Friday, November 16, 2018

MAKATIBU WAKUU OFISI YA WAZIRI MKUU WAKUTANA NA WATAALAMU WA TAASISI MBALIMBALI KUJADILI MPANGO WA UJENZI WA MJI WA SERIKALI WA IHUMWA

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akizungumza jambo wakati wa kikao cha kujadili Mpango wa Ujenzi wa Mji wa Serikali wa Ihumwa Dodoma walipokutana na wataalamu kutoka Taasisi mbalimbali tarehe 16 Novemba, 2018 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.

Mbunifu Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania Bw.Eward Kayombo akitoa ufafanuzi kuhusu mpango wa ujenzi wa majengo ya Ofisi za Serikali katika eneo la Ihumwa Dodoma wakati wa kikao cha kujadili hatua za ujenzi huo pamoja na Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu (hawapo pichani)

Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia uwasilishwaji wa mada kutoka kwa Mbunifu Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania Bw.Eward Kayombo (hayupo pichani) wa kwanza kushoto ni Bi. Maimuna Tarishi (Bunge na Waziri Mkuu) kulia kwake ni Prof.Faustin Kamuzora anayeshughulikia Sera na Uratibu.
Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia uwasilishaji wa ramani ya Ujenzi wa Ofisi za Serikali katika Mji wa Serikali Ihumwa kutoka kwa Mbunifu Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania Bw.Eward Kayombo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.