WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea msaada wa magari
matatu yenye thamani ya Dola za Marekani 99,700 kutoka Kampuni ya Foton International
Trade Co. Ltd ya nchini China.
Amepokea msaada huo leo (Jumatano, Agosti 9, 2017) jijini
Dar es Salaam, ambapo amesema magari hayo yatatumika katika shughuli mbalimbali
za maendeleo ya jamii nchini. Magari hayo ni Sauvana SUV moja na Tunland Double
cabin mbili
.
“Nashukuru kwa msaada huu wa magari uliotolewa na Kampuni
ya Foton kwa Serikali yetu. Magari haya yanaweza kutumika katika Hospitali za
wilaya kwa ajili ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba pamoja na kutolea elimu
mbalimbali kwa umma.”
Pia, Waziri Mkuu ameikaribisha Kampuni hiyo kuja nchini
kuwekeza katika ujenzi wa kiwanda cha kuunganisha magari. Amesema mbali na
utulivu wa kisiasa uliopo Tanzania, pia kuna sera na mazingira mazuri ya uwekezaji.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo Bw. Zhao Xiao amesema wametoa msaada huo wa magari kwa
ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya Tanzania
hususan maeneo ya vijijini.
Bw. Xiao amesema Kampuni ya Foton inatengeneza magari
700,000 kwa mwaka, ambayo yanauzwa
katika nchi 125 duniani. Amesea ifikapo mwaka 2020 wanatarajia kuongeza
uzalishaji na kufikia magari milioni 1.4 kwa mwaka.
Kuhusu suala la kuja kuwekeza kwenye ujenzi wa kiwanda
cha kuunganisha magari nchini, Bw. Xiao amesema wanampango wa kuwekeza nchini
kwa kuwa kuna fursa nzuri za uwekezaji
na uhakika wa masoko katika nchi zingine za Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.