Wednesday, December 21, 2022

MAWAZIRI WAKUTANA KUIMARISHA MIKAKATI YA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO


 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ahimiza ushirikishwaji wa wadau wote katika kuunganisha nguvu ili kupambana na ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Kauli hiyo ameitoa wakati akiongoza kikao kilichowakutanisha Mawaziri wa kisekta kilichofanyika leo jijini Dar es salaam, kilicholenga kuimarisha mikakati ya kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto.

“Waziri Simbachawene, amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na wataalamu waandae miongozo yote izungumze kwa pamoja kuhusu ukatili wa kijinsia na baada ya kikao cha Mawaziri ushauri upelekwe kwa Waziri Mkuu ili aridhie.”

Ili hatua za muda mfupi hatua za muda wa kati na hatua za muda mrefu ziweze kuchukuliwa katika kupambana na vita hii, binadamu wamekuwa waajabu kuliko wanyama matukio mengi ya ukatili wa kijinsia yanafanywa na ndugu wa karibu.

Katika kikao hicho amesema Mwaka 2021 viliripotiwa vitendo vya unyanyasaji wa watoto 110499 ni asilimia chache yawalioripoti.

“Uliongoza ni ukatili wa ubakaji 5899 na waliolawitiwa 1114 na waliopata mimba za utotoni ni 1677 na utafiti ukaonesha namba hizi uzigawe kwa 60, utaona asilimia 60 inafanyika nyumbani walipo baba na mama ndugu jamaa na marafiki na asilimia 40 ni nje ya nyumbani, wakiwa shuleni au wanapoenda shuleni.”

Lazima tuimarishe mifumo izungumze na uwajibikaji, sheria tunazo tayari tuna miongozo mbalimbali sasa tunahitaji mawasiliano yaanzie kwa Mawaziri yashuke kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, ishuke kwenye kata zetu, ishuke kwenye mitaa na vijiji.

“Mfumo wa mawasiliano uende kwenye kamati za mabaraza ya madiwani kwenye Halmashauri zetu, lakini kwenye vikao vya maendeleo vya kata ili viwe na nguvu ya kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ili hata marekebisho ya sheria ndogo ndogo yaanzie kule chini,” alisema Waziri Gwajima.

 

Read More

Friday, December 9, 2022

MIAKA 61 YA UHURU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene  amesema nchi imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa maendeleo ambayo ni shirikishi na yamelenga watu.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu katika kilele cha maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara kilichofanyika Kibakwe Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.

“Katika ujenzi wa maendeleo ukisema ujenzi wa sekondari za kata, ujenzi wa vituo vya afya ujenzi wa barabara vyote vimetekelezwa kwa kushirikisha wananchi.”

Kauli mbiu ya miaka 61 ya uhuru ambayo inasema, Amani na Umoja ni nguvu ya maendeleo yetu.” Imetusaidia kutimiza shabaha zetu.

“Mabadiliko ya kisiasa, mabadiliko ya kiuchumi, Mhe. Rais amepeleka maendeleo hayo kwa watu na maendeleo ya watu yanahitaji rasilimali fedha,” alisema waziri .

Sisi watanzania tuna misingi yetu kila awamu inayoingia  inategemea misingi ya awamu iliyopita ndio maana tumefika hapa tulipofika.

 “Watanzania wanapenda furaha watanzania hawapendi hofu watanzania ni watii kwa mamlaka, tuendelee kuheshimiana na kuipenda nchi yetu.”

Hata wenye mawazo mbadala Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua mipaka ndio maana anazungumzia R-nne watu wawe na utaratibu wa maridhiano; maelewano, kujenga upya, na kuendelea mbele.

“Tunaiona Tanzania iliyobadilika sana kimaendeleo, lakini imebakia na misingi ile ile iliyoachwa na waasisi wa Taifa letu katika mioyo ya watu.”

Tulivyopata uhuru falsafa ya Baba wa Taifa alisema, Uhuru ni kazi ndio maana wananchi wamejikita katika kufanya kazi.

Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Mhe. George Fuime amesema nchi imepiga hatua kwenye miundo mbinu ya Mawasiliano.

“Ujenzi wa miundo mbinu ya afya, ujenzi wa miundo mbinu ya elimu, mabadiliko haya yameasisiwa na viongozi wetu kutokana  na Amani na utulivu uliojengwa na wazee wetu.”

Naye muwasilishaji mada Mwl Charles Malugu amesema serikali ya awamu ya sita imefanya ujenzi wa sekondari vyumba 20000, na ujenzi wa vyumba 3000 kwa shule shikizi  ambao utasaidia wanafunzi wa kidato cha kwanza na wanafunzi wa darasa la kwanza kuanza masomo bila kuwa na kikwazo cha aina yoyote.

“Serikali ya awamu ya sita imeruhusu wanafunzi walikatisha masomo kutokana na ujauzito, kuendelea na masomo ili wasikatize ndoto zao.”

 

Read More

Thursday, December 8, 2022

RAIS WA JAMHURI YA WATU WA SAHRAWI ATEMBELEA MJI WA SERIKALI MTUMBA

 

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Sahrawi, Mhe. Brahim Ghali leo amefanya ziara ndogo katika mji wa Serikali  Mtumba ambapo alitembelea jengo la Ofisi ya Rais Menejiment na Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Katika ziara hiyo ndogo Mhe. Rais Brahim Ghali alikaribishwa na kuoneshwa Mji wa Serikali na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Bunge na Uratibu ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu Bwn. Omar S Ilyas, pamoja na Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa Mji wa Serikali Bwn.  Meshack Bandawe, ambapo walipata nafasi ya kuonyeshwa kiwanja cha Ubalozi wa Taifa la watu wa Sahrawi.

Read More

Tuesday, December 6, 2022

DKT. GWAJIMA: ELIMU YA LISHE IPEWE KIPAUMBELE

Serikali imesisitiza utoaji wa elimu kwa jamii namna ya kuzingatia masuala ya lishe nchini ili kuwa na Taifa lenye afya bora na kujiletea maendeleo yake.

 

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt.Doroth Gwajima wakati akimwakilisha  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa  wakati wa Mkutano wa Nane wa Mwaka wa Wadau wa Lishe nchini uliofanyika uwanja wa shule ya Msingi Mukendo  Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.

 

Akizugumza kuhusu Mkutano huo alisema, umewezesha washiriki kupata maelezo kuhusu utekelezaji wa afua za lishe kwa kipindi cha mwaka wa kwanza (2021/2022) wa utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Pili wa Kitaifa wa Lishe (2021/22 - 2025/26) na kusema kuwa tathmini hizo ni za muhimu kwani ndio kipimo cha kujua hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Mpango.

 

Kaulimbiu ya mkutano wa mwaka huu ni“KUONGEZA KASI KATIKA KUBORESHA HALI YA LISHE KWA MAENDELEO YA RASILIMALI WATU NA UCHUMI” .

 

Waziri alisema katika kutekeleza mpango Juishi wa Lishe suala la elimu lina umuhimu wa kipekee kwa kila mmoja ili kufikia malengo.

 

Alifafanua kuwa Serikali itaendelea kutoa kipaumbele juu ya jamii kupewa elimu ya namna ya kuzingatia lishe bora ili kuweza kuepukana na udumavu kwa watoto na kuwa na afya bora.

 

“Ili kupata matokeo chanya katika kuboresha hali ya lishe nchini ni muhimu kuendelea kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya lishe. Pamoja na uhamasishaji kufanyika kabla ya mkutano na wakati wa  mkutano huu, natoa rai kwa Taasisi ya Chakula na Lishe na wadau wengine kuhakikisha tunabuni mikakati zaidi ya kufikisha elimu sahihi ya lishe kwa umma ili kusaidia jamii kuelewa changamoto,”Alisisitiza Dkt.  Gwajima

 

Aliekeza  kuwa,  upo  umuhimu  wa  kuwa  na  jitihada za makusudi ili kuhakikisha wadau wa sekta binafsi wanashirikishwa na kuwa na utaratibu mzuri wa kuchangia utekelezaji wa afua za lishe.

 

Aidha, Serikali chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kulipa umuhimu wa kipekee suala la lishe nchini ili kuifanya nchi yetu kuwa na uchumi imara kupitia maendeleo ya viwanda ambapo alieleza kuwa Maendeleo haya hayawezi kupatikana iwapo hatutaimarisha kasi ya kujenga na kulinda kizazi chenye nguvu, afya njema na uwezo wa kufikiri.

 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde aliasema Wizara yake itaendelea kutoa kipaumbele katika kutenga fedha nyingi kwenye masuala ya lishe na kuimarisha kilimo cha umwagiliaji ili kuchagiza ongezeko la upatikanaji wa chakula nchini.

 

"Uwekezaji katika kilimo utaleta matokeo chanya katika lishe, lazima tuwekeze katika uzalishaji wa mbegu, huduma za ugani, umwagiliaji na miundombinu ya uhifadhi wa mazao ili kufikia malengo kama yalivyotarajiwa," alisema Mhe. Mavunde

Naye, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega alisema kumekuwa na  chagamoto ya ulaji kwa kutozingatia  kauni za lishe bora inayosababisha changamoto za kifya kwa wengi.

“Takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha ulaji wa nyama kwa wastani wa mtu mmoja kwa mwaka ni kilo 15 wakati kiwango kinachopendekezwa na FAO kwa mtu mmoja kwa mwaka ni wastani wa kilo 50, upande wa ulaji wa samaki wastani wa kilo nane na nusu kwa mtu mmoja kwa mwaka, kiwango hichi kipo chini kulinganisha kiwango kinachopendekezwa cha kilo 23 kwa mtu mmoja kwa mwaka, aidha ulaji wa mayai na kuku bado si wa kuridhisha," alisisitiza Ulega.

Aidha  wizara imeendelea kutekeleza afua mbalimbali za kuhamasisha hali ya ulaji nchini ambapo wanahamasisha ulaji na utumiaji mazao ya mifugo kwa kushirikina na wadau mbalimbali sambamba na kuongeza uzalishaji nchini.

 

Read More

Monday, December 5, 2022

FEDHA ZA MAADHIMISHO YA UHURU KUJENGA MABWENI YA SHULE NANE

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema fedha zilizokuwa zimetengwa na Wizara na Taasisi kwa ajili ya Maadhimisho ya Sherehe za Uhuru mwaka huu zitapelekwe Ofisi ya Rais – TAMISEMI nakutumika kujenga mabweni katika shule nane za Msingi za wanafunzi wenye mahitaji maalum hapa nchini.

Taarifa hiyo na Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene katika mkutano wake na waandishi wa habari Mjini Dodoma.

“Shilingi Milioni 960,000,000/- (Tshs Milioni Mia Tisa Sitini)  zitatumika kujenga shule ya msingi Buhangija Shinyanga, Goweko Tabora, Darajani Singida, Mtanga Lindi, Songambele Lindi, Msanzi Rukwa,  Idofi Njombe, na Longido Arusha.”

Ni dhamira ya dhati ya Mheshimiwa Rais wetu ya kuwajali na kuwajengea mazingira rafiki watu wenye mahitaji maalum hapa nchini. Hili ni jambo kubwa la kishujaa na la kupongezwa sana na Wananchi wote wa Tanzania.

Aidha Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara mwaka huu 2022 yatafanyika kwa Midahalo na Makongamano mbalimbali yatakayofanyika katika Wilaya zote hapa nchini kujadili, kutafakari kwa pamoja na kukumbuka tulikotoka, tulipo na tunakoelekea kuhusu Maendeleo Endelevu ambayo Nchi yetu adhimu Tanzania imeyafikia. Hivyo hakutakuwa na Gwaride na shughuli nyingine za Kitaifa.

 

Waziri amesema, Maadhimisho ya MIAKA 61 YA UHURU yataadhimishwa kwa Kauli mbiu inayosema  “AMANI NA UMOJA NI NGUZO YA MAENDELEO YETU”.

“Makongamano hayo yatatanguliwa na ratiba mbalimbali kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya kufanya shughuli za Kijamii kama vile kufanya usafi katika maeneo ya Hospitali, shule, nyumba za Wazee na makundi yenye mahitaji maalum”

Waziri ameelekeza Ofisi zote za Serikali hapa nchini kupambwa kwa mapambo ya rangi za Bendera ya Taifa pamoja na picha ya Mheshimiwa Rais.

Read More

MKUU WA WILAYA YA MUSOMA DKT. HAULE AHIMIZA UPANDAJI WA MITI

MKUU wa Wilaya ya Musoma Dkt. Khalifan Haule amehimiza wananchi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika upandaji wa miti ya matunda ili kupata matunda na vivuli katika maeneo yao.

 

Ametoa kauli hiyo  wakati wa zoezi la upandaji miti ya matunda katika shule ya Msingi ya Mwisenge iliyopo mkoani Mara.Zoezi hili ni moja ya shughuli zinazoambatana na Mkutano Mkuu wa Nane wa mwaka wa Wadau wa Lishe.

 

Aidha jumla ya miti 300 imetolewa na kugawa katika shule sita ikiwemo; Mwisenge, Mtakuja, Nyarigamba A, Nyarigamba B, Nyabisare na Nyarugusu ambapo kila shule itapewa miti 50.

 

“Leo tunazindua upandaji wa miti hii kwenye shule ya Kihistoria aliyosoma Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyeyere ikiwa ni ishara ya kuunga mkono jitihada za kuhamasisha ulaji wa matunda kwa lengo la kuimarisha masuala ya lishe nchini,”aslisema Dkt. Haule

 

Aidha lengo la zoezi hilo ni kuimarisha utekelezaji wa masuala ya  lishe nchini kwa kuhamasisha ulaji wa matunda na mbogamboga katika jamii zetu.

 

Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe nchini Dkt.Germana Leyna amesema taasisi yake imejithatiti kuhakikisha elimu ya masuala ya chakula na lishe bora inatolewa kwa makundi yote ikiwemo watoto waliopo mashuleni.

 

Aliongezea kuwa watu wengi wanakula kwa mazoea na si kula lishe bora hivyo jamii haina budi kubadilisha mitazamo juu ya masuala ya lishe na kuyapa kipaumbele.

 

"Hakuna mtu anayeweza kufanikiwa ikiwa anachamoto za kiafya zinazochangiwa na lishe duni, hivyo kila mmoja anajukumu la kuzingatia lishe bora kwa afya bora,"alisisitiza Dkt. Germana

 

Alitoa neno la Shukrani Mstahiki Meya wa Manispaa la Musoma Kapteni Mstaafu Patrick Gumbo alipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi ya Chakula na Lishe pamoja na Mkoa kwa kuratibu zoezi hilo huku akitoa rai kwa kila shule kuhakikisha wanatunza miti hiyo ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.

 

"Ni jambo jema limefanyika leo, jukumu lililopo mbele yetu ni kuhakikisha miti inatunzwa na inaleta manufaa kama ilivyokusudiwa," alisema Patrick

 

Naye Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Sigawa Mwita alitoa shukrani kwa kuitumia shule hiyo yenye historia kubwa nchini kwa kuzingatia Rais wa Awamu ya Kwanza Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisoma hapo na kueleza zoezi hilo ni sehemu ya kumuenzi mwalimu kwa kuzingatia alikuwa kinara wa masuala ya upandaji wa miti.

 

"Shule yetu inajumuisha na wanafunzi wenye mahitaji maalum na imendelea kuwa na ufaulu mzuri sana hii imetupa hamasa na kuonesha mnajali na mnatambua mchango wa shule hii," alisema Mwalimu Mwita

 

Read More

Saturday, December 3, 2022

SERIKALI KUJA NA MAELEKEZO KUIMARISHA UTENDAJI KAZI OFISI ZA KONGA

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amesema serikali itatoa maelekezo kwa Halmashauri kuweka mipango maalumu ya kuziwezesha ofisi za vikundi vya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (Konga) katika maeneo ya usimamizi, ruzuku na mikopo. Ili kuwa imara na endelevu na kuwa na mchango mkubwa katika kufikia malengo ya kitaifa na dunia kuhusu UKIMWI.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati wa uzinduzi wa magari nane ya mradi wa HEBU TUYAJENGE uliofanyika katika Ofisi za NACOPHA Mbezi Beach Dar es salaam.

“Serikali inatambua umuhimu wa mifumo ya kijamii kwa sababu ina mchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa. Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Tume ya Kudhibiti UKIMWI itaendelea kuhakikisha Uratibu wa Sera na miongozo unatoa fursa ya kuziwezesha Konga za WAVIU”

Aidha, katika hotuba yake, Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo mahususi kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia TACAID, Wizara ya Afya na wadau wengine kuweka jitihada na mikakati madhubuti katika kuzuia maambukizi mapya ili tuweze kufikia hatua ya kutokomeza kabisa.

 Ikiwa ni pamoja na Kuimarisha huduma za upimaji wa VVU na matumizi ya ARV ili kutokomeza vifo vitokanavyo na UKIMWI, kuweka mikakati ya kutokomeza ubaguzi na unyanyapaa kwa WAVIU.

“Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itayatekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa haraka ikiwa ni pamoja na kuziratibu Wizara husika na Wadau katika kuhakikisha maelekezo haya yanatekelezwa kwa wakati, alisema Waziri.”

Naye Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bwn. Kaspar Mmuya amewapongeza NACOPHA kwa kazi nzuri ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

“Kuhamasisha watu kujitokeza na kupima afya zao ni njia mojawapo ya kukabiliana na maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.”

Akitoa taarifa Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) Bi, Leticia Mourice Kapela, amesema baraza limeneemeka kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu kwa upande wa vijana, wanawake na WAVIU kwa ujumla.

“Uwezeshi huu katika fursa za mafunzo, mitaji ya kifedha, vifaa vya kuanzia shughuli za ujasiriamali, umesaidia vijana WAVIU kupata ujasiri wa kukabiliana na kuziepuka changamoto mbalimbali zinazowaweka katika hatari ya kupata maambukizi, ikiwemo kuanza ngono katika umri mdogo, kuwa na mahusiano na watu wenye umri mkubwa  na ulevi wa kupindukia”

Naye Mkurugenzi TACAIDS Bi. Audrey Njelekela, amesema Konga ziko kwenye Halmashauri 184 na Afua zote zinatekelezwa kwa kushirikiana na Halmashauri.

“Kupata magari kutasaidia kuongeza kasi na ufanisi katika kuhakikisha muitikio wa kitaifa unatekelezwa”

Read More