WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuongoza mazishi ya Mwenyekiti
Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi yatakayofanyika leo
Mei 9, 2019 kijijini kwake, Kisereni, Machame, wilayani Hai,
Kilimanjaro.
Waziri
Mkuu anatarajiwa kuongoza mazishi hayo kwa niaba ya Serikali. Ibada ya
mazishi itafanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT) la Kisereni, Machame.
Mwili wa Dkt. Mengi ambaye alifariki dunia alfajiri ya Mei 2, mwaka huu akiwa kwenye matibabu huko Dubai, Falme za Kiarabu, umewasili Moshi leo ukitokea Dar es Salaam na kupokekelewa na mamia ya wananchi waliojipanga barabarani.
Juzi,
(Jumanne, Mei 6, 2019) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na
viongozi wengine wa Serikali, waliongoza maelfu ya wananchi kutoa
heshima za mwisho wakati wa shughuli za kuaga mwili huo katika ukumbi wa
Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Hadi
mauti yanamfika, Dkt. Mengi alikuwa Mwenyekiti wa Wamiliki wa Vyombo
Vya Habari Tanzania (Chairman of the Media Owners Association of
Tanzania - MOAT). Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta
Binafsi Tanzania (Tanzania Private Sector Foundation – TPSF).
Baadhi
ya nyandhifa ambazo Dkt. Mengi aliwahi kushika ni pamoja na Kamishna wa
kamati inayoshughulikia mishahara (Salary Review Commission);
Mwenyekiti wa Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA); Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Mazingira Tanzania (NEMC); Mwenyekiti wa vyombo
vya habari vya Jumuia ya Madola Tanzania (Chairman of the Tanzania
Chapter-Commonwealth Press Union-CPU); Kamishna wa TACAIDS na Mwenyekiti
wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki.
(mwisho)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.