Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka.
Waziri
Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Alhamisi, Februari 28, 2019)
amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari,
minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.
Kufuatia
kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha taratibu za
kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.
Kadhalika,
Waziri Mkuu ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri
waliyoifanya kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza
Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.
Awali,
akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania
(TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo
hilo limekamilika kwa asilimia 95.
Mhandisi
huyo alisema tayari wamefanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa
mbalimbali na kwamba mkandarasi anatarajia kukabidhi mradi huo Mei 31
mwaka huu. Jengo hilo linauwezo kubeba abiria milioni sita.
(mwisho)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.