*Ni baada kuifunga Lipuli fainali za ASFC
TIMU
ya Azam FC imefuzu michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika msimu ujao
baada ya kuifunga Lipuli FC bao 1-0 kwenye fainali za Kombe la
Shirikisho la Azam (ASFC).
Mbali
na kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, timu ya
Azam imeondoka na kitita cha sh. milioni 50, medani pamoja na kombe.
Fainali
hizo zimefanyika leo (Jumamosi, Juni 1, 2019 katika uwanja wa Ilulu,
Manispaa ya Lindi ambapo ushindi huo unaifanya Azam FC kuungana na Simba
kuliwakirisha Taifa kwenye michezo ya Kimataifa itakayoanza Novemba
mwaka huu.
Mshambuliaji
wa Azam Obrey Chirwa ndio aliyeiwezesha timu yake ya Azam kuibuka na
ushindi katika mchezo huo baada ya kufunga bao la ushindi katika kipindi
cha pili.
Katika
mchezo huo ulioshuhudiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, timu ya Lipuli
FC iliyong’ara kwa kutawala mchezo kwenye kipindi cha kwanza,
ilishindwa kutumia nafasi nyingi ilizozipata kuifunga Azam.
Mbali
na timu ya Lipuli kuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo, pia timu
hiyo imetoa mchezaji bora wa mechi ya fainali, Paul Ngalema pamoja na
mfungaji bora wa mashindano hayo Seif Rashid.
(mwisho) |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.