Serikali imeazimia kuboresha
mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kuweka mifumo ya kielektroniki
katika utoaji wa huduma ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi na kuondoa
urasimu usio wa lazima .
Akizungumza wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa mapangokazi baina ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi
Prof. Faustin Kamuzora alisema leo tarehe 30 Januari, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano
wa JNICC Dar es Salaam, mkutano huu ni ushahidi kwamba Serikali na Sekta
Binafsi ni wadau muhimu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii na
kwamba mazingira wezeshi ya biashara ni kichocheo muhimu katika jitihada za
Serikali kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi.
“Serikali ya Awamu ya Tano
imeweka kipaumbele katika utekelezaji wa Mpangokazi wa Kuboresha Mazingira ya
Biashara na Uwekezaji (Roadmap for Improvement of Business Environment and
Investment Climate in Tanzania), utekelezaji wa Mpangokazi huu utaiwezesha nchi
yetu kufikia malengo yake ya kujenga uchumi wa viwanda, na kuongeza fursa za ajira na kuiwezesha
Sekta Binafsi kuchangia katika ukuaji wa uchumi na kuwa nchi ya kipato cha kati
ifikapo mwaka 2025”, Alisema Prof. Kamuzora.
Prof. Kamuzora alieleza
kuwa, miongoni mwa maboresho yaliyofanyiwa kazi na Serikali ni pamoja na
kuboresha mfumo wa usajili wa biashara na kampuni kwa kuanzisha mfumo wa
usajili kwa njia ya mtandao (On-line
Registration System) utakao anza kutumika hivi karibuni, pamoja na
kuimarisha mfumo wa usimamizi wa ardhi kwa kuanzisha mfumo unganishi wa
kielektroniki wa utunzaji wa kumbukumbu
kwenye masjala ya ardhi (Integrated
Land Management Information System) na kuongeza ufanisi katika utendaji
bandarini kwa kuimarisha mifumo ya kielektroniki ya malipo na utoaji wa huduma
kwa wasafirishaji wa shehena.
“Napenda kutoa rai kwa waratibu wa mazingira
ya biashara kutoka Wizara na Taasisi za Serikali kutumia fursa ya mkutano huu
kujifunza kutoka kwa wadau wa sekta
binafsi kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa kuzingatia kazi na ufanisi wa
biashara”, alisema Kamuzora.
Tumeunda kikosi kazi cha
taifa cha uanzishwaji wa mfumo “Building codes” za nchi nzima, ili kuweza
kufanikisha mashirikiano haya baina ya sekta umma na sekta binafsi kwa haraka na
itasaidia kuleta ubunifu kulingana na mabadiliko kwenye ulimwengu wa kibiashara
na mahitaji ya nyakati, alisisitiza Kamuzora.
Uchambuzi wa awali wa
taarifa ya wepesi wa kufanya biashara ya mwaka 2018 umeonesha kwamba Wizara na
Taasisi za Serikali zina jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na
mazingira rafiki na yanayotabirika ya kufanya biashara ili kuvutia uwekezaji wa
ndani na nje na kuiwezesh seta binafsi kuongeza fursa za ajira.
Mkutano huo wa siku moja umelenga
kuleta mikakati bora itakayoiwezesha Tanzania kuboresha mazingira ya ufanyaji
biashara baina ya Sekta a Umma na Sekta Binafsi , hiini pamoja na kuboresha
mazingira ya kutoa huduma kwa sekta binafsi tutakuwa tumeshiriki kikamilifu
katika kulifikia azma ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda kama
inavyoelekezwa kwenye Mpango wa pili wa Maendeleo wa miaka mitano
2016/2017-2020/21.
Baadhi ya wageni waalikwa na wawakilishi mbalimbali kutoka sekta binafsi na Sekta ya Umma walioshiriki mkutano huo uliofanyika Januari 30 2018 Jijni Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.