Thursday, September 13, 2018

PROF. KAMUZORA - TUWAJENGEE VIJANA WETU UWEZO KIFIKRA.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ujasiriamali na Ushindani Nchini (TECC) Sosthenes Sambua (wa kwanza Kulia) akieleza jambo kwa Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu ) Prof .Faustin Kamuzora (wa pili kulia) katika mjadala kuhusu njia bora ya kuwainua vijana kiuchumi kupitia ujasiariamali. Kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF). Kongamano hilo limefanyika leo (jana) alhamisi Septemba 13, 2018 katika ofisi za TPSF zilizopo Msasani Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu ) Prof .Faustin Kamuzora akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF, mara baada ya mkutano baina yake na Watendaji wa Taasisi hiyo kuhusu kuwainua vijana kiuchumi kupitia ujasiariamali uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu ) Prof .Faustin Kamuzora akiwasili katika Ofisi za Taasisi ya Sekta Binafsi zilizoko Msasani leo (jana) alhamisi Septemba 13, 2018 Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano baina yake na Watendaji wa Taasisi hiyo kuhusu namna bora ya kuwainua vijana kiuchumi kupitia ujasialiamali. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ujasiriamali na Ushindani Nchini (TECC) Sosthenes Sambua na wa pili kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wanchi Kiuchumi (NEEC) Bang’i Issa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.