatokanayo na magonjwa ya mlipuko, hivyo ushauri huo wa wanasheria na wataalam wa sekta hizo za afya utaratibiwa kwa uhakika ili kuweza kuijenga jamii salama.

Tarehe 13 Februari 2018, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa alizindua Dawati la Uratibu la Afya moja chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, likiwa na lengo la kusimamia na kuratibu shughui za Afya moja nchini.


MWISHO.
Mkurugenzi wa  Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe, (Wa kwanza kulia) na Mwanasheria wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Luteni Kanali, Godwill Benda pamoja na Mwanasheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Inspekta. William Mkamba, wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha tarehe 31, Mei, 2019.
Mtaalamu anayeshughulikia masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi katika wizara ya Afya, Jacob Lusekelo,akifafanua masuala ya Ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hivyo, Jijini Arusha tarehe 31, Mei, 2019.
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, wanyamapori, Mifugo na Mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha tarehe 31, Mei, 2019.
Mwanasheria kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Wa kwanza kulia), Mhe. Verynice Kawiche, na Mwanasheria kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mhe. Gilbert Ndeoruo, (katikati) pamoja na Mwanasheria wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Merick Luvinga, wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha tarehe 31,Mei, 2019.
Baadhi ya wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, wanyamapori, Mifugo na Mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo wakifuatilia mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha tarehe 31, Mei, 2019.
Mkurugenzi wa  Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali, Jimmy Matamwe, (walio kaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  wataalamu wa sekta za Afya ya Binadamu, wanyamapori, Mifugo na Mazingira pamoja na wanasheria wa sekta hizo wakati wa  mkutano wa kujadili masuala ya kisheria ya Kudhibiti ulinzi na Usalama wa vimelea hatarishi, Jijini Arusha tarehe 31, Mei, 2019.


Read More

Thursday, May 30, 2019

MAJALIWA AITISHA MKUTANO WA DHARURA WA BAADHI YA WADAU WA ZAO LA PAMBA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika mkutano wa  dharura wa baadhi ya wadau wa zao la pamba aliouiitisha kwenye Ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Mei 29, 2019. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela na kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi  wa Maendeleo wa Wilaya  zinazolima zao la pamba katika mkutano wa dharura wa baadhi ya wadau wa zao la pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Mei 29, 2019. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika mkutano wa dharura wa baadhi ya wadau wa zao la pamba aliouiitisha kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Mei 29, 2019.  Katikati ni Naibu Waziri wa  Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya na kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika mkutano wa dharura wa baadhi ya wadau wa zao la pamba aliouiitisha kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Mei 29, 2019.  Kulia ni Naibu Waziri wa Biashara na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya na katikati ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa dharura wa baadhi ya wadau wa zao la pamba wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipozungumza katika mkutano  aliouitisha kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Mei 29, 2019.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa dharura wa baadhi ya wadau wa zao la pamba wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati alipozungumza katika mkutano  aliouitisha kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Mei 29, 2019.



Read More

Wednesday, May 29, 2019

SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI NCHINI.

NA. MWANDISHI WETU
Serikali imedhamiria kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili wawekezaji nchini ili kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki yatakayowavutia kuwekeza nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki wakati akifungua mkutano wa wawekezaji wa Uingereza waliopo nchini walipokutana kujadili masuala ya Uwekezaji uliofanyika Mei 29, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Coral Beach Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde, Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke pamoja na Mwenyekiti wa Makampuni ya Biashara ya Uingereza Bw.Kalpesh Mehta, viongozi wa makampuni ya uwekezaji nchini, pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi za Sekta ya Umma na Binafsi.
Akizungumza wakati wa mkutano huo, Waziri Kairuki alieleza lengo la kukutana na wawekezaji kutoka Uingereza ni pamoja na kujadili masuala yote yanayowahusu wawekezaji kwa kuzingatia changamoto zinazowakabili na kuona namna bora ya kuzitatua ili kuendelea kufikia lengo la kuwa na mazingira bora ya biashara na uwekezaji nchini.
“Tumezingati umuhimu wa wawekezaji nchini, hivyo tumekutana hii leo ili kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili ili kuona namna bora ya kuboresha mazingira na kutambua fursa zilizopo nchini ili kuendelea kuwekeza nchini”, alisema Waziri Kairuki.
Waziri aliongezea kwamba, kwa kuzingatia kuwa mnamo mwezi Machi mwaka 2019 Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli aliutangaza mwaka huu kuwa ni mwaka wa uwekezaji alipokutana na waheshimiwa mabalozi wa nchi za nje ambao wapo nchini ikiwa ni kiashiria cha kufungua mwaka mpya.
Aliongezea kuwa, kwa kuzingatia mchango wa sekta binafsi katika ukuaji wa uchumi ikiwemo ongezeko la ajira hivyo tunapaswa kuzingatia na kuboresha mazingira yatakayochochea kuendelea kuchangia katika uzalishaji wa ajira nyingi nchini.
“Sekta binafsi ndiyo kiini cha ukuaji wa uchumi kwa upande wa kuongeza ajira hivyo tunatambua mchango huo ambapo hadi sasa wawekezaji wa uingereza wamechangia katika ukuaji wa ajira kwa kuzalisha ajira laki tatu,”alisisitiza Waziri Kairuki.
Kwa upande wake Balozi wa Uingereza Nchini Mhe.Sarah Cooke aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuona umuhimu wa kukutana pamoja kujadili masuala ya uwekezaji na kuendelea kujadili namna ya kuwezesha wawekezaji kutoka uingereza kuendelea kuwa wadau muhimu nchini na kuhakikisha nchi zote mbili zinanufaika.
“Ni kweli tumeenedelea kuwekeza Tanzania kwa kuzingatia mazingira yaliyopo hivyo ni vyema kukawa na maboresho zaidi katika mazingira hayo kwa kuendelea kutatua changamoto zilizopo kwa sasa ili tuendelea kushirikiana pamoja,” alieleza Balozi.Cooke
Aliongezea kuwa nchi ya Uingereza imelenga kuwa kinara cha uwekezaji katika nchi za Afrika hiyo ni wakati sahihi wa kuendelea kutumia fursa zilizopo barani humo ili kufikia malengo.
“Ifikapo mwaka 2022 Nchi yetu imeweka malengo ya kuwa wawekezaji bora barani Afrika hivyo tunaendelea kushirikianana nchi za Afrika ili kuwa na nia moja na kuwa na mahusiano yenye tija hasa katika masuala ya uwekezaji”,alisema Balozi Cooke.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde alieleza kuwa, Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya biashara ili kuchangia ongezeko la ajira kwa vijana wa Kitanzania ili kujikwamua kiuchumi.
Aidha alifafanua kuwa, ili kuendelea kukuza ujuzi kwa vijana na kuondokana na changamoto za ukosefu wa ajira Serikali itaendelea kulinda ajira za watanzania na kuboresha mazingira ya sekta binafsi ambao ni wadau muhimu katika kuzalisha ajira nchini.

=MWISHO=
Read More

SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI NCHINI.

Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akitoa neon la ufunguzi wakati wa mkutano wake na wawekezaji wa Uingereza nchini alipokutana nao Mei 29, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Coral Beach Jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala ya uwekezaji nchini.
Balozi wa Uingereza Nchini, Mhe. Sarah Cooke akizungumza jambo wakati wa mkutano wa wawekezaji wa nchi hiyo walipokutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki alipokutana nao Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony Mavunde akichangia jambo wakati wa mahojiano na waandishi wa habari walipokutana kujadili masuala ya wawekezaji nchini Jijini Dar es Salaam.Katikati ni Waziri wa Nchi wa ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki na wa kwanza kushoto ni Balozi wa Uingereza Nchini Mhe. Sarah Cooke.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo Bw. Russell Stuart akiuliza swali wakati wa Mkutano huo.
Kaimu Mkurugenzi wa Uwekezaji Ofisi ya Waziri Mkuu Aristides Mbwasi akijibu hoja za wajumbe kuhusu masuala ya uwekezaji wakati wa mkutano huo
Sehemu ya wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) wakati wa mkutano huo.

Mkurugenzi wa Uhamasishaji Uwekezaji Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Bw. John Mnali akiwasilisha mada ya fursa za uwekezaji nchini wakati wa mkutano huo.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiteta jambo na Naibu Waziri wa Ofisi hiyo anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira  Mhe. Anthony Mavunde wakati wa Mkutano huo.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC) Bi. Oliver Vengula akichangia hoja wakati wa mkuatano huo.
Kamishna wa Kazi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw.Gabriel Malata akichangia hoja kuhusu vibali vya ajira wakati wa mkutano wa wawekezaji wa Uingereza uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb)akiteta jambo na Balozi wa Uingereza Nchine Mhe. Sarah Cooke wakati wa mkutano huo.
Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki (Mb) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa mahojiano kuhusu masuala ya uwekezaji nchini.


Read More

BEI YA PAMBA NI SH. 1,200 KWA KILO - WAZIRI MKUU


*Amwagiza Katibu Mkuu Kilimo atume timu ichunguze Bodi ya Pamba

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ana imani kuwa ununuzi wa zao la pamba utaanza mara moja kwa bei ya sh. 1,200 kwa kilo moja katika mikoa yote inayozalisha zao hilo.

Amefikia uamuzi huo baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya bei kwa takriban ya wiki nne tangu bei elekezi ilipotangazwa Aprili 30, 2019 mkoani Shinyanga kwamba bei hiyo ianze kutumika kuanzia Mei 2, 2019.

Alikuwa akizungumza na wadau wa sekta ndogo ya pamba kwenye kikao kilichofanyika leo (Jumatano, Mei 29, 2019) kwenye ukumbi wa Chuo cha Benki Kuu, jijini Mwanza. Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Mawaziri wa Kilimo na Viwanda, Makatibu Wakuu wa Kilimo na Ofisi ya Rais – TAMISEMI na  Wakuu wa Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu na Geita.

Wengine ni wawakilishi wa Wabunge wa mikoa hiyo, Makatibu Tawala wa mikoa, Wakuu wa Wilaya zote za mikoa hiyo, na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya hizo. Pia kilihudhuriwa na wanunuzi wa pamba, wakulima na maafisa wa benki kadhaa.

Waziri Mkuu aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba Serikali bado inaendelea kutafuta njia nzuri ya kuwakutanisha wadau wa mazao ya kibiashara ili yaweze kuwa na tija kwa wakulima. Alisema kazi hiyo inafanywa wa Wizara ya Kilimo. Mazao hayo ni pamba, chai, kahawa, korosho, tumbaku na chikichi.

Pia alisema Bodi ya Pamba iachiwe jukumu la kutoa leseni za ununuzi wa zao hilo na kwamba Wakurugenzi wa Halmashauri waliokuwa wakifanya kazi hiyo waache mara moja. “Kuna baadhi ya Wakurugenzi wanatoa leseni za ununuzi, lakini wenye Mamlaka ni Bodi ya Pamba. Mnunuzi nenda Bodi ukapate leseni yako,” alisema Waziri Mkuu.

Alitumia fursa hiyo kuwakemea baadhi ya wakurugenzi ambao wamekuwa wakizuia wanunuzi wapya kwenye maeneo na kuendelea kuwakumbatia wanaowataka wao. “Wakurugenzi baadhi yenu mnazuia wanunuzi wapya, mnamtaka fulani tu. Kwa kufanya hivyo, unapungua kiwango cha kilo ambacho wakulima wako wangeuza,” alionya.

‘Wanunuzi nendeni mkajitambulishe kwa Wakuu wa Wilaya au Wakurugenzi ili watambue kwamba mpo kwenye maeneo yao lakini kila mnunuzi anayo haki ya kwenda kununua pamba mahali popote hapa nchini.”
Kuhusu ubora wa pamba, Waziri Mkuu alitaka wananchi waelimishwe ili waache kuweka maji au mchanga kwenye pamba kwa minajili ya kuongeza uzito kwani kwa kufanya hivyo wanachafua jina la Tanzania pindi inapopelekwa kuuzwa nje ya nchi.

Pia alitaka vyama vikuu vya ushirika vijiridhishe kuhusu ubora wa maghala ya kuhifadhia pamba kwenye vyama vya msingi (AMCOS) kwani kwa kufanya hivyo, itawasaidia wakulima wauze mapema pamba yao mara baada ya kuivuna.

Kuhusu mizani, Waziri Mkuu aliiagiza wakala wa vipimo nchini (WMA) waende wakakague mizani ya kwenye AMCOS na kwenye vinu vya kuchambulia pamba (ginneries) kwa sbabu ya tofauti kubwa ya uzito inayojitokeza na kuwalazimisha wakulima kulipia upotevu wa kilo hizo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mhandisi Mathew Mtigumwe atume wakaguzi kwenye Bodi ya Pamba ili wabainishe matumizi ya sh.100 kwa kila kilo ambazo zimekuwa zikilipwa kwenye bodi hiyo.

“Katibu Mkuu Kilimo lete wakaguzi ndani ya bodi ya pamba, waangalie kwa kipindi cha miaka mitatu toka tulipoanza kukusanya sh. 100 kwa kilo, zimekusanywa shilingi ngapi, na zimetumika kulipia nini.

“Na Mrajisi wa Ushirika nchini ufanye ukaguzi kwenye vyama vikuu vya Ushirika na AMCOS. Uangalie ziko ngapi na zinafanya nini. Kuna AMCOS zina hela, je fedha hiyo imetumika kufanya nini ili kuendeleza zao la pamba. Je zimenunua matrekta au zimelipia posho za vikao,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wanunuzi Binafsi wa Pamba (TCA), Bw. Christopher Gachuma ameshukuru Waziri Mkuu kwa maelekezo aliyoyatoa kuhusu utoaji wa leseni kwani yalikuwa ni kikwazo kikubwa kwa baadhi ya wanunuzi wa zao hilo.

“Suala la utoaji leseni linapaswa lianze mapema lakini kuna wengine hadi sasa bado hawajapata leseni zao.” Aliwataka wanunuzi wa pamba waanze kununua pamba ili msimu wa mauzo uanze kwa kasi.

(mwisho)
Read More

Tuesday, May 28, 2019

WAZIRI MKUU AITAKA AKDN IKAMILISHE MJADALA NA NHIF

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN) ukamilishe majadiliano yao na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuhusu matumizi ya kadi za NHIF kwenye hospitali zao ili Watanzania wengi zaidi waweze kunufaika.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 28, 2019) alipokutana na viongozi kadhaa wa taasisi hiyo pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua mchango unaotolewa na taasisi ya AKDN katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya.

“Nilijionea kazi kazi kubwa inayofanyika pale Hospitali ya Aga Khan Machi, mwaka huu, niliongea na wagonjwa na kupata maoni yao, lakini kikubwa tu mpunguze gharama na muimarishe huduma zenu,” amesema.

Amewapongeza viongozi hao kwa utoaji wao wa huduma kwenye sekta nyingine kama elimu, maji na kilimo. “Tunategemea mtaendelea kuimarisha huduma hizo ili ziwasaidie Watanzania wengi zaidi,” amesisitiza.

Viongozi hao walikutana na Waziri Mkuu ili kumuarifu juu ya mpango wa taasisi hiyo wa kuanzisha kituo maalum cha matibabu ya saratani nchini (Specialised Cancer Care Facility) ambao unatarajiwa kugharimu dola za marekani milioni 15. Kituo hicho kitaendeshwa kwa ubia baina ya hospitali za Ocean Road, Muhimbili, Bugando na Aga Khan.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bi. Ummy Mwalimu alimweleza Waziri Mkuu kwamba hospitali za Ocean Road na Bugando zinatoa huduma za radiotherapy na chemotherapy, wakati hospitali ya KCMC inatoa huduma ya chemotherapy tu. “Hospitali ya Rufaa ya Mbeya bado huduma hizo zinaadaliwa ili ziweze kutolewa,” alisema.

Hata hivyo, Waziri Ummy alisema hivi sasa kwa nchi nzima, kuna vituo zaidi ya 120 ambavyo vinatoa huduma ya utambuzi wa saratani (cancer screening).

Mapema, akitoa maelezo kuhusu mpango wa kujenga kituo hicho, Mwakilishi Mkazi wa AKDN, Bw. Amin Kurji, alisema wameshawasiliana na hiospitali zote tajwa na sasa wanashirikiana na wataalamu wa wizara ya afya ili kukamilisha suala hilo.

“Tatizo la saratani hapa nchini ni kubwa kwa sasa. Lakini tunataka watu watambue kwamba ukiugua saratani haimaanishi kwamba utakufa mara moja (it’s not a death sentence). Inaweza kutibika endapo mgonjwa atawahi kupata matibabu,” alisema Bw. Kurji.

Alisema kwa sasa hivi hapa nchini hakuna kituo maalum cha matibabu ya saratani nchini lakini kitu cha pekee kuhusu kituo hicho ni uwepo wa huduma zinazotembea za upimaji na utoaji tiba hadi mikoani. “Huduma hizi zitakuwa zinatolewa kwenye mikoa yote kupitia njia ya mtandao, ilhali vituo vikuu vya Dar es Salaam na Mwanza vitakuwa vikitoa majibu kwa madaktari husika,” alisema.

Alisema lengo lao pia ni kutoa elimu juu ya kuzuia, upimaji wa mapema na upatikanaji wa tiba (prevention, early diagnosis and cure).

(mwisho)
Read More

Thursday, May 23, 2019

TOZO ZINAZOKWAMISHA BIASHARA NCHINI KUFUTWA-MAJALIWA


*Ni baada ya Serikali kusikia kilio kutoka kwa wafanyabiashara

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanza jitihada za kufuta tozo zote ambazo zinakwamisha mazingira ya ufanyaji wa biashara nchini zikiwemo za kwenye pembejeo ili kuwawezesha wafanyabiashara kuzifikisha hadi ngazi ya kijiji kwa wakulima.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 23, 2019) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Madaba, Kizito Mhagama katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu. Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kupunguza tozo kwa maduka yanayouza pembejeo ili kumwezesha mkulima kupata pembejeo.

Waziri Mkuu amesema Serikali imepokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo na wauzaji wa pembejeo juu ya tozo mbalimbali katika uendeshaji wa shughuli nzima wa biasharazao.

“Serikali imesikia vilio vyenu na sasa inafanya mapitio ya tozo hizo na itakapofikia hatua nzuri itawajulisha na kuwashirikisha kujua ni aina gani ya tozo ambayo itaondolewa au kuibadilisha ili muendelee kufanya biashara zenu katika mazingira rahisi.”

Waziri Mkuu amesema kazi kubwa inayofanywa na Serikali kwa sasa ni kufanya mapitio ya tozo zote kuanzia kwa wakulima hadi kwa wafanyabiashara na kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara nchini, ikiwemo ya pembejeo ili kuzifikisha kiurahisi kwa wakulima.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kwamba tayari Mawaziri wa kisekta wenye dhamana ambao wana tozo mbalimbali kwenye wizara zao zinazokwamisha ufanyaji biashara katika mazingira rafiki wameshakutana kwa ajili ya kujadili namna ya kulipatia ufumbuzi suala hilo.

“Hata juzi nilikuwa na mawaziri hao kupata taarifa zao kwa pamoja kuona maeneo yote waliyoyapitia na tozo zote zinazokusudiwa kupitiwa upya na kazi hiyo ikikamilika watakutana na Kamati ya Bajeti ya Bunge, Wizara ya Fedha ili kuona namna nzuri ya kuondoa tozo hizo. Lakini baadaye suala hilo litaenda kwenye mamlaka inayotoa ridhaa ya kuondoa au kupunguza tozo.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema miradi mingi ya maji ambayo inatekelezwa kwenye maeneo mbalimbali nchini baadhi yake haitekelezwi kwa viwango vilivyokusudiwa, hivyo haiwiani na thamani halisi ya kiasi cha fedha kinachotolewa.

Hata hivyo Waziri wa Maji wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2019/2020 alieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya miradi yote ambayo haiwiani na kiasi cha fedha kilichotolewa pamoja na hatua zilizochukuliwa dhidi ya miradi yote.

“Moja kati ya hatua ambazo amezifanya ni pamoja na kuunda timu inayopita kukagua miradi yote nchini na kujiridhisha kama matengenezo yake yanakidhi thamani ya fedha iliyotolewa katika mradi huo na kama haukidhi hatua kali zinachukuliwa kwa wahusika.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Korogwe Mjini Mary Chatanda aliyetaka kujua Serikali kama ipo tayari kuchunguza na kuchukua hatua kwa watendaji walioshindwa kusimamia miradi ya maji na kuisababishia hasara pamoja na wananchi kukosa huduma waliyokusudiwa.


Read More

TOZO ZINAZOKWAMISHA BIASHARA NCHINI KUFUTWA-MAJALIWA

*Ni baada ya Serikali kusikia kilio kutoka kwa wafanyabiashara

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanza jitihada za kufuta tozo zote ambazo zinakwamisha mazingira ya ufanyaji wa biashara nchini zikiwemo za kwenye pembejeo ili kuwawezesha wafanyabiashara kuzifikisha hadi ngazi ya kijiji kwa wakulima.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 23, 2019) Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Madaba, Kizito Mhagama katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu. Mbunge huyo alitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kupunguza tozo kwa maduka yanayouza pembejeo ili kumwezesha mkulima kupata pembejeo.

Waziri Mkuu amesema Serikali imepokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo na wauzaji wa pembejeo juu ya tozo mbalimbali katika uendeshaji wa shughuli nzima wa biasharazao.

“Serikali imesikia vilio vyenu na sasa inafanya mapitio ya tozo hizo na itakapofikia hatua nzuri itawajulisha na kuwashirikisha kujua ni aina gani ya tozo ambayo itaondolewa au kuibadilisha ili muendelee kufanya biashara zenu katika mazingira rahisi.”

Waziri Mkuu amesema kazi kubwa inayofanywa na Serikali kwa sasa ni kufanya mapitio ya tozo zote kuanzia kwa wakulima hadi kwa wafanyabiashara na kutengeneza mazingira mazuri ya kufanya biashara nchini, ikiwemo ya pembejeo ili kuzifikisha kiurahisi kwa wakulima.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kwamba tayari Mawaziri wa kisekta wenye dhamana ambao wana tozo mbalimbali kwenye wizara zao zinazokwamisha ufanyaji biashara katika mazingira rafiki wameshakutana kwa ajili ya kujadili namna ya kulipatia ufumbuzi suala hilo.

“Hata juzi nilikuwa na mawaziri hao kupata taarifa zao kwa pamoja kuona maeneo yote waliyoyapitia na tozo zote zinazokusudiwa kupitiwa upya na kazi hiyo ikikamilika watakutana na Kamati ya Bajeti ya Bunge, Wizara ya Fedha ili kuona namna nzuri ya kuondoa tozo hizo. Lakini baadaye suala hilo litaenda kwenye mamlaka inayotoa ridhaa ya kuondoa au kupunguza tozo.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema miradi mingi ya maji ambayo inatekelezwa kwenye maeneo mbalimbali nchini baadhi yake haitekelezwi kwa viwango vilivyokusudiwa, hivyo haiwiani na thamani halisi ya kiasi cha fedha kinachotolewa.

Hata hivyo Waziri wa Maji wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kwa mwaka 2019/2020 alieleza hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya miradi yote ambayo haiwiani na kiasi cha fedha kilichotolewa pamoja na hatua zilizochukuliwa dhidi ya miradi yote.

“Moja kati ya hatua ambazo amezifanya ni pamoja na kuunda timu inayopita kukagua miradi yote nchini na kujiridhisha kama matengenezo yake yanakidhi thamani ya fedha iliyotolewa katika mradi huo na kama haukidhi hatua kali zinachukuliwa kwa wahusika.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la mbunge wa Korogwe Mjini Mary Chatanda aliyetaka kujua Serikali kama ipo tayari kuchunguza na kuchukua hatua kwa watendaji walioshindwa kusimamia miradi ya maji na kuisababishia hasara pamoja na wananchi kukosa huduma waliyokusudiwa.


 (mwisho)
Read More

BUNGENI LEO 23.05.2019

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla  akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi  ya Wazara  yake kwa Mwaka 2019/2020, Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019. 
Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele akizungumza Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019. 
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Stella  Ikupa (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Time ya Taifa ya Soka  ya Walemavu- Tembo Worriors kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Mei 23, 2019.  Waliosimama,  wa tatu  kushoto ni Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto, wa tatu kulia ni Mbunge wa Urambo, Margareth Sitta na wa nne kulia ni Mbunge wa Viti Maalum Amina Mollel.

Read More

WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WA FINLAND, USWISI


*Akaribisha wawekezaji kwenye TEHAMA, uchakataji wa mazao ya kilimo na misitu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya mazungumzo na Balozi wa Finland hapa nchini, Mhe. Pekka Hukka na kumshukuru kwa jitihada za nchi hiyo kuisadia Tanzania kuondokana na umaskini.

“Tunaishukuru Serikali ya Finland kwa misaada ambayo imeendelea kuitoa kama njia ya kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania za kuondoa umaskini pamoja na kuongeza makusanyo ya mapato ili kukuza uchumi wa nchi yetu,” amesema Waziri Mkuu.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Mei 23, 2019) alipokutana na Balozi huyo anayemaliza muda wake wa kazi hapa nchini, ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amemweleza balozi huyo kwamba Tanzania bado ina fursa za uwekezaji na kwamba Serikali inaendelea kutengeneza mazingira rafiki na bora kwa uwekezaji. “Sekta ambazo makampuni ya Finland yanaweza kuwekeza hapa nchini ni pamoja na TEHAMA, nishati, usafiri, uchakataji wa mazao ya kilimo na misitu,” amesema.

Waziri Mkuu alimtakia heri Balozi Hukka ambaye anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi huu kwenda Tunisia ambako ndiko kutakuwa na kituo chake kipya cha kazi.

Kwa upande wake, Balozi Hukka alisema ataondoka Tanzania akiwa na kumbukumbu nzuri ambazo atazienzi na anataraji kukutana na Watanzania wengine ili aendelee kukuza mahusiano yaliyokuwepo.

Alisema Serikali za Tanzania na Finland zilisaini mkataba wa programu iitwayo Forestry and Value Chain Programme (FORVAC) ambao unalenga kuongeza faida za kiuchumi na kijamii kwa kupitia sekta ya misitu pamoja na kupunguza ukataji wa miti. “Malengo hayo yatafikiwa kwa kukuza mnyororo wa thamani kwenye sekta ya misitu pamoja na kuimarisha mifumo ya ufuatiliaji, sheria na sera katika sekta ya misitu,” alisema.

Finland inasaidia sekta ya misitu nchini Tanzania kupitia Programu ya Private Forestry Programme (PFP) ambayo ililenga kuongeza mapato kwa wakazi wa vijijini katika Halmashauri 10 za Njombe TC, Njombe DC, Makete, Ludewa, Kilombero, Mufindi, Kilolo, Madaba, Mbinga na Nyasa) kwa kusaidia upandaji wa miti na kuongeza thamani ya mazao ya misitu.

Programu hiyo imesaidia kujenga uwezo kwa wahusika wote katika mnyororo wa thamani wa biashara ya mazao ya misitu. Awamu ya kwanza ya programu hiyo imesaidia kuongeza kipato cha familia zaidi ya 9,000 kwenye wilaya hizo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekutana na Balozi wa Uswisi hapa nchini, Mhe. Florence Mattli ambaye pia alienda kumuaga ofisini kwake bungeni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu alimweleza balozi huyo dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kudumisha ushirikiano na Uswisi na kusisitiza kwamba iko tayari kufanya kazi na Balozi mpya wa Uswisi atakayekuja kwa manufaa ya pande zote mbili.

“Ni muhimu sana ushirikiano wa Tanzania na Uswisi ukadumishwa kwa kuzingatia pia masuala ya biashara na uwekezaji hususan kwenye sekta za afya, kilimo, elimu na teknolojia,” alisema Waziri Mkuu.

Alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Uswisi kwa misaada ambayo imeendelea kutolewa na nchi hiyo katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania za kuondoa umaskini hususan kwenye miradi ya afya, kilimo na uwekezaji katika elimu na biashara kwa ajili ya kukuza uchumi.

Kwa upande wake, Balozi Mattli alisema Serikali ya Uswisi imekuwa ikiunga mkono na kusaidia jitihada za kukuza uwazi na uwajibikaji kwa watendaji wa Serikali na wale wasiokuwa wa Serikali kuzingatia mazingira ya kitaasisi na kijamii yanayopiga vita masuala ya rushwa.

“Msaada huo wa kupambana na rushwa umechangia kuimarisha ufanisi wa uendeshaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kukuza uelewa wa kijamii kuhusu masuala ya rushwa,” alisema.

Alisema mwaka 2018, Serikali ya Uswisi ilitoa dola za Marekani milioni 24 kusaidia Mpango wa Ukuzaji Ujuzi kwa Ajira Tanzania, ambao ulianza kutekelezwa Agosti Mosi, 2018 kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

“Mpango huo unalenga kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa vitendo na kuimarisha mafunzo ya ufundi nchini. Hivyo, mpango huo umechangia kuboresha matarajio ya vijana kwa kuwapatia ujuzi katika kazi na ubunifu unaochangia kuondokana na suala la ukosefu wa ajira,” alisema.

Alisema Serikali ya Uswisi inasaidia maendeleo ya vijana kupitia Mpango wa Ajira ya Vijana (OYE) ambao unalenga kuimarisha maisha ya vijana wa kiume na wa kike kwa kuwafundisha fursa za ajira katika sekta za biashara, kilimo, nishati mbadala, usafi wa mazingira na kuboresha ujuzi.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Finland nchini,  Mhe. Pekka Hukka kabla ya mazungumzo yao, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Switzerland nchini, Mhe. Florence Tinguely Mattli, ofisini kwa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Switzerland nchini, Mhe.  Florence Tinguely Mattli kabla ya mazungumzo yao, Ofisini kwa Waziri Mkuu Bungeni jijini Dodoma, Mei 23, 2019.



Read More