Sunday, April 7, 2019

WAZIRI MKUU AMUWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KUMBUKUMBU ZA MAUAJI YA KIMBARI

*Awasisitiza Watanzania kudumisha amani, umoja na mshikamano

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kudumisha amani, umoja na mshikamano ambavyo ni tunu walizoachiwa na waasisi wa Taifa.

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Aprili 7, 2019) katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauaji ya Kimbari iliyofanyika katika jiji la Kigali nchini Rwanda.

Waziri Mkuu ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika kumbukumbu hizo, amewasisitiza Watanzania kudumisha amani na utulivu.

Awali,Waziri Mkuu alijumuika na viongozi kutoka nchi mbalimbali kutoa heshima kwenye eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo la Gisozi lililopo jijini Kigali.

Baada ya kutoa heshima kwenye eneo la kumbukumbu za mauaji hayo, Rais wa Rwanda, Paul Kagame alitoa maelezo ya kina kuhusu mauaji hayo yaliyotokea Rwanda 1994.

Viongozi wengine waliohudhuria kumbukumbu hizo ni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Nigeria, Ulusegun Obasanjo.

 (mwisho)

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.