NA. MWANDISHI WETU
Kamati
ya Kudumu ya
Bunge ya Katiba na Sheria Yaridhishwa
na hatua iliyofikiwa katika kuwawezesha
vijana takribani 3440 kukuza ujuzi wao kupitia programu ya Ukuzaji
ujuzi inayotekelezwa na Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu .
Akizungumza wakati wa
ziara hiyo Makamu Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
Mhe. Nagma Giga amesema kuwa mradi huo ni muhimu katika kuiwezesha nguvu kazi
ya Taifa hasa vijana kuwa na ujuzi stahiki.
“Tunaipongeza Serikali kwa mkakati huu utakaowezesha
kupanua wigo wa ajira na kuchochea ukuaji wa uchumi katika nchi yetu”alisema
Giga.
Mradi wa mafunzo ya
ufundi stadi kwa Vijana unatekelezwa kupitia chuo cha ufundi stadi DONBOSCO kwa
ufadhili wa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo katika mwaka wa fedha
2019/2020 vijana elfu 10,000 wanatarajiwa kunufaika na mpango huo.
Akizungumza wakati wa
ziara ya Wabunge hao mwishoni mwa wiki Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Kazi,Vijana na Ajira Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa dhamira
ya Serikali ni kuhakikisha kuwa nguvu kazi ya Taifa inakuwa na ujuzi unaoendana
na mahitaji ya ujenzi wa uchumi wa Viwanda.
Aliongeza kuwa
kuwajengea uwezo Vijana kwa kuwapa ujuzi stahiki kunawawezesha kujiajiri na
kuzalisha ajira hali inayowawezesha kuchangia katika kukuza uchumi na kuchangia
maendeleo ya Taifa.
Naye Naibu Waziri Ofisi
ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Watu Wenye Ulemavu Mhe. Stella Ikupa amesema kuwa Vijana wanayo
nafasi kubwa ya kuchangia katika kuleta mageuzi ya kiuchumi kupitia ujuzi
wanaopata kupitia programu hiyo.
"Pamoja na
changamoto ya ajira kwa vijana, Serikali yetu sikivu imeendelea kuwapa
kipaumbele vijana katika kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo suala la ukosefu
wa ajira kupitia utekelezaji wa programu hii itawezesha vijana wengi kujiajiri
na kuchangia kukuza uchumi"
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ally Msaki amesema kuwa uwezeshaji
Vijana umepewa kipaumbele kupitia programu hiyo na utaratibu huo ni endelevu
kwa dhamira yakuwafanya vijana wachangie katika kukuza uzalishaji na tija.
Wakizungumza wakati
wa ziara ya Kamati hiyo Katika Chuo cha Ufundi Stadi DONBOSCO cha Jijini Dodoma
baadhi ya wanufaika akiwemo Bi. Esther Ngallya
amepongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano kuwawezesha Vijana kujikwamua
kiuchumi kupitia programu ya kukuza ujuzi inayotekelezwa kupitia chuo hicho.
Akiafafanua amesema
kuwa Serikali imebadili mwelekeo wa maisha ya Vijana walionufaika na Programu
hiyo ambao wanauwezo mkubwa kwa sasa nyanja za umeme, ujenzi, tarazo,useremala,
umeme, ufundi bomba na nyingine nyingi.
Dhamira ya Serikali
ya Awamu ya Tano ni kuwawezesha Vijana kupitia programu mbalimbali ikiwemo ya
kukuza ujuzi na ile ya ujenzi wa vitalu nyumba katika kila Halmashauri ambapo
vijana 100 katika kila halmashauri wanajengewa uwezo ili waweze kutekeleza azma
ya kuchangia katika kukuza uchumi na ujenzi wa viwanda.
=MWISHO=
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.