Tuesday, April 4, 2017

BALOZI WA ISRAEL ATEMBELEA IDARA YA URATIBU WA MAAFA OFISI YA WAZIRI MKUU - DODOMA

Balozi wa Israel Nchini Mhe. Yahel Vilan akiongea jambo kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza kulia) wakati wa ziara yake katika Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 4, 2017 Dodoma.

Mwambata Jeshi wa Israel Barani Afrika Bw. Aviezer Segal akionesha michoro ya muundo wa Ofisi yake wakati wa ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Idara ya Maafa ili kuangalia eneo lililotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Kituo cha Kitaifa na Kimataifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Dodoma.
Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles Msangi akionesha muundo wa Idara hiyo wakati wa ziara ya ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma Aprili 4, 2017.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (wa kwanza mwenye miwani) akifuatilia mada ya muundo wa Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan Dodoma.

Wakala wa Maendeleo wa Kimataifa wa MASHAV Bw. Yuval Fuchs akitoa hoja wakati wa Ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan kwa Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kushoto) akizungumza na baadhi wa wageni walioambatana na Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Idara ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 4, 2017 Dodoma.
Mkurugenzi wa Idaya ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Brig. Jenerali, Mbazi Msuya (wa kwanza kushoto) akimuonesha Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan ramani ya  eneo lililotengwa kwaajili ya Ujenzi wa Kituo cha Kitaifa na Kimataifa cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura, Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na baadhi ya Watendaji wa Serikali walioshiriki katika ziara ya Balozi wa Israel Mhe. Yahel Vilan mara baada ya kumpokea Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.