WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha
ushirikiano wake wa kiuchumi na kidiplomasia baina yake na Uganda.
Amesema
Tanzania na Uganda zinauhusiano wa muda mrefu na kwamba Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli inafarijika na
ushirikiano huo.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Alhamisi, Oktoba 12, 2017) alipokutana na
kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania, Bw. Richard
Kaonero jijini Dar es Salaam.
“Tunaimani
kubwa na ushirikiano wetu na Serikali ya Uganda. Tutaendelea kuimarisha
miradi mbalimbali ya maendeleo tunayoitekeleza kwa pamoja ukiwemo
ujenzi wa bomba la gesi.”
Hivyo ametumia fursa hiyo kuwakaribisha
wawekezaji kutoka nchini Uganda ili waje kuwekeza kwenye viwanda
mbalimbali vikiwemo vya kuchakata mazao ya kilimo.
Pia
amewakaribisha raia wa Uganda kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii
vilivyoko nchini Tanzania kama mlima wa Kilimanjaro, fukwe, mali kale na
mbuga za wanyama.
Kwa upande wake,
Balozi Kaonero ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuwa na dhamira ya
dhati ya kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya viwanda.
Pia Balozi huyo ameiomba Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Ndege Tanzania
(ATCL) kuanzisha safari ya kwenda Entebe nchini Uganda ili kuimarisha usafiri kati ya nchi hizo mbili.
Akizungumzia
kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, Balozi Kaonero amesema
Serikali ya Uganda na Tanzania zinaundugu wa damu na kwamba wataendelea
kuudumisha.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.