Monday, April 30, 2018
KATIBU MKUU OFISI YA WAZIRI MKUU ATEMBELEA BOHARI KUU YA DAWA MSD
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akisisitiza jambo wakati akifanya mazungumzo na viongozi wa Bohari ya Dawa alipowatembelea leo katika Ofisi zao Jijini Dar es salaam April 30,2018. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Rugambwa Bwanakunu. |
MAANDALIZI YA SHEREHE ZA MEI MOSI YAKAMILIKA.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha kukamilisha maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano mara baada ya kukamilisha maandalizi ya sherehe hizo. |
Saturday, April 28, 2018
SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO
Kaimu Mtendaji Mkuu OSHA Bi.Khadija Mwenda akizungumza jambo wakati wa Kilele cha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani yaliyoadhimishwa mkoani Iringa.
|
SERIKALI KUENDELEA KUKOMESHA AJIRA HATARISHI ZA WATOTO
Na.MWANDISHI WETU
Serikali imedhamiria kuendelea kukomesha ajira hatarishi za watoto ili kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa na kuwapa nafasi stahiki kulingana na sheria na kanuni zilizopo nchini.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi Ofisi (Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama alipohudhuria katika kilele cha Siku ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi Duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 28 Aprili ambapo Kitaifa ilifanyika Mkoani Iringa.
Waziri alieleza kuwa, katika mapambano haya ya ajira hatarishi kwa watoto ni moja ya utekelezaji wa kampeni zinazolenga kuharakisha utekeleezaji wa vipaumbele vilivyomo kwenye lengo namba (8) la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ambalo ni kuboresha mazingira ya wafanyakazi na kukomesha ajira mbaya kwa watoto.
“Tuendelee kupiga vita ajira mbaya kwa watoto kwa kuzingatia kampeni zilizopo hasa ile ya kuboresha mazingira ya wafanyakazi ifikapo mwaka 2030 pamoja na kukomesha ajira mbaya za watoto ifikapo mwaka 2025,” alisema Waziri
Waziri aliongezea kuwa katika kuhakikisha watoto wanakuwa na mazingira salama , Lazima kuwe na mikakati ya pamoja baina ya utatu katika masuala ya kazi na ajira ikiwemo na kujenga utamaduni wa kujikinga na vihatarishi sehemu za kazi vinavyoweza kusababisha kuhatarisha afya na usalama wa wafanyakazi.
Aidha kama Taifa lazima tuoneshe umuhimu wa kuhakikisha kampeni hii inakuwa na matokeo chanya na kuendelea kuwa na Taifa lenye maendeleo.
Waziri aliongezea kuwa kulingana na Matokeo ya Utafiti wa Mtakwimu Mkuu wa Serikali uliofanyika mwaka 2014 na matokeo yake kuchapishwa mwaka 2016 ulibainisha kuwa, hali ya ajira hatarishi za watoto kuzidi kuwa mbaya zaidi katika sehemu za mashambani, sekta ya madini, misitu na uvuvi.
“Kwa mujibu wa taarifa za Mtakwimu Mkuu wa Serikali za mwaka 2014 zilibaini kuwa watoto wenye umri kati ya miaka 5-17 walioko kwenye ajira ni takribani milioni 4.2 ambayo ni asilimia 28.8 ya wafanyakazi wote na kati ya hao asilimia 21.5 wako kwenye ajira hatarishi hususan sehemu za mashambani ambako asilimia 35.6 ya wafanyakazi wote ni watoto”,alisisitiza Mhe.Waziri
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda alieleza kuwa wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuhakikisha sheria zilizopo zinafuatwa bila kukiukwa hususan kwa makundi maalum iliwemo yale ya vijana na makundi ya watu wenye ulemavu.
“kwa kuwa Vijana wadogo ndiyo nguvu kazi ya taifa hivyo wanastahiri kulindwa na kuangaliwa kwa jicho la pekee ili kuwa na kizazi endelevu,”alisema Mwenda
AWALI
Aprili 28 ya kila mwaka ni siku ya Kimataifa ya kuadhimisha masuala ya Afya na Usalama Mahali Pa Kazi, ambapo huwa na Kauli Mbiu inayotumika duniani kote ambayo inatolewa na Shirika la Kazi la Duniani.Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Kizazi Salama chenye Afya –Generation Safe and Health”.Kaulimbiu hiyo ili kuendana na mazingira ya nchi yetu iliboreshwa na kuwa “Kizazi Salama Chenye Afya kwa Uchumi wa Viwanda –Generation Safe and Health for Industrial Economy”.
Friday, April 27, 2018
KONGAMANO LA TANZANIA YA VIWANDA LAFANA MKOANI IRINGA.
Baadhi ya wajumbe wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda wakati wa maandalizi ya kuifikia Siku ya Mei Mosi wakiimba wimbo wa umoja na mshikamano, Mkoani Iringa. |
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage akiongea umuhimu wa kuwa na Tanzania ya Viwanda wakati wa Kongamano la maandalizi ya Mei Mosi lililofanyika mkoani Iringa Aprili 27, 2018. |
Baadhi ya wajume wakifuatilia Kongamano la maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi walipokutana kujadili masuala ya Tanzania ya Viwanda Aprili 27, 2018. |
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza jambo wakati wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda lililohusu maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi lililofanyika Mkoani Iringa Aprili 27, 2018. |
Katibu Mkuu TUCTA Dk Yahaya Msingwa akizungumza jambo wakati wa Kongamano la Tanzania ya Viwanda lililohusu maandalizi ya Sherehe za Mei Mosi lililofanyika Mkoani Iringa Aprili 27, 2018 |
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Amina Masenza akizungumza wakati wa Kongamano la kuelekea sikukuu ya wafanyakazi duniani lililofanyika mkoani Iringa Aprili 27, 2018. |
VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WATAKIWA KUWA MAKINI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewataka viongozi wa vyama vya siasa wajitahidi kuwa makini na namna wanavyoendesha vyama vyao kwa sababu wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote.
Pia amewaasa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa waendelee kushikamana ili waweze kulifikisha Taifa mahali ambapo Watanzania wanapatarajia ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini.
Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Aprili 27, 2018) wakati akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu ulioko Mlimwa jijini Dodoma.
“Viongozi wa vyama vya siasa wanatakiwa wajitahidi kuwa makini na namna ambavyo wanaendesha siasa katika vyama vyao, wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote hivyo tupeleke ujumbe ambao utawaongoza kujileta maendeleo.”
Waziri Mkuu amesema kuwa mazungumzo yaliyofanyika leo baina ya Serikali na viongozi hao yameonesha nia ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano. Pia amesema wana wajibu wa kuendeleza historia nzuri kwani siasa ni moja ya nyenzo zinazochochea maendeleo.
Akijibu ombi la viongozi hao kuhusu changamoto ya upatikanaji wa fedha za kuendesha shughuli za baraza hilo ikiwemo mikutano, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itafanyia kazi maombi hayo ili waweze kutimiza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.
MAJALIWA AKUTANA NA WAJUMBE WA KAMATI YA UONGOZI YA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA NCHINI
Thursday, April 26, 2018
WAZIRI MKUU AHUDHURIA MECHI YA WABUNGE LA TANZANIA NA LILE LA EA
Wednesday, April 25, 2018
WAZIRI MHAGAMA: USALAMA MAHALI PA KAZI KUCHOCHEA UCHUMI WA VIWANDA
BUNGENI LEO 25.04.2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Naibu Waziri , Ofisi ya Rais TAMISEMI, Josephat Kandege, bungeni mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (katikati) na Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Aprili 25, 2018. |
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma, Aprili 25, 2018. |