MKE wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa amewaomba wazazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi wahakikishe
wanatumia sehemu ya kipato chao katika kuwekeza kwenye elimu ya watoto wao.
Amesema elimu ndiyo jambo
pekee linaoweza kumsaidia mtoto katika kutimiza ndoto zake za maisha pamoja na
kumtoa katika kundi la wategemezi.
Mama Mary aliyasema hayo
jana (Jumamosi, Desemba
2, 2017), katika maafali ya shule ya awali na msingi ya Wonder Kids, iliyopo
wilayani Ruangwa, Lindi.
Mke wa Waziri Mkuu alialikwa katika maafali hayo kama mdau
wa elimu. Maafali hayo yaliyohusisha watoto wa awali ambao wanaingia darasa la
kwanza.
“Walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao
wanajua kusoma vizuri, hivyo wazazi watumie kipato chao kuwekeza katika elimu
kwani faida watakuja kuiona baadaye.”
Alisema kitaaluma yeye ni mwalimu hivyo anatambua kuwa
walimu wanafanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi hao wanajua kusoma vizuri
na wanakuwa na tabia nzuri, hivyo wazazi hawana budi kushirikiana nao.
Pia Mama Mary alitumia fursa hiyo kuwaomba wazazi wawatie
moyo walimu kwa sababu kazi wanayoifanya ni kubwa. “Wote ni mashahidi watoto
wetu tulivyowaleta na sasa ni tofauti.”
Alisema ni vizuri wazazi wakashiriki kikamilifu katika suala
la elimu kwa watoto wao ikiwa ni pamoja na kufuatilia maendeleo ya masomo yao
badala ya kuwaachia walimu peke yao.
Kwa upande wake ,mgeni rasmi katika maafali hayo ambaye
ni Muwakilishi Mkazi wa Children in Crossifire Bw Craig Ferla aliwapongeza
wanafunzi hao kwa kutimiza moja ya hatua
katika safari yao ya elimu na aliwasihi waendele kupenda kwenda shule na kusoma
kwa bidii.
Pia aliwapongeza wazazi kwa kutambua umuhimu wa elimu ya
awali na kuwapeleka watoto wao kwenye shule hiyo ya Wonder Kids. “Wonder Kids
ni mahali sahihi ambapo mtoto anapata elimu
na malezi bora.
Alisema elimu ya awali ninzuri kwa mtoto kwa kuwa
inawawezesha kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, hivyo aliwaeleza Wanaruangwa
kutumia vizuri fursa ya uwepo wa shule hiyo
katika wilaya yao.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bibi
Nancy Tausi alisema Wonder Kid ilianzishwa
Januari, 2017 ikiwa na wanafunzi 117 ambao ni wa kuanzia darasa la awali hadi
darasa la tatu.
Alisema lengo la kuanzisha shule hiyo ni kuhakikisha watoto
wanapata kujua kusoma vizuri na kwamba wanatarajia kuanzisha darasa la kompyuta
kwa ajili ya watoto kujifunza TEHAMA pamoja na kuanza kufundisha lugha ya
Kifaransa.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.