NA.MWANDISHI
WETU
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa ameeleza kuwa
Serikali itaendelea kuimarisha kitengo kinachoshughulikia masuala ya watu wenye
ulemavu ili kuendana na mahitaji halisi nchini.
Ameyasema hayo hii leo
Aprili 09, 2019 alipokuwa akijibu hoja Bungeni Dodoma ikiwa ni moja ya hoja
iliyotolewa kuhusu uboreshwaji wa kitengo hicho ili kuendelea kuongeza nguvu
katika kushughulikia mahitaji ya kundi hilo.
Naibu Waziri alieleza kuwa
Ofisi yake imejipanga kuhakikisha inaboresha kitengo hicho kwa kuendelea
kuwajengea uwezo watumishi na kuongeza watumishi watakaohudumia makundi hayo.
“Serikali imeoa ipo haja ya kuwajengea
uwezo watumishi wa kitengo hiki wanaosimamia na kuratibu masuala ya watu wenye
ulemavu ili kuongeza nguvu na kuboresha utendaji,”alisema Ikupa
Aliongezea kuwa, umuhimu wa
kuongeza watumishi utasaidia kuendana na mahitaji halisi ya kundi hilo na
kupunguza changamoto zilizopo kwa sasa.
Katika kuendelea kuboresha
utekelezaji wa masuala hayo Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kuandaa mazingira
wezeshi ikiwemo kuanzishwa kwa Mfuko wa Taifa kwa Watu Wenye Ulemavu
utakaosaidia kushughulikia masuala ya ruzuku
za vyama vya watu wenye ulemavu, kuwezesha programu za elimu na mafunzo,
kuwezesha huduma za utengamavu kwa watu wenye ulemavu pamoja na kutumika katika
tafiti mbalimbali.
“Kwa mwaka wa Fedha 2019/2020
jumla ya shilingi Milioni 103 zimetengwa kwa ajili ya Mfuko huo ambazo zitakuwa
ni mbegu kwa mfuko hivyo ni vyema sasa kukawa na wadau wataochangia kutunisha
mfuko huu,”alisisitiza Ikupa
Aidha, Serikali imeendelea
kutoa elimu kwa mamlaka mbalimbali kuhusu ujenzi wa miundombinu rafiki
inayoendana na makundi ya watu wenye mahitaji maalum nchini ili kuondokana na
changamoto za uwepo wa miundombinu isiyoendana na mahitaji halisi kwa kundi
hilo.
”Suala la Miundombinu ni la
kila mtu hivyo basi ni vyema tukahakikisha kunakuwa na ujenzi unaozingatia
uhitaji wa wenye ulemavu ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza”,
alisisitiza Ikupa
=MWISHO=
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.