Na. OWM, Dar es salaam.
Tangu mwaka 2015 Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), kilianzisha rasmi
Tuzo ya Mwajiri Bora kwa kila mwaka, lengo la tuzo hizo ni kuwatambua Waajiri wenye mikakati bora ya usimamizi wa rasilimali
watu kwa ajili ya kuongeza uzalishaji kibiashara na
kuwahamasisha Waajiri kufuata taratibu za
kitaifa na kimataifa katika uendeshaji wa biashara zao, ambapo makampuni wanachama
kutoka sekta binafsi hushindanishwa kwa kila mwaka.
Kutokana
na tuzo hizo kuwashirikisha kwa wingi wanachama wa chama hicho wa sekta
binafsi, ambapo kwa mwaka huu , Katika ushindi wa
jumla Tanzania Breweries Limited (TBL) wameweza Kuibuka kinara na kushika
nafasi ya kwanza, wakifuatiwa na Geita Gold Mines na wa tatu wakiwa Puma Energy.
Serikali
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imedhamiria
Tuzo za mwakani 2020 kwa kushirikiana na
ATE pamoja na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA),
kuishindanisha sekta ya Umma ili ushindani huo unaofanywa katika sekta binafsi
uyashirikishe mashirika ya umma kwa
kiwango kikubwa kwa ajili ya kuweza
kuboresha mazingira ya kazi na Ajira na
kuongeza tija hapa nchini.
Akiongea
katika wa hafla ya Tuzo ya mwaajiri bora wa mwaka 2019
iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), jijini Dar es salaam, tarehe 18 Desemba, Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,
na watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama, aliye mwakilisha Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amefafanua kuwa ustawi wa
wafanyakazi sio kwa sekta binafsi peke yake ni pamoja na sekta ya umma, hivyo
ili sekta binafsi iwe injini ya kuendesha uchumi wa Taifa, ni lazima pia sekta ya Umma nayo iwekeze
rasilimali watu ili kuweza kuongeza tija katika maeneo ya kazi.
“Niipongeze ATE kwa kuwa na Tuzo hizi, Tungependa kuona ni mashirika
gani ya Umma yanafanya vizuri katika kuangalia ustawi wa wafanyakazi na kuleta
tija nchini. Maamuzi ya kuwa na washindi wa jumla katika makundi ya kisekta yataongeza chachu
mpya ya mashindano ambayo itakuza sekta mbalimbali na hatimaye yataboresha na
kuleta tija katika ukuaji wa uchumi wa Taifa letu” Amesisitiza, Mhe. Mhagama.
Waziri Mhagama ameitaka ATE kuendelea kutoa mafunzo katika maeneo ya kazi
na juu ya sheria za kazi na Usimamizi wa rasilimali watu, ambapo kutokana na
mafunzo hayo yatasaidia kupunguza migogoro mahala pa kazi na hivyo kujenga
mazingira tulivu ya kibiashara ndani ya maeneo ya kazi. lakini pia mafunzo hayo yatawasaidia wafanyakazi kukidhi ushindani wa mazingira ya kibiashara kwa sasa.
“Takwimu zinaonesha mafunzo ambayo yameratibiwa na kuandaliwa na ATE
kuwa vijana 1, 437, waliidhinishwa na
kupata nafasi kwa waajiri huku kwenye tovuti ya serikali wapo vijana 6,919, walijiandikisha hadi Julai mwaka huu, hivyo
nitoe rai kwa waajiri wapeni fursa vijana ili waweze kujifunza kwa vitendo, niipongeze Kampuni ya TCC kwa kuwa mstari wa
mbele kutoa nafasi kwa vijana kujifunza kwa vitendo hapa nchini.” Amesema ,
Mhe. Mhagama.
Aidha. Amewataka waajiri kuendelea kushirikiana na serikali katika kutekeleza
mpango wa kitaifa wa miaka 5 wa kukuza ujuzi ambao hufadhiliwa na serikali
kupitia tozo ya kukuza ujuzi mahala pa kazi ili kuweza kuongeza ujuzi kwa
vijana na kutatua tatizo la ajira nchini huku akiwasisitiza kuzingatia sheria
za kazi zinazo onya ajira kwa watoto.
“Utafiti wa hali ya maambukizi
mapya ya UKIMWI hapa nchini unabainisha kuwa katika maabukizi mapya 72,000 kwa
mwaka 40% ya maabukizi hayo ni kwa vijana kati ya miaka 15-24, ambapo 80% ya
maabukizi hayo ni kwa watoto wa kike ” Hivyo waajiri mnayo kazi ya kufanya katika kuilinda
nguvu kazi hii” Alisisitiza Mhagama.
Mhe. Mhagama amewataka waajiri kuendelea kuchangia katika mfuko wa
fidia kwa wafanyakazi ili kuweza kuwakinga wafanyakazi dhidi ya majanga
yatokanayo na kazi. Pia amewasisitiza waajiri kuzingatia haki, usawa mahala pa kazi ili kuondoa unyanyasaji wa kijinsia
katika maeneo ya kazi hivyo katika kuhakikisha hilo linafanikiwa serikali
tayari imeshazindua mkakati wa Kitaifa wa usawa wa kijinsia mahala pa kazi.
Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye ulemavu) Mhe. Stella Ikupa amewapongeza ATE kwa juhudi zao
za kuunga juhudi za serikali za kuwawezesha watu wenye Ulemavu hivyo amewasihi
waendelee kujenga mazingira rafiki mahala pa kazi ili watu wenye ulemavu na
watu wenye mahitaji maalum waweze kufanya kazi
na kuchangia kwenye maendeleo ya Taifa.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ATE, Jayne Nyimbo amefafanua kuwa
ushirikiano wanaoupata serikalini wa kushirikiana na sekta binafsi umesaidia
kuboreshwa kwa tuzo hizo ambazo zimekuwa zikiboresha mazingira ya kazi na ajira
hapa nchini.
Awali akiongea katika Hafla hiyo, Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE, Dkt Aggrey Mlimuka amesema tuzo ya Mwajiri
Bora wa Mwaka kwa mwaka huu imefanyia kazi ushauri uliotolewa na seriikali mwaka na
Waziri Mhagama kuwa katika tuzo za mwaka
huu ziongeze vipengele vipya vitatu (3) ambavyo viezifanya tuzo za mwaka huu kuwa
na Jumla ya vipengele 38 kutoka vipengele 35.
"Vipengele vilivyoongezeka ni Mwajiri
Bora anayeendeleza Mafunzo ya Ujuzi wa Kazi kwa wahitimu (Internship), Mwajiri
Bora anayetoa mafunzo ya Uanagenzi (Apprentiship), Mwajiri Bora anayezingatia
Haki Rasilimali ijulikanavyo kama “Local Content”, " Alisema, Dkt. Mlimuka.
Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka hufanyika kila mwaka na Chama cha Waajiri
Tanzania (ATE), ambapo zilianza mwaka 2005. Wanachama i kutoka sekta binafsi na wengine wasio wanachama wa moja kwa
moja wanaotoka makampuni ya biashara na baadhi ya mashirika ya umma wameshiriki
Tuzo hizo za mwaka huu.
MWISHO
Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi TUCTA Said Wamba akizungumza kwa
niaba ya wafanyakazi na kuwashukuru Chama cha Waajiri Tanzania ATE kwa kutambua
mchango wa wafanyakazi wawapo mahala pa kazi. wakati wa hafla ya Tuzo ya
mwaajiri bora wa mwaka 2019 iliyoandaliwa na Chama hicho katika Hotel ya Serena
jijini Dar es Salaam, tarehe 18 Desemba,
2019.
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.