* Asema changamoto ya
kukatika umeme Mkoa wa Lindi kuwa historia
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
changamoto ya kukatika umeme katika mkoa wa Lindi kuwa historia baada ya
kukamilika kwa mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 132 Mtwara-Lindi.
Amesema
hayo leo (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipotembelea mradi huo wa kuzalisha umeme
unaojengwa katika kijiji cha Mahumbika wilayani Lindi.
Waziri Mkuu amesema kukamilika kwa mradi huo uliogharimu sh. bilioni
16 kutamaliza changamoto ya upatikanaji wa umeme katika mkoa wa Lindi.
Amesema mkakati wa Serikali ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa
umeme ili Watanzania wapate umeme mwingi utakaosambazwa hadi vijijini kwa
gharama nafuu.
“Mikoa wa Lindi ulikuwa na shida kubwa ya kukatika kwa umeme,
kukamilika kwa mradi huu ni mkombozi kwetu, tunawakaribisha wawekezaji waje kuwekeza
kwa sababu sasa tunanishati ya uhakika.”
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini, Profesa James Mdoe amesema kuimarika kwa upatikanaji wa umeme
kutawezesha safari ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema atahakikisha anapambana
na watu wote watakaokwamisha jitihada za Rais Dkt. John Magufuli za kuwahudumia
wananchi.
Pia ameahidi kusimamia shughuli
za maendeleo ya wananchi wote Tanzania bila ya kujali maeneo wanakotoka wala itikadi
zao za kisiasa na kidini.
Ameyasema hayo wakati akizungumza
kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata za Nanganga, Nyangao, Mtama na Nyengedi
alipowasilisi wilayani Lindi, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.
“Tunataka fedha zinazotolewa na Serikali kwa
ajili ya kuwahudumia wananchi zitumike ipasavyo na hatutakubali kuona mtu
napewa fedha na kuzitumia atakavyo.”
Pia Waziri Mkuu amewataka
wananchi hao kuweka pembeni itikadi zao
za kisiasa na badala yake washirikiane kwa pamoja katika kufanya shughuli za
maendeleo kwenye maeneo yao.
“Rais Dkt. Magufuli amesema
Watanzania kwa sasa hatuhitaji kufanya siasa, sasa ni kazi tu, hivyo tutumie
muda wetu mwingi kwa kufanya kazi za maendeleo. Tupunguze muda wa kubishana
hakuna tija watu wanataka maji, afya.”
Awali Mbunge wa jimbo la Mtama
Mheshimiwa Nape Nnauye kwa niaba ya wananchi wa jimbo hilo aliishukuru Serikali
kwa kuboresha huduma mbalimbali kwenye jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.