Monday, January 28, 2019

SERIKALI KUENDELEA KUKABILIANA NA MAJANGA NCHINI


NA.MWANDISHI WETU
Serikali kwa ushirikiana na wadau wengine imejipanga kuendelea kukabiliana na majanga yanayoikumba nchi ili kuhakikisha inashughulikia na kutatua majanga hayo pindi yanapotokea.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu, Maimuna Tarishi Januari 28, 2019 wakati akifungua warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Tarishi alibainisha jitihada zinazofanywa na Serikali ili kukabili maafa ikiwa ni pamoja na kuendelea kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kuimarisha ustahimilivu wa majanga ya asili kwa kuongeza idadi ya wilaya zenye mipango ya kupunguza madhara ya maafa, kuboresha mifumo ya tahadhari za awali, kuongeza utoaji wa elimu kwa umma na kuimarisha shughuli za kujiandaa, kukabili na kuimarisha mfumo wa uratibu wa masuala ya maafa.
“Kwa kuzingatia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka wa Mitano, 2016/17- 2020/21 tutaendelea kuimarisha ustahimilivu wa majanga ya asili pamoja na kukabili majanga kwa kuzingatia utekelezaji wa malengo ya msingi ya Mfumo wa Sendai wa Kupunguza Madhara ya Maafa wa mwaka 2015 – 2030, tumedhamiria kuhakikisha tunakabiliana na majanga ili kujiletea maendeleo,”alisema Tarishi
Aliongezea kuwa, kwa kuzingatia majanga yanayoikabili nchi ikiwemo mafuriko nchi haina budi kuwa mikakati hiyo ili kuhakikisha inakabili na kuweka mikakati yenye tija katika masuala ya menejimenti ya maafa nchini.
Tarishi alibainisha kuwa, mafuriko yamekuwa na athari nyingi kwa kulinganisha na majanga mengine yanayoikabili nchi mara kwa mara kwa kuzingatia takwimu zilizopo kwa sasa.
 “Takwimu zinaonesha kuwa kwa kipindi cha Januari hadi Desemba, 2018 mafuriko yameathiri wilaya 50 na kusababisha vifo kwa watu 71, majeruhi kwa watu 64, kuharibiwa nyumba 15,802 kwa viwango tofauti, kuathiri miundombinu katika shule 43, mashamba ya mazao mbalimbali, na vituo vya afya,”alisisitiza Tarishi
Alieleza kuwa, takwimu zilizopo tangu tupate uhuru nchi imeathiriwa na ukame zaidi ya mara 18 ikimo yale  ya mwaka 2006/2007 na 2007/2008 ambayo yaliathiri zaidi mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga, Lindi, Singida, Tabora na Mwanza.
Sambamba na hilo Ukame mwingine mkubwa ulitokea mwaka 2008/2009 ulioathiri zaidi mikoa ya kaskazini ya nchi hasa Arusha na Manyara. Mikoa ambayo mara nyingi huathiriwa na ukame ni Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga, ambayo kawaida hupata mvua ya chini kwa kiwango cha kati ya milimita 200 - 600 kwa mwaka.
Naye Mkuu wa Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Afrika, Amjad Abbashar, alieleza mipango mikakati ya kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuzingatia ongezeko la madhara yatokanayo ya maafa ikiwemo vifo, upotevu wa makazi, pamoja na uharibifu wa mali za watu.
“Tutaendelea kushirikiana na kuhakikisha tunakabili na kuzuia maafa yasitokee pale itakapotokea ili kuendelea kuwa na maendeleo endelevu katika mazingira tuliyonayo,”alieleza Abbashar
Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,Alvaro Rodriques, aliwataka wajumbe kuitumia fursa ya warsha hiyo kwa kuzingatia mada zitakazowasilishwa ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na wataalam na mikakati yenye kutatua madhara yatokanayo na majanga na kuahidi kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kushughulikia maafa.
AWALI
Warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya asili katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara imeratibiwa na Idara ya Usimamizi wa shughuli za Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa na Taasisi ya Utafiti ya CIMA kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya. Aidha warsha inatarajiwa kudumu kwa siku tano hadi Februari 01, 2019 Jijini Dodoma. Warsha hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya Umoja wa Ulaya (EU) katika nchi za Africa, Caribbean na Pacific (ACP), ambayo inalenga kupunguza majanga katika nchi hizo.
Mkuu wa Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Afrika, Amjad Abbashar akizungumza kuhusu namna bora za kukabili majanga  wakati wa warsha hiyo.

Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw.Alvaro Rodriques akiwasilisha hotuba yake wakati wa warsha hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania,Alvaro Rodriques wakati wa warsha ya kupunguza madhara ya maafa nchini na kuimarisha uthabiti kwa nchi na jamii dhidi ya majanga ya asili katika  ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara iliyofanyika katika Ukumbi wa mikutano Dodoma hoteli Januari 28, 2019.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi pamoja na wajumbe wa meza kuu wakifuatilia uwasilishwaji wa mada wakati wa warsha hiyo.

Sehemu ya wajumbe wakifuatilia uwasilishwaji wa hotuba ya Mwakilishi Mkazi wa Taasisi za Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bwana Alvaro Rodriques (hayupo pichani) wakati wa warsha hiyo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe walioshiriki katika warsha hiyo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akizungumza jambo na Mkuu wa Sekretarieti ya Kupunguza Madhara ya Maafa ya Umoja wa Mataifa kwa Kanda ya Afrika, Amjad Abbashar (wa kwanza kushoto) na katikati ni Mratibu wa Maafa wa Idara ya Maafa Bw.Charles Msangi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu) Bi.Maimuna Tarishi akiteta jambo na Watendaji wa Ofisi yake, katikati ni Kanali Matamwe Said, Mkurugenzi, Idara ya Uratibu wa Maafa na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo anayeshughulikia Mipango na Utafiti Bw.Bashiru Taratibu

1 comment:

  1. Huyu mwenyekiti wa alat gulamhafeez mukadam ni mtu mbaya kabisa.Yeye alisaidia mtoto yake mmoja kula pesa kwa MCHINA MMOJA.Lakini RAIS YETU MHE JOHN MAGUFULI ANASEMA WACHINA NI MARAFIKI YETU WA KWELI.Kwa nini huyu mindia afanya hivi?Labda kwa sababu huyu mukadam ni MOTHER FUCKER MINDIA.FUCKING INDIA.KAMA MO DEWJI,ALSO FROM INDIA. THEY MAKE MONEY BY STEALING AND CHEATING!!

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.