Friday, April 13, 2018

KATIBU MKUU TARISHI ATETA NA KIKOSI KAZI CHA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI CHA KUBORESHA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akifuatilia  kikao na Kikosi kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi,   leo mjini Dodoma tarehe 13 Aprili, 2018.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Waziri Mkuu na Bunge) Maimuna Tarishi akiongoza kikao na Kikosi kazi  cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachohusika  na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura walipokutana   leo mjini Dodoma tarehe 13 Aprili, 2018.

Mkurugenzi Idara ya Sera na Bunge Ofisi ya Waziri Mkuu,Yona Mwakilembe akitoa ufafanuzi katika  kikao hicho wakati Kikosi Kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi  kinachohusika  na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura kilipokutana na Katibu Mkuu (hayupo pichani)   leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa  Kikosi Kazi cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi  kinachohusika  na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura wakifuatilia kikao na  Katibu Mkuu (hayupo pichani)  leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma.     
NA MWANDISHI MAALUM:
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo ni Taasisi mojawapo iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Waziri Mkuu na Bunge), Maimuna Tarishi amekutana na Kikosi Kazi cha Tume hiyo kinachohusika  na Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura leo tarehe 13 Aprili, 2018, mjini Dodoma,  lengo ni kuangalia namna serikali inavyoweza kusaidia kwa maeneo inayoruhusiwa  kikatiba katika  kuwasaidia kutekeleza majukumu yake.
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 Ibara ya 5 kifungu kidogo cha 3 (a) ambacho kimeweka uanzishwaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini na Ibara ya 74 kifungu kidogo cha 6 (a) na (e), kinaipa Tume madaraka ya kuchukua jukumu la kuandikisha wapiga Kura nchini Tanzania.
Sheria ya Uchaguzi kifungu cha 15 (3) kinaipa madaraka Tume ya Uchaguzi  kutengeneza mfumo na utaratibu wa  uandikishaji wa wapiga Kura nchini na uboreshaji wa daftari hilo mara mbili kati ya Uchaguzi mkuu mmoja na unaofuata.     
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ni miongoni mwa Taasisi ambazo zipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi hiyo ni Taasisi huru ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 1993 chini ya Ibara ya 74(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.