*Asema ni
utekelezaji wa Waraka na Kanuni za Elimu za mwaka 2002
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa kutoruhusu
wanafunzi waliopata ujauzito kuendelea na masomo katika mfumo rasmi wa elimu umetolewa
kwa mujibu wa Sheria na sio utaratibu mpya kama inavyopotoshwa na baadhi ya
wanaharakati.
Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi
huo leo (Jumatano, Julai 5, 2017) katika hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa
Saba wa Bunge mjini Dodoma.
Amesema msimamo
huo wa kisheria unalenga kuwafanya watoto wa kike wajishughulishe na masomo yao
zaidi badala ya kushiriki kwenye vitendo vya ukiukwaji wa maadili.
Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2015,
jumla ya wanafunzi 3,637 waliacha
masomo kutokana na kupata ujauzito.
“Kuwaachisha masomo wanafunzi
waliopata ujauzito ni utekelezaji wa Waraka na Kanuni za Elimu za mwaka 2002,
zinazoruhusu kufukuza na kuondoa wanafunzi shuleni kutokana na makosa
mbalimbali ikiwemo uasherati, wizi, ulevi, kutumia dawa za kulevya pamoja na
utoro.”
“Lengo hili lina nia ya kuwahimiza wazazi wawafundishe
watoto wao mambo mema ndani ya familia na wawakataze kushiriki vitendo vya
ngono katika umri dhamira ya Serikali ni kumlinda mtoto wa kike ili apate elimu
kwa ajili ya manufaa yake na Taifa kwa ujumla.”
Waziri
Mkuu amesema kila Mtanzania ana
wajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata elimu. Hivyo ni lazima
tuhakikishe mtoto wa kike anapata elimu stahiki na masomo yake hayakatizwi kwa
kupata ujauzito.”
Amesema
Serikali imewekeza kwenye mtoto wa kike, ambapo kifungu Na. 60 (b) cha Sheria
ya Elimu Sura ya 353, kinatoa adhabu ya miaka 30 jela kwa yeyote atakayeoa au
kumpa ujauzito mwanafunzi.
Pia,
sheria inatoa adhabu ya kifungo cha miaka mitano jela au faini ya shilingi
milioni tano, au vyote kwa pamoja kwa anayeshiriki kumuozesha mtoto wa
shule.
“Natoa
wito kwa Wakuu wa Wilaya kusimamia utekelezaji wa Sheria za nchi zenye lengo la
kumlinda mtoto wa kike. Aidha, nawashauri Waheshimiwa Wabunge, mshirikiane na
Halmashauri zenu kuweka mikakati ya kudhibiti ujauzito kwa watoto wa shule.”
Wahamasisheni wananchi watoe ushirikiano kwa
vyombo vya dola, ili wanaowapa wanafunzi ujauzito au kuwakatisha masomo ili
waozeshwe wapate adhabu stahiki.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.