Kampuni
ya Tanzania Motorcycle and Bajaj Association (TAMOBA) imefanya wasilisho
maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi
na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa
Pikipiki za miguu miwili na mitatu.Lengo la wasilisho hilo ni kuutambulisha rasmi mfumo huo kwa
Wizara, Idara na Taasisi za serikali.
Kwa mujibu wa
wasilisho la TAMOBA,liliowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,
Joseph Kimisha, limebainisha kuwa zipo faida za kiuchumi na kijamii ikiwa ni
pamoja na mfumo huo Kurahisisha
udhibiti wa uhalifu kwa kupitia mfumo wa kielektroniki katika kupashana taarifa
za wahalifu na kihalifu, Kukuza ajira kwa Vijana kwa kurasimisha biashara ya
pikipiki (Bodaboda) na bajaji. Pia mfumo huo utaongeza ushirikishwaji wa jamii
katika shughuli za polisi.
Kikao hicho kimeongozwa na Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), Kaspar Kaspar Mmuya, na
kuhudhuriwa na Wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya ndani - Jeshi la Polisi, Kamishina wa Ushirikishwaji Jamii kutoka Makao Makuu ya Polisi Dkt.
Mussa Ali Mussa, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mamlaka ya Serikali Mtandao pamoja na Ofisi ya WazirI Mkuu – Idara ya Uratibu wa Shughuli
za serikali.
Mfumo huo ulizinduliwa rasmi mwaka 2019 na aliyekuwa makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ally Idd, jijini Dar
es Salaam. Aidha, TAMOBA tayari wameandaa Kitabu cha Mwongozo wa kufichua na
kuzuia Uhalifu kwa Polisi, Maafisa Watendaji wa Kata, Mitaa na Vijiji ambapo
wataanza na Usajili wa Pikipiki (Boda Boda) kwa kuanza na mkoa wa Dar es salaam
kama mkoa wa majaribio, lengo likiwa ni kuifikia mikoa yote nchini.
Mnamo mwaka 1980 serikali iliruhusu kampuni binafsi za ulinzi kutoa huduma za ulinzi hapa nchini,
chini ya uangalizi , uratibu na usimamizi
wa Jeshi la polisi kwa mujibu wa
Katiba na sheria ya Jeshi la Polisi na Polisi wasaidizi kwa mujibu wa Sura ya 322, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
MWISHO.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), Kaspar Kaspar Mmuya akifuatilia wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa Pikipiki za miguu miwili na mitatu, kutoka kwa Kampuni ya TAMOBA, Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TAMOBA, Joseph Kimisha, akibainisha faida za kiuchumi na kijamii za mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa Pikipiki za miguu miwili na mitatu, wakati wa wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dodoma.
Kamishina wa
Ushirikishwaji Jamii kutoka Makao Makuu ya Polisi Dkt. Mussa Ali Mussa akifuatilia wasilisho maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa kielektroniki
wa ulinzi na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya
moto hasa Pikipiki za miguu miwili na mitatu, kutoka kwa Kampuni ya TAMOBA, Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu, Idara ya Uratibu wa
Shughuli za Serikali (Ufuatiliaji), Devotha Gabriel, akifuatilia wasilisho maaluum kwa
Ofisi hiyo, kuhusu mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi na usalama kwa kuzuia
na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa Pikipiki za miguu
miwili na mitatu, kutoka
kwa Kampuni
ya TAMOBA Jijini Dodoma, kulia kwake ni Afisa Uratibu wa Shughuli za Serikali
Ofisi na Idara hiyo, Ewald Bonifasi.
Baadhi ya wajumbe wa kikao wakifuatilia wasilisho
maaluum kwa Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu mfumo maalum wa kielektroniki wa ulinzi
na usalama kwa kuzuia na kudhibiti uhalifu unaotokana na vyombo vya moto hasa
Pikipiki za miguu miwili na mitatu, kutoka kwa Kampuni ya TAMOBA Jijini Dodoma, Wajumbe
hao ni kutoka Wizara ya Mambo ya ndani - Jeshi la Polisi, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mamlaka ya Serikali Mtandao pamoja na Ofisi ya WazirI Mkuu – Idara ya Uratibu wa Shughuli
za serikali.