Friday, August 31, 2018

WAZIRI MKUU KUHUDHURIA MKUTANO WA FOCAC


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameondoka nchini leo (Ijumaa, Oktoba 31, 2018) kuelekea nchini China kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Mkutano huo wa siku mbili unatarajiwa kuanza Jumatatu, Septemba 03, 2018 jijini Beijing nchini China, ambapo utafunguliwa na Rais wa China, Xi Jinping. Katika mkutano huo Waziri Mkuu anamuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli.

Mbali na kuhudhuria mkutano huo pia, Waziri Mkuu anatarajia kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa kampuni mbalimbali akiwemo Rais wa Kampuni ya CCECC, Rais wa Shirika la NORINCO, Rais wa Kampuni ya Zijin Gold Mine pamoja na Mwenyekiti wa Kampuni ya saruji ya HEGNYA.
Read More

MAJALIWA AMWAKILISHA JPM MKUTANO WA FOCAC NCHINI NCHINI

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akienda China kuwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika  na China  (FOCAC), Agosti 31, 2018. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere akienda China kuwakilisha Rais John Magufuli katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika  na China  (FOCAC), Agosti 31, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka nichini kwenda China kumwakilisha Rais John Magufuli  Katika Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya Afrika na China (FOCAC), Agosti 31, 2018. 

Read More

Wednesday, August 29, 2018

FLYOVER YA TAZARA IMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 98-MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesemaujenzi wa barabara ya juu katika eneo la Tazara umekamilika kwa asilimia 98 na itafunguliwa Oktoba mwaka huu na Rais Dkt. John Magufuli.

Mradi wa barabara ya juu (Mfugale flyover) chini ya ufadhili wa Serikali ya Japani, unalengo la kupunguza msongamano wa magari katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 29 ,2018) baada ya kukagua ujenzi wa mradi huowa barabara ya juu katika eneo la Tazara jijini Dar Es Salaam

Waziri Mkuu amesema ameridhishwa kazi ya umaliziaji wa mradi huo inayoendelea kwenye hilo.

“Mradi utapunguza muda wa usafiri katika barabara ya Nyerere hususani  kwa wananchi wanaotoka katikati ya jiji kwenda uwanja wa ndege na wanaotoka Buguruni, Temeke.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaagiza viongozi Mkoa wa Dar Es Salaam watafute eneo kwa ajili ya  wafanyabiashara ndogondogo ili waweze kuondoka kandokando ya barabara hizo za juu zinazojengwa.

Waziri Mkuu ameyasema hayo baada ya kukagua ujenzi wa barabara za juu (interchange) eneo la Ubungo, katika makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma, eneo la Ubungo jijini Dar Es Salaam.

Amesema ni vema wafanyabiashara hao wakaondolewa na kutafutiwa eneo lingine ili kulinda usalama wao kutokana na kazi za ujenzi zinazoendelea kwenye maeneo hayo. Pia amewataka viongozi hao wawaelekeze wananchi maeneo watakapowahamishia wafanyabiashara hao ili waweze kwenda kununua bidhaa.

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema mradi huo nao unalengo la kupunguza msongamano wa magari kwa kutenganisha njia za barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma ili kuwa na ngazi mbili juu ya barabara za sasa.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ujenzi wa mradi wa barabara ya juu katika eneo la Tanzara (Mfugale flyover) unagharimu sh. bilioni 100.52 na unajengwa na kampuni  ya Sumitomo Mitsui ya nchini Japan.

Amesema mradi huo umezingatia jinsi ya kuwezesha muunganiko wa mfumo wa usafiri jijini Dar Es Salaam na ule wa mabasi yaendayo haraka awamu ya pili, tatu na ya nne. “Tumeacha eneo la mita 12 katikati ya barabara kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.”

Read More

DAWA YA KUUA VILUILUI ITUMIKE KUTOKOMEZA MARALIA-MAJALIWA

 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mikoa yote nchini waendeleze kampeni ya kutokomeza ugonjwa malaria kwa kutumia dawa ya kuua viluilui vya mbu.

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 29, 2018) alipofanya ziara katika kiwanda cha kutengeneza dawa ya kuua viluilui vya mbu kilichopo katika wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.

Amesema nchi inakabiliwa na matatizo makubwa ya ugojwa wa malaria, hivyo ni vema viongozi wa mikoa wakatokomeza viluilui vya mbu kwa kuwa dawa inatengenezwa nchini.

Waziri Mkuu amesema kiwanda hicho cha Labiofam ni cha pekee barani Afrika kwa kuwa na uwezo wa kutengeneza dawa za aina hiyo.”Tutumie fursa hii kutokomeza maralia nchini.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa kiwanda hicho kutumia vyombo vya habari  kwa kuandaa vipindi vya kuelimisha umma kuhusu dawa wanayozitengeneza.

Amesema wananchi wanatakiwa kuelimishwa juu ya umuhimu wa kutumia dawa hiyo kwa ajili ya kuua viluilui katika maeneo ya makazi yao ili kuutokomeza ugonjwa wa maralia nchini.

Naye,Meneja Uzalishaji wa kiwanda hicho, Bw. Aggrey Ndunguru amesema dawa zinazotengenezwa kiwandani hapo zina uwezo wa kuua viluilui vya mbu tu na haina madhara kwa binadamu.

Amesemma dawa hiyo ambayo ipo katika ujazo tofauti tofauti inaweza kuwekwa kwenye makaro ya vyoo, maji yaliyotuama pamoja na katika matanki ya maji ili kuua viluilui.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu alifuatana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarest Ndikilo na maafisa wengine wa Serikali.

Read More

Monday, August 27, 2018

CAF YARIDHISHWA NA MAANDILIZI YA AFCON


RAIS wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Bw. Ahamd Ahmadamesema ameridhishwa na maandalizi ya michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON).

Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya  miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Agosti 27, 2018) wakati akizungumza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Pia ameihakikishia Serikali kwamba hakuna mabadiliyo yoyote ya ratiba yatakayofanyika kuhusu wenyeji wa mashindano na kwamba CAF itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufanikisha michuano hiyo.

Rais wa CAF yupo nchini kwa ajili ya kuongoza mkutano maalum wa mabadiliko ya katiba ya Baraza la Vyama vya Soka katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam, umehudhuriwa na viongozi wa juu wa nchi wanachama wote 12 wa CECAFA wakiwemo marais.
Kwa upande wake,Waziri Mkuu WAZIRI amesema mechi zoteza michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON) zitafanyika jijini Dar es Salaam.mashindano 

“Tupo katika hatua za mwisho za maandalijzi ya michuano hiyo itakayofanyika jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Taifa, Uhuru, Chamanzi na JK Park utatumika kwa mazoezi.”

Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa nchi kushiriki katika mashindano makubwa kama hayo kwa kuwa yanasaidia kwenye ukuzaji wa vipaji kwa vijana ambao wengi wao ni wanafunzi.
Read More

Sunday, August 26, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMJLIA HALI DR HAMISI KIGWANGALA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla,  leo Agosti 26.2018 akiwa anaendelea kupatiwa  matibabu katika Wodi aliyolazwa ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa,  Muhimbili (MOI).

Read More

Friday, August 24, 2018

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKUTANA NA BALOZI WA CHINA JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa China Nchini Tanzani Bibi Wang Ke kabla ya kufanya naye mazungumzo ya kikazi katika Ofisi yake ndogo Jijini Dar es salaam leo Agosti 24/2017.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Balozi wa China Nchini Tanzani Bibi Wang Ke wakifanya mazungumzo ya kikazi katika Ofisi yake ndogo Jijini Dar es salaam leo Agosti 24/2017.

Read More

Wednesday, August 22, 2018

MAJALIWA ASAFIRI KWA DREAMLINER KUTOKA MWANZA HADI DAR

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Phillip Mangula (watatu kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia) kwenye uwanja wa  Ndege wa Mwanza kabla kuondoka kuelekea Dar es salaam kwa ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner Agosti 22, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakisafiri kwa Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner wakitoka Mwanza kwenda Dar es salaam kupitia KIA, Agosti 22, 2018.

Read More

Sunday, August 19, 2018

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MJINI TABORA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta  na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Tabora, Hassan Kasubi katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye kiwanja cha Chipukizi katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora, Munde Tambwe katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye kiwanja cha chipukizi katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018.

Wananchi wa Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri Mkuuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha Chipukizi, Agosti 18, 2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kiwanja cha Chipukizi katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani wa Tabora Mjini, Aden Rage baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Chipukizi kwenye Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Emmanuel Nley jumla ya shilingi 1,500,000/= kwa ajili ya ujenzi wa dawati la Jinsia katika Mji wa Tabora na ujenzi wa nyumba ya Mkuu wa polisi  katika wilaya ya Igunga.  Makabidhiano ya fedha hizo  zilizotolewa na Mbunge wa Manonga, Seif Khamis Gulamali (kushoto) yalifanyika baada ya Waziri Mkuu kuhutubiua mkutano wa hadhara katika kiwanja cha Chipukizi kwenye Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na wapili kushotoi ni Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe.
Read More

Saturday, August 18, 2018

WAZIRI MKUU AWAWASHIA MOTO MADIWANI MANISPAA YA TABORA


*Awataka wajiondoe kufanya biashara na halmashauri hiyo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wajiondoe katika kufanyabiashara na halmashauri hiyo kwa kuwa wanakiuka maadili ya utumishi wa umma.

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Agosti 18 ,2018) wakati akizungumza na watumishi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Manispaa ya Tabora na Hospitali ya Rufaa ya Kitete katika ukumbi wa Isike Mwanakiyungi.

“Madiwani mjiondoe kuwa wasimamizi wa kampuni zinazozofayakazi na halmashauri yenu na wakuu wa idara nanyi muwe makini mfanye kazi na kampuni huru ili muweze kuchukua hatua pale linapotokea tatizo,”.

“Nyie Madiwani ndio mnaopaswa kuisimamia halmashauri, sasa kama watu mliopewa dhamana mkiingia katika kufanya shughuli nyingine mnawakwaza wakuu wa idara na kuharibu mambo. Fanyeni kazi yenu ya kuisimamia halmashauri kwa mujibu wa dhamana mliyopewa,”.

Waziri Mkuu amesema Madiwani wawe wanafanya tathmini ya ushauri unaotolewa na wakuu wa idara na wasijihusishe na biashara ndani ya halmashauri zao na badala yake waziachie kampuni zifanye kazi zenyewe na Serikali bila ya kuzisimamia.

Waziri Mkuu alitolea mfano wa mradi wa ununuzi maroli mawili na makontena 20 ya kukusanyia taka mitaani ya Manispaa hiyo na kampuni inayomilikiwa na diwani ilipewa zabuni ya kununua vifaa hivyo, ambapo ilikabidhi roli moja likiwa bovu na kukataliwa. “ Yeye akaenda kulipaka rangi na kuwaletea, walilikataa tena,”.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Bw. Msalika Makungu aifanyie uchunguzi ofisi ya Mwekahazina  wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora baada ya kuwepo kwa utafunaji wa fedha za umma kwa visingizio mbalimbali.

Amesema zaidi ya sh. milioni 12.4 zimelipwa na Mwekahazina wa Halmashairi ya Manispaa hiyo, Bw. Abbas Mwanzori kwa ajili ya malipo ya wahasibu waliofanya kazi muda wa ziada na watumishi, huku kukiwa hakuna fomu zilizojazwa na watumishi hao.

“Hatuwezi kwenda mbele tukiwa na watu wa namna hii. Halmashauri haiwezi kuendelea mtu anatumia vibaya ofisi kwa manufaa yake binafsi. Na kati ya fedha hizo sh. milioni 8.4 mlizitoa kwa kutumia ‘password’ ya Halima (Mhasibu) bila ya kumjulisha na alipogundua akahoji mkamuhamishia sokoni, Naagiza arudishwe mara moja,”.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wajikite katika kufanya kazi vizuri na watambue dhamana waliyopewa na Serikali ambayo ni kuwatumikia wananchi wa Tabora na si vinginevyo. “Tunahitaji kuona mabadiliko ya maendeleo kwenye maeneo yenu ya kazi,”.

Waziri Mkuu amewaambia watumishi hao kuwa ili waweze kupata mafanikio ya kiutendaji lazima wawe na mpangokazi utakamuwezesha kila mmoja wao kutimiza wajibu wake. Mipango hiyo iwe shirikishi kwa kila mtumishi ndani ya idara husika.

Pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya wasimamie utendaji wa pamoja katika idara zilizo ndani ya halmashauri zao na wahakikishe watendaji hao wanawatembelea wananchi katika maeneo  yao ili wanapokutana kwenye Mabaraza ya Madiwani wafanye tathmini ya kina juu ya mafanikio na changamoto zinazowakabili wananchi.

Kadhalika Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete na kukagua maendeleo ya chuo cha Afya kinachojengwa hospitalini hapo pamoja na kutembelea wodi ya akinamama waliojifungua.
Read More

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA NYUZI CHA TABORA NA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA HUO YA KITETE.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Chuo cha Afya katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete  Agosti 18, 2018.  Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia akinamama waliojifungua katika wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete Agosti 18, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua chumba cha upasuaji kilichojengwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete wakati alipotembela hospitali hiyo katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha nyuzi cha Tabora, Urvesh Rajani (kulia) kuhusu    pamba chafu wakati alipotembelea kiwanda  hicho katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha nyuzi cha Tabora, Urvesh Rajani (kulia) kuhusu kinu cha kuchambua pamba  wakati alipotembelea kiwanda  hicho katika Manispaa ya Tabora, Agosti 18, 2018. 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyuzi za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Tabora kiichopo kwenye Manispaa hiyo, Agosti 18, 2018. Kulia  ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Urvesh Rajani. 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama nyuzi za pamba wakati alipotembelea kiwanda cha nyuzi cha Tabora kiichopo kwenye Manispaa hiyo, Agosti 18, 2018. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,  Aggrey Mwanri.

Read More

KERO ZA ARDHI TABORA ZITATATULIWA NA WAZIRI WA ARDHI -MAJALIWA


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi atakwenda katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora ili kutatua kero kubwa za ardhi.

Ameyasema hayo jana jioni (Jumamosi, Agosti 18 ,2018) wakati akizungumza na wananchi wa Manispaa hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chipukizi.

Waziri Mkuu aliyasema hayo baada ya wabunge na wananchi kueleza changamoto kubwa zinazowakabili ikiwe ya migogoro ya ardhi iliyodumu kwa muda mrefu.

“Waziri wa Ardhi atakuja hapa na ramani zake, atakutana na watendaji na kumaliza matatizo yote makubwa ya ardhi na yale madogo madogo yatashughulikiwa na Mkuu wa Wilaya,”.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu alisema wilaya zote zinatakiwa zihakikishe zinakuwa na shule moja ya kidato cha tano na sita kwenye kila tarafa nchini na Serikali itapeleka walimu.

Alisema uwepo wa shule hizo utaamsha ari ya wanafunzi kusoma kwa bidii, jambo litakaloongeza idadi ya wanaoendelea na masomo ya kidato cha tano na sita.

Kadhalika Waziri Mkuu aliwaagiza watendaji wote kuanzia ngazi ya halmashauri hadi vijiji wawasimamie wanafunzi wa kike na wahakikishe wanamaliza masomo bila ya kukatishwa.

“Huu ni mkakati wa Taifa tunataka watoto wa kike wote walindwe ili waweze kumaliza shule na marufuku kukatisha elimu yao, iwe kwa kuwapa ujauzito au kuwaoa, adhabu yake ni kali,”.

Waziri Mkuu jana jioni alimaliza ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora baada ya kuwa amefanya ziara katika wilaya za Igunga, Nzega na Halmashauri ya Manispaa ya Tabora.


Read More

Friday, August 17, 2018

WATENDAJI WA HALMASHAURI HAMUENDI KWA WANANCHI-MAJALIWA


*Asema wingi wa mabango kwenye mikutano ya viongozi ni ishara tosha

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwepo kwa mabango mengi kwenye mikutano ya hadhara  ya viongozi wakuu kunadhihirisha wazi kwamba watendaji wa  Halmashauri hawawatembelei  wananchi katika maeneo yao na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

“Watendaji hamuendi kuwatembelea wananchi na kusikiliza matatizo yao, haiwezekana wawe wanawasubiri viongozi wa juu na kuwasilisha kero zao, sasa jipangeni haya mabango yote mtakuja kuyajibu kwa sababu hoja zote ni za ngazi ya halmashauri,” alisema.

Aliyasema hayo jana jioni (Ijumaa, Agosti 17, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Nzega Mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Parking, ambapo aliwataka viongozi wa halmashauri hiyo kutenga siku maalumu kwa ajili ya kwenda vijijini kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Waziri Mkuu alisema Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.

Alisema Serikali inataka kuona wananchi wakihudumiwa, Makatibu Tawala wa Wilaya wanatakiwa kujiridhisha kwenye halmashauri zao kama watumishi wa umma wanafanyakazi ipasavyo  na iwapo hawaridhishwi wanatakiwa kutoa taarifa kwenye ngazi husika.

“Serikali hii haimlindi mfanyakazi ambaye ni mbadhilifu, mwizi na ambaye hafanyi kazi kwa weledi au anayebagua wananchi eti kwa uwezo wake wa kifedha au rangi au dini yake au chama chake. Hivi vitu havipo katika Serikali kila mwananchi aliyeko Nzega anatakiwa kuhudumiwa,”alisisitiza

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwaagiza Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Wilaya wafuatilie na kujua kiasi cha fedha kinachopelekwa na Serikali katika halmashauri zao kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kujiridhisha kama zinatumika kama ilivyokusudiwa.
“Ni lazima viongozi hao wajue fedha za miradi zilizopatikana katika halmashauri zao ili waweze kwenda kukagua utekelezwaji wa miradi husika na kujiridhisha kama inakidhi viwango na inalingana na kiasi cha fedha kilichotumika,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu alitoa siku 30 kwa  uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Nzega uwe umekamilisha ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule ya sekondari ya Magengati. Miaka minne iliyopita wananchi walijitolea kwa kujenga maboma na kuiachia halmashauri imalizie hatua zilizofuata.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Nzega Vijijini katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Usagali, ambapo alisema ni lazima ujenzi wa vyumba hivyo vya maabara ukamilike. “Haiwezekani miaka minne vyumba hivyo viwe havijakamilika,”.

Read More

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA KATIKA MJI MDOGO WA NZEGA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na  Mbunge wa Viti Maalum, Munde Tambwe wakati alipowasili kwenye uwanja wa Parking katika mji mdogo wa Nzega kuhutubia mkutano wa hadhara, Agosti 17, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye uwanja wa Parking katika mji mdogo wa Nzega kuhutubia mkutano wa hadhara, Agosti 17, 2018. 

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Parking katika mji mdogo wa Nzega Agosti 17, 2018.

Read More

Tuesday, August 7, 2018

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WADAU WA ZAO LA MCHIKICHI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Kilimo Charles Tizeba, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni, Mrajis wa Vyama vya Ushirika Taifa Titto Haule, Mkuu wa JKT Meja Jenerali Martin Busungu, Mkuu wa Jeshi la Magereza Phaustin Kasike na Wadau wa zao la mchikichi, kuhusu maendeleo ya zao hilo, kwenye ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam Agosti 7, 2018.

Read More

Monday, August 6, 2018

WAZIRI MKUU AFUNGUA MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI

*Awasisitiza wayatumie kwa kubadilishana taarifa za kiintelejensia

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka askari wanaoshiriki katika michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki watumie mashindano hayo kama fursa ya kubadilishana taarifa za kiintelijensia, kujadili namna ya kufanya operesheni za pamoja na kwa wakati mmoja.

Pia namna ya kushirikiana katika masuala ya kisheria ambayo mara nyingi yamekuwa vikwazo katika utendaji wao hasa katika shughuli za upelelezi ili kuendelea kuwatia hatiani wahalifu wanaovuka mipaka.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Agosti 6, 2018) wakati akifungua michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki yanayofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam.

“Wote tunaelewa kuwa makosa yanayovuka mipaka kama vile vitendo vya ugaidi, ujangili, usafirishaji haramu wa binadamu, biashara haramu ya silaha ndogo ndogo, bidhaa bandia, utakatishaji wa fedha haramu, biashara ya dawa za kulevya na mienendo ya wahalifu wanaovuka mipaka huathiri amani, usalama na maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kanda yetu,” amesema.

Amesema uhalifu huo hauwezi kuzuiwa pasipo jitihada za makusudi na mikakati ya pamoja ya kupambana nayo, hivyo anatarajia kuwa michezo hiyo itatoa fursa ya kipekee kwa nchi wanachama kubuni mikakati mbalimbali ya kupambana na kuzuia uhalifu hasa ule unaovuka mipaka ya nchi zao.

Waziri Mkuu amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wametimiza lengo la Shirikisho la Wakuu wa Polisi la Ukanda wa Afrika Mashariki. “Hivyo tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuendeleza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ambayo yameanza kuonekana katika Nchi zetu,”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka askari hao waendeleze ushirikiano huo kwa usalama wa ukanda wa Afrika Mashariki kwa sababu michezo ni moja ya nyenzo za kuleta na kuimarisha usalama na amani kwenye jamii. 

Amesema kaulimbi ya mwaka huu ambayo ni ‘Michezo katika Kukuza Ushirikiano wa Kikanda wa Polisi, Amani na Usalama”. (“Sports for Promoting Police Regional Cooperation, Integration, Peace and Security”). inajieleza yenyewe kuhusu umuhimu wa kushirikiana katika kuleta amani na usalama.

Ufunguzi wa mashindano hayo yanayoshirikisha nchi saba kati 14 za Ukanda wa Afrika Mashiriki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Uganda, Kenya, Sudani, Sudani Kusini, Burundi na Rwanda yameanza leo na yanatarajia kukamilika Agosti 12, 2018.
Read More

WAZIRI MKUU AFUNGUA MICHEZO YA MAJESHI YA POLISI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia mashindano ya mpira wa miguu kati ya timu ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Uganda,kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wananchi, katika ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es bAgosti 6, 2018.
 Wanamichezo kutoka Jeshi la Polisi la Tanzania,  wakipita mbele ya mgeni rasmi, ambaye ni Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi  ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018.
Wanamichezo kutoka Jeshi la Polisi la Rwanda  wakipita mbele ya mgeni rasmi, ambaye ni Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018.

Kikundi cha Ngoma cha Maringo kikitoa burudani, kwenye ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipuliza firimbi kuashiria ufunguzi rasmi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018



Wachezaji wa timu ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Uganda, wakicheza mpira mara baada ya ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018.

Wachezaji wa timu ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Uganda, wakicheza mpira mara baada ya ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki yaliyofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018.

 Wachezaji wa timu ya Jeshi la Polisi la Tanzania na Uganda, wakicheza mpira mara baada ya ufunguzi wa Mashindano ya Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki  katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Agosti 6, 2018

Read More

Saturday, August 4, 2018

WAZIRI MKUU AUPONGEZA UONGOZI WA MAKUMBUSHO


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa kuchora ramani ya Tanzania katika Kijiji cha Makumbusho ambayo itatumika kwenye ujenzi wa nyumba za utamaduni wa makabila mbalimbali nchini.

Amesema uamuzi huo utarahisisha watu kufika kwa urahisi katika nyumza za tamaduni za mikoa yao kwa kuwa watakuwa wanatumia ramani Tanzania.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumapili, Agosti 4, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa mkoa wa Lindi kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania katika Kijiji cha Makumbusho, jijini Dar es Salaam.

“Kwa kutumia ramani hii kila mkoa utaweza kufika kwenye eneo lake kwa kutumia ramani ya Tanzania na mkoa wa Lindi tayari umeshaoneshwa eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba inayozingatia utamaduni wetu,” alisema.

Alisema kwa tamaduni za makabila ya mkoa wa Lindi nyumba zote hujengwa kwa udongo na kuezekwa kwa makuti upande wa maeneo ya pwani ya upande mwingine huezeka kwa nyasi, ambapo aina zote zitajengwa ili kuwakilisha tamaduni za wakazi wa mkoa huo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaasa wananchi wa mkoa wa Lindi ambao kwa mwaka huu ndio waandaaji wa tamasha hilo wadumishe mshikamano wao ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea katika kuboresha maendeleo.

Alisema katika tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuanza Agosti 26 hadi 29 wahakikishe wanapeleka kila kitu ambacho kinahusiana na utamaduni wa mkoa huo ili kuwawezesha Watanzania wengine wajue kama vyakula na mavazi .

Pia alishauri wawepo wazee wenye kujua historia ambao watasimulia utamaduni wa wananchi wa Lindi pamoja na kutambulisha ngoma zao za utamaduni. “Halmashauri zote za mkoa wa Lindi zitumie fursa hii kutangaza vivuti vya utalii vilivyopo na Kilwa walete mtu atakayeelezea kuhusu magofu,”.

Waziri Mkuu alisema tamasha hilo ni muhumu kwa sababu utamaduni ulianza kufifia nchini kutokana  na mabadiliko ya kiteknolojia jambo ambalo lingeweza kuuondoa katika kumbukumbu, hivyo aliwashauri siku ya tamasha hilo wavae nguo za kitamaduni kulingana na kabila husika.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwapongeza viongozi wa mkoa wa Lindi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Bw. Godfrey Zambi kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri mwenendo wa zao la korosho.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla alisema mwaka huu Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania linawakilishwa na jamii kutoka mkoa wa Lindi na kwamba anatumaini watafanya vizuri kwa kuwa uwezo na nia wanayo.

Profesa Mabula alisema mwaka 1994 Bodi ya Makumbusho ya Taifa ilianzisha siku ya utamaduni ili kutoa fursa kwa jamii mbalimbali nchini kuonesha utajiri walionao katika tamaduni zao na ufanisi wa siku hiyo unatokana ushirikishwaji wa wanajamii husika.
Read More

Friday, August 3, 2018

TANZANIA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA KUWAIT-MAJALIWA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiagana na Balozi wa Kuweit Nchini Tanzania .Jasem Ibrahim AI Najem ,ambaye amemaliza  muda wake .Balozi Jasem. amekutana na Waziri Mkuu kwa lengo la kumuaga leo Julai 3/u Jijini Dar es salaam
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mazungumzo na Balazi wa Kuweit Mh Jasem Ibrahim AI Najem ,ambaye amemaliza  muda wake .Balozi Jasem. amekutana na Waziri Mkuu kwa lengo la kumuaga leo Julai 3/2018 Jijini Dar es salaam


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano na Serikali ya Kuwait katika sekta mbalimbali ikiwemo ya usafiri wa anga.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Agosti 3, 2018) wakati alipokutana na Balozi wa Kuwait nchini, Balozi Jasem Al Najemkatikamakazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Balozi Al Najem ambaye anamaliza muda wake, amekutana na Waziri Mkuu kwa lengo la kumuaga na kwamba leo anatarajia kuondoka nchini na kurejea Kuwait.

Waziri Mkuu amemshukuru balozi huyo kwa ushirikiano alioutoa Tanzania katika kipindi chote cha uwakilishi wake na kwamba nchi hizo zinatarajia kuanza ushirikiano katika usafiri wa anga.

Amesema Kuwait ni moja kati ya nchi rafiki, ambayo imeshirikiana na Tanzania katika uboreshaji wa shughuli za maendeleo kupitia Balozi Najem, hivyo wataendelea kumkumbuka.

“Balozi Najem amejitoa sana katika kuwasaidia Watanzania hususan kwenye miradi ya huduma za jamii kwa kupeleka maji mashuleni, vituo vya afya, zahanati na hospitalini,”.

“Pia Ubalozi wa Kuwait umesaidia kuleta vifaa tiba katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na madaktari katika baadhi ya hospitali nchini. Ushirikiano huu umeleta tija sana,” amesema.

Waziri Mkuu amesema mbali na miradi hiyo ya huduma za jamii, pia balozi huyo ameshiriki kuendeleza Sekta ya utalii nchini kwa kuleta watalii wengi kutoka nchini Kuwait kuja Tanzania.

Waziri Mkuu meongeza kuwa Balozi Al Najem ameshiriki kikamilifu katika kuratibu shugughuli zote za maendeleo kati ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kuunganisha sekta binafsi.

Kadhalika, Waziri Mkuu amemuhakikisha balozi huyo kwamba Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Kuwait na kwamba ipo tayari kumpokea mwakilishi mwingine.

Kwa upande wake, Balozi Al Najem ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano iliyompa katika kipindi chote alichokuwa akiiwakisha Serikali ya Kuwait nchini.

Amesema tangu alipowasili nchini amekuwa akipewa ushirikiano mkubwa na viongozi wote wa Serikali jambo lililomrahisishia utekelezaji wa majukumu yake nchini.
Read More