Wednesday, November 21, 2018

MAJALIWA ATEMBELEA MAONYESHO YA JUKWAA LA BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOANI TABORA


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa Saidi Kanimba  kuhusu viatu vya ngozi vinavyotengenezwa   katika Halmashuri ya wilaya Uyui mkoani Tabora katika Maonyesho ya  Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yailyofanyika kwenye Viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakisalimina na Kaimu Mhariri Mtendaji wa  Magazeti ya Serikali (TSN),  Tuma Abdallah (kushoto) wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege  wa Tabora kushiriki katika  Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora, Novemba 21, 2018.  Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Imani Matabula  (kulia)  kuhusu sabuni zinazotengenezwa na Kampuni yake ya Matabula Soap Investment ya Kaliua mkoani Tabora katika maonyesho   ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama chupa yenye ujazo wa nusu lita ya mkojo wa sungura wakati alipotembelea banda la wanawake wajasiriamali wasindikaji wa Tabora katika maonyesho ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji katika Mkoa wa Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018.Kwa mujibu wa Mratibu wa Wajasiriamali hao, Bibi Ashura Mwazembe, mkojo wa Sungura unatumiwa kama mbolea ya mazao ya kilimo na pia ni dawa nzuri sana ya kuua wadudu waharibifu wa mazao. Lita moja ya mkojo huo inauzwa sh. 10, 000/=. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na viongozi wa Magazeti ya Serikali  (TSN) baada ya kufungua Jukwaa la Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora kwenye ukumbi wa  Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo , Novemba 21, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Viongozi wa dini baada ya kufungua Jukwaa la Biashra na Uwekezaji Mkoani Tabora kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo, Novemba 21, 2018.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sabuni za Kampuni ya Matabula Soap Investment ya Kaliua mkoani Tabora, Imani Matabula  (kulia)  katika  maonyesho   ya Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji Mkoani Tabora yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Novemba 21, 2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Aggrey Mwanri. Wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Imani Matabula. 


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.