Mkazi wa Msamala katika Manispaa
ya Songea, Bibi Monica Joseph Miti akitoa maelezo yake mbele ya Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa (hayupo pichani) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya
Mwengemshindo. Bibi Miti aliomba asaidiwe kurejeshewa nyumba yake aliyotapeliwa
na mtumishi wa Manispaa hiyo baada ya mumewe kufariki.
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amewatoa hofu wakazi 1,000 wa Manispaa ya Songea wanaoidai
fidia ya sh. bilioni 3.8 ya eneo lao ambalo limechukuliwa na kuwa eneo la
kiuchumi mkoani Ruvuma (Ruvuma SEZ) kwa ajili ya ujenzi wa viwanda.
Ametoa
ahadi hiyo leo (Jumamosi, Desemba 23, 2017) wakati akizungumza na wakazi wa
kata ya Mwengemshindo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Manispaa
hiyo.
Amesema
Serikali ya awamu ya tano inatambua kilio chao ambacho alisema ni cha muda
mrefu na kwamba alishawahi kupata ombi maalum kutoka kwa mbunge wao wa zamani,
Bw. Leonidas Gama ambaye sasa ni marehemu.
“Alipotoka
kutibiwa India alikuja ofisini kwangu na kunieleza kwamba ana mambo mawili ambayo
nikifanya ziara mkoani Ruvuma anaomba niyatafutie ufumbuzi. La kwanza lilikuwa
ni hili la fidia kwa wakazi wa Mwengemshindo na la pili lilikuwa ni la ujenzi
wa kituo cha mabasi cha mjini Songea,” alisema.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.