Wednesday, February 13, 2019

WAZIRI KAIRUKI: SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MAZINGIRA WEZESHI NA ENDELEVU KATIKA SEKTA YA KILIMO.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki akihutubia washiriki wa Kongamano la Tano al Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi lililofanyika katika Ukumbi wa Hazina Dodoma Februari 13, 2019 kwa lengo la Kuchambua na Kujadili sera ili kuboresha maeneo ya kisera ya kilimo lililoratibiwa na Jukwaa la Watafiti na Wachambuzi wa Sera za kilimo kwa kushirikisha wadau mbalimbali nchini.
Naibu Waziri Kilimo Mhe.Omari Mgumba akiwasilisha hotuba yake wakati wa kongamano hilo.
Sehemu ya wajumbe walioshiriki kongamano hilo wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah Kairuki linaloendelea Jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia tarehe 13 hadi 15 Februari, 2019.
Mratibu wa Jukwaa la Uchambuzi wa Sera za Kilimo Prof. David Nyange akiwasilisha mada wakati wa Kongamano hilo.
Mwenyekiti Mwenza wa Timu ya Wadau Bi.Michellle Cornize akichangia jambo wakati wa Kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Joseph Kiraiya akizungumza jambo kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi hiyo anayeshughulikia Sera, Uratibu na Uwekezaji Bi.Dorothy Mwaluko wakati wa Kongamano hilo.
Mwenyekiri TPSF Bw.Salum Shamte akieleza masuala yanayohusu sekta Binafsi wakati wa Kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.