Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka udongo kwenye kaburi la Waziri Kiongozi wa Zanzibar Mstaafu, Brigedia Jenerali Mstaafu, Ramadhani Haji Faki yaliyofanyika Mkwajuni Zanzibar, Machi 29, 2020. |
Home
Archives for March 2020
Sunday, March 29, 2020
MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA WAZIRI KIONGOZI MSTAAFU WA ZANZIBAR
✔
HABARI PMO
3/29/2020 07:46:00 PM
MAJALIWA ATOA POLE KWA FAMILIA YA SOKOINE
✔
HABARI PMO
3/29/2020 09:07:00 AM
Thursday, March 26, 2020
MAJALIWA: KAMATI ZA MAAFA ZIUNGANE NA WARATIBU WA KUKABILIANA NA CORONA
✔
HABARI PMO
3/26/2020 08:14:00 PM
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza kamati za Maafa katika ngazi za mikoa na wilaya ziungane na waratibu wa kupambana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) waliopo katika maeneo yao.
Pia, Waziri Mkuu amewasisitiza Watanzania waendelee kujikinga na ugonjwa huo kwa kuhakikisha wanajiepusha na misongamano isiyokuwa ya lazima na hata wakienda kwenye maeneo ya kutolea huduma kama sokoni, vituo vya mabasi wapeane nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 26, 2020) wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Kitaifa cha Kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma. Kikao hicho kimehusisha wajumbe kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ipeleke wataalamu katika maeneo yenye mahitaji makubwa kama kwenye viwanja vya ndege, vituo vya mabasi na bandarini.
“Lengo letu ni kuhakikisha nchi inabaki salama hivyo Watanzania tuendelee kuwa na tahadhari ya kutosambaa kwa ugonjwa huu na pale tunapokwenda kwenye maeneo ya kutolea huduma tujipe nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine.”
Waziri Mkuu amesema kamati hiyo inatakiwa ifuatilie na isimamie vizuri ili kuhakikisha watu wote wanaoingia nchini wanapimwa na wanafuatilia ili kujua historia zao za safari katika kipindi cha siku 14, lengo likiwa ni kuzuia maambukizi hayo yasisambae kwa jamii.
Amesema watu wote waliopewa dhamana ya kuratibu zoezi la kupeleka watu walioko kwenye karantini, wahakikishe wahusika wanafika kwenye hoteli walizozichagua. Pia Serikali inafanya utaratibu wa kutenga maeneo ambayo watu watakuwa wanakaa bila gharama na yatakuwa na huduma zote muhimu.
Pia, Waziri Mkuu amevishukuru vyombo vya habari nchini kwa ushirikiano wanaoutoa kwa Serikali katika kuelimisha umma namna ya kujikinga na virusi vya corona, ambapo amevitaka viendelee na utaratibu huo kwani utasaidia wananchi kupata elimu na kuweza kujikinga na maabukizi hayo.
Machi 23, 2020, Waziri Mkuu aliunda kamati tatu kwa ajili ya kukabiliana na homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi ya corona (COVID-19).
Kamati hizo ni ya Kitaifa ambayo inaongozwa na Waziri Mkuu na itahusisha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Wenye Ulemavu, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Wengine ni Waziri Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Pia, Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Msemaji Mkuu wa Serikali, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Fedha wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Katika kikao cha leo, Waziri Mkuu ameongeza wajumbe wawili ili waongeze nguvu katika kukabiliana na virusi vua corona ambao ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
(mwisho)
MAJALIWA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA KITAIFA YA KUKABILIANA NA CORONA
✔
HABARI PMO
3/26/2020 07:51:00 PM
Tuesday, March 24, 2020
MAJALIWA AONGOZA KIKAO KAZI CHA MAWAZIRI NA MAKATIBU WAKUU KUHUSU CORONA
✔
HABARI PMO
3/24/2020 02:36:00 PM
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID – 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID – 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika kikao kazi cha Mawaziri na Makatibu Wakuu kuhusu ugonjwa wa Corona (COVID – 19) nchini kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma, Machi 23, 2020. |
Monday, March 23, 2020
KAMATI YA USIMAMIZI MAAFA RUFIJI YATAKIWA KUREJESHA MIUNDOMBINU ILIYOATHIRIKA NA MAFURIKO
✔
Hamidu
3/23/2020 05:23:00 PM
KAMATI YA USIMAMIZI MAAFA RUFIJI YATAKIWA KUREJESHA MIUNDOMBINU ILIYOATHIRIKA NA MAFURIKO
Na. OWM, RUFIJI
Kufuatia miundombinu ya
barabara, shule na Zahanati kuathirika kutokana na maafa ya mafuriko wilayani
Rufiji. Kamati za Usimamizi wa maafa za wilaya hiyo zimeshauriwa kuchukua hatua
za haraka katika kukabiliana na maafa hayo kwa kurejesha hali ya kawaida ya
miundombinu iliyoathirika na maafa hayo katika kata zote 13 za wilaya hiyo.
Kata ya Muhoro na Chumbi ni miongoni mwa kata
zilizoathirika sana na maafa hayo, ambapo kwa sasa madaraja matatu yaliyopo
barabara ya Nyamwage- Utete inayoelekea makao makuu ya wilaya hiyo tayari
yameathirika, Daraja lililopo kwenye barabara ya kuelekea Mradi wa kufua Umeme
wa Mwalimu Nyerere nalo limeathirika pamoja na Daraja la Mkapa nalo limeanza
kupata athari ya mafuriko hayo.
Akiongea mara baada ya
kukagua athari za maafa na kukabidhi
misaada kwa waathirika wa maafa hayo tarehe 23 Machi 2020, Mkurugenzi Idara ya
Uratibu wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, ameeleza
kuwa Kamati za Usimamizi wa kuanzia
ngazi ya kijiji hadi wilaya, kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa maafa Na. 7 ya mwaka 2015
zinawajibika kutekeleza operesheni za dharura.
“Nimezishauri kamati za usimamizi wa maafa katika wilaya hii kuwa na mipango ya
muda mfupi ya kuhakikisha barabara zinapitika kipindi chote ili wananchi
wasishindwe kutumia miundombinu hiyo, kwani zipo barabara zinaunganisha mikoa ya
kusini na zipo barabara zinawasaidiia wananchi kuweza kuzifikia huduma za
kijamii”amesisitiza Kanali Matamwe.
Awali akiongea mara baada ya kupokea misaada
kutoka kwa Idara ya Uratibu wa maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mkuu wa wa wilaya
hiyo, Mhe. Juma Njwayo amefafanua kuwa
misaada hiyo itakuwa ni msaada mkubwa kwa kuwa hadi sasa wapo watu zaidi ya elfu
ishirini wameathirika na maafa hayo kwa kuwa zidi ya nyumba mia moja
zimezingirwa na maji.
“Tunaishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutuletea
Magodoro, Mikeka, Vyandarua, Ndoo na Sabuni na naamini kamati za maafa zitawajibika
kugawa vifaa hivi kwa mujibu wa taratibu za menejimenti ya maafa. Wilaya
tunaendelea na kukabiliana na maafa kwa
kaya takribani elfu sita, kama
tulivyoshauriwa kuhusu miundombinu, kwa kushirikiana na TANROADS tunaendelea
kwa kasi kuchukua hatua za kurejesha miundombinu yote iliyo athirika ”
Amesisitiza Mhe. Njwayo.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Mhe. Mohamed
Mchengerwa, ameeleza kuwa tangu maafa ya mafuriko yatokee wilayani humo, wamekuwa
wakipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Ofisi hiyo, kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
mwenye dhamana ya masuala ya maafa Mhe. Jenista Mhagama, ambapo amekuwa akiwatuma
wataalamu na kufika kwa wakati kwa ajili ya kuzisaidia kamati za usimamizi wa maafa.
“Wananchi wa Rufiji wanafarijika sana kwa jinsi
serikali yao inavyowajali, tunatambua mafuriko yamewaathiri sana ikiwemo na
kuharibika kwa vyakula vyao, tunaomba
mtuletee mbegu ama chakula cha bei nafuu na wananchi hawataki chakula cha
bure, sisi tunataka tufanye kazi na tukipata mbegu tutafanya kazi ya kilimo
mara mafuriko yakiisha” amesisitiza , Mhe. Mchengerwa.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Mamlaka ya Hali hewa
iliyotolewa mwezi Februari mwaka huu imeeleza kuwa kutakuwa na mvua za juu ya
wastani katika eneo kubwa la nchi kati ya mwezi Machi hadi mwezi Mei, mwak huu,
ambapo mvu ahizo zilitarajiwa kuanza kati ya wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi
Machi na kutaraji akumaliziaka kati ya wiki ya kwanza au ya pili yamwezi Mei.
Hivyo kutokana na mvua hizo wananchi hawanbudi kuchukua tahadhari za athari za
mvua hizo.
MWISHO.
KATIBU MKUU MWALUKO AWAASA WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA
✔
HABARI PMO
3/23/2020 05:02:00 PM
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Ernajoyce Hallo akichangia jambo wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi Jijini Doodma.
|
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu hoja wakati wa kikao cha Baraza hilo.
|
Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Waziri Mkuu wakifuatilia hoja wakati wa kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi hiyo Jijini Dodoma.
|
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Paschal Vyagusa akizungumza wakati wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika Machi 23, 2020 Jijini Dodoma.
|
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Augustino Tendwa akichangia jambo wakati wa kikao cha baraza hilo kilichofanyika Machi 23, 2020 Jijini Dodoma.
|
KATIBU MKUU MWALUKO AWAASA WATUMISHI OFISI YA WAZIRI MKUU KUENDELEA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA VIRUSI VYA CORONA
✔
HABARI PMO
3/23/2020 04:52:00 PM
NA. MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziti Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi. Dorothy Mwaluko amewaasa watumishi wa ofisi yake kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya mlipiko wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona nchini ili kuendelea kupambana na maambukizi ya virusi hivyo.
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichohusu Mapitio ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na Makadirio ya Mpango na Bajeti ya Ofisi hiyo kwa mwaka 2020/2021kilichofanyika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma tarehe 23 Machi, 2020.
Katibu Mkuu aliwaeleza watumishi kuendelea kujilinda katika mazingira yote kwa kuhakikisha wanafuata maelekezo yanayotolewa na Serikali ili kulinda na janga hilo lililopo nchini.
“Watumishi lazima muwe kielelezo kwa kuzingatia ofisi hii ndiyo inayoratibu na kusimamia shughuli zote za Serikali hivyo lazima mzingatie tahadhari zote ili kuepuka mlipuko wa virusi vya Corona katika nchi yetu ”alisema Mwaluko
Aliongezea kuwa, kila Mtanzania ana nafasi ya kujilinda kuanzia ngazi ya mtu mmoja hadi Taifa kwa kuangalia namna ugonjwa ulivyoathiri nchi zingine na kusababaisha vifo vya watu wengi.
Mwaluko aliwaasa watumishi waendelee kunawa mikono na kuepuka makusanyiko yasiyo ya lazima huku wakijihadhari kwa kuzingatia matumizi sahihi ya vifaa saidiizi katika kujikinga na maambuki ya virusi vya Corona.
Aliongezea kuwa, nchi imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuona inakabiliana na mlipuko wa COVID 19 kwa kutoa elimu kwa umma juu ya kujikinga na maambukizi na kuhakikisha idadi ya wanaoathiriwa na Corona inapungua badala ya kuongezeka.
“Kila mtumishi aelewe kuwa hadi sasa hakuna dawa wala chanjo ya virusi hivyo, na ugonjwa huu upo nchini, hili silipuuzwe na lazima tuzingatie tuwapo kazini kila mmoja wetu awe makini na endapo ukiona una dalili moja wapo ya ugonjwa huu ni vyema kutoa taarifa ili kuepuka madhara kwa wengine,”alisisitiza Mwaluko
Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUGHE wa ofisi hiyo, Bw. Mohamed Athuman alimpongeza Katibu Mkuu kwa kuchukua fursa ya kuwakumbusha watumishi na kuendelea kutoa elimu juu ya kujikinga na kuwalinda wengine.
“Leo tumepata nafasi ya kukumbushwa na kiongozi wetu kuhusu namna bora ya kuendelela kuwa makini na kuzingatia maelekezo ya Serikali ili kuepuka maambukizi ya virusi vya Corona,”alisema Athuman
Aidha aliendelea kutoa wito kwa watumishi wa ofisi hiyo kuona namna bora ya kuyazingatia maelekezo yanayotolewa ili kuendelea kuwa na afya bora katika utekelezaji wa majukumu wawapo kazini.
“Sisi viongozi wa TUGHE tunaunga mkono tahadhari zinazotolewa na viongozi wetu , hivyo ni vyema tukazingatia na kukumbuka kuwa kinga ni bora kuliko tiba,”alieleza
Sambamba na hilo alieleza kuwa kila mtumishi wa umma ana nafasi nzuri ya kuendelea kuunga mkono na kuwa kinara namba moja katika vita kwa kuachana na mizaa na kuendelea kuelimishana kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa kwa ujumla kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo hilo.
Naye mmoja wa wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Numpe Mwambenja alieleza wameendelea kuchukua tahadhari zote zinazotolewa kwa kuzingatia mchango wa watumishi wa umma katika nchi na maendeleo kwa ujumla.
“Ofisi imetimiza wajibu wake kwetu, na sisi tunapaswa kuwajibika na tuhakikishe tunapambana na wanaopotosha umma kwa kuhakikisha tunasambaza taarifa sahihi zinazotolewa na Serikali yetu,”alifafanua Bi.Numpe.
Sunday, March 22, 2020
KAMATI YA USIMAMIZI MAAFA KILOMBERO YATAKIWA KUFANYA TATHMINI YA ATHARI ZA MAAFA YA MAFURIKO
✔
Hamidu
3/22/2020 03:36:00 PM
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Nyange, wilayani Kilombero, wakitoa vifaa vyao kwenye makazi yao yaliyozingirwa na maji kutokana na athari ya maafa ya mafuriko |
Na. OWM, MOROGORO
Kufuatia Kaya 250 katika kata ya Msolwa Stesheni katika kijiji cha Nyange Wilayani Kilombero kuathirika na athari za maafa ya mafuriko. Kamati ya Usimamizi wa Maafa ya Wilaya hiyo imeelekezwa kufanya tathmini ya awali kwa kata ya Mbanane na Kichangani ambazo takribani watu 350 wameathiriika na maafa hayo yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini.
Akiongea mara baada ya kukagua athari za maafa katika kata hizo Machi
20, 2020, wilayani Kilombero, Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya maafa Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kanali Jimmy Matamwe, amesema tathmini ya awali ya athari za maafa
katika kata hizo hainabudi kufanyika kwa haraka ili kubaini hatua za kuchukua
katika kukabiliana na maafa hayo.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa maafa
Na. 7 ya mwaka 2015, inaainisha majukumu ya kamati za usimamizi wa
Maafa kuanzia ngazi ya Kijiji hadi mkoa, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo,
jukumu la msingi ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya usimamizi wa maafa katika
ngazi husika, pamoja na Kuratibu na kusimamia shughuli za usimamizi wa
maafa na operesheni za dharura ndani ya Kijiji wilaya au mkoa. Hivyo
kamati hii haina budi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria.”amesisitiza Kanali Matamwe
Awali akieeleza hatua ambazo
kamati ya Menejimenti Usimamizi wa Maafa ya Wilaya hiyo ilizo zichukua, Mkuu wa
Wilaya ya Kilombero, Mhe. James Ihunyo, amefafanua kuwa hadi kufikia tarehe 20
Machi 2020, kamati hiyo ilikuwa imefanikiwa kuwaokoa watu 350 ambao wamehifadhiwa
kwenye shule ya sekondari Nyange.
“Tunaishukuru serikali
kupitia, Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya uratibu wa shughuli za maafa kwa miongozo, lakini pia na kufika kwa wakati
katika kata zetu, tumefurahi na mmetuletea blanketi ambayo naamini yatawasaidia
waathirika wa maafa haya ambao tumewahifadhi hapa shuleni. Kwa sasa wapo
wanaume 172 na wanawake 178 huku watoto ni 30 ambao tumewahifadhi” Ameeleza Mhe. Ihunyo.
Kwa mujibu wa Taarifa ya
Mamlaka ya Hali hewa iliyotolewa mwezi Februari mwaka huu imeeleza kuwa
kutakuwa na mvua za juu ya wastani katika eneo kubwa la nchi kati ya mwezi
Machi hadi mwezi Mei, mwak huu, ambapo mvu ahizo zilitarajiwa kuanza kati ya
wiki ya kwanza au ya pili ya mwezi Machi na kutaraji akumaliziaka kati ya wiki
ya kwanza au ya pili yamwezi Mei. Hivyo kutokana na mvua hizo wananchi
hawanbudi kuchukua tahadhari za athari za mvua hizo.
MWISHO.
Saturday, March 21, 2020
WAZIRI MKUU AONYA WANAOPOTOSHA KUHUSU CORONA
✔
HABARI PMO
3/21/2020 02:43:00 PM
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameonya juu ya upotoshwaji na utoaji holela wa taarifa kuhusu ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababisha na virusi vya corona (COVID 19) unaofanywa na watu mbalimbali nchini.
Amesema kuanzia sasa taarifa hizo zitatolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na ikilazimika zitatolewa na Waziri Mkuu na ikilazimika sana zitatolewa na viongozi wakuu wa nchi ili kuepusha mikanganyiko.
Waziri Mkuu ametoa onyo hilo leo (Jumamosi, Machi 21, 2020) wakati akizungumza na Wakuu wa Mikoa yote nchini, Makatibu Tawala wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Mikoa kwa njia video kutokea ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.
Kufuatia hali hiyo, Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ifuatile watu wote wanaofanya upotoshaji kwa kupitia mitandao ya kijamii ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
“Watu wote wanaopotosha umma na kuleta taharuki kuhusu ugonjwa wa corona badala ya kuelimisha namna ya kujikinga, wafuatiliwe na kuchukuliwa hatua,” amesisitiza.
Waziri Mkuu amesema licha ya hali ya maambukizi ya corona nchini kutia matumaini, viongozi hao hawana budi kupeana taratibu za namna ya kukabiliana na tatizo hilo.
“Wakuu wa mikoa kila mmoja ahakikishe eneo lake linakuwa salama na endapo kutakuwa na mgonjwa tumieni zahanati ambazo bado hazijaanza kutumika kwa ajili ya kutolea huduma kwa wagonjwa wa corona,” amesema.
Amewataka wakuu hao wa mikoa waimarishe utoaji wa elimu kwa umma na ikiwezekana watumie magari ya matangazo ili wananchi waelewe athari za ugonjwa huo na namna ya kujikinga pamoja na kuwaondolea hofu ili waweze kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo.
Pia amewataka watumie redio za kijamii katika maeneo yao kutoa elimu kwa umma juu ya kujikinga na ugonjwa huo na wasimamie maeneo ya utoaji huduma kama vituo vya mabasi na kuhakikisha kila abiria anakaa kwenye kiti.
“Nendeni kwenye maeneo ya mikusanyiko, vituo vya mabasi kutoa elimu kwa umma na kuwaondoa hofu. Upande wa maofisini, viwandani na kwenye mgodi kuwe na utaratibu wa kutoa elimu kwa wafanyakazi kila siku asubuhi watumie hata robo saa kabla ya kuanza kazi waelekezwe namna ya kujikinga.”
Waziri Mkuu amesema kwa wanaoishi katika maeneo ya makambi, viongozi wao waelekezwe namna ya kutoa elimu ya kujikinga na corona na pia wadhibiti utorokaji na Serikali kwa upande wake inaendelea kuimarisha udhibiti mipakani, uwezo wa kupima sampuli na upatikanaji wa vifaa.
Amewataka wakuu hao wa mikoa, wawashirikishe wakuu wa wilaya kwenye mikoa yao ili wasimamie utekelezaji wa maagizo hayo.
Wakati huohuo,Waziri Mkuu amewaagiza wakuu hao wa mikoa wahakikishe wanawafuatilia na kuwachukulia hatua wafanyabiashara wote watakaobainika kuongeza bei kwa bidhaa ambazo zinatumika katika udhibiti wa maambukizi ya ugonjwa wa corona.
Kuhusu viongozi wa dini, Waziri Mkuu amewaomba waendelee kushirikiana na Serikali katika kuwaelimisha waumini wao wote kuzingatia tahadhari za ugonjwa huu. Pia awaendelee kuliombea Taifa.
(mwisho)
MAJALIWA AZUNGUMZA NA WAKUU WA MIKOA KWA NJIA YA VIDEO
✔
HABARI PMO
3/21/2020 01:25:00 PM
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa , Makatibu Tawala wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Mikoa kwa njia ya video akiwa ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma, Machi 21, 2020. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wakuu wa Mikoa , Makatibu Tawala wa Mikoa na Waganga Wakuu wa Mikoa kwa njia ya video akiwa ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma, Machi 21, 2020. |
Tuesday, March 17, 2020
SERIKALI YAZIFUNGA SHULE ZOTE KUANZIA LEO SABABU YA CORONA
✔
Hamidu
3/17/2020 05:52:00 PM
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
SERIKALI
YAZIFUNGA SHULE ZOTE KUANZIA LEO SABABU YA CORONA
SERIKALI imesema shule zote za awali, msingi na
sekondari zitafungwa kwa siku 30 kuanzia leo Machi 17, 2020.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumanne, Machi 17, 2020) wakati akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salam.
Amesema wanafuzi wa kidato
cha sita walipaswa kuanza mitihani Mei 4, 2020 lakini nao pia watapaswa kusibiri
Wizara ifanye utaratibu mwingine kulingana na matokeo ya hali ya maambukizi.
Amesema mikusanyiko yote mikubwa ya ndani na nje isiyo
ya lazima imesitishwa kuanzia sasa ikiwemo shughuli za michezo, matamasha ya
muziki, mikutano mbalimbali ikiwemo ya shughuli za kisiasa, mahafali na shughuli
nyingine za kijamii.
Amezitaka wizara na taasisi zizitishe semina,
warsha, makongamano na mikutano yote hapa nchini ambayo inahusisha washiriki
toka nchi zenye maambukizi makubwa. “Watanzania wenye safari zisizo za lazima
kwenye nchi zenye maambukizi makubwa, wanashauriwa wasitishe safari hizo,” amesisitiza.
Akielezea hatua nyingine zinazochukuliwa na Serikali
ili kudhibiti ugonjwa huo, Waziri Mkuu amesema: “Serikali imesitisha michezo
yote inayokusanya makundi ya watu ikiwemo Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL), Ligi
Daraja la Kwanza (FDL), Ligi Daraja la Pili (SDL) na aina nyngine. Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iziandikie taasisi zake.”
Pia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe
maeneo yote yaliyobainishwa na kutengwa (vituo vya huduma na ufuatiliaji) kwa
ajili ya kuwahudumia wagonjwa endapo watajitokeza katika maeneo yao yanakuwa na
mahitaji yote muhimu na yanahudumiwa ipasavyo.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema Serikali
tayari imetoa shilingi milioni 500 kati ya sh. bilioni moja zilizokuwa
zimetengwa kwa ajili ya Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizokuwa zianze Aprili 2,
mwaka huu.
“Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameahirisha Mbio za
Mwenge wa Uhuru zilizokuwa zianze Aprili 2, mwaka huu na kuagiza shilingi
bilioni moja zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya shughuli hiyo, zipelekwa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa ajili ya
maandalizi ya kujiweka tayari kudhubiti maambukizi ya CORONA. Serikali tayari
imetoa shilingi milioni 500.”
Akielezea hatua zilizochukuliwa baada ya mgonjwa wa
kwanza kubainika kuwepo nchini Tanzania, Waziri Mkuu amesema Serikali imechukua
hatua kwa kumchukua mgonjwa huyo na kumhifadhi kwenye eneo maalum kwa ajili ya
kumpatia huduma (isolation).
“Pia, Serikali imefanya ufuatiliaji wa watu
waliokutana na mgonjwa huyu tangu aingie nchini na kuwaweka kwenye karantini ya
siku 14, na pia kuchukua sampuli kwa lengo la kubaini kama wameambukizwa virusi
hivi,” amesema.
Ugonjwa huu umeingia nchini baada ya Mtanzania
mwenye miaka 46 aliyesafiri kwenda nchi za Ubeligiji, Sweden na Denmark hivi
karibuni, kupimwa na kuthibitika kuwa na virusi vya Corona (COVID-19).
Akielezea hatua zaidi zinazochukuliwa, Waziri Mkuu amesema
licha ya hatua ambazo zimechukuliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Serikali itaimarisha ukaguzi na ufuatiliaji wa wasafiri
wanaoingia nchini kupitia viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi kavu ili
kuwabaini wasafiri wenye dalili za ugonjwa na viashiria vyenye hatari.
“Tutaimarisha uwezo wa kupima sampuli kwa watu
wanaohisiwa kuwa na viashiria au dalili za ugonjwa huu ambapo maabara yetu ya
Taifa kwa sasa inao uwezo wa kutoa majibu kwa haraka.”
Amesema Serikali inaendelea kuwajengea uwezo
(mafunzo) watumishi wa sekta ya afya katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko
ikiwemo jinsi ya kutoa tiba, kuchukua sampuli, uelimishaji na kuzingatia kanuni
za afya.
“Serikali imetenga hospitali maalum za Mloganzila
(DSM), Kituo cha Buswelu (Mwanza) na Hospitali ya Mawenzi (Kilimanjaro), Mnazi Mmoja
(Zanzibar) na ChakeChake (Pemba) kwa ajili ya kutoa huduma kwa waathirika.”
Ameiagiza Wizara ya Afya ihakikishe vifaa vya kinga
ikiwemo vimiminika vya kudhibiti maambukizi (hand sanitizer) vinapatikana
katika maduka yote husika na kwa bei ya kawaida na kuongeza kwamba Serikali
itachukua hatua kwa wafanyabiashara watakaobainika kufanya ulanguzi wa vifaa
hivyo.
Amewataka Watanzania wazingatie ushauri unaotolewa
na Serikali na kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
“Watanzania tuache mzaha wa kutumia mitandao ya kijamii kufanya upotoshaji wa
tahadhari katika jambo hili,” ameonya.
Amewaomba
viongozi wa dini waendelee kushirikiana na Serikali katika kuwaelimisha waumini
wao wote kuzingatia tahadhari za ugonjwa huu. Pia amevitaka vyombo vyote vya habari vishirikiane na Serikali
katika utoaji wa elimu kwa umma kuhusu kujikinga na Corona bila kufanya
upotoshaji wala kuipa jamii hofu.
Amewataka wananchi watoe taarifa kuhusu uwepo wa
mgonjwa au kupata ufafanuzi kuhusu ugonjwa huu kupitia namba za bure za 0800110124,
0800110125 na 0800110037.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MACHI 17, 2020.
Subscribe to:
Posts (Atom)
MITANDAO YA KIJAMII
Popular Posts
-
Na. OWM, Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, imefanya ukaguzi wa utekelezaji wa sheria Na.5 y...
-
Wataalamu wa Afya moja wakiwa katikapicha ya pamoja wakati wa mkutano wa wataalamu wa Afya moja uliojikita katika ulinzi na usalama...
-
Na. OWM, ARUSHA Wataalam wa sheria kutoka katika sekta ya Afya ya binadamu, Afya ya wanyamapori na mifugo pamoja na mazingira wameshauri...
-
Washiriki wa Mkutano wa mwaka wa Wataalamu wa Maabara wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano wa mwaka kwa wataalam wa maabara w...
-
TAMOBA wafanya wasilisho la mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama wa Bodaboda na BajajiKampuni ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa ...
Formulir Kontak
Contributors
Powered by Blogger.