MKUU wa Wilaya ya Musoma Dkt.
Khalifan Haule amehimiza wananchi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika
upandaji wa miti ya matunda ili kupata matunda na vivuli katika maeneo yao.
Ametoa kauli hiyo wakati wa zoezi la upandaji miti ya matunda katika shule ya
Msingi ya Mwisenge iliyopo mkoani Mara.Zoezi hili ni moja ya shughuli
zinazoambatana na Mkutano Mkuu wa Nane wa mwaka wa Wadau wa Lishe.
Aidha jumla ya miti 300
imetolewa na kugawa katika shule sita ikiwemo; Mwisenge, Mtakuja, Nyarigamba A,
Nyarigamba B, Nyabisare na Nyarugusu ambapo kila shule itapewa miti 50.
“Leo tunazindua upandaji wa
miti hii kwenye shule ya Kihistoria aliyosoma Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Kambarage Nyeyere ikiwa ni ishara ya kuunga mkono jitihada za kuhamasisha ulaji
wa matunda kwa lengo la kuimarisha masuala ya lishe nchini,”aslisema Dkt. Haule
Aidha lengo la zoezi hilo ni
kuimarisha utekelezaji wa masuala ya
lishe nchini kwa kuhamasisha ulaji wa matunda na mbogamboga katika jamii
zetu.
Akizungumza wakati wa zoezi
hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe nchini Dkt.Germana
Leyna amesema taasisi yake imejithatiti kuhakikisha elimu ya masuala ya chakula
na lishe bora inatolewa kwa makundi yote ikiwemo watoto waliopo mashuleni.
Aliongezea kuwa watu wengi wanakula
kwa mazoea na si kula lishe bora hivyo jamii haina budi kubadilisha mitazamo
juu ya masuala ya lishe na kuyapa kipaumbele.
"Hakuna mtu anayeweza
kufanikiwa ikiwa anachamoto za kiafya zinazochangiwa na lishe duni, hivyo kila
mmoja anajukumu la kuzingatia lishe bora kwa afya bora,"alisisitiza Dkt.
Germana
Alitoa neno la Shukrani
Mstahiki Meya wa Manispaa la Musoma Kapteni Mstaafu Patrick Gumbo alipongeza
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi ya Chakula na Lishe pamoja na
Mkoa kwa kuratibu zoezi hilo huku akitoa rai kwa kila shule kuhakikisha wanatunza
miti hiyo ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa.
"Ni jambo jema
limefanyika leo, jukumu lililopo mbele yetu ni kuhakikisha miti inatunzwa na
inaleta manufaa kama ilivyokusudiwa," alisema Patrick
Naye Mkuu wa Shule hiyo
Mwalimu Sigawa Mwita alitoa shukrani kwa kuitumia shule hiyo yenye historia
kubwa nchini kwa kuzingatia Rais wa Awamu ya Kwanza Hayati Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere alisoma hapo na kueleza zoezi hilo ni sehemu ya kumuenzi
mwalimu kwa kuzingatia alikuwa kinara wa masuala ya upandaji wa miti.
"Shule yetu inajumuisha
na wanafunzi wenye mahitaji maalum na imendelea kuwa na ufaulu mzuri sana hii
imetupa hamasa na kuonesha mnajali na mnatambua mchango wa shule hii,"
alisema Mwalimu Mwita
EmoticonEmoticon
Note: Only a member of this blog may post a comment.