NA.MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Dernmark nchini Einar Jensen juu ya masuala ya maboresho ya mazingira ya biashara pamoja na uwekezaji nchini.
Mazungumzo hayo yamefanyika hii leo Februari 13, 2019 katika Ofisi yake Jijini Dodoma kwa lengo la kujadili na kuona namna bora ya kuimarisha masuala ya uwekezaji nchini kwa kuzingatia fursa zilizopo katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Alimtaka balozi kuendelea kuona fursa na kuzitumia hususan katika kuwekeza kwenye viwanda hasa vya nguo, mazao ya biashara pamoja na kilimo kwa kuwa ndiyo maeneo yenye fursa nyingi pamoja na kuleta chachu ya ukuaji wa viwanda nchini.
“Ni vizuri kuendelea kuimarisha mazingira ya biashara ili kuendelea kuvutia wawekezaji hasa maeneo ya kilimo na viwanda vya nguo kwa kuwa vinatija katika ukuaji wa uchumi,”Alisitiza Kairuki
Aidha aliendelea kumpongeza balozi huyo kwa kutumia muda wake kumtembelea ofisi kwake kwa lengo la kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masula ya kuboresha mazingira ya biashara pamoja na kuendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili.
“Kipekee nikushukiuru kwa kutembelea ofisi yetu na hii ni ishara nzuri yakuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ambayo yatasaidia Serikali yetu kuendelea kuwa na mazingira rafiki kwa wawekezaji kuzingatia fursa zilizopo katika maeneo mengi ikiwemo; Sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini”alisisitiza kairuki
Kwa upande wake Balozi wa Dernmark nchini, Einar Jensen aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika maeneo ya maboresho ya biashara ikiwa ni pamoja na kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali
“Nimefarijika kukutana na Waziri mwenye dhamana ya uwekezaji na kupata muongozo wa masuala ya uwekezaji nchini na kuendelea kutumia fursa zilizopo Tanzania na ninaahidi kutoa ushirikiano ili kuleta chachu katika ukuaji wa viwanda kwa kuleta wawekezaji katika sekta mbalimbali,”alisistiza Jensen.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akisalimiana na Balozi wa Denmark Nchini Einar Jensen walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake Februari 13, 2019 Jijini Dodoma.
|
Bw.Oscar mkude mwakilishi kutoka Trade Council and EAC Affairs akiwa ameambatana na Balozi wa Denmark Bw. Einar Jensen akichangia jambo kwenye kikao hicho.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.