WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba ya chama ili
kuepusha migogoro kwenye maeneo yao.
Amesema
chama chochote ambacho viongozi wake hawazingatii katiba lazima kiwe na
migogoro kwani uzingatiaji wa katiba ni miongoni mwa mambo
yanayokitofautisha Chama Cha Mapinduzi na vyama vingine vya siasa
nchini.
Ametoa
agizo hilo leo (Alhamisi, Februari 21, 2019) wakati akizungumza na
viongozi wa CCM, wabunge pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kagera
kwenye Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera kilichofanyika
katika ukumbi wa ELCT.
Waziri
Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM
mkoa wa Kagera amesema ni muhimu kwa viongozi hao kusoma na kuizingatia
katiba ya chama kwa sababu inaelekeza misingi yote ya utendaji.
Amewasisitiza
wanachama na wapenzi wa CCM wasome katiba ya chama na kuzielewa kanuni,
taratibu na sera ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Akisisitiza jambo hilo Waziri Mkuu amegawa nakala za katiba ya hiyo kwa
viongozi hao na kuwataka wazifikishe hadi kwenye ngazi ya mashina.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa
nchi nzima unaendelea vizuri na kuhusu changamoto zilizopo katika baadhi
ya maeneo nchini wanaendelea kuzirekebisha.
Amesema
lengo lao ni kuhakikisha wanatekeleza ilani kama CCM ilivyoelekeza na
ili kujiridhisha kama wanafanya vizuri lazima viongozi wawasimamie
watendaji katika maeneo yao na watakapobaini kasoro wasisite kutoa
taarifa.
Waziri
Mkuu amesema viongozi chama lazima wajiridhishe kama huduma za maji,
elimu, miundombinu ya barabara, kilimo pamoja nishati ya umeme
zinapatikana kwenye maeneo yao yote na ni kwa kiasi gani.
(mwisho)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.